Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

huyo mwendawazimu muacheni tu aende mahakamani ile ajianike vzr na tumjue.. ngoja nimkumbushe jambo.... majambazi walijilipua kesi ya zombe kwa kutoa ushahidi kuwa wao ndo wezi, sasa huyu mtu anaenuka nyie muacheni kama hajaonja joto watu watakapo jilipua... p.mbafu...... hii nchi sio yake watanzania ndio wenyenchi lowassa mwakahuu utashangaa na roho yako nyama we.....
 
Hawezi kwenda mahakamani alikuwa anatingisha kiberiti kama yale ya mafisadi na Dr. Slaa.
 
Wanabodi,

Kwanza kabisa nitasema hakuna sheria yoyote inayozuia vyombo vya habari kutoa Account za watu iwe amount ama namba zake dunia nzima ikiwa kuna ukweli wa kuwepo hizo account.

Kama kuna uvujaji wa habari hizi toka Benki inayohusika basi ndiko kunakotakiwa kuelekezwa mashtaka ama upelelezi..

Hadi sasa hivi nachoona ni Ubabe wa viongozi wetu lakini kisheria sioni kabisa sababu ya kulishtaki gazeti ati kwa kutoa account za watu as if hayo magazeti ndio wanaomiliki hizo account..

Mkataba wa siri za account upo kati ya mwenye account na benki, Mwanahalisi anaweza kuwa shahidi kuonyesha kwamba siri hiyo imevunjwa..

MASWALI MAGUMU"
Hakika, kesi hii itamdhalilisha sana Lowassa tena kwa muda mrefu usiotabirika kuanzia sasa. Ningekuwa mshauri wake ningemwambia "mzee mezea tu!" Kama ilivyokuwa kwa Richmond, katumia jazba, anakwenda mahakamani! Sasa itabidi ajibu mahakamani maswali magumu yafuatayo kwa ukamilifu:
(a) Je, kwa nini utekelezaji wa mradi wa jengo la vijana umeanza bila mkataba mahsusi kusainiwa kwanza?
(b) Je, alitumia vigezo vipi kumwingiza Bosi wa Tan Roads, Mrema, kwenye kampuni ya Vijana Development Corporation?
(c) Je, kwa nini alimtoa Mhe. Wilson Masilingi kwenye Baraza la Wadhamini la UVCCM bila sababu wala taarifa yoyote?
(d) Je, alitumia msingi upi kumteua fisadi Nazir Karamagi kuziba nafasi ya Masilingi?
(e) Je, kwa msingi upi mwekezaji amepewa asilimia 75 ya ya umiliki wa kiwanja (ardhi) bila kibali cha Kabidhi Wasii wa Serikali?
(f) Je, uhalali wa utekelezaji wa mradi huu unatoka wapi wakati wenye mali, Baraza Kuu la UVCCM, hawakuridhia?
(g) Je, kulikuwa na Mkataba wa Utekelezaji au MOU tu? Kama ni MOU tu, basi jibu katika (a) hapo juu linatosha. Ikiwa kuna Mkataba wa Utekelezaji, kama MwanaHalisi na wanasheria wake wanavyodai, kwa nini Lowasa na wenzake wasishitakiwe kwa udanganyifu?

Yapo maswali mengine mengi ambayo Lowassa atalazimika kuyajibu atakapotinga mahakamani. Nachelea kusema, Lowassa atashindwa kuyajibu kwa kinaganaga maswali yote! Lazaros
 
Umepotoka sana rafiki yangu.wewe ni kati ya wanaofata mkumbo bila kuujua ukweli.nenda kasome mwenyewe kwanza ripoti ya mwakyembe na uonyeshe ni wapi ambapo lowasa ametajwa kuwa amuhusika na ufisadi zaidi ya preamle ambayo haikiuwa na ukweli wowote kwani watu wameongea nje ya viapo...siku moja wanahistoria watasema ukweli na sie sisi ambao tayaritumehalibiwa akili na magazeti na tuna uoande ambao kamwe hatutaki ata kisikia upende wa pili wa shilingi
sasa kama hakutajwa alilalama nini kua ameonewa sana, amedhalilishwa sana.................mwenyewe anatuhakikishia kua kila kitu kilimuhusu.....huyu Lowasa ni chanzo cha Ufisadi wa kila namna.
 
