Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Huu ufisadi sasa unafikia pabaya.
Yaani hao wanaoitwa wa usalama wanafuata nini huko kwa kubenea?Mbona hawajampekua EPA hata mmoja?
Huyu Lowassanae alishalaaniwa tangu zamani hana staha ya kuwa kiongozi.kila mahali anataka kula tu eti anajiandaa kuwa rais.Kweli anaweza kuongoza nchi hii?
Siku inakuja na ukweli huwa always unasimama.
Tutajua makapi ni yapi,pumba ni zipi nk
 
PCCB walichunguza kesi ya Mahalu ambayo sasa iko mahakamani, kipindi kile kile wakachunguza skendo ya Richmond wakasema hakuna kesi na deal lilikuwa safi kabisa. Bunge lilipokuja kupata matokeo tofauti wakaja kusema kwamba sheria ya PCCB iliyotumika kuchunguza Richmond ilikuwa butu, lakini sheria hiyo hiyo ilikuwa kali kwenye kuchunguza kesi ya Prof. Mahalu. Unapata picha gani ukilinganisha hayo matukio mawili?

Hivi kumbe PCCB walipoharibu kwenye uchunguzi wa Richmond walisema tatizo lilikuwa sheria zilikuwa butu. Sasa Tume ya muda tu ya Bunge, ya Mwakyembe, ilitumia sheria gani ambazo Tume maalum ya kushughulikia rushwa nchini haina?

Na baada ya kusema sheria wanazotumia ni butu halafu ikawaje? Waliongezewa nguvu au ndio bado ni butu?
 
Huu ufisadi sasa unafikia pabaya.
Yaani hao wanaoitwa wa usalama wanafuata nini huko kwa kubenea?Mbona hawajampekua EPA hata mmoja?
Huyu Lowassanae alishalaaniwa tangu zamani hana staha ya kuwa kiongozi.kila mahali anataka kula tu eti anajiandaa kuwa rais.Kweli anaweza kuongoza nchi hii?
Siku inakuja na ukweli huwa always unasimama.
Tutajua makapi ni yapi,pumba ni zipi nk
Umepotoka sana rafiki yangu.wewe ni kati ya wanaofata mkumbo bila kuujua ukweli.nenda kasome mwenyewe kwanza ripoti ya mwakyembe na uonyeshe ni wapi ambapo lowasa ametajwa kuwa amuhusika na ufisadi zaidi ya preamle ambayo haikiuwa na ukweli wowote kwani watu wameongea nje ya viapo...siku moja wanahistoria watasema ukweli na sie sisi ambao tayaritumehalibiwa akili na magazeti na tuna uoande ambao kamwe hatutaki ata kisikia upende wa pili wa shilingi
 
Hivi kumbe PCCB walipoharibu kwenye uchunguzi wa Richmond walisema tatizo lilikuwa sheria zilikuwa butu. Sasa Tume ya muda tu ya Bunge, ya Mwakyembe, ilitumia sheria gani ambazo Tume maalum ya kushughulikia rushwa nchini haina?

Na baada ya kusema sheria wanazotumia ni butu halafu ikawaje? Waliongezewa nguvu au ndio bado ni butu?

Wakati wanachunguza hizo skendo mbili walikuwa wakitumia sheria ya TAKURU (PCB).

Baadaye Denmark ilikuja kutishia kuzuwia misaada kwenye bajeti mpaka serikali itakapoipa makali sheria ya TAKURU (PCB), na ndipo serikali ilipokuja kupeleka sheria nyingine butu iliyozaa TAKUKURU (PCCB). Kwa hiyo ni sheria butu ilikuwa replaced na sheria nyingine butu.

Pia serikali haikuwa tayari kuondoa huo ubutu mpaka Denmark ilitishia na mswada wa TAKUKURU ulipelekwa kwa kasi ya ajabu na ukapita na ubutu wake huo huo. Kwa kifupi ni kwamba serikali ilishaliona Bunge ni kama rubber stamp na inaleta miswada butu kwa malengo maalum ya kuendelea kutumia sheria butu ili kulinda ufisadi unaoendelea kufanyika kila kukicha.

Nadhani hata hao wafadhili wakati mwingine huwa wanatucheka. Hivi kweli serikali haiwezi kufanya marekebisho ya sheria butu mpaka kuwe na pressure ya kutoka kwa wafadhili?

Bunge letu nalo ni la chama kimoja, kila kinachopelekwa na serikali kinapita kama kilivyo na matokeo yake ndo hayo. Baada ya muda fulani watendaji wanakibanwa wanatumia sheria kujitetea, na hilo siyo kosa lao bali ni la Bunge ambalo linakubali miswada butu inayoletwa na serikali.
 
Sasa mahakama imewapaje search warrant ambayo ina neno "criminal" something, kama ambavyo Kubenea alitamka redioni?

