Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

kaka wembemkali unamjua vizuri mkwere xxxxx jamaa hapendi kunyooshewa kidole xxxx mara nyingi hupenda lawama ziwaendee wengine lakini sio yeye xxxxx nakumbuka alivyoonyeshwa ripoti ya mwakyembe,alitoa go ahead,lakini baadaye alijifanya kuwa nae alisikia ripoti ile siku iliposomwa bungeni xxxxx tatizo la mkwere pamoja na urais wake,lakini wapo wengi anaowaheshimu na kuwaogopa xxxxxxx kwa kuwa issue hii ya nape inamuhusisha lowassa, nawahakikishieni hakutokuwa na jipya......

mzee asante kwa kuwa muwazi... Our tanzania family ni kama ile ya baba asiyesema lolote kwa watoto wake ili wampende akiashau kwamba mama anapata tabu kulea peke yake

anyway, miracles happen and this may be the first one in our historic country and jk needs to write his name in our country history... So far we only have nyerere after independency
 
Kutoka Dom; CC imeunda tume kuchunguza mradi wa jengo la vijana, Dk. Kigoda amepewa kazi ya kuongoza tume hiyo, baada ya matokeo yake ndio mbivu na mbichi zitajulikana. CC imekubali kuwa Nape bado ni mjumbe halali wa NEC. Ni kweli kuwa Lowassa na Nchimbi waliwekwa kitimoto katika kikao hicho jana


Kiini macho au kwa ligha nyingine ni mazingaombwe yaleyale ya CCM. May kwa vile ni mtoto wa kigogo mwenzao ndiyo sababu kuna kautata kidogo. Angekuwa ni mtoto wa mkataa minyaa kama sisi nafikiri hata huko NEC angeshaenguliwa. May be Nchimbi amekamata pabaya this time.
 
kuna watu watavuliwa uanachama kama the real first strike ya JK... hapo ndipo maandamano yataanza kuzizima!

Nakuamini mkuu lkn ninawwasi wasi sana na JK he is the weakest president ever happened, hana ubavu huo, jamaa wata mblackmail tuu hao, angekuwa yuko hapo alipo kihalali angeweza labda amvue uanachama NAPE "mtoto yatima"
 
Hapana, maelezo ya FMES ni sahihi, kilichofanyika ni UVCCM wamependekeza kwa CC Nape avuliwe uanachama wa vijana na nyadhifa zake nyingine ikiwemo U_NEC vijana. Mpaka hapo kamati kuu itakapo bariki mapendezo ya UVCCM ndipo atakuwa amevuliwa rasmi uanachama wa UVCCM. In the mean time he still M-NEC vijana. If that make a sense....

Unatuambia unachodhani kina make sense au unatuambia facts? Wewe na mwenzio FMES wote hamko sahihi.

Kwanza, Nape amefukuzwa uanachama wa UVCCM. Hakuna utata.

Francis Isaac, Kaimu Katibu Mkuu, UVCCM. TANZANIA DAIMA, Jumatatu, Sept 8, 2008:

"Ni kweli Baraza Kuu limeamua kumfukuza kwenye uanachama wa UVCCM Nape Moses Nnauye, kwa makosa matatu,..."

Mbili, japokuwa Nape aligombea ujumbe wa NEC kupitia tiketi ya UVCCM, na japo ameondolewa UVCCM, yeye bado ataendelea kuwa mjumbe wa NEC.

Yusuf Makamba, Katibu Mkuu, CCM, HABARI LEO, Wednesday, Sept. 10, 2008:
"Katika Katiba ya CCM hakuna sehemu inayoeleza kuwa mwanachama akifukuzwa uanachama na Umoja wa Vijana wa CCM lazima afukuzwe uanachama na kuvuliwa ujumbe au madaraka aliyonayo,"

Tatu, kilichopendekezwa ni Nape kuvuliwa nafasi nyingine za CCM nje ya UVCCM, ikiwemo ya Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Ofisi Ndogo Makao Makuu CCM, Lumumba, na ujumbe wa NEC.

Francis Isaac, Kaimu Katibu Mkuu, UVCCM. NIPASHE, Jumanne, Sept. 9, 2008:
``Kanuni zinaturuhusu kumfukuza, UNEC wake tumependekeza CC (Kamati Kuu) kumvua,...``

Habari ndio hiyo.
 
1. Makamba majuzi kwenye CC alitaka wabunge wanaokosoa CCM waadhibiwe, akatukanwa kama mbwa na muungwana.

2. Nipashe wakasema Nape amekaangwa na mkataba wa jengo umepita, muungwana akamtwangia waya mengi kutaka kujua nani aliyewapa hizo habari wanazoziiita za CC,

-Muungwana akawalazimisha kuzifuta na kuomba masamaha na pia kumtaja aliyewapa hizo habari, they did kwamba ni Nchimbi anayewapa habari.