Kabla ya kusema sana kama kweli umeuona huo mkataba kwanza niambie toauti kati ya Contract na MoU.then niambie ni feature gani ulioiona kwenye what you so called mkataba ambayo inaonyesha kuwa ni mkataba na siyo MoU.baada ya hapo tunaweza kuendelea kuurgue

Sasa wewe na Lowassa wako sijui haya mambo mnayapelekeje?

Kwani Memorandum of understanding sio mkataba?unataka kuniambia MoU haina force of law? Mbona basi kiswahili chake ni mkataba wa maelewano?sasa kubenea in a layman language akisema Lowassa amesaini mkataba yupo sahihi kwani yeye hawezi kujua fine distinction kati ya hiyo unayosema MoU na Contract.Kikubwa hapa whatever name you call is whether the same has a force of law.

Yapo mambo mengi sana hapa nchini yanayoendeshwa kwa MoU,tofauti ya MoU na ordinary contract ni kwenye damages tu.Sasa Lowasa awe kasaini,Makubaliano,MoU au ordinary contract kwa kiswahili yote ni mikataba tu hakuna distinction.

Cha kufahamu hapa mikataba kwa kiingereza ina majina mengi sana kutokana na nature yake words like pact, agreement, covenant, Mou,Treaty, convention, contract, nk yote haya kwa kiswahili hayana majina mengine zaidi ya kuita mkataba.Hapa naona Lowasa na Kubenea wametofautiana lugha tu."no consensus ad idem"
 
Lowassa ameahirisha kwenda mahakamani kutoka na ushauri wa wanasheria wake. At least that is the grapevine in Dodoma.
 
Lowassa ameahirisha kwenda mahakamani kutoka na ushauri wa wanasheria wake. At least that is the grapevine in Dodoma.

Alipaswa kuwataka ushauri wanasheria wake kabla ya kutoa kitisho. Mkuu hivi bado kunazabibu Dodoma! kwi kwi kwi nilidhani fox wamezimaliza zote.
 
Jamani mbona tunasahau hata uumbaji kwa wale wanao-amini "creation" Baada ya shetani kumwasi Muumbaji alipewa adhabu kali na baada ya kutambua miongoni mwa "privileji" alizopoteza ni kuishi IKULU YA MBINGUNI aliomba walau apewe nafasi ya kumsumbua mwanadamu --- kama Kubenea vile.

Akisema nipatie walau dakika chache nimjaribu Kubenea. Muumbaji kwa kuwa humpa mtu kitu aombacho kwa dhati ali-m-grant. Lakini pia Muumbaji aliwaletea baunsa wanadamu ambaye ni Yesu. Hivyo shetani hatashinda vita hivi.

Tumpe nafasi "white hairs" lakini, labda atarudisha sifa na thamani yake kwa taifa lake lililompatia fedha nyingi na madaraka makubwa siku za nyuma. Shuleni pia itashangaza ikiwa mwanafunzi ameshindwa kujibu maswali aliyoulizwa kisha akatunga maswali yake mwenyewe na kuyajibu vyema atakuwa amepasi? Hap jamaa anajitungia maswali.

Seniors and wenye nywele watakuwa wameelewa na michango yao ni muhimu kama Slaa, Kabwe, n.k.
 
Hili linathibitisha kwamba mafisadi ndiyo wameshika 'utamu' katika chama cha mafisadi. Hakuna hata mwenye busara huko.

Nape aigawa CCM

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


MGOMBEA wa nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Nape Nnauye, ameigawa CCM kutokana na mkakati uliopo wa kutaka kuliengua jina lake.

Chini ya mkakati huo, kigezo cha umri ndicho kitakachotumika na wabaya wake, na kukipenyeza katika vikao vya juu vya chama katika kuamua hatma yake, kuwania nafasi hiyo nyeti ndani ya umoja huo ambayo pia itamwezesha kuingia katika vikao vya Kamati Kuu ya CCM (CC).