Unajua katika sheria sio busara kuseme lolote kabla hujaona, sio tu shitaka, bali hata ushahidi, ambao mwenzio atakuja nao mahakamani. Huwezi kuanza kusema hakuna kesi hapa wakati hujui mwenzio analalamika nini.

Ingekuwa ni nchi yenye viable press tungekuwa tumeshafahamu yule Jaji alitoa search warrant kuhusiana na uvunjaji wa sheria gani. Bahati mbaya press yenyewe ndio hivyo tena.

samahani kaka kidogo,
kisutu hakuna jaji,ni hakimu.Endelea..............
 
Yashakuwa hayo!
Hahahahaha! Kuhani hapa umepatikana.

Well, sikujua kama Mheshimiwa ana kesi ya kuburuza gazeti. Ngoja nijaribu kuchimba kidogo tu nione nitaibuka na nini... Then tutaona kipi ni kipi... Kesho tu!
 
Hahahahaha! Kuhani hapa umepatikana.

Mkuu kinachoendelea hapa hukijui, it's really funny, ha haa hahahahaahaa…

Jana mwingine kanikosoa niliposema "malfaesance" badala ya "malfeasance."
Nikacheka sana kwa sababu huwa hatukosoani tahajia wala sarufi hapa, hususan kwenye Kiingereza. Sasa sijui hawa watu washakuwa petty wananitafuta kwenye sarufi na tahajia, au wanataka kunitumia ujumbe kwamba mimi sitakiwi kukosea hata tahajia. Tofauti ni kwamba mimi sikosoi mtu wa JF kwenye tahajia, sarufi au lugha kwa ujumla.

Jaji v/s Hakimu…. Malfaesance v/s Malfeasance…… Ha haaa ahaaaa!

Tukianza kukosoana na kufundishana sarufi na tahajia hapa patakuwa petty.

Ngoja nianze na wewe Invisible: Unajua "tahajia" ni nini we mtu?

This is hilarious! Tuanze?

I'm just kidding man. That would be just puerile ma man.
 
Wewe haya maneno uliambia na Lowassa Jana,naona ndiye anayaekutuma?tuambie Utajiri aliona alutoa wapi?Mie mwalimu aliniambi siku kimuona Lowassa nimuulize hilo swali

Unajua mwizi wa kuku ama mwizi wa mifukoni akishtukiwa na watu wakianza kumpa kibano basi mara nyingi anatimua mbio kuelekea kituo cha polisi kwa usalama wake. Bila shaka na Lowasa anaona kibano hiki kikubwa hivyo bora aende mahakamani ambako atapata nafasi ya kuwataja wahusika wakubwa katika dili la richmond maana inasemekana lilikuwa dili la mtu "mkubwa".

Kwako Gembe, tafadhali ninakuomba badilisha hiyo picha. Nikiiona tu ninajisikia kutapika na ninashikwa na hasira kiasi cha kushindwa kula. Ukweli nina hasira sana na Mkapa na bila shaka si mimi tu bali wananchi wengi wa Tanzania.
 
Bwn Tom,

..........sitaki kuamini kuwa ndio wewe mbunge wa kuteuliwa, kwani maneno yako hapo juu yametulia na yako deep....anyway..........well said Tom.......kijana Nape anahitaji ushauri.

.....sasa mkuu Tom hebu tueleze....inakuwaje mradi umeanza kabla ya kupata baraka za CC?........kwanini mradi uanze wakati vijana wanaupinga??...........na pengine hapo ndipo kijana Nape anazo inside information zote.........

.
Mkuu kwanza kabisa ni kweli mimi siyo yule Mh.Thomas Mwang'onda, mbunge wa kuteuliwa.Hata hivyo, niko njiani kuwa na hadhi kama yake kwani natarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kwa uchaguzi ujao wa 2010 na kunyakua moja ya majimbo muhimu.Bora uzima!

Mkuu kwa kujibu hoja zako ni kwamba,hili sakata la mradi wa jengo la UVCCM lina utata kidogo kutokana na ukweli kwamba taarifa za pande zote mbili yaani kutoka kwa bwana Nape na kutoka kwa uongozi wa UVCCM haziko wazi sana.

Bwana Nape alitoa shutuma tu,lakini hakuwa na ushahidi wowote ule wa kuuwasilisha mbele ya waandishi wa habari kama hatua muhimu ya kuipa nguvu hoja yake.Ningemuelewa Nape kama angetuletea hata nakala ya mkataba wenyewe, muhtsari wa kikao cha baraza kuu lililokaa kujadili mradi ili tuone kama ni kweli baraza liliupinga mkataba ama lah.

Unajua kama nilivyosema awali kwamba, kutokana na taratibu za vikao, inawezekana kabisa kuna baadhi ya wajumbe hawakuunga mkono. Hilo ni sawa kabisa kwa demokrasia ya vikao. Lakini linapokuja suala la kufikia maamuzi,kinachoangaliwa ni idadi ya wingi wa wajumbe waliounga au kutounga mkono hoja.

