Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Kamati Kuu CCM yabaini mkataba wa jengo la Vijana una kasoro saba

Na Kizitto Noya


TUHUMA zilizotolewa na mwanasiasa kijana, Nape Nnauye dhidi ya mkataba wa uendeshaji wa jengo la makao makuu ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), zinaonekana kuwa na nguvu baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kukataa kuupitisha mkataba huo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu za kugombea uenyekiti wa UVCCM Julai 15, Nape, ambaye ni mtoto wa mwanasiasa aliyekuwa na heshima ndani ya CCM, Moses Nnauye, alidai kuwa mkataba huo unanuka rushwa na kumashambulia mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini la vijana, Edward Lowassa, mwenyekiti wa wake Dk Emmanuel Nchimbi na aliyekuwa katibu mkuu Amos Makalla kuwa walihusika.

Na juzi ilibainika kuwa mkataba huo una matatizo na hivyo kuifanya Kamati Kuu, maarufu kama CC, kusita kuupitisha baada ya kikao chake kilichoisha usiku mwingi mjini Dodoma.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana kutoka vyanzo vilivyo ndani ya kikao hicho kilichofanyika kwa awamu mbili kuanzia juzi alasiri, zinasema CC imegoma kupitisha mkataba huo kwa kuwa una kasoro kuu saba na imeagiza ukaangaliwe upya na kufanyiwa marekebisho kabla ya kusainiwa.

Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya kuutupa mkataba huo, kamati imeunda tume ya watu watatu kuchunguza mazingira ya namna ulivyoingiwa na kuuboresha ili uwe wa faida.

Vyanzo hivyo vya habari vimewataja wajumbe wa tume hiyo kuwa ni Pindi Chana, Andrew Chenge na Abdalah Kigoda.

"Ni kweli mkataba leo (jana) umejadiliwa lakini haukupitishwa na imeundwa tume kwa ajili ya kuuchunguza na kuuboresha ili uwe wa faida," alisema mmoja wa wajumbe wa kikao hicho ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Taarifa zilieleza pia kwamba tume hiyo haitafanya kazi peke yake bali itafanya kazi kwa pamoja na viongozi wa Umoja wa Vijana, hatua kwa hatua na watakapomaliza suala hilo litakabidhiwa kwa kamati ya utekelezaji na hatimaye Baraza Kuu na hatimaye Kamati Kuu tena.

Mkataba huo uliwasilishwa katika kikao cha CC kwa ajili ya kusomwa, kupitiwa, kukubalika na baadaye kusainiwa, lakini baada ya kusomwa na kupitiwa, haukukubalika na wajumbe wakataka usisainiwe.

Habari zaidi zinasema wajumbe wa CC walitaka mkataba huo usisainiwe hadi ufanyiwe marekebisho katika vipengele saba ambavyo waliona kuwa vinautia kasoro, lakini kasoro hizo saba hazikuwekwa bayana.

Habari zaidi zinasema kuwa kutupwa kwa mkataba huo jana, kulimpa wakati mgumu katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha Sekretarieti ya chama hicho kujadili uamuzi huo wa CC.

Makamba amekuwa mstari wa mbele kuelezea kitendo cha Nape kukosoa mkataba huo kuwa ni utovu wa nidhamu na alimwita kijana huyo ofisini kwake na kumuweka kiti moto mara baada ya kutangaza hisia zake kuwa kuna harufu ya ufisadi katika uingiaji wa mkataba huo.

Makamba pia aliwaambia waandishi mapema wiki hii kuwa demokrasia inaheshimiwa pale tu watu wanapokuwa na nidhamu, akimaanisha kuwa kitendo cha Nape kukikosoa chama nje kuwa ni cha utovu wa nidhamu.

Katika tuhuma zake, Nape alienda mbali zaidi kwa kuwataka Lowassa, Nchimbi na kaimu katibu mkuu wa UVCCM, Frank Isaack kuwajibika kutokana na ama uzembe au kuhusika moja kwa moja na mkataba huo.

Alisema Lowassa kwa mamlaka yake ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya UVCCM alishindwa kutekeleza majukumu yake ya kusimamia mali za jumuiya hiyo.

Alisema mkataba huo una kasoro nyingi, ikiwemo mkataba huo kuwa wa maisha na kipengele kinachosema mwekezaji atamiliki asilimia 75 ya hisa wakati UVCCM wataambulia asilimia 25.

Nape alitaja kasoro nyingine za mkataba huo kuwa ni mwekezaji kukosa mtaji wake na kutumia hati za jengo la UVCCM kwenda kuomba fedha benki, jambo alilosema kuwa hata UVCCM yenyewe ingeweza kulifanya.