Habari kutoka ndani ya UVCCM zinasema kuwa, mkakati wa kumuengua Nape katika kinyang'anyiro hicho ni wa muda mrefu, lakini umekuja kukolezwa zaidi na hatua yake ya kufichua ufisadi mzito, unaodaiwa kufanywa kupitia mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu la umoja huo, huku akiwataka baadhi ya watendaji wawajibike kwa madai kuwa mkataba huo hauna maslahi kwa umoja wa vijana nchini.

Hivi karibuni, wakati akichukua fomu, Nape alidai kuwapo kwa ufisadi katika mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM, na kumtaka Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Edward Lowassa, Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Dk. Emmanuel Nchimbi pamoja na Katibu wake, kuwajibika.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari kutoka ndani ya UVCCM, baadhi ya viongozi wa juu ndani ya umoja huo, hawataki kuona Nape anachukua nafasi hiyo inayoshikiliwa kwa sasa na Dk. Nchimbi, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Nape ambaye hadi siku alipojaza fomu, alikuwa na umri wa miaka 30, lakini itakapofika Novemba mwaka huu, siku chache kabla ya uchaguzi, unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, atakuwa ametimiza miaka 31, hivyo kukosa sifa ya kuwa mwenyekiti wa umoja huo. Umri wa mwisho kwa mgombea wa jumuiya hiyo, unapaswa kuwa miaka 30.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, uchaguzi huo awali ulipangwa kufanyika Septemba mwaka huu, lakini ulisogezwa mbele hadi Desemba kwa madai ya kutokuwapo kwa fedha za kutosha kuuendesha.

Hatua ya kuusogeza uchaguzi huo hadi Desemba, imetafsiriwa pia kuwa ni sehemu ya kumwondoa Nape kwenye kinyang'anyiro, kwani msimamo wake wa kuwania tena nafasi hiyo baada ya mara ya mwisho kubwagwa na Dk. Nchimbi, ulishakuwa wazi.

"Wapo viongozi walioapa kuwa Nape hawezi kuchukua nafasi hii, hao wako tayari kufa kuliko kumwona Nape akishika nafasi hiyo, na hawana sababu ya msingi. Kwa hiyo wanataka kumbana kwenye kigezo cha umri na itakapofika Desemba mwaka huu, atakuwa tayari amefikisha umri wa miaka 31, hivyo hatakuwa na sifa," kilisema chanzo chetu cha habari.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kuchukua fomu, Nape alisema watakaotumia kigezo cha umri kumuengua, watashindwa kwani wakati anajaza fomu, alikuwa na miaka 30 na hadi sasa ana umri huo.

"Hoja hiyo sawa na kuua tembo kwa ubua. Mimi sasa hivi nina miaka 30, niko ndani ya sifa, sasa kama uchaguzi unafanyika Desemba, halafu tayari nina umri wa miaka 31, tena kwa kupitisha mwezi mmoja tu, sijui kama itawezekana kuniengua kwa sababu hiyo, lakini vikao ndivyo vitakavyoamua," alisema Nape.

Baadhi wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM, waliozungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao kwa nyakati tofauti, walisema suala la Nape huenda likaibua mabadiliko ya sheria katika kuwania nafasi hiyo.

"Nafikiri kuna sababu ya kubadilisha kanuni na sheria zetu za uchaguzi. Ni makosa kusema kijana wa miaka 31 asigombee kwa kigezo cha umri. Yaani taasisi kubwa kama hii, tunataka iongozwe na kijana wa kuanzia miaka 25 hadi 30. Huyo hajakomaa bado," alisema mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.

Hata hivyo, kigezo cha umri na hoja ya ufisadi, huenda vikawagawa wajumbe wa vikao vya maamuzi, kwani wapo wanaomuunga mkono kwa hatua yake ya kupasua jipu la ufisadi katika mradi huo.

Vyanzo vyetu vya habari vilisema, wapo wazee muhimu ndani ya chama wanaomuunga mkono kijana huyo kwa ujasiri wa kusema ukweli, na kuahidi kumuunga mkono kwenye vikao vya maamuzi.

Hata hivyo, wapo baadhi ya wazee walioeleza waziwazi kukerwa na hatua ya kijana huyo kuwashambulia baadhi ya viongozi na kuwatuhumu kwa ufisadi katika mradi huo.