Huo ndio utaratibu wa vikao.Sasa hatuwezi kuhitimisha kwa kusema vijana waliupinga mkataba,kumbe walioupinga ni 10, 20 au 50, ambao kwa mujibu wa ikama ya wajumbe wa kikao, hoja zao zilimezwa na idadi kubwa ya wajumbe waliounga mkono.

Sasa ili kuondoa utata katika hili ilipaswa Nape, kwakuwa alishaamua kulipua bomu, basi angekuja kamili kamili. Angepaswa kubeba sehemu ya mkataba anayoipinga pamoja na muhstari wa kikao husika mbele ya mkutano wake na waandishi wa habari. Haya yote Nape hakuyafanya. Ndio maana binafsi inanipa tabu kuamini kama Nape anaelewa kwa undani mchakato mzima wa mkataba kwa ushahidi mahususi,ukiachilia mbali kuujua mchanganuo wa mradi pekee.

Mimi ninashawishika kuamini kwamba, kwa kujua kuwa vikao halali vya awali kama, baraza kuu na baraza la wadhamini la UVCCM vimeubariki mkataba wa mradi,uongozi wa UVCCM ukaona kuwa wanaweza kuanza shughuli za ujenzi wakati wanasubiri baraka za Kamati Kuu.Sasa hili kibiashara sioni kama ni tatizo.Kwa sababu,ukimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Mzee Makamba,anadai kuwa hata sekretarieti ya NEC iliuunga mkono mradi na hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni kufikisha agenda ya mradi huo mbele ya CC.

Sasa, kwa uozefu wangu ndani ya CCM,ni nadra sana sana, CC kupinga maamuzi ya sekretarieti.Na hii ni kwasababu sekretarieti inaundwa na wajumbe takribani saba wa CC pamoja na makatibu wakuu wa jumuiya za chama. Sasa hawa wajumbe walioko kwenye sekretarieti ndio watapaswa kutetea hoja walizozipitisha kwenye sekretareiti mbele ya CC.

Kinachoweza kufanyika ni kuagiza yafanyike baadhi ya marekebisho kwenye vifungu fulani fulani kama ikibidi. Na daima marekebisho hayo mara nyingi huwa yanalenga kuboresha tu.

Kwa hiyo, kimsingi mimi kwangu suala la mradi kuanza kabla ya baraka za CC sio hoja sana kwa kuzingatia ufafanuzi wa itafaki za vikao vya CCM kama nlivyojaribu kuuelezea hapo juu. Maana kuna suala la muda wa kuanza ujenzi kama ulivyokubalika katika mkataba pia lazima lizingatiwe. Mwekezaji yeye hatambui ratiba za vikao vya chama, yeye haingii mkataba wa kupiga propaganda, yeye anaingia mkataba wa kibiashara.Na katika biashara, kujali muda ni moja ya mambo ya msingi ili faida iliyokusudiwa iweze patikana kwa muda muafaka.

Tatizo kwangu lingekuwa kama kweli baraza kuu na baraza la wadhamini halikuidhinisha mradi husika,halafu itokee ghafla uongozi wa UVCCM makao makuu wanaanza ujenzi.Hapa kungekuwa na tatizo la kimaadili na ingepaswa uchunguzi wa kina ufanyike katika kubaini nani amehusika na maamuzi hayo kinyume cha kanuni na taratibu za UVCCM.

Nimewasikia wajumbe kadhaa wa baraza kuu wakiunga mkono hoja ya bwana Nape. Ni sawa. Lakini nasema hiyo haitoshi kama hawakuweza kuwashawishi wajumbe wengi wa baraza kupinga mradi kwa taratibu za vikao, kwa mujibu wa kanuni.

Kimsingi mimi sipo hapa kujadili kama mradi una manufaa kwa UVCCM ama la.Maana sijausoma mradi husika.Nimesikia kutoka upande mmoja tu, wa Nape. Sasa kwa misingi yangu, ni lazima nipate maelezo ya pande zote husika ndipo nifike mahali nitoe maoni ni nani yuko sahihi juu ya umuhimu na manufaa ya mradi.Ninachojadili ni kama tararibu za kufikia maamuzi ya kuwepo kwa mradi zilifuatwa.

Nadhani nimejibu hoja mkuu. Hatahivyo, nakaribisha maswali zaidi kama yapo.
 
Jamani jamani hizi sheria za ushahidi zimetoka wapi siku hizi?... Hivi kweli Zitto angeweza kuwa na ushaidi wa nyaraka za mkataba wa Buzwagi kuonyesha kila kilichokubaliwa bila yeye kuingia matatani kwa kuwa na nyaraka hizo?..Na angeweza vipi kuzipata zote wakati hakushiriki ktk mkataba huo!..Tuangalie Richmond nani kati yetu alikuwa na mkataba wa Richmond ndipo alipoweza kusikilizwa... Nambieni nani aliyepeleka madai ya kwanza kuhusiana na Richmond na ushahidi gani alikuwa nao?