Alibainisha kuwa mradi wa jengo hilo ni mkubwa lakini una mikono ya vigogo ambao wamepanga kukata majina ya baadhi ya wagombea watakaokuwa na msimamo wa kuuhoji.

Siku moja baada ya Nape kutoa kauli hiyo, Makamba alimwita ofisini kwake kwa nia ya kumkaripia na kueleza kuwa Baraza la Wadhamini halipaswi kuwajibika kuhusu mradi huo kwa kuwa limetimiza wajibu wake, tena kwa kuvuka mpaka kwa sababu limelifikisha suala hilo katika vikao vya chama kwa ajili ya kuona linafanyika kwa uhakika.

Makamba alisema baada ya Baraza hilo kupelekewa na uongozi wa UVCCM mapendekezo ya mkataba huo, iliyapitia na kufanya marekebisho ambayo imeyaona yanafaa na kuyafikisha ofisini kwake Julai 7 mwaka huu ili ayapeleke kwenye vikao vya juu vya chama hicho.

Hata hivyo, kauli ya Makamba ilipingwa na baadhi ya wajumbe wa baraza la UVCCM ambao kwa nyakati tofauti walisema mkataba huo ni batili kwa kuwa hakuna kikao cha baraza hilo kilichoupitisha.

Wajumbe hao walisema asilani hawajabariki mkataba wa jengo hilo jipya na kusisitiza kuwa taratibu za kuupitisha zilikiukwa na kwamba ujenzi wake unasukumwa na vigogo wenye maslahi binafsi

Utata wa kauli ya Makamba ulianza kujitokeza pale aliposhindwa kueleza sababu za mwekezaji kusogeza vifaa eneo la ujenzi na kuanza kazi wakati alisema kuwa mkataba huo haujasainiwa.

Makamba alishindwa kueleza suala hilo na kuwatupia mpira viongozi wa UVCCM ambao hadi leo wanashindwa kuondoa utata huo, akidai kuwa hahusiki na masuala ya ujenzi.

Mwenyekiti wa UVCCM anayemaliza muda wake, Dk Emmanuel Nchimbi alikwepa kuzungumzia utata huo kwa maelezo kuwa yeye si mtendaji wa taasisi, bali kiongozi wa vikao vya taasisi hiyo.

Naye kaimu katibu mkuu wa UVCCM, Francis Isack alisema suala la mwekezaji kusogeza vifaa eneo la ujenzi kabla ya mkataba kusainiwa, ni la kawaida katika mikataba.

Kauli ya Nape kwamba baadhi ya vigogo wamepanga kukata majina ya wagombea wa uchaguzi wa UVCCM watakaohoji uhalali wa makataba huo, imeanza kujidhihirisha baada ya Baraza Kuu la UVCCM kumvua uanachama na kupendekeza kwa CCM kumvua nyadhifa zote ndani ya CCM kwa tuhuma za kusema uongo kuhusu mkataba huo.

Mbali na maamuzi hayo ya Baraza Kuu, tayari Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM imemwekea alama E inayomaanisha hafai kuwa kiongozi kwa kigezo cha umri.

Mkataba huo umeshaamsha mvutano mkubwa ndani ya UVCCM ambayo tayari wanachama wake wamegawanyika kwa misimamo ya Nape.

Source: Mwananchi
 
NchimbNnauye110908.JPG


Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Dk Emmanuel Nchimbi na Nape Nnauye wakijadili jambo wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kinachofanyika mjini Dodoma jumatano. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 
Kamati Kuu CCM yabaini mkataba wa jengo la Vijana una kasoro saba

Na Kizitto Noya


Habari zaidi zinasema kuwa kutupwa kwa mkataba huo jana, kulimpa wakati mgumu katibu mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, ambaye alilazimika kuitisha kikao cha dharura cha Sekretarieti ya chama hicho kujadili uamuzi huo wa CC.

Makamba amekuwa mstari wa mbele kuelezea kitendo cha Nape kukosoa mkataba huo kuwa ni utovu wa nidhamu na alimwita kijana huyo ofisini kwake na kumuweka kiti moto mara baada ya kutangaza hisia zake kuwa kuna harufu ya ufisadi katika uingiaji wa mkataba huo.

Source: Mwananchi

Makamba na uzee wake wote kwa nini anakuwa na njaa kali namna hii?? Kelele nyingi akiwa anaingilia mambo ya UVCCM akiwa kwenye CC anakuwa mpole kama kifaranga kilicholowa maji.
 
