Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

kubenea kazidi jamani akka......andika habari lakini kuita in point black fulani muongo naona kidogo tunakwenda kinyume cha maadili.
 
kubenea kazidi jamani akka......andika habari lakini kuita in point black fulani muongo naona kidogo tunakwenda kinyume cha maadili.

Sasa aandike vipi wakati ushidi unaonyesha kama alipokuwa akipeleka habari kwa Kikwete alikuwa akijua kwamba tayari watu wameshamwaga wino.
Watu wamekwimba tusimwonee haya mvivu na mzururaji Makamba ni mzururaji tu hana dhamna kwenye chama chake wengine wanasema ni mchekeshaji.
 
Nafikiri kama EL ana akiri timamu hata ile kesi yake ya kumshtaki Kubenea anaweza akafuta na kuingi mitini kwani ataumbuka sana.Angalia sasa jamaa kamwaga kila kitu,tatizo la Makamba polojo nyingi sana anasahau kuwa siku hizi watu wamefunguka macho hawaambiwi tena inabidi kuelimishwa watu wamesha elimika wanajua mchele ni upi na pumba ni zipi.Kazi kwako Makamba kijana huyo atakuumbua mtu mzima shauri yako.
 
CCM yajimaliza kukumbatia ulaji

Mwandishi Wetu Julai 30, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo


Imejiweka pabaya 2010
Nape ni ‘moshi' wa moto wa ndani

MGONGANO wa kauli na misimamo ndani ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UV CCM) kuhusiana na uwekezaji katika kiwanja cha makao makuu ya umoja huo Dar es Salaam ni matokeo ya chama tawala kuyumbishwa na kujiruhusu kwake kukumbatia fedha katika shughuli zake nyingi, Raia Mwema imeambiwa.

Baadhi ya wanasiasa waliozungumza na Raia Mwema wiki hii, wanasema hulka iliyokithiri ya kupenda fedha kwa njia yoyote ndiyo ambayo sasa inatafuna mzizi mkuu wa UVCCM na jumuiya nyingine za CCM, Umoja wa Wanawake (UWT) na Jumuiya ya Wazazi.

Tokea kuasisiwa kwake, jumuiya zote za CCM zilikuwa ndio nguzo kuu za kisiasa na kiuchumi za chama hicho tawala tokea enzi za TANU na ASP, lakini katika miaka ya karibuni hali imekua kinyume chake na sasa muanguko wa chama hicho unaweza kuchangiwa na jumuiya zake.

Kwa karibu mwezi sasa UVCCM imekuwa katika malumbano yaliyoibuliwa na mmoja wa vijana ambao wamejitokeza kuwania uongozi wa juu wa umoja huo, Nape Nnauye.

Nnauye ambaye anataka kugombea uenyekiti wa umoja huo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu, amekuwa akisema katika matukio mbalimbali kwamba kuna dalili za ufisadi katika mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM unaofanywa na kampuni moja ya binafsi.

Kwa mujibu wa Nnauye, mradi huo mkubwa haukupata kuridhiwa na vyombo husika ndani ya UVCCM na hata Kamati Kuu ya CCM na kwamba hata wakati mkataba wenyewe wa ujenzi una utata tayari mjenzi amekwisha kuanza kazi.

Kauli hiyo ya Nnauye imevuta majibu kadhaa kutoka ndani ya CCM yakiwamo ya Katibu Mkuu, Yusuf Makamba, Mwenyekiri wa UVCCM anayemaliza muda wake Emmanuel Nchimbi na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa UVCCM Edward Lowassa, lakini ambayo yamekuwa hayasaidii kueleza ni nini hasa kinachoendelea kuhusiana na mradi huo mkubwa.

Kati ya mambo aliyotaja Nnauye yanayozua utata ni kwamba mwekezaji, kwa mujibu wa hati ya makubaliano ya awali, atamiliki jengo jipya litakalojengwa katika kiwanja hicho kwa asilimia 75 huku UVCCM ikibakiza asilimia 25 milele.

Aidha, Nnauye amesema kwamba mwekezaji huyo ametumia hati ya kiwanja hicho kuombea mkopo benki, jambo ambalo hata UVCCM wangeweza kulifanya na hivyo wao wenyewe kuweza kusimamia ujenzi bila kuhitaji msaada wa mwekezaji.

Lakini wafuatialiaji wa mambo ndani ya CCM wanasema kwamba kuibuka kwa habari hizo kuhusiana na UVCCM kunaeleza tu mambo ambayo yamekuwa yakitokota ndani ya CCM na kwenye jumuiya zake.