Zaidi ya hapo hivi kweli mnaamini madai ya Zitto ama dr. Slaa hayakuwa na msingi kwa sababu hakuwa na ushahidi wa kutosha ama ni tetesi kama hivi hufanyiwa uchunguzi ili kupata ushahidi unaothibitisha madai ya pande zote mbili..

Mimi kwa muda wote nilioishi nimeona scandal nyingi na kubwa kubwa zinazowahusu watawala wa mataifa makubwa kama Marekani, Canada, Uingereza, Italy na hata Israel zote zimeanza kwa tetesi kutokana na kile kinachojionyesha wazi kisha uchunguzi hufuata kuthibitisha..Kwa maana hii ni kweli jengo la Umoja wa vijana lipo ktk mkataba ambao una mashaka. Hivyo uchunguzi unaweza kufanyika kutokana na hali halisi ya kile kilichopo yaani mkataba usiofahamika...Hapo ndipo ukweli utakuja patikana na mtu kama Nape aliyeongoza madai haya anaweza kuchukuliwa hatua pindi ikija fahamika kaongopa ama mzushi.

Hata Crime huchunguzwa kwanza kwa fikra huru za utata wa kifo kabla haijadaiwa kuwa ni Homicide na wachunguzi wenyewe lakini mtoa mashtaka anaweza kabisa kusema ndugu yangu kauawa na hataulizwa ushahidi zaidi ya kuwepo kwa hiyo maiti, kuchukua statement yake dhidi ya mkisiwa ambaye hufanyiwa uchunguzi...

Ajabu ya Tanzania hata hicho kifo ama maiti inakataliwa kufanyiwa uchunguzi (kazi ya Mungu) kwa sababu hakuna ushahidi wa mauaji, ushahidi ambao hakuna mtu aliyeutafuta isipokuwa wanasubiri mtu yeote mwenye ushahidi huo autoe.Jamani kama kweli ingekuwa hivi sidhani kama kuna hata murder yoyote ingeweza kuwa solved duniani. Ukiibiwa mali zako nyumbani unaambiwa toa ushahidi kwanza sijui nawe ukauibe wapi?...
 
Mkuu kwanza kabisa ni kweli mimi siyo yule Mh.Thomas Mwang'onda, mbunge wa kuteuliwa.Hata hivyo, niko njiani kuwa na hadhi kama yake kwani natarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kwa uchaguzi ujao wa 2010 na kunyakua moja ya majimbo muhimu.Bora uzima!

Mkuu kwa kujibu hoja zako ni kwamba,hili sakata la mradi wa jengo la UVCCM lina utata kidogo kutokana na ukweli kwamba taarifa za pande zote mbili yaani kutoka kwa bwana Nape na kutoka kwa uongozi wa UVCCM haziko wazi sana.

Bwana Nape alitoa shutuma tu,lakini hakuwa na ushahidi wowote ule wa kuuwasilisha mbele ya waandishi wa habari kama hatua muhimu ya kuipa nguvu hoja yake.Ningemuelewa Nape kama angetuletea hata nakala ya mkataba wenyewe, muhtsari wa kikao cha baraza kuu lililokaa kujadili mradi ili tuone kama ni kweli baraza liliupinga mkataba ama lah.

Unajua kama nilivyosema awali kwamba, kutokana na taratibu za vikao, inawezekana kabisa kuna baadhi ya wajumbe hawakuunga mkono. Hilo ni sawa kabisa kwa demokrasia ya vikao. Lakini linapokuja suala la kufikia maamuzi,kinachoangaliwa ni idadi ya wingi wa wajumbe waliounga au kutounga mkono hoja.

Huo ndio utaratibu wa vikao.Sasa hatuwezi kuhitimisha kwa kusema vijana waliupinga mkataba,kumbe walioupinga ni 10, 20 au 50, ambao kwa mujibu wa ikama ya wajumbe wa kikao, hoja zao zilimezwa na idadi kubwa ya wajumbe waliounga mkono.

Sasa ili kuondoa utata katika hili ilipaswa Nape, kwakuwa alishaamua kulipua bomu, basi angekuja kamili kamili. Angepaswa kubeba sehemu ya mkataba anayoipinga pamoja na muhstari wa kikao husika mbele ya mkutano wake na waandishi wa habari. Haya yote Nape hakuyafanya. Ndio maana binafsi inanipa tabu kuamini kama Nape anaelewa kwa undani mchakato mzima wa mkataba kwa ushahidi mahususi,ukiachilia mbali kuujua mchanganuo wa mradi pekee.

Mimi ninashawishika kuamini kwamba, kwa kujua kuwa vikao halali vya awali kama, baraza kuu na baraza la wadhamini la UVCCM vimeubariki mkataba wa mradi,uongozi wa UVCCM ukaona kuwa wanaweza kuanza shughuli za ujenzi wakati wanasubiri baraka za Kamati Kuu.Sasa hili kibiashara sioni kama ni tatizo.Kwa sababu,ukimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Mzee Makamba,anadai kuwa hata sekretarieti ya NEC iliuunga mkono mradi na hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni kufikisha agenda ya mradi huo mbele ya CC.

