Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Nahisi jaji atakayepangwa ni yuleee kutoka kwa kijiwe cha Masha kama ndo mpango wa mafisadi
 
Lowassa sasa amkabili Kubenea

*Awaagiza wanasheria wake washitaki gazeti la MwanaHalisi
*Ni kwa kuandika jana kuwa alisaini mkataba wa UVCCM usiku
*Alalamikia kupikiwa majungu na uzushi kwa lengo la ziada


Na Mwandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa zamani, Mbunge wa Monduli, Bw. Edward Lowassa, ameamua kupambana na gazeti la MwanaHalisi kwa alichoeleza kuwa ni kumchafua.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Bw. Lowassa amewaelekeza mawakili wake, kampuni ya Rex Attorney kulifungulia gazeti hilo mashitaka mara moja, ili lichukuliwe hatua za kisheria.


Hatua hiyo inakuja siku moja tu baada ya wadau wa habari wakiwamo wahariri na wanaharakati kutoa tamko la kulaani kitendo cha Polisi kumpekua Mhariri Mtendaji wa Gazeti hilo, Bw. Saed Kubenea ofisini na nyumbani.


Bw. Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM, analalamikia habari iliyoandikwa jana na Bw. Kubenea kwenye gazeti hilo, ikisema "Lowassa katika kashfa mpya". Amesaini mkataba usiku. Ni mradi wa UVCCM. Makamba amdanganya Kikwete.


Habari hiyo iliyo ukurasa wa kwanza wa gazeti hilo, inaendelea katika kurasa za nane na tisa katika makala isemayo: Msumari wa mwisho katika 'jeneza' la Lowassa.


Kwa mujibu wa gazeti la MwanaHalisi, habari hiyo inazungumzia sakata la uuzwaji wa uwanja na jengo la Umoja wa Vijana wa CCM, katika barabara ya Morogoro, Dar es Salaam.


Katika habari hizo mbili, kwa mujibu wa Bw. Lowassa, anakaririwa akidaiwa kuandika barua Julai mwaka huu kwa Katibu Mkuu wa CCM, Bw. yusufu Makamba, akisema Baraza la Wadhamini limekubali mradi, lakini "usisainiwe mpaka kupatikana kwa kibali cha Kamati Kuu (CC)."


"Napenda kuifahamisha jamii kuwa habari hii ni uzushi na majungu yanayopikwa yakiwa na lengo la ziada. Wakati kichwa cha habari kinataja kuwa nimesaini mkataba usiku, ukisoma habari yenyewe ndani, hakuna sehemu inapotaja iwapo nimesaini mkataba huo usiku," alilalamika Bw. Lowassa.


Alisema anachofahamu yeye ni kuwa Baraza la Wadhamini la UV-CCM, ambalo yeye ni Mwenyekiti wake, lilisaini hati ya makubaliano (Memorandum of Understanding) na si mkataba.


Bw. Lowassa katika maelezo yake hayo, anasisitiza kuwa maelezo ya Bw. Makamba ni sahihi kuwa mkataba huo umepelekwa katika chama kwa ajili ya kusubiri uamuzi wa Kamati Kuu.


"Gazeti hili limethibitisha upungufu mkubwa katika taaluma. Namba yangu ya simu wanayo na wanajua niko bungeni, wangefika wakaniuliza, ila kwa nia ya kuendelea kutimiza malengo yao, hawakufanya hivyo," alisema Bw. Lowassa.


Huyu ni kiongozi wa pili wa ngazi za juu wa CCM kulishitaki gazeti la MwanaHalisi kwa madai ya kuwachafua, mwingine akiwa ni mjumbe mwingine wa CC, Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz.


Mbali na kushitakiwa, Mhariri Mtendaji wa MwanaHalisi naye ana kesi mahakamani dhidi ya watu wanaodaiwa kumshambulia yeye na Mhariri Mshauri wa Gazeti hilo, Bw. Ndimara Tegambwage.


Hivi karibuni, Mhariri huyo alijikuta akipekuliwa ofisini na nyumbani kwa kile kilichokuja kudaiwa na Jeshi la Polisi nchini, kwamba ni kushirikiana na mtumishi wa benki ya NBC kuchukua akaunti za wateja wa benki hiyo na kuziingiza kwenye mtandao wa intaneti.