Nape ambwaga Makamba NEC, Kikwete ampa ruksa kukata rufaa

Na Ramadhan Semtawa


MWENYEKITI wa CCM, Jakaya Kikwete jana alimpa ruksa mwanasiasa kinda wa chama hicho, Nape Moses Nnauye kukata rufaa iwapo anaona hakuridhika na uamuzi wa kumvua uanachama wa Umoja wa Vijana wa chama hicho, UVCCM, akitofautiana na katibu wake, Yusuf Makamba, ambaye alisema kijana huyo hawezi kukata rufaa katika chombo chochote.

Kikwete, akitoa taarifa fupi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) jana, pia alisema chama hicho tawala kitaendelea kumtambua Nape kama mjumbe wake, mwanachama na kutambua nyadhifa zake zote ndani ya CCM, tofauti na mapendekezo ya Baraza Kuu la UVCCM lililotaka mtoto huyo wa mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama hicho, marehemu Moses Nnauye, avuliwe nyadhifa zake zote.

Baraza hilo, ambalo lilimjumuisha Makamba, ambaye ni mtendaji mkuu wa CCM na mwanasiasa mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye ni kaimu kamanda wa vijana Tanzania Bara, lilimvua Nape uanachama na kupendekeza avuliwe nyadhifa nyingine zote ndani ya CCM kwa madai kuwa alisema uongo alipotoa tuhuma nzito kuwa mkataba wa uwekezaji wa jengo la makao makuu ya UV-CCM unanuka rushwa.

Lakini jana, kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha NEC kilichofanyika mjini Dodoma, Kikwete, ambaye ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliuambia mkutano huo kuwa Halmashauri Kuu inamtambua Nape kama mjumbe halali, mwanachama wa CCM na pia inatambua nyadhifa zake zote ndani ya chama na kwamba kijana huyo machachari anayo haki ya kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM.

"Hiyo ilikuwa ni taarifa fupi ya mwenyekiti mwenyewe," alisema mtoaji habari wetu. "Aliichomeka hoja hiyo na kuweka bayana kuwa NEC inamtambua Nape kama mjumbe, nyadhifa zake na uanachama wake. Baada ya kauli hiyo, wajumbe walipiga makofi na kuunga mkono."

Chanzo hicho kutoka NEC kilifafanua zaidi kuwa mwenyekiti alisema maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM ni ya vijana wenyewe na kwamba kama Nape akiamua kukata rufaa, anaruhusiwa kufanya hivyo kwa kufuata ngazi husika, kwa mujibu wa taratibu za chama na jumuiya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo za kuaminika, Kikwete aliweka bayana kwamba maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM ni ya vijana wenyewe na chama hakiwezi kuingilia wala kuhusishwa nayo.

Alipoulizwa kuhusu msimamo huo wa NEC, Nape alisema alikuwa mwenye furaha na akarudia kauli yake kuwa ana imani na vikao vya juu vya CCM.

"Nimepokea habari hizi kwa furaha kubwa na nina matumaini makubwa na imani na vikao vya juu vya chama," alisema.

"Ushindi uliopatikana katika hatua hii si wangu binafsi, bali ni ushindi wa wale wote wanaopenda kusema ukweli na kuusimamia.

"Nawataka wale wote wanaoniunga mkono, wasikate tamaa kwa sababu safari inaendelea na inanionyesha kwamba, kuna mwelekeo wa mafanikio.

"Kwa matokeo haya angalau ninaweza kusema kwamba ukweli umeshinda na hii inatupa changamoto wote kwamba mtu unaposimamia ukweli, basi daima uwongo unajitenga."

Ushindi wa Nape pia ulijidhihirisha katika uamuzi mwingine wa Kamati Kuu, iliyokutana juzi na kuamua kutoupitisha mkataba wa uendeshaji wa jengo la makao makuu ya UV-CCM ikitaka uangaliwe upya.

Makamba, ambaye aliingia kwenye Baraza Kuu la UV-CCM kwa wadhifa wake wa katibu mkuu wa chama, amekuwa akiwaambia waandishi kuwa uamuzi wa kumvua Nape uanachama ni wa mwisho na kwamba kijana huyo hawezi kukata rufaa popote pale mbinguni na duniani.

Mara kadhaa amekuwa akiripotiwa kueleza kuwa kitendo cha Nape kukosoa chama nje ni cha utovu wa nidhamu na kuwajibu wale waliokuwa wakipinga uamuzi wa Baraza Kuu kuwa demokrasia haikutendeka kwa kusema demokrasia haiendani na utovu wa nidhamu.

Lakini maamuzi hayo yalipingwa na makada waandamizi wa CCM, wakiwemo mawaziri wakuu wastaafu, Cleopa David Msuya na Frederick Sumaye, ambao walisema waziwazi kuwa Baraza Kuu liliamua kwa jazba.