3. Muungwana akawapandisha kuwa mawaziri kamili washikaji wote wa Nchimbi kasoro Nchimbi tu!

4. Muungwana akairukia ishu ya jengo, hata kabla haijapitia vikao vyake kikatiba na kutafuta mawakili wa kuuchunguza mkataba, ambao taayari wameifahamisha CC majuzi kwa maandishi kuwa mkataba ni ufisadi! Na kila mjumbe anayo nakala!

5. Muungwana akamuamuru Nchimbi kwenda Dodoma, haraka kukutana UV-CCM ili waamue kuhusu jina la Nape! Yeye akaenda kupendekeza Nape afukuzwe uanachama!

Now ni vipi mafisadi wanaweza ku-pull this one up mbele ya macho yetu wote wananchi, my reading ni kwamba hakuna mtandao tena ila kuna kundi jipya la mafisadi likiongozwa na Lowassa, yeye mwenyewe ana wasi wasi mkubwa sana mpaka ameshatayarisha alternative ya mtu kuchukua nafasi yake kuliongoza hilo kundi incase something happens to him, swali kama what? Na Kwa nini ana wasi wasi hivi?

Mara ya mwisho muungwana alikuwa Lusaka, akaambiwa kuhusu kusimamishwa kwa Zitto bungeni na matokeo yake jinsi Zitto alivyojengeka kisiasa in one night, alipouliza nani anahusika akaambiwa Lowassa, kwa hasira tena akifoka sana alisema this should be an end to mtandao, the next step mamvi akapandsihwa ndege ya uchumi, waliomuona muungwana kwenye kikao cha CC majuzi wanasema hakuwa yeye wa kawaida,

Hivi karibu nimekuwa nikitumiwa ujumbe mwingi sana in private mzito kuhusiana na thread ya Nape na UV-CCM, tumetumia kila njia kuzi-trace hizo message zinakotoka, mpaka kwenye makampuni ya simu bongo, lakini ni dead end,

Mkuu Mamamia, ninajaribu kuamini kuwa muungwana anwaogopa mafisadi na haweiz fanya kitu, lakini my instinct inakataa kabisaa kwa hiyo nimeamua kuyaaminia maneno yako kuwa kuna moto utawaka huko.... lakini..... I do not know nina feeling kuwa uzi wa mwisho wa mtandao huenda ukakatwa this time, ikawa kila mtu na lwake!

Mtandao uliisha siku nyingi, ilichobaki ni official announcement na ninaamini inakuja this time, I mean mafisadi wakiweza ku-pull this one basi 2010 wametinga, maana huu ndio mtihani wa mwisho kwa muungwana, na believe me analijua hilo, tena sana.
Nasubiri Updates kutoka kwako mkuu na wengine wenye info za ndani.
 
May be Nchimbi amekamata pabaya this time.

Taarifa ni kuwa Nchimbi na Lowassa ndio walibanwa kwenye CC. Nchimbi aliambiwa na wakulu kuwa alichokifanya ni sawa na kutumia bomu la atomiki kuua sisimizi, jambo ambalo halikubaliki popote
 
Unatuambia unachodhani kina make sense au unatuambia facts? Wewe na mwenzio FMES wote hamko sahihi.

Kwanza, Nape amefukuzwa uanachama wa UVCCM. Hakuna utata.

Francis Isaac, Kaimu Katibu Mkuu, UVCCM. TANZANIA DAIMA, Jumatatu, Sept 8, 2008:

"Ni kweli Baraza Kuu limeamua kumfukuza kwenye uanachama wa UVCCM Nape Moses Nnauye, kwa makosa matatu,..."

Mbili, japokuwa Nape aligombea ujumbe wa NEC kupitia tiketi ya UVCCM, na japo ameondolewa UVCCM, yeye bado ataendelea kuwa mjumbe wa NEC.

Yusuf Makamba, Katibu Mkuu, CCM, HABARI LEO, Wednesday, Sept. 10, 2008:
"Katika Katiba ya CCM hakuna sehemu inayoeleza kuwa mwanachama akifukuzwa uanachama na Umoja wa Vijana wa CCM lazima afukuzwe uanachama na kuvuliwa ujumbe au madaraka aliyonayo,"

Tatu, kilichopendekezwa ni Nape kuvuliwa nafasi nyingine za CCM nje ya UVCCM, ikiwemo ya Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Ofisi Ndogo Makao Makuu CCM, Lumumba, na ujumbe wa NEC.