Bw. Lowassa alilazimika kujiuzulu uwaziri mkuu Aprili mwaka huu, baada ya kutajwa katika ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, kwamba alijihusisha na mkataba wa kuipa zabuni kampuni ya Richmond kufua umeme wa dharura.


Kashfa hiyo iliwaathiri pia aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi na aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ibrahim Msabaha, ambaye alikuwa waziri wa Nishati na Madini kabla ya Bw. Karamagi.
 
Ni wazi lazima apelekwe mahakamani...jamaa ni muongo sana.anasma kuwa mkataba ulisainiwa usiku,wakati hakuna mkataba uliosainiwa kwa kweli.na hata makala yenyewe hakuna mahali walipofafanua zaidi kuwa kusaini usiku maana yake ni nini...pia si kweli mkataba umesainiwa bali ni ujinga wa kulewa wa Kubena.kwani kilichosainiwa ni memorundum of understanding.Kesi zote zinaendelea vema na muda si mrefu Kubenea atajua hayuko above the law.

Wewe haya maneno uliambia na Lowassa Jana,naona ndiye anayaekutuma?tuambie Utajiri aliona alutoa wapi?Mie mwalimu aliniambi siku kimuona Lowassa nimuulize hilo swali
 
Jamani hii vita ni kali,wala huwezi tabiri mshindi sasa hivi,
Tena EL akiingia kotini ni mahali pazuri na huru kupumua yote.Tunajua mafisadi nao wamejiandaa baada ya kubanwa kila kona pia sasa hawaaminiani kabisa.

Tusimwangalie kubenea kama yeye peke yake,siku alipoingia vitani anajua anatumia silaha za B57 au patriot kuzima scud za Mafisadi.
Vita kama hii huingia kichwa kichwa bila kuwa na wafadhili wa kukuuzia silaha na kukupatia hata madawa ya kutibu majeruhi.

Dr Slaa alitaja pale Mwembe yanga mafisadi,ni kesi ngapi zilizo mahakamani?

Amandla ..........Ngawethu
 
"MASWALI MAGUMU"
Hakika, kesi hii itamdhalilisha sana Lowassa tena kwa muda mrefu usiotabirika kuanzia sasa. Ningekuwa mshauri wake ningemwambia "mzee mezea tu!" Kama ilivyokuwa kwa Richmond, katumia jazba, anakwenda mahakamani! Sasa itabidi ajibu mahakamani maswali magumu yafuatayo kwa ukamilifu:
(a) Je, kwa nini utekelezaji wa mradi wa jengo la vijana umeanza bila mkataba mahsusi kusainiwa kwanza?HII SIYO KAZI YA BARAZA NI WATENDAJI WA UVCCM
(b) Je, alitumia vigezo vipi kumwingiza Bosi wa Tan Roads, Mrema, kwenye kampuni ya Vijana Development Corporation?MREMA ALITEULIWA NA KAMATI YA UTEKELEZAJI NA SIYO WADHAMINI
(c) Je, kwa nini alimtoa Mhe. Wilson Masilingi kwenye Baraza la Wadhamini la UVCCM bila sababu wala taarifa yoyote?LOWASA ATEUI WALA KUONDOA MTU BALI NI BARAZA KUU.
(d) Je, alitumia msingi upi kumteua fisadi Nazir Karamagi kuziba nafasi ya Masilingi?ALIEMTEUA NI BARAZA KUU NA SIYO LOWASA
(e) Je, kwa msingi upi mwekezaji amepewa asilimia 75 ya ya umiliki wa kiwanja (ardhi) bila kibali cha Kabidhi Wasii wa Serikali?BADO MKATABA HAUJASAINIWA NA UNAPITIWA NA CHAMA
(f) Je, uhalali wa utekelezaji wa mradi huu unatoka wapi wakati wenye mali, Baraza Kuu la UVCCM, hawakuridhia?BARAZA KUU LILIPITISHA NA MIHTASARI IPO SEMA ULIANDIKWA KWA KIZUNGU HAWAKUELEWA HILE MoU
(g) Je, kulikuwa na Mkataba wa Utekelezaji au MOU tu? Kama ni MOU tu, basi jibu katika (a) hapo juu linatosha. Ikiwa kuna Mkataba wa Utekelezaji, kama MwanaHalisi na wanasheria wake wanavyodai, kwa nini Lowasa na wenzake wasishitakiwe kwa udanganyifu?WANASHERIA WATAKUWA WAMEMIX JAMAA ILI APIGWE KESI YA UZUSHI
Yapo maswali mengine mengi ambayo Lowassa atalazimika kuyajibu atakapotinga mahakamani. Nachelea kusema, Lowassa atashindwa kuyajibu kwa kinaganaga maswali yote! Lazaros
Hata hivyo ni kwamba haya maswali wanaotakiwa kujibu ni uvccm na siyo Lowasa kwa kuwa lazima kwanza ujue kazi na wajibu wa baraza la wazamini kabla ya kujitungia maelezo yako hapa.
 
