Wezi, Matapeli na Vishoka Stendi Mbezi Loius Wachekelea

Wezi, Matapeli na Vishoka Stendi Mbezi Loius Wachekelea

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,016
Reaction score
26,192
Kufungwa rasmi na milele kwa stendi zilizokuwa shekilango, Lumumba na mnazi mmoja imekuwa kicheko kwa matapeli, wezi, vibaka , wabakaji na waganga wa kienyeji waliokuwa wamekosa kazi:

MADALALI:
Ukishuka tu stendi pale , una mizigo, walet mfukoni na mabegi unavamiwa na vijana , MMOJA ANA TIKETI, MWENGINE ANAKUPIGA FINGA, MWENGINE ANAKUVUTA BEGI NA KUELEKEA UPANDE MWENGINE.

Dalali anakwambia Gari fulaniMbovu inaua sana, njoo nikupe hii haina ajali, abiria anaogopa na anamfuata dalali.

TIKETI FEKI:
Abiria anakatiwa tiketi ina jina la basi , ila ya mkononi anaambiwa akifika kwenye gari atapewa nyingine, mkononi say unaenda Arusha unalipa 40,000 kwa Dalali, alafu dalali anampa kondakta 30,000/- yeye anakupiga 10 na hujui kama ni mu wa lile basi ama la na amevaa flana ya basi husika tofauti na shekilango aboria aikuwa anafikam ofisi za basi ndani kabia.

WABAKAJI:
Genge la wahuni, wala mirungi na wanywa visungura, wao wanafanya kulaghai wanafunzi nanaotoka mikoani kuja DAr, kuwadanganya kuwapeleka chuo lakini wanaawapeleka magetoni na kuwabaka.

MUDA WA SAFARI:
Kwakuwa abiria anakatiwa tiketi na kishoka, akisema anataka basi la muda huo huo, basi mkata tiketi anamwambia basi ndio linaondoka, unakuta ni saa moja asubuhi kumbe basi linaondoka saa tano na mtu alikuwa anawahi maziko mkoani. Wale wakata tiketi si waajiriwa wa mabasi , hivyo huwezi shitaki basi. Hizi ni changamoto kubwa.

WAUZA VYAKULA:
Mtu anauza chips mayai ambayo ishapikwa inauzwa dirishani, hivi kwenye kituo cha daldala kweli chakula kinauzwa dirishani na mkuu wa mkoa anamuacha afisa afya wa jiji ofisini?

WAKATA USHURU WA KUINGIA GETINI:
Alfajiri ukingia , ukiwapa hela hawakupi tiketi, wanaibia serikali mpaka kamwanga katoke ndio wanaaacha. Hapa pawe na kamera.

Mengine tuwaachie washangiliaji siku RC alipoenda pale, inaonyesh namna maskini wanavyowachukia matajiri ambapo hao matajiri ndio wanawapa ajira.

UMASKINI ni mbaya kuliko ibilisi. Bora kukutana na mtu anafuga majini kuliko maskini anaayefanya kazi mbezi Luis, ni wachawi na ndio walikuwa wanafurahia Tilisho kufikishwa na pingu badala ya kutaka kujua ukweli.

#RC amejitahidi na ameonuyesha anaweza irekebisha Dar, bado suala la machinga na Bodaboda.
 
Mara ya mwisho kukata ticket ofisini au kwa agents ilikuwa 2020.

Siku hizi unamaliza kila kitu na simu janja yako, tena ukiwa umelala kwenye kochi kwa raha mustarehe.
20% ya wasafiri tu ndio wana smart phone, na wenye nazo 10% ndio wanajua kuingia kwenye website na kusajili tiketi.

Wengi hawana NIDa hivyo namba zimesajiliwa na ndugu zao, hawawezi lina online maana namba si zao.
 