Sasa, kwa uozefu wangu ndani ya CCM,ni nadra sana sana, CC kupinga maamuzi ya sekretarieti.Na hii ni kwasababu sekretarieti inaundwa na wajumbe takribani saba wa CC pamoja na makatibu wakuu wa jumuiya za chama. Sasa hawa wajumbe walioko kwenye sekretarieti ndio watapaswa kutetea hoja walizozipitisha kwenye sekretareiti mbele ya CC.

Kinachoweza kufanyika ni kuagiza yafanyike baadhi ya marekebisho kwenye vifungu fulani fulani kama ikibidi. Na daima marekebisho hayo mara nyingi huwa yanalenga kuboresha tu.

Kwa hiyo, kimsingi mimi kwangu suala la mradi kuanza kabla ya baraka za CC sio hoja sana kwa kuzingatia ufafanuzi wa itafaki za vikao vya CCM kama nlivyojaribu kuuelezea hapo juu. Maana kuna suala la muda wa kuanza ujenzi kama ulivyokubalika katika mkataba pia lazima lizingatiwe. Mwekezaji yeye hatambui ratiba za vikao vya chama, yeye haingii mkataba wa kupiga propaganda, yeye anaingia mkataba wa kibiashara.Na katika biashara, kujali muda ni moja ya mambo ya msingi ili faida iliyokusudiwa iweze patikana kwa muda muafaka.

Tatizo kwangu lingekuwa kama kweli baraza kuu na baraza la wadhamini halikuidhinisha mradi husika,halafu itokee ghafla uongozi wa UVCCM makao makuu wanaanza ujenzi.Hapa kungekuwa na tatizo la kimaadili na ingepaswa uchunguzi wa kina ufanyike katika kubaini nani amehusika na maamuzi hayo kinyume cha kanuni na taratibu za UVCCM.

Nimewasikia wajumbe kadhaa wa baraza kuu wakiunga mkono hoja ya bwana Nape. Ni sawa. Lakini nasema hiyo haitoshi kama hawakuweza kuwashawishi wajumbe wengi wa baraza kupinga mradi kwa taratibu za vikao, kwa mujibu wa kanuni.

Kimsingi mimi sipo hapa kujadili kama mradi una manufaa kwa UVCCM ama la.Maana sijausoma mradi husika.Nimesikia kutoka upande mmoja tu, wa Nape. Sasa kwa misingi yangu, ni lazima nipate maelezo ya pande zote husika ndipo nifike mahali nitoe maoni ni nani yuko sahihi juu ya umuhimu na manufaa ya mradi.Ninachojadili ni kama tararibu za kufikia maamuzi ya kuwepo kwa mradi zilifuatwa.

Nadhani nimejibu hoja mkuu. Hatahivyo, nakaribisha maswali zaidi kama yapo.

........you make a lot of sense Tom.......sina la kuongeza,....nakutakia siasa njema ndani ya CCM ( ila roho yaniuma kichwa...... wewe kuwa huko)

Mwenye CV ya Nape please
 
TATIZO NDANI YA UVCCM NI NCHIMBI: elimu ndogo (kazi kununua digrii za Ph.D wakati ana Diploma tu ya Mzumbe), ushamba (kipofu kaona mwezi!), ufisadi (ni errand boy wa Rostam, Lowassa na Karamagi na usanii wa kuact as if ni msomi kumbe hata kuandika jina lake ni taabu.

Hongera kwa kutupa correct analysis ya huyo jamaa NCHIMBI ongezea na roho mbaya
 
Mkuu yawe ya dhati au siyo kwanza hatapita hilo la kwanza tulitambue kabisa kwa sababu amegusa mabapo hapagusiki na tena haparuhusiwi kuguswa.wewe unamchokonoa Lowassa unategemea nini?Vile vile hayo siyo maneno ya kuombea kura.CCM waahidi fedha then watakupa kura.

nnape amekosea gia aliyotumia hatapata u,kiti,yeye angeahidi vitu kama kanga,t-shirts,kofia ,pilau na pesa juu na kuonyesha kuwa hapati makamba alishampinga kauli ya nnape akitaka atumie vikao,zengwe hilo tayari
 
Mkuu Mkandara,

ukiona wanauliza ushaidi ujue umewakamata pabaya sasa wanataka kujiosha na kuwa wasafi mbele ya wananchi, ili hatuna muda mrefu tutapata ukweli kwani EL akienda mahakamani tutajua ukweli na siku zote tunaomba hawa watu waende mahakamani lakini hawataki kwani mahakamani tunaweza kutoa ushaidi wa ukweli na wananchi wakaupta na sio kwingine kwani utaangukia mikononi mwao wenyewe na hakuna kitakachofanyika zaidi utfunguliwa wewe mashitaka ya kusema uongo kama walivyofanya kwa Mrema kwenye kesi ya mil. 900
 
Hii ndiyo habari iliyopandisha mori wa Mzee wa Monduli:

Msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Lowassa abakia na 'galasa'

  • Mradi wa UV-CCM
Na Saed Kubenea

Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Makamba sasa wanaelekea ukingoni kisiasa.