Francis Isaac, Kaimu Katibu Mkuu, UVCCM. NIPASHE, Jumanne, Sept. 9, 2008:
``Kanuni zinaturuhusu kumfukuza, UNEC wake tumependekeza CC (Kamati Kuu) kumvua,...``

Habari ndio hiyo.


Masatu na FMES mmeghafilika.

Kuhani upo sahihi...isipokuwa hapo mwisho; CC haina mamlaka ya kumvua, ila inapendekeza NEC then ni jukumu la NEC kuamua. NEC ndio yenye jukumu la mwisho kwa uelewa wangu.


NEC-UVCCM wana uwezo wa kumfuta Mwanachama yoyote wa UVCCM; hawapeleki mapendekezo kokote kuomba afutwe Uanachama wa UVCCM. Na mpaka sasa Nape kwa mujibu wa kikao cha juzi cha NEC-UVCCM sio mwanachama wa UVCCM.

NEC-UVCCM wamepeleka mapendekezo CC kuomba avuliwe ujumbe wa NEC na Ukurugenzi...hayo ndio majibu tunayoyasubiri.

Pia, hakuna ULAZIMA wa maamuzi ya "KUMVUA UANACHAMA WA JUMUIYA YA UVCCM" yathibitishwe na NEC TAIFA. Lakini NEC Taifa ina Madaraka ya "KUAGIZA" maamuzi "YOYOTE" yaliyofikiwa na UVCCM kupitia vikao vyake yatenguliwe.

Mwisho: Nape mpaka dakika hii ni kwamba "ALIKUWA" mwanachama wa UVCCM unless NEC waagize NEC-UVCCM watengue uamuzi huo.
 
Nimesoma kwenye magazeti ya leo huyo Francis anasema kuwa jana ndio alikuwa anaandaa MAPENDEKEZO ya baraza kuu la kumvua Nape uanachama ili ayapeleke kwenye ngazi za juu, labda walichemka mwanzo walipotangaza kuwa wamemfuta uanachama. Kama ingekuwa iamuzi wa baraza ni final, nadhani Francis angepeleka TAARIFA na si MAPENDEKEZO
 
Nimejaribu kutafuta katiba ya UV-CCM, sijaipata......nataka kujua hiyo timu inayodai imemvua Nape uanachama wa UV-CCM madaraka/uwezo ya/wa-ke ya/u-koje...........tafadhali kwa atakayekuwa nayo naomba aweke hivyo vipengele......................kwa upande mwingine

"Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na uwezo wa kushauri, kutoa
maagizo ya jumla, na maelekezo maalum kwa Jumuiya zinazoongozwa na CCM."
...............ofcourse UV-CCM ikiwemo
 
Nimejaribu kutafuta katiba ya UV-CCM, sijaipata......nataka kujua hiyo timu inayodai imemvua Nape uanachama wa UV-CCM madaraka/uwezo ya/wa-ke ya/u-koje...........tafadhali kwa atakayekuwa nayo naomba aweke hivyo vipengele......................kwa upande mwingine

"Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa itakuwa na uwezo wa kushauri, kutoa
maagizo ya jumla, na maelekezo maalum kwa Jumuiya zinazoongozwa na CCM."
...............ofcourse UV-CCM ikiwemo


Kwa mujibu wa kipengele hicho 108(13)(i) cha Katiba ya CCM lolote litakaloandikwa kwenye katiba ya UVCCM halitaipa UVCCM nguzu zaidi ya hiyo.
 
Kikwete majaribu (Raia Mwema)

Mwandishi Wetu Septemba 10, 2008

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) bado kinasukwasukwa, na safari hii tatizo kubwa ni hatua ya Jumuiya ya Vijana wa chama hicho (UVCCM) kutangaza kumtema mwenzao, Nape Nnauye, Raia Mwema imeambiwa.

Nnauye, mtoto wa mwanasiasa maarufu, Moses Nnauye (sasa marehemu), amekuwa katika chati za juu za vyombo vya habari kwa muda sasa tangu atangaze kuwania uenyekiti wa UVCCM ambao sasa unashikiliwa na Emmanuel Nchimbi anayeondoka kwa sababu ya umri.

Wiki hii, taarifa ya Nchimbi ilieleza kwamba Nnauye amefutwa uanachama wa UVCCM kwa kukiuka kanuni za umoja huo na taarifa zaidi zimekuwa zikisema kwamba sasa suala lake itabidi lifike katika ngazi nyingine za juu za chama hicho tawala; Kamati Kuu na Halmashauri Kuu, kwa kuwa yeye mwenyewe amekuwa akisema UVCCM si mwisho.