kama mkataba haujasainiwa kwa nini mwekezaji kaanza kujenga kwa kweli lowasa kashikwa pabaya
Katika MoU wameweka kipengele cha kuonyesha GOOD WILL ambapo mwekezaji atafunga mitambo ya ujenzi na kuanza kujenga foundation wakati uvccm watakuwa wanaprocess kuseparate hati ya kiwanja hicho.kama mkataba unashindikana kuna mambo yataanyika kuivunja MoU
 
Wewe haya maneno uliambia na Lowassa Jana,naona ndiye anayaekutuma?tuambie Utajiri aliona alutoa wapi?Mie mwalimu aliniambi siku kimuona Lowassa nimuulize hilo swali
Hakuna maneno nilioambiwa na Lowasa bali natauta ukweli na kuuatilia,mimi binafsi sijuani na Lowasa na wala akiniona hanijui...swala la utajiri wa lowasa kama ulikuwepo toka enzi za nyerere ina maana hauna uhusiano na tuhuma za karibuni za ufisadi..ni jasho lake itakuwa...sasa mimi naweza kujibu swali lako kwa urahisi kabisa wewe niambie tu ana utajiri wa kiasi gani na uko wapi mimi pasi na shaka nitakwambia ameutoa wapi?maana hisije kuwa unaleta nawe maneno ya mitaani tu hapa.
 
I bet, hakuna atakayeenda mahakamani!
Hii ni lugha ya kujitetea tu.

Hivi - by the way, kwa wataalamu wa saikolojia na mambo kama hayo, hivi ufisadi unaweza kuwa ni genetical? au ni kilevi cha aina fulani - ukishaanza basi ni lazima uendelee nacho na hakijali kama ulishaathirika awali.
 
I bet, hakuna atakayeenda mahakamani!
Hii ni lugha ya kujitetea tu.

Hivi - by the way, kwa wataalamu wa saikolojia na mambo kama hayo, hivi ufisadi unaweza kuwa ni genetical? au ni kilevi cha aina fulani - ukishaanza basi ni lazima uendelee nacho na hakijali kama ulishaathirika awali.
Watu wanamaanisha wanaposema wanakwenda mahakamani,wait and you will see.swala la ufisadi kuwa ni genetical nadhani wanasaikologia siyo mahali muafaka kuwauliza may be kaulize wana baiolojia.
 
Huyu jana usiku alipohojiwa na TBC alisema kuwa amedhalilishwa sana ,na hakupewa haki ya kusikilizwa na kutoa maoni yake ,hivyo amewaamuru wanasheria wake waende mahakamani.
 
Ni wazi lazima apelekwe mahakamani...jamaa ni muongo sana.anasma kuwa mkataba ulisainiwa usiku,wakati hakuna mkataba uliosainiwa kwa kweli.na hata makala yenyewe hakuna mahali walipofafanua zaidi kuwa kusaini usiku maana yake ni nini...pia si kweli mkataba umesainiwa bali ni ujinga wa kulewa wa Kubena.kwani kilichosainiwa ni memorundum of understanding.Kesi zote zinaendelea vema na muda si mrefu Kubenea atajua hayuko above the law.


FM,

Ninauhakika huyo anayeenda mahakamani mwisho wake ni kuchemsha na kuambulia more political deterioration! Namuonea imani!
 
Lowassa aishiwa uvumilivu

na Kulwa Karedia

ALIYEKUWA Waziri Mkuu, Edward Lowassa, ametangaza nia ya kulifungulia mashitaka gazeti la kila wiki la MwanaHalisi, kwa madai ya kumkashifu na kumchafulia jina.