Kitakachowaumbua na hata kusababisha wajiuzulu nyadhifa zao au waodolewe kwenye uongozi ni mgogoro unaotokota kuhusu utoaji wa mradi wa ujenzi wa kitega uchumi cha Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wenye thamani ya Sh. 30 bilioni.

Mgogoro ni kwamba Baraza la Wadhamini la UVCCM, chini ya Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili ya kwanza ya utawala wa Kikwete, lilisaini mkataba kati yake na mwekezaji Subash Patel bila kuhusisha Baraza Kuu la umoja huo, Kamati Kuu ya CCM wala kumfahamisha Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete.

Sasa Makamba amejiingiza kichwakichwa katika kumtetea Lowassa. Lakini kila anayeelewa hali ilivyo, anaona wazi kuwa Makamba amejitia kitanzi.

Hawezi kutetea anachokisema; hafahamu anachokitaka; na anachojaribu kuficha hakifichiki.

Hapa anathibitisha kauli za waliompinga tangu awali kuwa viatu vya ukatibu mkuu wa CCM vilikuwa vikubwa mno kwake; wakati huo na sasa bado vinampwaya.

Makamba anajua Baraza la Wadhamini halina mamlaka ya kuingia katika mradi huo bila idhini ya Baraza Kuu la UVCCM na Kamati Kuu ya chama hicho, lakini anacheza mchezo wa karata kwa kudai kwamba Baraza la Lowassa tayari limefikisha mkataba huo katika Kamati Kuu (CC) ya CCM.

Akiongea kwa msisitizo, Makamba alisema: "Baraza la Wadhamini limefanya kazi nzuri sana. Limefikisha mkataba Kamati Kuu kwa ajili ya kupata ridhaa ya vikao vya juu vya chama. Hivyo, hawapaswi kulaumiwa, bali kupongezwa kwa kazi waliyoifanya."

Hoja hapa siyo kupeleka mkataba katika CC ya CCM hivi sasa. Hoja ni kwamba tayari mkataba ulisainiwa bila idhini ya vyombo husika; jambo ambalo linamfanya Lowassa awajibike na anayemtetea, Makamba atoswe pia kwa kula njama na kufanikiwa kutenda nje ya utaratibu wa chama chao.

Ajabu ni kwamba tayari ujenzi wa mradi wa kitega uchumi hicho umeanza nyuma ya jengo la sasa la makao makuu ya UV-CCM bila wenye mali kuidhinisha. Wakati Makamba anajitutumua kumtetea Lowassa, bila shaka Lowassa anajua kuwa suala hili linaweza kumsogeza mbali zaidi na rais wake na hata kumtosa zaidi kisiasa.

Kauli ya Makamba ilikuja siku moja baada ya mjumbe wa Baraza Kuu la UV-CCM na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Nape Nnauye, kulaumu Baraza la Wadhamini kuruhusu mkataba huo bila ridhaa ya wenye mali.

Nnauye alisema Baraza la Wadhamini limeiingiza jumuiya katika mkataba wa kinyonyaji. Kimsingi alisema, hapinganani na wazo la kuingia ubia na mwekezaji, isipokuwa njia iliyotumika kupitisha mkataba huo.

Hebu tuulizane: Hivi mwekezaji anapata wapi ujasiri, nguvu na kiburi cha kuanza ujenzi hata kabla ya mkataba kusainiwa na kukubaliwa na wenye mali? Lowassa na wenzake walipata wapi ujasiri na uwezo wa kuingia mkataba huo? Kitu gani walichoahidiwa?

Je, iwapo vikao vya juu vya chama vitaukataa mradi, nani atalipa gharama za ujenzi uliokwishafanyika? Muda na usumbufu ambao mwekezaji ameupata utalipwa na nani?

Ni lipi lililosukuma Baraza la Wadhamini kuingia ubia na mtu asiye na mtaji wala teknolojia? Kilichofanyika si kinyume cha kauli ya CCM ya kukaribisha wawekezaji wenye uwezo?

CCM inasema, "Ili mwekezaji wa ndani au nje aitwe mwekezaji, lazima awe na mtaji na teknolojia."

Taarifa zinasema kuwa mwekezaji huyu wa UVCCM, hakuja na mtaji, bali ametumia hati ya kiwanja cha umoja huo kujipatia mkopo katika vyombo vya fedha.

Sasa swali la kujiuliza ni kwa nini UVCCM isitumie hati yake yenyewe kukopa kwenye vyombo hivyo, badala ya kumwachia mbia huyo atumie raslimali za UVCCM kukopa na kujenga?