Awali, suala la Nape halikuwa ajenda kwenye kikao hicho cha NEC na kwa maana hiyo halikuweza kujadiliwa kutokana na kutokuwepo rasmi. Ajenda zilizokuwepo zilikuwa ni uchaguzi wa Tarime.

Katika ajenda hiyo, Ryoba Christopher Nangoye alipitishwa kuwa mgombea wa CCM wa kiti cha ubunge cha Tarime, jimbo ambalo limeachwa wazi na Chacha Wangwe, ambaye alifariki dunia kwa ajali ya gari.

Kauli ya mwenyekiti wa CCM inadhihirisha jinsi Nape anavyoitikisa CCM baada ya uamuzi wa Baraza Kuu, ambalo linahusisha wazee ambao ni makada waandamizi ndani ya chama, kuonekana unapwea.

Mtikisiko huo unaonyesha kwamba kundi linalomkingia kifua Nape ni lenye kuona kama hatua dhidi ya kinda hiyo kisiasa ni za juu na jazba na ambazo ambazo hazikuwa na nia njema ya kumjenga, zaidi ya kumkomoa na kummaliza kisiasa.

Kauli za Msuya na Sumaye kuhoji na kutaka ufafanuzi wa hatua hizo dhidi ya Nape kabla ya mkutano wa NEC, zilikuwa ni ishara ya mtikisiko ndani ya chama kutokana na ukweli kuwa maamuzi ya Baraza Kuu UV-CCM, yalimhusisha mtendaji mkuu wa CCM.

Wazee wengine ambao walionekana dhahiri kutoa kauli za kumshughulikia Nape katika mkutano Baraza Kuu siku ya Jumapili, mbali ya Makamba, alikuwepo pia kada mwingine mwandamizi mzee Kingunge Ngombale Mwiru.

Michael Uledi kutoka Dodoma anaripoti kuwa naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Saleh Ramadhan Ferouz ameeleza kuwa Nangoye alipitishwa kwa wingi wa kura.

Ferouz, akizungumzia yaliyojiri ndani ya kikao cha NEC, alisema: "NEC haijatoa maamuzi yoyote kuhusu suala la Nape kwa sababu halikufikishwa rasmi kwetu."

Alisema kuwa Baraza Kuu la UVCCM haliwezi kumfutia uanachama wa chama na wala haki zake ningine ndani ya chama, bali lina ukomo wake.

Kwa kuchambua kauli hizo za makada hao waandamizi kuhoji na kutilia shaka maamuzi ya wazee wenzao, ni ishara uamuzi wa Baraza Kuu la UV CCM kumvua uanachama Nape na kutaka aadhibiwe na chama, unathibitisha kwamba kinda hilo kisiasa linaitikisa CCM.

Source: Mwananchi
 
Swali kwa wataalam wa siasa za CCM ama wenye ujuzi na utaratibu mzima wa kugombea uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake.

Je, kitendo cha JK kusema kwamba Nape anaruhusiwa kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza Kuu la UVCCM (hapa nina maanisha kumvua uanachama wa UVCCM), siyo kwamba anahalalisha jamaa kuondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM?

Je, hiyo rufaa inachukua muda gani kupatiwa majibu/maamuzi ya vikao vya juu? Je, rufaa inakatwa kwa CC ama kwa NEC? Je, kuna uwezekano wa NEC kuitishwa kwa ajili ya kujadili rufaa ya Nape kurejeshewa uanachama wake wa UVCCM?

Hapa kuna harufu ya ule mchezo wa Arusha wakati wa uchaguzi wa CCM, kesi za kupika na baadaye zinafutwa na huku uchaguzi umeishapita tayari. Maana Nape anaweza kukata rufaa ikaja kusikilizwa na kutolewa maamuzi wakati mchakato wa kujadili wagombea umeishakwisha na hivyo kupoteza hata maana ya kukata rufaa.
 
Swali kwa wataalam wa siasa za CCM ama wenye ujuzi na utaratibu mzima wa kugombea uongozi ndani ya CCM na Jumuiya zake.

Je, kitendo cha JK kusema kwamba Nape anaruhusiwa kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza Kuu la UVCCM (hapa nina maanisha kumvua uanachama wa UVCCM), siyo kwamba anahalalisha jamaa kuondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM?

Je, hiyo rufaa inachukua muda gani kupatiwa majibu/maamuzi ya vikao vya juu? Je, rufaa inakatwa kwa CC ama kwa NEC? Je, kuna uwezekano wa NEC kuitishwa kwa ajili ya kujadili rufaa ya Nape kurejeshewa uanachama wake wa UVCCM?