Dhambi ya kijana huyo ni maoni yake kwamba kulikuwa na walakini na dalili za ufisadi katika uamuzi wa uwekezaji katika kiwanja cha umoja huo, Barabara ya Morogoro, Dar es Salaam na kwamba Bodi ya Wadhamini haikuwa imetenda haki katika kutoa kiwanja hicho.

Baadhi ya wanasiasa, wakongwe na wengineo, wamekuwa wakiuona uamuzi wa kumfukuza kijana huyo kama unaorudisha nyuma demokrasia iliyokwisha kuanza kujijenga ndani ya CCM na ambayo chama hicho kimekuwa kikiiimba sana nje ya mtandao wake.

Wanasema hatua hiyo ambayo imekuwa ikitangazwa sana na Katibu Mkuu Yusuf Makamba ni kama inaashiria kwamba Nnauye, kwa kusema maoni ya moyoni mwake, ametenda dhambi kubwa kushinda zote ndani ya chama hicho na ambayo haisameheki.

Makamba, ambaye naye amekuwa akipingwa na baadhi ya watu ndani ya CCM wengine wakipendekeza apumzishwe kwa kuwa katika kipindi chake kifupi cha ukatibu mkuu kimeshuhudia maamuzi kadhaa ya kupindapinda, ameviambia baadhi ya vyombo vya habari kwamba Nnauye, hawezi kusamehewa hata mbinguni.

Amenukuliwa Makamba akisema kuhusu kufukuzwa huko kwa Nnauye: "Imeandikwa kwenye Biblia kwamba mtakaowafungia duniani wamefungiwa na mbinguni".




Jaji Joseph Warioba

Baadhi ya waliozungumzia suala hilo ni pamoja na Jaji Joseph Warioba, kijana wa zamani na mwanasiasa mkongwe ambaye ameiambia Raia Mwema kwamba haya yaliyofanyika kwa Nnauye, kama hatimaye ndiyo yatakayopitishwa, yatakuwa yakienda nje ya utaratibu wa chama anachokijua yeye.

Alisema Warioba: "Kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) nilichokuwa nakijua, kwa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) niliokuwa naujua, sikutarajia wangechukua hatua kama hiyo na kwa sababu walizotoa.

"Kama alitoa kauli za kupinga jambo lililokuwa linahusiana na Umoja huo si ajabu. Mbona ndani ya CCM kwenyewe kumekuwa na kauli nzito zilizosemwa na watu hao hawakufukuzwa, bado wamo."

Aliongeza Warioba katika mahojiano ya simu kuhusiana na hatua hiyo: " Lakini kweli yeye anaweza kuwa ameusema vibaya UVCCM au CCM kushinda Wapinzani ambao wamekuwa wakitusema vibaya muda wote?

"Na licha ya kusemwa huko na Wapinzani sisi wenyewe mbona tumekuwa na utaratibu wa kuwasaka mamluki katika Upinzani, waliotukana sana CCM, kwa mbwebwe tukawakumbatia katika chama?

"Sasa lipi ni zito, kumkumbatia kwa mbwembwe aliyekuwa akiitukana sana CCM nje akiwa mpinzani, ambaye amekaribishwa kwa vifijo, au mwanachama anayeamua kusema kile kilichokuwa kinasemwa na hao tuliowachukua kutoka Upinzani?

"Mtindo huu maana yake ni kwamba aliyeko nje anakaribishwa, aliyeko ndani anafukuzwa. Na bahati mbaya Katibu Mkuu amehusika sana katika hili. Amekuwa akikaribisha wapinzani. Kwa mwendo huu wana CCM watatupwa nje, wapinzani ndio watakuwa wana CCM.

"Demokrasia yetu ndani ya CCM imekwenda wapi? Hili ni suala la Vijana, inakuwaje Katibu Mkuu analivalia njuga? Na wala si Vijana tu, hata jumuiya nyingine za CCM zimeingiliwa sana katika siku za karibuni na CCM yenyewe. Ni kana kwamba kuna mpango wa kuengua baadhi kwenye chama na kutafuta wengine".




Cleopa Msuya

Juzi mkongwe mwingine Cleopa Msuya alieleza kushangazwa kwake na uamuzi wa kumfukuza Nnauye akisema kwamba naye alikuwa ametafuta sababu za hatua hiyo bila mafanikio.

"Wangekuwa angalau wamemsimamisha (awali) uanachama wa Umoja wa Vijana tungeshangaa kidogo, lakini kumfukuza… nimeshangaa… wanaposema avuliwa nyadhifa zote maana yake nini? Yule ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, kofia hiyo nayo avuliwe? Hapa hoja ni kosa lake la kuhoji mradi wa jengo la UVCCM au kuna jambo jingine," amekaririwa akisema mzee Msuya.

