Bwn Tom,
..........sitaki kuamini kuwa ndio wewe mbunge wa kuteuliwa, kwani maneno yako hapo juu yametulia na yako deep....anyway..........well said Tom.......kijana Nape anahitaji ushauri.
.....sasa mkuu Tom hebu tueleze....inakuwaje mradi umeanza kabla ya kupata baraka za CC?........kwanini mradi uanze wakati vijana wanaupinga??...........na pengine hapo ndipo kijana Nape anazo inside information zote.........
.
Mkuu kwanza kabisa ni kweli mimi siyo yule Mh.Thomas Mwang'onda, mbunge wa kuteuliwa.Hata hivyo, niko njiani kuwa na hadhi kama yake kwani natarajia kuingia kwenye kinyang'anyiro kwa uchaguzi ujao wa 2010 na kunyakua moja ya majimbo muhimu.Bora uzima!
Mkuu kwa kujibu hoja zako ni kwamba,hili sakata la mradi wa jengo la UVCCM lina utata kidogo kutokana na ukweli kwamba taarifa za pande zote mbili yaani kutoka kwa bwana Nape na kutoka kwa uongozi wa UVCCM haziko wazi sana.
Bwana Nape alitoa shutuma tu,lakini hakuwa na ushahidi wowote ule wa kuuwasilisha mbele ya waandishi wa habari kama hatua muhimu ya kuipa nguvu hoja yake.Ningemuelewa Nape kama angetuletea hata nakala ya mkataba wenyewe, muhtsari wa kikao cha baraza kuu lililokaa kujadili mradi ili tuone kama ni kweli baraza liliupinga mkataba ama lah.
Unajua kama nilivyosema awali kwamba, kutokana na taratibu za vikao, inawezekana kabisa kuna baadhi ya wajumbe hawakuunga mkono. Hilo ni sawa kabisa kwa demokrasia ya vikao. Lakini linapokuja suala la kufikia maamuzi,kinachoangaliwa ni idadi ya wingi wa wajumbe waliounga au kutounga mkono hoja.
Huo ndio utaratibu wa vikao.Sasa hatuwezi kuhitimisha kwa kusema vijana waliupinga mkataba,kumbe walioupinga ni 10, 20 au 50, ambao kwa mujibu wa ikama ya wajumbe wa kikao, hoja zao zilimezwa na idadi kubwa ya wajumbe waliounga mkono.
Sasa ili kuondoa utata katika hili ilipaswa Nape, kwakuwa alishaamua kulipua bomu, basi angekuja kamili kamili. Angepaswa kubeba sehemu ya mkataba anayoipinga pamoja na muhstari wa kikao husika mbele ya mkutano wake na waandishi wa habari. Haya yote Nape hakuyafanya. Ndio maana binafsi inanipa tabu kuamini kama Nape anaelewa kwa undani mchakato mzima wa mkataba kwa ushahidi mahususi,ukiachilia mbali kuujua mchanganuo wa mradi pekee.
Mimi ninashawishika kuamini kwamba, kwa kujua kuwa vikao halali vya awali kama, baraza kuu na baraza la wadhamini la UVCCM vimeubariki mkataba wa mradi,uongozi wa UVCCM ukaona kuwa wanaweza kuanza shughuli za ujenzi wakati wanasubiri baraka za Kamati Kuu.Sasa hili kibiashara sioni kama ni tatizo.Kwa sababu,ukimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Mzee Makamba,anadai kuwa hata sekretarieti ya NEC iliuunga mkono mradi na hivyo kilichokuwa kinasubiriwa ni kufikisha agenda ya mradi huo mbele ya CC.
Sasa, kwa uozefu wangu ndani ya CCM,ni nadra sana sana, CC kupinga maamuzi ya sekretarieti.Na hii ni kwasababu sekretarieti inaundwa na wajumbe takribani saba wa CC pamoja na makatibu wakuu wa jumuiya za chama. Sasa hawa wajumbe walioko kwenye sekretarieti ndio watapaswa kutetea hoja walizozipitisha kwenye sekretareiti mbele ya CC.
Kinachoweza kufanyika ni kuagiza yafanyike baadhi ya marekebisho kwenye vifungu fulani fulani kama ikibidi. Na daima marekebisho hayo mara nyingi huwa yanalenga kuboresha tu.
Kwa hiyo, kimsingi mimi kwangu suala la mradi kuanza kabla ya baraka za CC sio hoja sana kwa kuzingatia ufafanuzi wa itafaki za vikao vya CCM kama nlivyojaribu kuuelezea hapo juu. Maana kuna suala la muda wa kuanza ujenzi kama ulivyokubalika katika mkataba pia lazima lizingatiwe. Mwekezaji yeye hatambui ratiba za vikao vya chama, yeye haingii mkataba wa kupiga propaganda, yeye anaingia mkataba wa kibiashara.Na katika biashara, kujali muda ni moja ya mambo ya msingi ili faida iliyokusudiwa iweze patikana kwa muda muafaka.
Tatizo kwangu lingekuwa kama kweli baraza kuu na baraza la wadhamini halikuidhinisha mradi husika,halafu itokee ghafla uongozi wa UVCCM makao makuu wanaanza ujenzi.Hapa kungekuwa na tatizo la kimaadili na ingepaswa uchunguzi wa kina ufanyike katika kubaini nani amehusika na maamuzi hayo kinyume cha kanuni na taratibu za UVCCM.
Nimewasikia wajumbe kadhaa wa baraza kuu wakiunga mkono hoja ya bwana Nape. Ni sawa. Lakini nasema hiyo haitoshi kama hawakuweza kuwashawishi wajumbe wengi wa baraza kupinga mradi kwa taratibu za vikao, kwa mujibu wa kanuni.
Kimsingi mimi sipo hapa kujadili kama mradi una manufaa kwa UVCCM ama la.Maana sijausoma mradi husika.Nimesikia kutoka upande mmoja tu, wa Nape. Sasa kwa misingi yangu, ni lazima nipate maelezo ya pande zote husika ndipo nifike mahali nitoe maoni ni nani yuko sahihi juu ya umuhimu na manufaa ya mradi.Ninachojadili ni kama tararibu za kufikia maamuzi ya kuwepo kwa mradi zilifuatwa.
Nadhani nimejibu hoja mkuu. Hatahivyo, nakaribisha maswali zaidi kama yapo.