Hapa kuna harufu ya ule mchezo wa Arusha wakati wa uchaguzi wa CCM, kesi za kupika na baadaye zinafutwa na huku uchaguzi umeishapita tayari. Maana Nape anaweza kukata rufaa ikaja kusikilizwa na kutolewa maamuzi wakati mchakato wa kujadili wagombea umeishakwisha na hivyo kupoteza hata maana ya kukata rufaa.

Kama Nape mjanja ang'ang'anie hili la kukata rufaa kufukuzwa uanachama. Nina imani atashinda na kisha kujipatia sifa kubwa ndani ya CCM.

Akichanganya na lile la kugombea UVCCM ambako hoja yake ni weak atafanya ashindwe na ngoma iwe draw.

Hii dhoruba imekuza jina lake, ana future ndani ya CCM na kwenye uongozi wa nchi.

Aige mfano wa mheshimiwa Zitto wa kukubali ile adhabu ya bungeni bila kurusha matusi na matokeo yake CCM wenyewe wakajifunga goli.
 
Nape ambwaga Makamba NEC, Kikwete ampa ruksa kukata rufaa

Na Ramadhan Semtawa



...Kikwete, akitoa taarifa fupi kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) jana, pia alisema chama hicho tawala kitaendelea kumtambua Nape kama mjumbe wake, mwanachama na kutambua nyadhifa zake zote ndani ya CCM, tofauti na mapendekezo ya Baraza Kuu la UVCCM lililotaka mtoto huyo wa mwanasiasa aliyekuwa na ushawishi mkubwa ndani ya chama hicho, marehemu Moses Nnauye, avuliwe nyadhifa zake zote.

Baraza hilo, ambalo lilimjumuisha Makamba, ambaye ni mtendaji mkuu wa CCM na mwanasiasa mkongwe wa CCM, Kingunge Ngombare Mwiru, ambaye ni kaimu kamanda wa vijana Tanzania Bara, lilimvua Nape uanachama na kupendekeza avuliwe nyadhifa nyingine zote ndani ya CCM kwa madai kuwa alisema uongo alipotoa tuhuma nzito kuwa mkataba wa uwekezaji wa jengo la makao makuu ya UV-CCM unanuka rushwa.

Lakini jana, kwa mujibu wa taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha NEC kilichofanyika mjini Dodoma, Kikwete, ambaye ni rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliuambia mkutano huo kuwa Halmashauri Kuu inamtambua Nape kama mjumbe halali, mwanachama wa CCM na pia inatambua nyadhifa zake zote ndani ya chama na kwamba kijana huyo machachari anayo haki ya kukata rufaa kupinga maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM.

"Hiyo ilikuwa ni taarifa fupi ya mwenyekiti mwenyewe," alisema mtoaji habari wetu. "Aliichomeka hoja hiyo na kuweka bayana kuwa NEC inamtambua Nape kama mjumbe, nyadhifa zake na uanachama wake. Baada ya kauli hiyo, wajumbe walipiga makofi na kuunga mkono."

Chanzo hicho kutoka NEC kilifafanua zaidi kuwa mwenyekiti alisema maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM ni ya vijana wenyewe na kwamba kama Nape akiamua kukata rufaa, anaruhusiwa kufanya hivyo kwa kufuata ngazi husika, kwa mujibu wa taratibu za chama na jumuiya.

Kwa mujibu wa taarifa hizo za kuaminika, Kikwete aliweka bayana kwamba maamuzi ya Baraza Kuu la UV-CCM ni ya vijana wenyewe na chama hakiwezi kuingilia wala kuhusishwa nayo....

kwa kweli mimi naona kienglish english tu. kama taarifa hizi ni sahihi basi mkulu anacheza na maneno tu na kukwepa kutoa maamuzi. yaani kwa matiki ya kauli hiyo ya mkuu nec imekubali kuvuliwa uanachama wa wa nape kutoka baraza kuu na uv-ccm (kama nimeelewa vizuri uamuzi wa baraza)

kisha nec inamtambua nape kama mjumbe wake halali ikiwa na maana wameyakataa mapendekezo ya baraza uv-ccm ya kumyang'anya nape nafasi za uongozi katika chama lakini ujumbe huo umeanzia uv-ccm ambako ndio wamemtema nape!

au huko nec moto uliwaka haswa na hii ndio "compromise" position?
 
Nape kakulia ndani ya CCM lakini bahati mbaya haijui CCM. Nashangaa anashangilia "ushindi" sijui ushindi gani hapa. Kubwa kuliko yote ni kuwa kama hawatampisha kugombea basi mshindwa ni yeye. Hayo ya kuvuliwa uanachama ni blah blah za wajinga wachache.
 