Hata wakijua haisaidi, hao vibaka na wazururaji wanaojiita wapiga debe ukifika stendi wanakusumbua mpaka unachanganyikiwa.
Hapo ndio watu wanapoibiwagaa. Na wanaona hawasemi maana wapo na hao vibaka kila siku.
Huwezi kwenye Tilisho offices ukavamiwa na wapiga debe wala vibaka, unakaa huku unakula TV, unaangalia mpira, unakula chakula na hata choo ni kisafi.

Unapata Wifi bure kwakuwa umelipia basi.

Mbezi stendi , haya
 
Kwani sasa hivi tiketi si zinakatwa online???? na Pal Magufuli mabasi yote yana Ofisi ndogo pale mtu kuibiwa ni ujinga wake hata shekilango kuliuwa na vibaka wanankushika kule nje wanakupiga. Kuibiwa ni uzembe na kupenda shortcut ingia kwenye simu yako kata ticket ya absi lako huwezi nenda kwa wakal hata wa Huduma za kifedha anaweza kukununulia ticket
 
UNAONGEA KWAKUWA MDOMO HAULIPIWI TOZO.
NENDA POLISAI UKONE WAMARIPOTI KUIBIWA, SI PROFESA, DOKTA WALA KANJAJA, NI KILA MTU ANA ENGO YA KUTAPELIWA.
ONLINE WANGAPI WANAJUA.
MATOKEO YA FOM 4 WAZAZI WANASAFIRI TOK MKOA KUA DAR NECTA KUULIZIA, SEUZE TIKETI?
 
Kuwa profesor sio kuwa na akili Mkuu. Akili ni kile kinachobaki ukitoa hizo Unazoita Degree sijui Phd nk . Unashindwa nini Kununua Ticket online lakin ku request malaya BIBO unaweza
 
Najadili na mtoto a mama amelala sebuleni oysterbay kwa shemeji yake, hujui maisha ya Watanzani wewe !
Yaan uende stand ofisi zipo, utaratibu unaujua vizuri ufike upewe Ticket bandia wewe si ni mwehu Mkuu??? siku hizi hakuna familia ambayo haina smart phone hapa DSM omba elimu itolewe zaidi kwa watau ili wajue namna ya kununua ticket online lakini sio kupinga mabus kuanzia safari Magufuli Terminal hili jiji haliwezi kugeuzwa stand za mabus kila kona.
 
20% ya wasafiri tu ndio wana smart phone, na wenye nazo 10% ndio wanajua kuingia kwenye website na kusajili tiketi.

Wengi hawana NIDa hivyo namba zimesajiliwa na ndugu zao, hawawezi lina online maana namba si zao.
Hoja yako ya "NIDA" haina ukweli wowote.

Ticket anakata yeyote yule, awe na nida au asiwe nayo, kinachotakiwa ni unaweka namba utakayolipia, haijalishi yako ama ya mtu mwingine.
 
Yaan uende stand ofisi zipo, utaratibu unaujua vizuri ufike upewe Ticket bandia wewe si ni mwehu Mkuu??? siku hizi hakuna familia ambayo haina smart phone hapa DSM omba elimu itolewe zaidi kwa watau ili wajue namna ya kununua ticket online lakini sio kupinga mabus kuanzia safari Magufuli Terminal hili jiji haliwezi kugeuzwa stand za mabus kila kona.
Siku moja moja toka hapo kwa shemeji , njoo huku kwa Watanganyika wenyewe, utajua unacho ongea unaongea kwa niaba ya jamii ipi.
 
Yaan uende stand ofisi zipo, utaratibu unaujua vizuri ufike upewe Ticket bandia wewe si ni mwehu Mkuu??? siku hizi hakuna familia ambayo haina smart phone hapa DSM omba elimu itolewe zaidi kwa watau ili wajue namna ya kununua ticket online lakini sio kupinga mabus kuanzia safari Magufuli Terminal hili jiji haliwezi kugeuzwa stand za mabus kila kona.
Huyu jamaa atakuwa ametapeliwa yeye.

Siku hizi kupigwa kwenye ticket ni nadra, unless uwe na akili ndogo sana!
 
Back
Top Bottom