Mwaka jana, wanasema kwa mfano, kwamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa UWT, Halima Mamuya, aliondoshwa katika wadhifa huo kwa sababu zinazohusiana na mgogoro mwingine wa kiwanja cha UWT, kilichoko Kinondoni, Dar es Salaam, na kilichokuwa na jengo kubwa la umoja huo, ambalo katika miaka ya mwanzo lilitumika kama hosteli ya wasichana.

Kama kilivyo kiwanja cha UVCCM, baadhi ya vigogo ndani ya CCM hawakufurahishwa na hatua ya UWT ya kuingia mkataba wa uwekezaji mkubwa katika kiwanja hicho na wakafanya jitihada za kutaka kina Mamuya wabadili msimamo na ikiwezekana hata kupata mwekezaji ambaye angekuwa ametafutwa na vigogo hao.

Habari zinasema ni mvutano huo ambao hatimaye ulimfanya Mamuya si tu kutupwa nje katika UWT bali pia kumkosesha nafasi ya ukuu wa wilaya aliyokuwa nayo, na habari za yeye na baadhi ya watendaji wengine zikaandikwa sana magazetini zikionyesha kwamba CCM ilikuwa inasafisha safu katika jumuiya zake.

"Ukweli ni kwamba kwa suala la Mamuya na UWT, CCM haikuwa inasafisha safu zake, bali ilikuwa ikiwasukuma nje waliogoma kufuata maelekezo ya vigogo ambao walitarajia kuneemeka kutokana na mikataba ya viwanja vya jumuiya za chama tawala.

"Kuna kundi la vigogo ndani ya CCM ambao biashara yao kubwa ni kamisheni, walikuwa wakihoji ni vipi jumuiya tanzu za CCM ziingie mikataba, tena mikubwa, ambayo dhahiri ingewanemeesha," anasema mwanasiasa mmoja ambaye ni mbunge wa CCM.

Raia Mwema imeaambiwa kwamba mvutano huo wa kiwanja cha UWT uliwalazimisha Mwenyekiti Anna Abdallah na Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini, waziri mkuu msitaafu, Jaji Joseph Warioba, kuja juu wakieleza kwamba UWT ni jumuiya inayojitegemea, ina mali ambazo ziko chini ya usimamizi wa wadhamini na kwa ajili hiyo ina haki ya kuamua kuhusiana na nini kifanyike kuhusu mali hizo.

Hoja ya vigogo ndani ya CCM ilikuwa ni kwamba kama jumuiya tanzu cha CCM, UWT haiwezi kuamua juu ya uwekezaji mkubwa kama unaofanyika katika uwanja wake wa Kinondoni bila baraka za Kamati Kuu.

Sasa inafahamika kwamba tayari vigogo hao walikuwa na wawekezaji kadhaa ambao walikwisha kutayarishwa kwa ajili ya uwekezaji katika kiwanja hicho cha UWT kwa ajili ya maslahi yao badala ya yale ya UWT.

Raia Mwema haikufanikiwa kuwapata Abdallah, Jaji Warioba na Mamuya kuzungumzia suala la kiwanja hicho kinachoendelea kujengwa. Baada ya kuwa nje tangu baada ya sakata hilo la kiwanja, wiki iliyopita, kama ilivyo kwa Nnauye, Mamuya alitangaza kuchukua fomu za kuwania uenyekiti wa UWT akieleza kwamba anakusudia kuendeleza yale mazuri aliyoshindwa kuyahitimisha alipoondoka.

Jumuiya ya Wazazi nayo haikubaki nyuma katika migongano hiyo mingi inayodhihirishwa na ugomvi wa fedha uliosababisha aliyekuwa Mwenyekiti, Abihudi Malegesi kuenguliwa.

Malegesi na viongozi wenzake ndani ya jumuiya hiyo walienguliwa wakituhumiwa kufuja fedha za jumuiya hiyo, tuhuma ambazo yeye alizigeuza kwa kudai kwamba zimetokana na muendelezo wa makundi ndani ya CCM.

Jumuiya hizo tatu sasa ziko katika hatua za awali za kuelekea katika uchaguzi na maoni ya baadhi ya waliozungumza na Raia Mwema ni kwamba kama hapatakuwa na uwazi wa kutosha basi kutashuhudiwa mapambano mengine ya makundi ya kifedha kupigana vikumbo hali ambayo imekuwa kielelezo kikubwa cha uchaguzi ndani ya chama tawala.