Uamuzi huo wa Lowassa unatokana na habari yenye kichwa cha habari kisemacho: ‘Lowassa katika kashfa mpya', ‘Amesaini mkataba usiku', ‘Ni mradi wa UV-CCM' iliyochapwa katika toleo namba 107 la gazeti hilo la kila wiki lililoingia mitaani jana.


Lowassa alitangaza uamuzi huo wa kwanza kuutoa tangu alipolazimika kujiuzulu uwaziri mkuu Februari mwaka huu kupitia taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na kusainiwa na yeye mwenyewe.


Uamuzi huo wa Lowassa unakuja baada ya jina lake kutajwa mara kadhaa likihusishwa na mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao yeye ni Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la jumuiya hiyo ya chama tawala.


Katika taarifa ya jana, Lowassa ambaye alilithibitishia Tanzania Daima kwa simu kuwa ni yake, alisema amefikia uamuzi huo kwa maelezo kuwa, gazeti hilo linalochapishwa na Kampuni ya Hali Halisi Publishers, limekuwa na utaratibu wa kumchafua katika matoleo yake mbalimbali. Hata hivyo hakutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo.


"Kwa kuwa gazeti hili limekuwa na utaratibu wa kunichafua, nimewaeleza mawakili wangu wa Kampuni ya Rex Attorney, wawafungulie mashitaka mara moja ili wachukuliwe hatua za kisheria," alisema Lowassa katika taarifa hiyo.


Katika taarifa hiyo, Lowassa anasema anapenda kuifahamisha jamii kuwa, habari hiyo imeandikwa kwa majungu yanayopikwa, yakiwa na lengo la ziada.


"Wakati kichwa cha habari kinataja kuwa nimesaini mkataba usiku, ukisoma habari yenyewe ndani hakuna sehemu inapotaja iwapo nimesaini mkataba huo usiku kama walivyoandika," alisema Lowassa katika taarifa hiyo ya ukurasa mmoja.


Alisema katika taarifa hiyo kuwa, maelezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu wa CCM, Yusufu Makamba, kuhusu mkataba huo, yalikuwa sahihi, ikiwa ni pamoja na kupeleka mkataba kwenye chama kwa ajili ya kusubiri maamuzi ya Kamati Kuu.


"Gazeti hili limethibitisha upungufu mkubwa katika taaluma. Namba yangu ya simu wanayo, na wanajua nipo bungeni, wangefika wakaniuliza, ila kwa nia ya kuendelea kutimiza malengo yao, hawakufanya hivyo," alisema Lowassa katika taarifa hiyo.


Lowassa aliongeza kuwa habari hiyo ilihamia ukurasa wa pili na kusisitizwa na makala ndefu kwenye kurasa za 8 na 9 iliyokuwa na kichwa cha habari: "Mradi wa UV-CCM; msumari wa mwisho katika ‘jeneza' la Lowassa.


Alisema habari na makala hiyo, vilikuwa vinazungumzia kiwanja namba 108/2, kilichopo jengo la UV- CCM, ambalo linadaiwa kuingia mkataba wenye utata.


Katika habari hiyo ya jana, MwanaHalisi lilieleza kuwapo kwa taarifa za Lowassa kusaini mkataba huo, tofauti na madai yaliyotolewa na Makamba wakati alipozungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita aliposema suala hilo lilikuwa limepelekwa katika Kamati Kuu ya CCM kwa ajili ya maamuzi.


Gazeti hilo lilieleza pia kuwa, Lowassa akiwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na Amos Makalla, wakati akiwa bado Katibu wa Baraza hilo, ndio waliosaini mkataba huo kwa niaba ya UV-CCM, wakati upande wa mwekezaji, waliosaini ni Shubhashbai M. Patel, anayejitambulisha kama Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya MM.IS.ML na Jamila Adam, ambaye ni shahidi.


Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana kutoka mjini Dodoma, anakohudhuria kikao cha Bunge, Lowassa alisema anachokifahamu ni kuwa Baraza la Wadhamani la UV- CCM ambalo yeye ni mwenyekiti wake, lilikuwa limesaini Hati ya Makubaliano (Memorandum of Understanding – MoU) na si mkataba.