Hiyo tume ya kuchunguza huo mkataba nayo ina uwalakini. Unamuweka fisadi Mzee wa Vijisenti kuchunguza mkataba wa kifisadi uliofanywa na fisadi mwenza Lowassa. Ama kweli Utamu wa Ngoma Muulize Kiuno.
 
Hiyo tume ya kuchunguza huo mkataba nayo ina uwalakini. Unamuweka fisadi Mzee wa Vijisenti kuchunguza mkataba wa kifisadi uliofanywa na fisadi mwenza Lowassa. Ama kweli Utamu wa Ngoma Muulize Kiuno.

Hii inathibitisha kwamba CCM ni chama cha kifisadi. Yaani wamekosa mtu mpaka wakamchague fisadi Chenge!? Kweli CCM ni muflisi!!
 
busara itumike zaidid kuliko jazba, nadhani hapa liko tatizo ila ninahakika nec haiwezi kusikiliza maamuzi ya uvccm kwenye hili mana hapa mshikamano utaondoka na kazi kubwa ndani ya ccm ni kuhakikisha jumuiya inabaki kuwa kit u kimoja na si vyenginevo, hiyo ilikuwa jazba na kila siku sisi kama vijana kuwa tuna mambo mengi ya kujadili na lazima liweko vuguvugu kila tunapokutana ila mwisho lazima busara itawale, hapa uvccm kama ni kweli walifanya uamuzi wa kumvua uanachama mjumbe wao wa nec kwa jumuiya, hilo ni kosa na ni uamuzi wa hasira na haukuzingatia taratibu zetu za kuweka mbele maslahi ya jumuiya na ccm, zaidi ni utashi wetu, hili ni kosa na tusilirudia mana ccm ni yetu kwa sayansi ya kawaida wazee wantuandaa sisi na lazima tutawaliwe na hekima zaidi na matashi ya nchi na chama mchetu na si yetu binafsi.
vijana kaeni kama vijana muwe na utaifa mbele .
 
Hii inathibitisha kwamba CCM ni chama cha kifisadi. Yaani wamekosa mtu mpaka wakamchague fisadi Chenge!? Kweli CCM ni muflisi!!

.......Duhh yaani mmeshusha hadhi Chenge hadi kufikia kuwa hawezi kuona makosa!!!!!...............mimi sikubaliani.........

Chenge makosa anayaona tena sana.....kwenye ufisadi wake....alitambua kabisa kuwa anafanya makosa.......na ndio haswaa sababu ya sisi kumuita FISADI.............

....hivi sasa katika kutaka kujisafisha ndio anaona ku*** la mwenzie na kuwaonyesha wengine............
 
Mimi nashangazwa na ugumu wa waandishi wetu kuelewa na kutafsiri mambo.Alichosema JK wala sio taarifa mya kama ambavyo mwananchi wanaidandia,kwa kuwa kama angekuwa Nape amefutwa uanachama wa ccm basi uvccm wasingekuwa na haja ya kumuombea afutwe nafasi zake za uongozi kwa kuwa zingekuwa tayari zimejifuta automatically.

LAKINI KWA SASA NAPE SIYO MJUMBE WA BARAZA KUU VIJANA,SIO MJUMBE WA MKUTANO MKUU VIJANA NA WALA SIO MWANACHAMA WA UVCCM,Hivyo ndoto za kugombea zimekufa hapo......Kuhusu jengo.pia wamepotosha kabisa ukweli ni huu,kamati kuu baaada ya kuona kuna maneno mengi ya uongo ikaunda kwa niaba yake team na sio kamati,ikiwa na wajibu wa kusaidia kurekebisha kasoro ndogo ndogo sana kwenye mkataba,jambo ambalo ni la kawaida kwenye mchakato wowote wa kupitisha mkataba,au walidhani mkataba hautakuwa na kasoro ata moja? hivyo team hio baada ya kuupitia mkataba huo utasainiwa bila ya kujadiliwa tena na kamati kuu,kwa mantiki hio hio kamati kuu imekubali mkataba upite....Mambo ya kurekebisha yalikuwa kama yafuatayo na ni matatu na siyo saba:

1.kwa kuwa ni joint venture mkataba uonyeshe nguvu ya kila bodi ktkt mradi huo
2.mkataba uoneshe stages mbalimbali za investment na gharama zake badala ya kuonyesha tu total cost.
3.Mkataba uoneshe hatua zitakazofatwa wakati wa kuvunja jointventure.

Kwa mtu mwenye akili ataona hapa kuwa haya ni marekebisho madogo sana ambayo hayatochukua hata wiki mbili kuyafanya na kusaini mkataba.

Madai ya Nape yalikuwa kuwa mkataba hauna kukomo,ratiol ya mgawo ni ndogo sana,ni wa kifisadi,umesiniwa kabla ya kupitishwa na kuwa mwekezaji ametumia hati za kiwanja kukopa na mwisho ilikuwa haukupitishwa na umoja wa vijana ktk vikao.

