Mkuu wa wilaya na Polisi wilaya ya Ukerewe wameshindwa kukomesha wizi na vibaka

Mkuu wa wilaya na Polisi wilaya ya Ukerewe wameshindwa kukomesha wizi na vibaka

Kizibo

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2018
Posts
4,607
Reaction score
10,468
Moja kwa moja kwenye mada.

Wilayani Ukerewe kumekuwepo na wimbi kubwa na wizi wa kuvunja maduka na vibaka mitaani hasa usiku.

Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi kubwa la watu kuvunja maduka na kuingia kuiba pesa. Wezi hao wanapitia kwenye paa, wanakata nyaya za cctv kamera na kuiba pesa.

Pia usiku vibaka ni wengi sana, wanakaba watu na wengine wanaiba mifugo hasa kuku majumbani na kwenda kuwauzia wenye migahawa.

Kuna watu wanamiliki genge la vijana ambao hao ndo hutumwa kwenda kuiba au kuvunja maduka usiku. Ikitokea vijana wamekamatwa, hao wamiliki wa hayo magenge hutoa rushwa polisi na huachiwa na wanaporudi mitaani hurudi kwenye wizi tena kwa jeuri kubwa wakijua hata wakikamatwa watatoka kwa rushwa.

Wengine wanajitapa kwa wenzao mitaani kuwa wana madawa hata wakikamatwa lazima waachiwe tu.

Polisi wilaya ya Ukerewe na Mkuh wa Wilaya ya Ukerewe ndo wanaosababisha tabia hizo za wizi kushamiri kwani hakuna mkazo au hatua kali zinazochukuliwa.

Mitaa korofi inajulikana.
Kule Mtaa wa sungura, vijana wengi ni wavuga bangi. Usiku wanacheza sana kamari (magalamuka) na ni wezi na ni vibaka. Lakini hata wakikamatwa hazipiti siku 2 mtuhumiwa mnamuona mtaani.

Nakatunguru nako kule maovu ni mengi.

Kuna baba mmoja ana mgahawa maeneo ya Labima, chini ukivuka barabara ya lami (ng'ambo ya pili ya Labima) yule ndo mteja wa kuku za wizi lakini kwanini hakamatwi kwa mahojiano??

Kuna jamaa anaitwa Rena, jamaa mweuzi ana mwili mkubwa kiasi na ndevu zenye mvi, pamoja na mwenzake Yusufu, jamaa mweupe amekomaa mwembamba. Hawa jamaa mara nyingi utawakuta kule mitaa ya sungura au kule mkunguni. Hawana kazi maalum. Hawa jamaa ndo wanamiliki genge la vijana wezi ambao ndo wanawatuma kwenda kuiba kwenye maduka ya wafanyabiashara au kwenye majumba ya watu.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe na Jeshi la polisi Ukerewe wachunguzeni hao watu Rena na Yusufu na kijana mwingine sijamjua jina lake ila ndani ya siku 3 nitamtaja jina.

Asanteni.

Active YinYang Maxence Melo please hide my Id
 
Back
Top Bottom