Nape ambaye ni mtoto wa marehemu Moses Nnauye, ni mgombea pekee aliyopo ndani ya Baraza Kuu na pia ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM na amekaa katika nafasi hizo kwa muda mrefu.

Wengine wanaowania nafasi hiyo pamoja na Nape ni Jerry William, Zainabu Kawawa, Hussein Bashe, Beno Malisa, Antony Mtaka, Said Mtanda, Hule Pangisa, Samwel Malelo, Stephen Deya na Gregory Mwankenja.

Wengine ni David Manoti, Mussa Mnyeti, Edson Lubuwa, Mwamini Lusingu, Asma Kalokola, Marco Zablon Alute, Harrod Adamson, Hamad Masauni, Suleiman Muhsin, Issa Haji Ussi, Idila Hillary Vuai, Ashura Ismail, Rashid Msalaka na Raha Ahamada Ali.

Wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Happy Mahava, Raha Ahamada, Ali Riziki, Pembe Juma, Michael Bundara, Rabia Hamid, Sadifa Khamis, Shaka Hamedu Shaka, Nuru Muhamed Ahmed na Twaha Ali.
 
Nilisema kuwa Lowassa alizungumza kabla hajashauriana na wanasheria wake kwani kama angeshauriana nao kabla wangemwambia kuwa asithubutu kwani hiyo ingekuwa ni disaster kwake.

Nitaomba kumfanyia cross examination mahakamani na swali langu la kwanza litakuwa ziko wai zile Ng'ombe ambazo zilikuwa kule kwenye Ranchi ya Taifa Lulindi? Najua hili ni jipya na angepanic sana.
 
Nilisema kuwa Lowassa alizungumza kabla hajashauriana na wanasheria wake kwani kama angeshauriana nao kabla wangemwambia kuwa asithubutu kwani hiyo ingekuwa ni disaster kwake.

Nitaomba kumfanyia cross examination mahakamani na swali langu la kwanza litakuwa ziko wai zile Ng'ombe ambazo zilikuwa kule kwenye Ranchi ya Taifa Lulindi? Najua hili ni jipya na angepanic sana.
Mpaka kieleweke,

Naomba uitunze hii,nilishawahi kuisema huko nyuma ..tuitunze mpaka 2014...mie ninayo hadi Document ya madudu aliyoyafanya
 
Gembe mimi si mwana CCM wana mfuasi wa Chama chochote hili la CCM kulijadili litanisaidiaje ?

Hakuna sababu kubwa ya kuwajadili hawa maana wote ni ufisadi tu. Hakuna mtu safi ndani ya ccm anayetaka uongozi kama huo. Hivi mnatarajia mwenyekiti wa UVCCM awakemee mafisadi?
Tusiwajadili, bali tutafute namna ya kuishinda na hatimaye kuifutilia mbali CCM
 
"Nafikiri kuna sababu ya kubadilisha kanuni na sheria zetu za uchaguzi. Ni makosa kusema kijana wa miaka 31 asigombee kwa kigezo cha umri. Yaani taasisi kubwa kama hii, tunataka iongozwe na kijana wa kuanzia miaka 25 hadi 30. Huyo hajakomaa bado," alisema mmoja wa wajumbe wa Baraza Kuu la UVCCM.


Ina maana E. Nchimbi mwaka 2003 alikuwa hajafikisha miaka 30?
 
Heshima Mbele wana Bodi,


Pia naomba tuwajadili kwa kina wale wote ambao wameonesha nia ya kugombea uongozi wa Uenyekiti UVCCM,nimeanisha majina hapa sabbu nimepewa majina hayo ndio wanaojipanga kwuania uongozi huo

1.Benno Malisa
2.Jerry Slaa
3.Nape Mnauye
4.Zamaradi kawawa
5.Mussa Mnyeti

Sioni sababu ya kuwajadili hawa kwani CCM ni ufisadi tu. Ni vyema tusipoteze muda, tujadili namna ya kuishinda CCM na hatimaye kuifutilia mbali.
 