Lakini wachungzi wa mambo wameiambia Raia Mwema kwamba hatua hii ni matokeo ya kuiva kwa migongano ya kimakundi yanayoendeshwa ndani ya CCM ya leo ya wanasiasa wafanyabiashara na wapambe wao na mengine yenye kutafuta wala haki kidogo.

Wanasema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwamba makundi haya si tu kwamba yamemyumbisha Katibu Mkuu, bali yanamsukasuka hata Mwenyekiti, Jakaya Kikwete.

"Ni makovu ya mchakato wa uchaguzi uliopita. Anaposimama Nnauye akasema wazi kwamba Mwenyekiti wa Wadhamini UVCCM, Edward Lowassa anahusika katika sakata ya kiwanja, usitarajie Lowassa au wapambe wake, ndani ya UVCCM na nje watakaa kimya," anasema mwanasiasa mmoja akiongeza kwamba Lowassa na Nnauye ni sura wakilishi za makundi mawili makuu kinzani ndani ya CCM.

Anaongeza mwanasiasa huyo: " Kwamba Nnauye ameanika suala hilo la jengo na ukweli kwamba kuna timu ya wanasheria kuhusiana na mradi huo na ukweli pia kwamba katika uchaguzi wa mwaka 2005 Nnauye hakuonekana kuwa upande wa Mwenyekiti wa sasa, maamuzi yoyote ya juu yataangalia zaidi mlengo huo".

Mjumbe mmoja wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) wa Kanda ya Ziwa ameiambia Raia Mwema kwamba alichofanya Nnauye ni kama "kuchokoza tu, lakini mikakati ilikuwa inakwenda kwa siri na kichinichini na inakwenda mbali zaidi hadi katika kuwashughulikia wale wote wanaohusika na kupiga vita miradi kama hiyo ya jengo la Vijana".




Mwenyekiti wa Wadhamini UVCCM, Edward Lowassa

Kabla ya sakata la Nnauye kufikia hapa lilipo, skandali zilizokuwa zimeshika uongozi ni pamoja na za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mradi hewa wa umeme wa Richmond ambayo ufumbuzi wake haujakata kiu yote ya wengi.

"Rais alipozungumzia Richmond kwa wepesi na kuona kama hakuna makosa, tulichanganyikiwa. Baadaye Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasilisha taarifa ya Serikali ilikuwa ni kana kwamba Serikali imebadili mwelekeo," anasema mbunge mmoja.

Kuhusu suala la Nnauye mbunge huyo ambaye ni mjumbe wa NEC, alisema kwa siku kadhaa kabla na baada ya kikao cha UVCCM kuchukua uamuzi wa kumdhibiti Nnauye, kulikuwa na heka heka nchi nzima na baadaye kuhitimishwa na matumizi makubwa ya fedha katika kuhakikisha kijana huyo anadhibitiwa.

"Waliwatafuta wenyeviti wa mikoa wa UVCCM, wakimtumia mwenzao mmoja na baadaye kumtumia mbunge mmoja kijana katika kufanikisha hilo. Kwa kweli nimethibitishiwa kuhusu fedha zilizomwagwa," anasema mjumbe mmoja wa Baraza Kuu la UVCCM.
 
Kumbe tuna deal na waarabu wa Pemba.....

2lk5svo.jpg



Haya mie yangu macho....


s4mgxd.jpg
 
Kumbe tuna deal na waarabu wa Pemba.....

2lk5svo.jpg



Haya mie yangu macho....


s4mgxd.jpg



Huyo jamaa wa kushoto Kapt Komba si anatafutwa na Polisi kwa kufanya vurugu katika Uchaguzi wa Kiteto? Au Polisi wamefuta kesi kwa kukosa ushahidi?
 
Jamani hili TABASAMU ni la kweli??

Hii picha ni leo kwenye mkutano wa NEC.

2lk5svo.jpg


Hili tabasamu wakiwa kwenye kikao cha nec leo kikiendelea.

s4mgxd.jpg

Jamaa wanabadilisha mawazo lakini inaonekana mmoja anakubali kwa shingo upande atafanya nini...
 
Jamani kuna mwenye taarifa ya kilichojiri Dodoma leo kwenye kikao naona picha tu sijui za leo? hebu leteni nyeti hizo tumekaa mkao wa kula hapa!
 
mioyoni mwao huwezi jua!hapo wanatabasamu ni kufunika kombe mwanaharamu apite
 
Back
Top Bottom