Alisema hatua ya gazeti hilo kutumia neno ‘jeneza' la Lowassa, lilikuwa ni kielelezo kwamba lilikuwa limefikia hatua hata ya kumchulia kifo, kwa sababu ambazo alisema hazijui.


Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Hali Halisi Publishers, Saed Kubenea, alisema walikuwa na uhakika na kile walichokiandika, kwani kabla ya kukichapa waliwasiliana na wanasheria waliobobea na wakawathibitishia kuwa walichokuwa nacho kilikuwa ni mkataba na si MoU kama anavyotaka ionekane Lowassa.


'‘Mwache aende mahakamani, tutaenda kukutana naye huko huko. Hatuna wasiwasi kabisa, kwani sisi tunao mkataba ambao Lowassa amesaini na ambao hata wanasheria wetu waliobobea walipoupitia walisema ule ni mkataba na si MoU kama anavyodai yeye," alisema Kubenea.


Alisema ushahidi mwingine unaowathibitishia kuwa kilichosainiwa ni mkataba ni ukweli kwamba, utekelezaji wa mradi ulioibua utata huu mzima, umeshaanza kutekelezwa kabla hata ya maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM.


Mtu wa kwanza kuibua utata katika mkataba huo wa UV-CCM alikuwa ni kada kijana wa chama hicho, Nape Nnauye, wakati akichukua fomu za kugombea uenyekiti wa umoja huo wa vijana, katika uchaguzi utakaofanyika baadaye mwaka huu.


Nape, mtoto wa kada wa siku nyingi wa CCM, marehemu Moses Nnauye na ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, alifikia hatua ya kumtaka Lowassa, Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Vijana, Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo kujiuzulu nyadhifa zao kutokana na kashfa ya mradi huo aliouelezea kuwa ni wa kinyonyaji.



Source: TANZANIA DAIMA.
 
FM,

Ninauhakika huyo anayeenda mahakamani mwisho wake ni kuchemsha na kuambulia more political deterioration! Namuonea imani!
Hayo ni maoni yako wewe lakini ukumbuke kuwa wewe siyo hakimu wala jaji...Bravo Lowasa pambana kwa nguvu zako zote,huna cha kupoteza zaidi ya kumwangamiza katika mikono ya sheria Kubenea na vibaraka wake wote,utaishangaza dunia haki itakapotoka na ukweli kujulikana,watainamisha sura zao chini kwa aibu pale watakapoumbuliwa majungu yao na watalipia madhila waliokupatia
 
Watu wanamaanisha wanaposema wanakwenda mahakamani,wait and you will see



Wengi walishaongea hivyo na wakaishia kuwasiliana na mawakili wao!
Siuoni ujasiri katika hili. Remember, uchaguzi wa UVCCM hauko mbali na hii kesi ina athari za moja kwa moja kwenye uchaguzi huo.
 
Last edited:
Watu wanamaanisha wanaposema wanakwenda mahakamani,wait and you will seeWengi walishaongea hivyo na wakaishia kuwasiliana na mawakili wao!
Siuoni ujasiri katika hili. Remember, uchaguzi wa UVCCM hauko mbali na hii kesi ina athari za moja kwa moja kwenye uchaguzi huo.
Tatizo unaposema wengi unamaana ya nani,nachojua mimi ni kuwa tayari ana kesi kadhaa,mojawapo ni ya RA,kesi namba 58 ya 2007 mahakama kuu ya tanzania.tatizo ni kuwa mwenyewe hazitangazi na Kubenea ameshapeleka utetezi wake kwa hatua za awali...ni wazi atashindwa ktk kesi hizi.
 
Naamini kuwa jana wakati Lowassa alipokuwa anatoa agizo hili alikuwa hajashauriana na wanasheria wake , kwani mkataba umesainiwa na hata mimi nimeuona na tayari mkandarasi yupo site sasa atasema je kuwa hakuna mkataba?

Mkataba una sahihi yake yeye Lowassa na Amos Makala.
 