Madai hayo yote ya Nape hayajaonekana kuwa ni ya kweli na ya msingi hivyo hayakujadiliwa na cc iliyatupa.Hivyo panapo uzima mkataba huu utasainiwa tarehe 26 mwezi huu mbele ya waandishi wa habari.
 
Inaelekea suala lenyewe hili llimefikia mwanzo wa mwisho wake. Nape ameshapigwa rungu la kisiasa, hasa katika ambition yake ya kugombea uenyekiti UVCCM.

Pamoja na hayo, wengi tumemfahamu huyo kijana sasa. Hiyo ni advantage kwake politically.
 
mkuu heshima yako sana, lakini huu ni uongo wa mchana kweupee, katika historia ya uongozi wa tanzania kama kungekuwa na mkuu wa wilaya aliyejenga shule za sekondari 17 in one year, tena katika wilaya ambayo hakuwepo, alikuwa kwenye kampeni za urais, angeshapewa nishani ya pekee ya taifa ya uongozi bora,

sio wewe tu unayetoka bunda, mshikaji wangu wa karibu sana alikuwa mbuneg kule, inawasiliana naye kuupata ukweli wote, na nimemuomba ukweli wote, kama nchimbi alijenga shule 17 katika mwaka mmoja aliokuwa dc pale nitauweka wazi si unajua kwenye ukweli huwa sina noma kukubali, lakini so fasr ni maneno yal;iyomshitua kila mtu aneyotka bunda ninayemfahamu,

it is about time nitauweka ukweli hapa, lakini ahsate kwa mchango wako.

nami nangojea kijua kama lithibitisha ni kweli au bado maana jibu bado halijatoka mpaka sasa kujua yupi alikuwa mkweli kwenye hili.
 
Baadhi ya Yaliyojiri kwenye kikao cha CC, according to the dataz:-

1. Mkataba wa Jengo:-

- Kamati kuu imeuona mkataba kuwa na kasoro zipatazo saba, na kwa mujibu wa katiba ya CCM, imeunda kamati ya wajumbe watatu; Dr. Abdallah Kigoda, Chenge, na Pindi Chana, kuupitia mkataba huo tena na kuyarekebisha matatizo hayo saba,

- Baada ya kumaliza marekebisho waupeleke kwanza Umoja wa Vijana, kwa mapendekezo na kama mujibu wa katiba urudishwe tena kamati kuu kwa majadiliano zaidi kabla ya kuidhinishwa upya na kamati kuu.

Sasa naona kuna a lot of spin kwamba mafisadi wameshinda, well kwangu hapa sioni kushinda, kwa sababu mkataba ulioshinda hauwezi kutengenezewa kamati za kuupitia upya na kurekebishwa upya na kutakiwa urudishwe ili ujadiliwe tena na kupitishwa upya, lakini ni haki ya kila mwananchi kuamua exactly uamuzi wa CC ulikuwa ni nini, ingawa naona mafisadi leo wamefanya kazi kubwa ya kujaribu kuficha ukweli wa kikao lakini ninaousema ndio ukweli hasa na sio filimbi za the losers!

2. Hoja ya Nape:-

- Asubuhi Rais alisema wazi mbele ya wajumbe wote waliohudhuria kuwa uamuzi wa baraza la UV-CCM dhidi ya Nape, yeye binafsi haamini kuwa ni uamuzi wa Vijana wote wa UV-CCM, anaamini kuwa ni wa viongozi wachache sana wasiowakilisha vijana wote.

-Rais amesema kwamba uamuzi mzima ni ujinga tena wa hali ya juu sana, na kwa kauli moja kamati kuu imeyakataa mapendkezo hayo ya UV-CCM ya kufukuzwa kwa Nape au kuvuliwa uanachama wa UV-CCM na CCM kwa ujumla,

-However, Rais akasema kwamba CCM inaongozwa na katiba na yeye hayuko juu ya katiba, akasema kuwa katiba ya CCM inamtaka Nape akate rufaa kwa CCM taifa na rais ametamka wazi kuwa Nape anayo baraka yake kwenye kukata huko rufaaa kwa CCM taifa.

- Rais akaongeza kuwa maneno ya Mkamba kwamba Nape hawezi kukata rufaa mahali popote ni ujinga tena hayana maana yoyote, na kwamba "...maneno ya Makamba ndani ya CCM sio final authority..." alisema Rais ndani ya CC kwa hasira sana.