YUSUPH Makamba, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni mwongo, MwanaHALISI limegundua

Na Saed Kubenea

Wiki iliyopita Makamba aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkataba kati ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na mwekezaji ulikuwa haujatiwa saini. Lakini gazeti hili lina taarifa madhubuti kuwa tayari mkataba uliishatiwa saini zamani na kinyemera.

Huo ni mradi unaohusisha jengo la UVCCM lililopo barabara ya Morogoro, Dar es Salaam katika kitalu Na. 108/2. Taarifa za awali zilisema wakati Baraza Kuu la UVCCM lilikataa mradi huo, unaokadiriwa kugharimu zaidi ya Sh. 30 bilioni, Baraza la Wadhamini, chini ya mwenyekiti wake Edward Lowassa, liliruhusu mradi kinyume na utaratibu.

Kwa hali hii ya "mtu mzima kusema uwongo, Makamba amejichimbia kaburi la kisiasa," ameeleza kiongozi mmoja wa ngazi ya juu katika CCM.

"Mwenyekiti Jakaya Kikwete, ambaye pia alikiukwa, hawezi kuendelea kuvumilia mtu mwenye tabia hii, amesema kiongozi huyo.

Katika barua yake ya Julai mwaka huu kwa Makamba, Lowassa alisema Baraza la Wadhamini limekubali mradi lakini "usisainiwe mpaka kupatikana kwa kibali cha Kamati Kuu (CC)."

Taarifa za uhakika zimesema kuwa mkataba wa ujenzi wa mradi huo uliopewa jina la "Development Agreement), ulisainiwa tarehe 2 Januari 2007 kati ya UVCCM na makampuni mawili ya M.M. Integrated Steel Mills Limited (MMISML) na Estim Construction Company Limited (ECCL).

Watiaji saini kwa upande wa UVCCM ni Edward Lowassa katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini na Amos Makalla (Katibu wa Baraza). Wakati wa kusainiwa mkataba, Makalla alikuwa Kaimu Katibu Mkuu wa UV-CCM.

Kwa upande wa mwekezaji, waliosaini mkataba ni Subhashbai M. Patel anayejitambulisha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya M.M.ISML ya Dar es Salaam na Jamila Adam ambaye ni shahidi. Nafasi ya Jamila katika kampuni ya M.M. Integrated Steel Mills Limited haikuweza kufahamika mara moja.

Kampuni nyingine ni Estim Construction Company Limited (ECCL), ambayo iliwakilishwa na mkurugenzi wake mkuu, Gilabhadi Pindolia na Jianesh Mandwama.

Imefahamika kuwa mkataba huo umeingia katika utata mwingine wa kisheria kutokana na hatua ya Lowassa na wenzake kuruhusu makampuni mawili kumiliki mradi mmoja kwa pamoja.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa makampuni hayo yatamiliki kwa pamoja hisa 75 wakati UVCCM itamiliki hisa 25 kwenye kitega uchumi hicho.

Mkataba unasema UVCCM pia imeridhia kugawanya mapato yote kutokana na mradi huo kwa kuzingatia mfumo huo.

Baada ya mradi kukamilika, mkataba unaelekeza kuwa UVCCM itakuwa na haki ya kutwaa hisa 10 za ziada kwa kuzinunua kwa bei ya hali ya soko katika kipindi cha miaka mitatu baada ya ujenzi kukamilika au katika kipindi chochote kitakachoridhiwa na pande zote.


Hata hivyo, MwanaHALISI imebaini, iwapo itatokea UVCCM imeshindwa kununua hisa hizo za ziada kwa kipindi kilichobainishwa, basi itakuwa imepoteza haki hiyo ya kupata hisa za ziada katika umilikaji kitega uchumi hicho.

Imeelezwakuwa miongoni mwa wajibu wa UVCCM katika mkataba huo ni kuhakikisha kuwa kabla ya shughuli za ujenzi wa mradi kuanza, italazimika kubadilisha hatimiliki ya eneo ili kuonyesha katika hati hiyo kuwa imekubaliana na washirika hao kuendeleza eneo hilo husika.

Kadhalika, ina wajibu wa kimkataba kuhakikisha kuwa kabla ya hatimiliki hiyo kukabidhiwa kwa washirika wake hao wawili, jengo hilo halitaguswa kwa mabadiliko yoyote.