Kuyumba kwa CCM ikianzia ndani ya jumuiya zake, ni muendelezo wa kuyumba mfululizo kwa chama hicho tokea serikali ya awamu ya nne iingie madarakani, hali ambayo imeelezwa kuwa si ishara njema kwa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.

Kwa zaidi ya miaka mitatu sasa CCM na serikali yake imekua ikikumbana na ‘mazonge' ya kisiasa na kiuchumi ambayo yamekifanya kila uchao kikifanya kazi ya ‘zima moto' na hivyo kuendelea kukidhoofisha machoni mwa wananchi.

Baadhi ya wanasiasa wakiwamo wabunge wa CCM na upinzani wameliambia Raia Mwema kwamba, Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, anapaswa kufanya maamuzi mazito katika kipindi kifupi kilichosalia kabla ya 2010, ikiwa ni pamoja na kuruhusu mageuzi makubwa ndani ya jumuiya za chama hicho na hata ndani ya serikali ili kurudisha imani ya wananchi.
 
Mnavuna Mlichopanda! Baada Ya Kuwadhulumu Watanzania Kwa Muda Mrefu Sasa Mtadhulumiwa Na Wahindi
 
hawa jamaa naona wazi wanakusanya kwa ajili ya 2010,matumbo gani yasiyoshiba?
 
Hicho alichosaini Lowassa kiwekwe hadharani ili Watanzania tuamue nani ni msema kweli katika hii kasheshe iliyojaa harufu ya ufisadi mwingine.

UVCCM: Alichosaini Lowassa si mkataba

na Sauli Giliard
Tanzania Daima~Sauti ya Watu


PAMOJA na kuwepo kwa taarifa za kusainiwa kwa mkataba wa mradi wa ujenzi kati ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na mwekezaji kutoka nje, Kaimu Katibu Mkuu wa umoja huo, Francis Isack, amesisitiza kuwa yaliyomo kwenye mkataba huo ni makubaliano ya awali, licha ya shughuli za ujenzi kuendelea.

Isack amekanusha madai kuwa aliyosaini Edward Lowassa, mwenyekiti wa baraza la wadhamini, si mkataba bali ni makubaliano ya awali yanayojumuisha uanzaji wa mradi huo kwa lengo la kupima uwezo wa mwekezaji.

Akiuelezea mradi huo, Isack alisema unatokana na kazi nzuri ya mwenyekiti anayemaliza muda wake, Dk. Emmanuel Nchimbi, kuhakikisha vijana wanakombolewa kiuchumi na kisiasa.

"Katika kipindi cha miaka 10 ya Nchimbi imekuwa ya mabadiliko makubwa, ikiwemo uanzishaji wa mradi huu," alisema.

Alisisitiza kuwa mradi huo ni kwa ajili ya vizazi vijavyo na jamii isipotoshwe kwani eneo hilo likibaki kama lilivyo bila ya uwekezaji, litavamiwa.

Hata hivyo hakuwa tayari kutaja jina la kampuni inayoendelea na shughuli zake katika kiwanja hicho kama Tanzania Daima ilivyoshuhudia.

Kwa mujibu wa Francis, makubaliano ya awali yanahusisha makampuni mawili ambayo yataungana na kuunda kampuni moja kabla ya kusaini mkataba mara baada ya kuupeleka kwa wazee wa CCM kukaa na kutoa baraka zao.

Amewataka vijana wa umoja huo kutoyumbishwa na propaganda juu ya mradi huo na kudai kuwa huo ni mradi wenye faida kwani watapata asilimia 25 tofauti na wawekezaji wazalendo wanaoishia asilimia 20 pekee.
 
Sasa kuna faida gani kupeleka huko wakati ujenzi umeshaanza ,maana kama haukupata baraka ndio mnataka kutuambia ,sizani kama mjenzi anaweza kuanza kujenga wakati mkataba wa ithibati haujakamilika na kusainiwa ,labda huyu nae hafahamu kitu ,inaonyesha kuna malipo ya awali ndio yameshafanywa na watu kutafuna zao au kugawana.
 