Again, naona kumekuwa na spin nyingi sana kwenye hili kwamba Nape ameuliwa kisiasa, no way! Nape bado ni mjumbe wa NEC, ni mwanachama wa CCM, lakini mpaka rufaa itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi hatoweza kushirki kwenye shughuli za Vijana, ingawa bado ataendelea kuwawakilisha kwenye NEC sasa does this sounds like mtu aliyeuliwa kisiasa na Nchimbi?
ni uamuzi wa msomaji na kuuchambua mchele na pumba zilipo!

3. Hoja ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga:-

- Mafisadi walikuwa wametayarisha idea ka kutaka kumkata nguvu Sitta kama walivyopania kumuondoa kwenye nafasi hiyo, kwa hiyo walimtuma mwenyekiti wa CCM Shinyanga kuanzisha hoja kwenye kiako hiki cha CC.

- Mwenyekiti huyo alismama na kudai kuwa ni lazima Sitta awajibishwe kwa kukosa nidhamu kwa serikali na CCM, kwani anahusika sana na kumkashifu rais na pia kuharibu kwa makusudi maamuzi mengi ya CCM bungeni, nia na madhumuni ilikuwa aanzishe hoja halafu wajumbe wengine waliokuwa wametayarishwa na mafisadi wairukie hoja na kumkandamiza Sitta, ili aadhibiwe!

- Kabla hajamaliza Sitta kwa hasira alisimama na kumtaka akae chini mara moja kwa sababu ni mpumbavu, "...wewe mjumbe wa Shinyanga lazima uwe na heshima na hiki kikako kizito cha taifa..." "...huwezi kuja hapa kuelta ujinga uijnga sisi tunaokosoa CCM tunaitakia mema na tunajaribu kujiweka sawa na hali halisi kwa kutetea masilahi ya wananchi sio viongozi wachache wasio na aibu wanajaribu kukiangusha chama kwa sababu ya ubinafsi..." alisema Sitta kuwa mawazo yenu ya kifisadi yamepitwa na wakati na wote huko ni wapumbavu, mje na hoja hapa sio kuleta ujinga na upumbavu!

- Holly cow! wajumbe wote kwenye kikao wali-freeze mafisadi wote wakanywea kimyaaa! Hatimaye kwa unyonge sana Fisadi Mama Anna Abdallah, akasimama na kusema kuwa hoja ya Mwenyekiti wa Shinyanga, ilikuwa ni finyu na haina mantiki, lakini akamuomba Spika apunguze jazba na pia afute kauli ya kuita wajumbe wengine wapumbavu kwamba hiyo lugha ilikuwa kali mno kwa kikao kama kile kizito cha taifa.

- Spika Sitta, akakubali kwa unyenyekevu, na kufuta kauli ya neno "wapumbavu" na "ujinga ujinga" lakini ukawa ndio mwisho wa hoja ya mafisadi.

Haya ndio niliyoyapata so far kutoka huko ndani, na kuthibitishwa na wajumbe wengi waliohudhuria kikao, kwangu binafsi nimeridhika tena sana kwa sababu this is better than ile hotuba ya rais bungeni, I mean ni better mara 100. Cha muhimu sasa ni kwa Nape kukata rufaa kama katiba invyosema, uenyekiti wa UV-CCM hilo hata yeye mwenyewe anaelewa kuwa ni out of the question na sidhani kama ana nguvu ya kutosha na hiyo nafasi, lakini the goal has been met na binafsi ninampa heshima zangu za juu na Salute! kwa kuweza kuli-freeze taifa kwa kupata a political attention akiwa ndani ya CCM, na pia ningemshauri kuwa sasa ni kuangalia mbele tu nyuma mwiko!

Mafisadi wanajua wazi kuwa lengo lao lilikuwa Nape kufukuzwa kabisa CCM, wameshindwa wala sio siri ndio maana leo wamejaribu kununua magazeti akribu yote ili kuficha ukweli wa kikao na maneno ya ujanja na wapambe wao masikini ya Mungu angalau kuna wanaowalipa, lakini wengine huwa ni kufanya kazi bure tu kwa mafisadi nawaona humu maneno mengi ya uongo mtupu, ndio maana tulingiaa hapa JF mapema, maana tulijua kua magazeti yote yalishanunuliwa ndio maana tukaja hapa kuweka ukweli straight!, Mafisadi hawawezi kutushinda wananchi wengi na wenye uchungu na taifa letu, kwa sababu ukweli tunao na tutaendeela kuwakosesha usingizi mpaka kieleweke, na tuko wengi sana kuliko wao!

Mungu Aibariki Tanzania na Bravo Nape! Na wewe mkuu huko juu maneno mengi ya uongo kama unaamini una ukweli wa yaliyojiri kwenye kikao njoo tuvine nipo sasa!
 
Back
Top Bottom