Kawaida ubia ni kwa mradi (majengo) na si ardhi. Sasa iweje UVCCM iingie ubia na mwekezaji huyu hadi katika suala la ardhi? Kipi walichoahidiwa wajumbe wa Baraza la Wadhamini mpaka wakaamua kufumba macho na kuziba masikio kiasi hiki?

Iwapo mwekezaji hakuwa na mtaji wala teknolojia, nini kigezo cha yeye kuipiku UVCCM? Kwa nini tusiwaze kwamba kuna kitu amewalisha wajumbe wa Baraza la Wadhamini hadi wakaingia katika mtego huu?

Kawaida na hata kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya mwaka 1999, hati itakuwa ya miaka 33 hadi 99. Lakini mwekezaji Patel amekabidhiwa hati hiyo kwa muda wa maisha yake yote! Kuna nini hapa?

Si hivyo tu, ameruhusiwa kuhamisha hisa zake na kurithiwa kwa ndugu, mke, ama yeyote anayemtaka. Ujuha huu unatoka wapi na utaisha lini? Baraza Kuu la UV-CCM, likiamua kuwafukuza kazi wajumbe wa Bodi na kufuta maamuzi walioyafanya, nani atalaumiwa?

Lakini ukiacha hilo, mkataba huu unaonyesha moja kwa moja kwamba Lowassa hakutaka madaraka kwa lengo la kutetea wanyonge. Alitaka madaraka ili kutetea kundi fulani la walionacho.

Kwa hali ya kawaida, Lowassa alitakiwa kutumia kila akili aliyonayo kuhakikisha UVCCM inapata mwekezaji mwenye tija; inakuwa na mkataba ambao kesho na kesho kutwa hauwi kitanzi kwa jumuiya hiyo.

Kwa Lowassa na yoyete yule ndani ya CCM, umoja wa vijana ni sawa na nyumba ya ibada. Kuingiza jumuiya hii katika mkataba wa aina hii, kunaonyesha jinsi wahusika wasivyokitakia mema chama chao.

Hivyo basi, kasoro zilizojionyesha katika mkataba huu zinazidi kumtokomeza moja kwa moja Lowassa katika jitihada zake za kutaka kujisafisha.

Mkataba unamuonyesha Lowassa halisi, hasa baada ya kilichotokea katika mkataba mbovu wa Richmond, ambao ulisababisha ajiuzulu uwaziri mkuu huku akidai ameonewa.

Lowassa alitakiwa kujifunza kutoka pale alipojikwaa awali. Hakutakiwa kujiruhusu kukumbwa na kashfa kubwa kama hii, tena ndani ya chama chake.

Lakini tukiachana na Lowassa, mkataba huu umeonyesha sura mbili za Makamba. Sura ya kwanza, ni ile ya Makamba kutetea yeyote hata kama anajua wazi kuwa anayemtetea hana sifa za kutetewa.

Hili analifanya ama kwa ahadi au kutokana na mapenzi yake binafsi na yule anayemtetea. Maana katika hali ya kawaida, haikutarajiwa kuwa Makamba ajitose kutetea mradi huu.

Hii ni kutokana na ukweli kwamba Makamba si mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini iliyotuhumiwa.

Hata hivyo, tabia hii ya Makamba ya kutetea hata wasio na sifa, haikuanza leo. Ni Makamba huyuhuyu (alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) aliyemtetea kwa nguvu zake zote mfanyabiashara Yusuf Manji hadi kumtangaza kuwa mbunge, wakati alikuwa hajapitishwa hata na vikao vya chama chake.

Sura ya pili ya Makamba ni ile ya kutumia nguvu kutokomeza wale asiowataka. Ni Makamba huyuhuyu aliyesimama kidete kupinga hatua ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Halima Mamuya, kwa hoja kwamba aliingia mkataba bila ridhaa ya Baraza la Wadhamini la umoja huo.

Mkataba wa UWT ni moja ya mikataba yenye tija. Umeandaliwa kwa kufuata umakini na uangalifu mkubwa chini ya Bodi ya Wadhamini inayoongozwa na Waziri Mkuu mstaafu, Joseph Warioba.

Chini ya Warioba, mkataba ulifikishwa katika Kamati Kuu. Lakini Makamba huyuhuyu ndiye alimtosa Mamuya, akisema, "Mamuya amekiuka" taratibu za wenye chama.

Lakini katika hili la UVCCM, Makamba anamtetea Lowassa, akisema amefuata taratibu, eti kwa vile amelipeleka suala hilo kwa Kamati Kuu. Anajifanya kutoelewa kuwa wenye chama hawajapitisha mradi huo; na kibaya zaidi hawautaki.

Je, si Patel huyohuyo aliyepewa tenda ya UVCCM, ambaye amekuwa anahusishwa na mapungufu makubwa katika miradi mingine?