UVCCM pia itawajibika kulipa kodi zote, ikiwemo ya majengo, kabla na hata kwa siku ile ambayo makabidhiano rasmi ya sehemu ya umiliki kwa washirika wake hao yamefanyika.

Wajibu mwingine kwa UVCCM ni kuhakikisha kuwa itachangia malipo ya kodi, ikiwemo ya majengo, kulingana na mpangilio wa mgawanyo wa hisa na washirika wake hao na itawajibika kuhakikisha washirika hao wanalikuta jengo bila wapangaji.

Imeelezwa pia UVCCM italazimika kuridhia uteuzi wa kampuni ya ECCL kama msanifu na mkandarasi wa ujenzi wa mradi; itatoa kila msaada kwa washirika utakaorahisisha kupatikana kwa vibali vyote vya kutekeleza mradi katika muda wa makubaliano.

Miongoni mwa wajibu wa washirika wa UVCCM ni kukidhi gharama zote za mradi; kuteua kikosi cha wataalam, wakiwemo wasanifu, wahandisi na wachoraji ramani kwa ajili ya masuala ya kiufundi, pamoja na taratibu za kupata fedha za ujenzi wa mradi.

Wajibu mwingine kwa "wawekezaji" ni kutumia muda wa miezi sita, kuanzia siku ya kusainiwa mkataba, ili kupata taarifa zote muhimu zinazohitajika kwa ajili ya kuanza shughuli za kutekeleza mradi.

Wajibu wa pamoja kwa washirika hao, imeelezwa kuwa likitokea tatizo lolote la kibiashara au sharti lolote la kimkataba, linalozuia kuendelea kwa mradi, watarudi walikotoka.

Pia wajibu mwingine ni pale inapotokea washirika wa UVCCM wameshindwa kukamilisha mradi kama ilivyokubaliwa, kwa sababu zilizo nje ya uwezo wao na hivyo kuchelewesha mradi, UVCCM itakuwa na haki ya kutwaa mradi na kuumalizia huku washirika wake wakiwa na haki ya kumiliki hisa kulingana na kazi waliyokwishafanya.

Wajibu wa jumla kwa wote ni kwamba ikitokea, kwa sababu yoyote ile, shughuli za mradi hazikuanza miezi 12 baada ya mkataba kusainiwa, mkataba huo utakuwa batili; na kwamba iwapo hilo likitokea, MMISML na ECCL watalazimika kukabidhi hatimiliki ya jengo kwa UVCCM.

MwanaHALISI halikuweza kufahamu mara moja mmiliki wa kampuni ya pili (ECCL) ni nani, lakini baadhi ya wanasheria wanasema sheria za Tanzania zinakataza makampuni mawili kuingia ubia kwa majina mawili tofauti katika mkataba mmoja.

"Haya makampuni yalitakiwa kuungana na kuunda kampuni moja kabla ya kusainiwa kwa mkataba. Lakini kwa hatua hii, ni wazi sheria na taratibu zimekiukwa," amesema mwanasheria huyo.

Taarifa nyingine kutoka ndani ya UVCCM zinasema mbali na jumuiya hiyo kuingia mkataba na akina Patel, viongozi wa jumuiya hiyo wamefunga mkataba na mmoja wa wafanyabiashara wakubwa mkoani Mwanza kwa lengo la kuwekeza.

Imeelezwa kuwa mkataba huo unahusu jengo na kiwanja hichohicho ambako ujenzi umeanza lakini baadhi ya viongozi wa UVCCM wanaendelea kupinga mkataba ambao wanaita wa "kinyonyaji."

Kwa nyakati tofauti, viongozi wa CCM, Makamba, Emmanuel Nchimbi na Katibu Mkuu wa UVCCM Francis Issack, wamenukuliwa wakitetea mkataba.

Nchimbi na Issack walisema Baraza la Wadhamini limeridhia kuanza kwa ujenzi, kauli iliyopingwa na wajumbe kadhaa wa Baraza Kuu la UVCCM.

Hata hivyo, shughuli za ujenzi wa mradi huo tayari zimeanza nyuma ya jengo la makao makuu.