Hakuna maneno nilioambiwa na Lowasa bali natauta ukweli na kuuatilia,mimi binafsi sijuani na Lowasa na wala akiniona hanijui...swala la utajiri wa lowasa kama ulikuwepo toka enzi za nyerere ina maana hauna uhusiano na tuhuma za karibuni za ufisadi..ni jasho lake itakuwa...sasa mimi naweza kujibu swali lako kwa urahisi kabisa wewe niambie tu ana utajiri wa kiasi gani na uko wapi mimi pasi na shaka nitakwambia ameutoa wapi?maana hisije kuwa unaleta nawe maneno ya mitaani tu hapa.


Hakika nimeamini mtoto wa nyoka ni nyoka tu!

Kwa msimamo wako mkuu Fisadi Mtoto, umenikumbusha maneno niliyoambiwa na mke wangu kwamba yeye(mke wangu) hakuamini katu maneno ya wanakijiji wa kijijini kwao waliyoyasema kwa muda mrefu kwamba, baba yake ni mwizi mpaka pale siku moja aliposhuhudia tena kwa macho yake mwenyewe pale alipomuona baba yake mzazi akiiba ng'ombe kwenye zizi la ngombe la jirani yao usiku wa manane. Hapo ndipo alipoamini maneno yote ya wanakijiji wa kijijini kwao.

Hata wewe Fisadi Mtoto sikushangai sana pale unapopata ujasili feki wa kumtetea huyo fisadi baba yako!

Naamini siku moja Mungu atakuonesha ukweli pale utakaposhuhudia baba yako fisadi anakuibia wewe mwenyewe iwe mali au mke/mme wako. Na hapo ndipo utakaporudi kundini na kuwaomba msamaha watz waliochoshwa na ufisadi wa baba yako tangu enzi za mwalimu!

Nahitimisha kwakukupa pole sana pale Mungu atakapowaonesha watanzania njia bora ya kurudisha mali yao yote iliyokwapuliwa na fisadi baba yako! Na hapo ndipo utakapolia na kusaga meno! Amen!
 
Hakuna maneno nilioambiwa na Lowasa bali natauta ukweli na kuuatilia,mimi binafsi sijuani na Lowasa na wala akiniona hanijui...swala la utajiri wa lowasa kama ulikuwepo toka enzi za nyerere ina maana hauna uhusiano na tuhuma za karibuni za ufisadi..ni jasho lake itakuwa...sasa mimi naweza kujibu swali lako kwa urahisi kabisa wewe niambie tu ana utajiri wa kiasi gani na uko wapi mimi pasi na shaka nitakwambia ameutoa wapi?maana hisije kuwa unaleta nawe maneno ya mitaani tu hapa.

Jinsi unavyochangia inaelekea wewe uko karibu sana na huyo Lowassa. Ama ni baba yako wakufikia, mjomba au amekukatia mshiko, siyo bure.
 
Hivi kama nikiuliza, kama mtu akivujisha namba za account za watu, anaeathirika ni nani? na anaetakiwa kuchukua hatua ni nani?, je ni yule anaeathirika na uvujishaji huo au ni yule third party asiyehusika na lolote na asiyeathirika na lolote kwenye ile account?

Mi nafikiri ktk banker customer relationship, there is a contract between the customer and the bank. therefore, the duty of secrecy resides on the banker for the account of his customer and the contract is for the two parties.

Kama kuna jambo lolote linaloathiri hawa watu wawili, basi ni either banker or customer to institute a suit in court, na sio third party. Labda kama hawa watu wawili walienda kushitaki polisi kuhusu hilo. Sasa kulikuwa na nini au polisi inawahusu nini hata wasuspect kuwa kubenea anazo account za watu? Kama anazo ni kosa gani hilo na ktk sheria gani? Mbona namba za account zetu wanazo watu wengi tu, kwani wanaweze kuzi appropriate bila ridhaa yetu? Mimi account zangu wanazo wengi tu kwasababu huwa nawapa waweke hela kwenye account yangu hukohuko waliko na hawana uwezo wa kuifanya lolote, siathiriki na lolote lile. kama huwa inaathiri jamani naomba mnieleweshe kwa hili.

Sijui polisi iliwaathiri nini au whether its their business kumwingilia kubenea home kwake kiasi kile. ni aibu kwao. Hivi Kubenea kama alikuwa na account namba za hao watu, angezifanyia nin? Yaani ingewaathiri nini kama hao watu ni clean? Manake mtu kama ni clean huwezi ogopa kitu kama hichi.

Kwaheri.
 
Back
Top Bottom