Mfano hai ni mradi wa makaa ya mawe wa Mchuchuma na Liganga, Iringa. Alikabidhiwa mradi huu katika mazingira ambayo baadhi ya watendaji wa serikali wamehusika kumbeba na hata "kumkabidhi" ardhi ya kijiji, na kumpigia debe kwa nguvu za kutisha apate mradi huo, huku wakijua hana mtaji wala teknolojia ya kutosha.

Kama si kelele za wabunge na vyombo vya habari, kuanika mapungufu katika mradi huo, huku baadhi ya wapiga debe ya Patel wakitumia jina la Rais Kikwete kutisha wanaompinga Patel, mradi wa Mchuchuma na Liganga ungeshakuwa kashfa nyingine kubwa kwa serikali hii ya awamu ya nne.

Hivi CCM bado inalipa fadhila za michango ya uchaguzi mkuu? Hata baada ya kilichotokea kwa Richmond na EPA? Je, viongozi wa CCM hawajajifunza kitu?
 
Waliopo UVCCM sasa watueleze ni nini hatma ya nape na uchaguzi baada ya lowassa kwenda mahakani?
 
Hongera kwa kutupa correct analysis ya huyo jamaa NCHIMBI ongezea na roho mbaya
Unajua mtu hasiye na madhara kwenu hamwezi kila siku kumtajataja na kumfanyia wtat the rubbish you call analysis...pamoja na yote ukweli unabakia palepale kuwa yeye ni kiboko yenu..hatingishiki na wala hapotezi mchezo....kwa mara ya pili tuone game kati ya Nape na Nchimbi,nani zaidi.Kwa uhakika ni kuwa Nape atachakazwa kwa aibu kubwa na pengine atahama mpaka ccm na kuja huko Chadema
 
Ok Ni Yule Mfanyakazi Wa Bakheresa Ambaye Kubenea Alikuwa Akimchukulia Mkewe.

Kwi kwi kwi kwi..... Fisadi mtoto, yuo must be kidding! Otherwise, this woman must be a prostitute! Yaani anagawa ur...d... kama hana akili nzuri?!! Wa kwanza mmewe wa bakhresa, halafu kubenea, kisha Mzee wa watu, pengine na mtoa habari hii... maana anaonekana kuwa na interest binafsi katika hili... sorry, is just a joke?!! Au labda huyo mzee wa watu alikuwa na kosa jingine tofauti na kubenea???! Sikuelewi mkuu!
 
Moja ya kitu cha msingi MwanaHALISI wanahitaji ni uwakilishi mzuri zaidi wa kisheria. Mwanasheria wake anafanya miscues fulani ambazo zinaweza kuboreshwa zaidi.

Kwa mfano, Kubenea alipohojiwa kuhusu uhalali wa utoaji taarifa za akaunti za watu, aliiambia KLH News kwamba wao hawatoi akaunti za "walima Kahawa wa vijijini," na wa wananchi wa "huko Buhemba" na kwingineko. Ila ni viongozi fulani fulani wa nchi. Sasa, huhitaji kuwa mwanasheria kujua kwamba, kama ni makosa kuvujisha akaunti za benki - assuming ndilo kosa - basi ni wazi kwamba kila mteja mwenye hizi akaunti analindwa na sheria ya nchi, na sio mlima Kahawa tu. Wakili wake hatakiwi kumruhusu atoe justification kama hivi za kujifunga kitanzi.

Mfano mwingine, wakili aliyeitwa kuja eneo la tukio, hakutakiwa kuruhusu isainiwe search warrant inayomtafuta "Msaki and others." Msaki hakuna anae mjua hapo MwanaHALISI. Na hao "others" wanaweza kuwa wako kwenye sayari ya Zebaki (kama ambavyo Kishoka huwa anasema.)

Hizi nadhani ni faux pas zinazoweza kuboreshwa zaidi. Humo ndani pia wawe na watu wanapitia vitu wanavyoandika. Vinginevyo wanaweza kuishia kulipa mapesa kama yale ya Sumaye. Tukikosoa press ya Bongo ni katika kujaribu kuijenga vile vile.

Unajua nchi hii imefika pabaya sana na ili mambo yatulie ni lazima misuguano ya namna hii itokee. Shida ni kuwa mambo hayako wazi, na viongozi wanawafanya watu wanashuku mambo ambayo huenda hata hayapo. Lowasa anasema ali-saini memorandum of understanding, halafu tunaambiwa ujenzi umeanza, hili silielewi, je MoU inanguvu ya kumruhusu mjenzi kuanza kujenga?

Kisha tunaambiwa Baraza kuu la vijana lilipiga kura ya kupinga mradi huo, na bado baraza la wadhamini likapitisha. Katika mkanganyiko huu kweli mtawalaumu watu kama akina Kubenea kushuku na kuandika? Achana na Kubenea, hata mjumbe wa halmashauri ya taifa ya CCM, Mnauye naye amesema mkataba ni wa kifisadi.

Tafdhalini viongozi wetu fanyeni mambo kwa kufuata taratibu, mtapunguza shuku na mifarakano.
 
Back
Top Bottom