Kweli tanzania hatuna viongozi na kama wapo basi ni kwa majina tu,na si kimatendo.leo utasikia huyu kasema hivi kesho yake yule kasema lile.lakini ukweli hakuna kila mtu anazunguka mbuyu.mara tutapata faida,hoo eneo litavamiwa,mara sio mkataba,lakini watu wanaendelea kujenga bila wasiwasi.
Kama kuna ukweli juu ya hili wato copy ya hicho kilicho sainiwa ili kukata mzizi wa fitina.na hiii kutuambia eti ni faida kwa vizazi vijavyo wakati vilivyopo havjaona faida ni uongo wa mchana.hapa wananikumbusha ule msemo wa vijana ni taifa la kesho
 
Makamba kweli viatu vya Ukatibu Mkuu wa CCM hazimtoshi......hajui analoliongea na anasahau haraka sanaa.......angeamua kupumzika anaaibisha hata familia yake...wana CCM wenzake na hata kudhalilisha Chama....anatetea sana mafisadi huyu mzee..najua yote hii ni njaa yake na kupenda mno pesa maana anaona jua limeshazama any time "wenye chama"kama anavyowaita yeye....watamwambia apumzike....ni kweli jua limekuchwa...
 

Hela zimeshaanza kutumika, ujenzi umeshanza halafu mnatuambia HAKUNA MKATABA BALI NI MAKUBALIANO YA AWALI..!!!

CCM ina virus wakali sana...sijui kama wataweza kujitibu..!!

Utabiri wa JKN kuwa "Bila CCM Imara, Nchi Itayumba" sasa unatimia.
 
kama haujasainiwa mkataba lakini ujenzi umeanza basi wapuuzi hao uvccm!
 
kama haujasainiwa mkataba lakini ujenzi umeanza basi wapuuzi hao uvccm!


Changa la macho hili mkataba ulisainiwa..!! Siamini naneno haya hata chembe; hasa anapokataa hata kutaja kampuni zilizoshiriki katika haya makubaliano ya awali.

Yaani hata majina ya makampuni nayo ni siri..!!!!!
 
Amewataka vijana wa umoja huo kutoyumbishwa na propaganda juu ya mradi huo na kudai kuwa huo ni mradi wenye faida kwani watapata asilimia 25 tofauti na wawekezaji wazalendo wanaoishia asilimia 20 pekee.
Ama kweli wajinga ndiyo waliwao. Hivi ukweli siku hizi unaitwa propaganda? sasa propaganda zitaitwa nini? Hawa watu wanadhani vijana wa leo ni wale wa miaka ile waliokuwa wanalishwa kila kitu?
Pole Francis na wenzio maana tumeamka. Tutawakaba koo mpaka macho yawatoke maana tumewabaini mu WEZI
 
HIVI Lowassa alishaenda kortini kama alivyoahidi?
Thubutu????????????!!!!!!!!!!!

Makamba kweli viatu vya Ukatibu Mkuu wa CCM hazimtoshi......hajui analoliongea na anasahau haraka sanaa.......angeamua kupumzika anaaibisha hata familia yake...wana CCM wenzake na hata kudhalilisha Chama....anatetea sana mafisadi huyu mzee..najua yote hii ni njaa yake na kupenda mno pesa maana anaona jua limeshazama any time "wenye chama"kama anavyowaita yeye....watamwambia apumzike....ni kweli jua limekuchwa...
Hawa ndio aina ya viongozi mnaojivunia CCM ndio maana sintakaa kuwapenda maana usanii umezidi mno kwa manufaa ya wenye chama.
 
Isack amekanusha madai kuwa aliyosaini Edward Lowassa, mwenyekiti wa baraza la wadhamini, si mkataba bali ni makubaliano ya awali yanayojumuisha uanzaji wa mradi huo kwa lengo la kupima uwezo wa mwekezaji.

Na huu utaalamu wa kumpima mkandarasi kwa kumwambia ajenge kidogo ili ujue uwezo wake ni umeasiswa na CCM?? Kweli ndivyo tunavyopima uwezo wa mkandarasi??????
 
Ukisikia mabingwa wa kupindua maneno ndo hawa, mara chenge alikwenda saa nane usiku bengeni kutafuta kiti, na kamera zilizimwa na chenge mwenyewe akakubali kweli alikwenda usiku kutafuta kiti baada ya siku tatu hoo! chenge hakuwai kwenda saa nane usiku bungeni na hili nalo tayari wamelipindua hivi wananona sisi ni watoto wadogo unaoweza kuwambia kura nitakupa pipi, akimaliza kula unamwambia kalale ukiamka kesha asubuhi nitakununulia pipi, akimka unamwambia kunywa chai ukimaliza nitakununulia pipi na circle inaendelea kila siku wakati pipi hainunuliwi.
 
Back
Top Bottom