Baada ya kuwepo utata wa mradi huo, MwanaHALISI limeelezwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye alipata taarifa kwa njia ya siri, alimwagiza Makamba kufanya uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo na kuhakikisha anawasilisha taarifa kwa Kamati Kuu ya CCM.

Makamba alimwandikia Lowassa tarehe 5 Julai 2008 akitaka Baraza la Wadhamini kusimamia kwa dhati mradi huo akisema, "Kwa kuwa mradi haujasainiwa, nimeona ni vema wewe, ukiwa Mwenyekiti wa Baraza, ufuatilie na usimamie." Makamba alinakili barua hiyo kwa Rais Kikwete na Katibu Mkuu wa UVCCM.

Makamba alifanya hivyo huku akijua kuwa tayari mkataba umesainiwa na taarifa zinasema hata Kikwete alikuwa tayari amefahamishwa taarifa hizo lakini "Mzee alitaka kuwatega. Sasa imebainika Makamba ni mwongo," ameeleza kiongozi wa CCM.

Tangu wiki iliyopita, kumekuwa na kauli tofauti kuhusiana na mradi huo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) na Baraza Kuu la UVCCM, Nape Nnauye, aliamua kupasua jipu alipolieleza suala hilo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu ya kuomba uteuzi wa kugombea uenyekiti wa jumuiya hiyo.

Nape, mwana wa mwanasiasa maarufu Moses Nnauye (marehemu), aliyetumia sehemu kubwa ya uhai wake kujenga chama tangu nyakati za TANU, alisema mradi huo ni wa kifisadi kwa kuwa umeidhinishwa kwa nguvu wakati Baraza Kuu liliukataa.

Kauli yake ilipokelewa kwa hisia tofauti huku wajumbe wenzake kadhaa hasa wenyeviti wa UVCCM wa mikoa wakimuunga mkono lakini alikaripiwa na Makamba na kutakiwa kulalamika kwenye vikao.

Makamba alimuita Nape ofisini kwake Jumatano iliyopita na Nape alipofika alishtukia akikaripiwa mbele ya kundi la waandishi wa habari waliokuwa wameandaliwa kumwandama na maswali.

Sakata la mradi wa UVCCM linaonekana kugawa viongozi wa jumuiya hiyo na chama, na litakuwa ajenda muhimu kwa uchaguzi mkuu wa jumuiya hiyo ambao mchakato wake umeanza. Uchaguzi utafanyika Desemba.
 
Jengo la Umpoja wa Vijana limechoka na liko ndembe ndembe kama Vijana wenyewe wa CCM.
 

Attachments

  • 6-23-2008 12-18-16 AM_0762.JPG
    6-23-2008 12-18-16 AM_0762.JPG
    190.9 KB · Views: 51
Wakuu,
Hakika njia ya mwongo fupi.........sasa MwanaHalisi.(kubenea) ameuanika mkataba nje nani mwongo kati ya hawa?Makamba,Lowassa,Kubenea na Nape? Nini hatma ya Nape CCM?Nini hatma ya kina Lowassa na mafisadi wenzake??????
 
Tatizo lipo hapo ,naamini kwenye ujengaji mkubwa na unaohusisha ushirika au Chama ,pengine na serikali kunakuwepo na zabuni sasa hapo sijui ,walikutana vipi na mwamuzi ambae inaonyesha alimegewa donge nono,usikute feza wameshaitafuna na kugawana ,si ajabu ukasikia wameanza kuzirudisha.
 
KWELI walichemsha,Sijui sisiem walitumia vigezo gani kumpitisha MGOSI kuwa katibu Mkuu, Lo!

Huyu utamlinganisha kweli na makatibu waliopita? Vijana wa CUF walisema ni darasa la 4 wakijibu mapigo ya Francis Isack kuwa Lipumba ni PROF wa mitishamba.

Utendaji wake umekuwa vituko wala huwezi kuulinganisha na akina Pius Msekwa, Horace Kolimba, Lawrence Gama, Phillip Mangula n.k.

Huyu atadanganywa mengi sana na yeye atabakia na mdomo tu wa kukariri vifungu vya misaafu ya bibilia na quran tukufu
 
Back
Top Bottom