Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Sakata la Nape Nnauye na UVCCM

Tazama inawezekana kabisa hapo imetumika lugha na usiku iliwakilisha hali ,kama unavyojua Usiku ni unawakilishwa na kiza totoro sasa kama mkataba haukujulikana wapi ulisainiwa ,majukumu hayakufuatwa watu wamesitukia tu asubuhi jamaa wanachimba hazina,huoni kama mipango ilikuwa haikuonekana kila watu wakitafuta wanaona kiza tu.
Wewe hauko sawa huwezi kutumia ligha ya picha au lugha ya kifasihi ktk gazeti,ammaanisha usiku wa muda.....mkataba haujasainiwa bali ni MoU.hivi ni vitu viwili tofauti.
 
Mwanahalisi limekubwa na misukosuko mingi sana ,sasa sijui kama litaendelea ama laa kwani limekuwa na kesi nyingi.

Moja ya kitu cha msingi MwanaHALISI wanahitaji ni uwakilishi mzuri zaidi wa kisheria. Mwanasheria wake anafanya miscues fulani ambazo zinaweza kuboreshwa zaidi.

Kwa mfano, Kubenea alipohojiwa kuhusu uhalali wa utoaji taarifa za akaunti za watu, aliiambia KLH News kwamba wao hawatoi akaunti za "walima Kahawa wa vijijini," na wa wananchi wa "huko Buhemba" na kwingineko. Ila ni viongozi fulani fulani wa nchi. Sasa, huhitaji kuwa mwanasheria kujua kwamba, kama ni makosa kuvujisha akaunti za benki - assuming ndilo kosa - basi ni wazi kwamba kila mteja mwenye hizi akaunti analindwa na sheria ya nchi, na sio mlima Kahawa tu. Wakili wake hatakiwi kumruhusu atoe justification kama hivi za kujifunga kitanzi.

Mfano mwingine, wakili aliyeitwa kuja eneo la tukio, hakutakiwa kuruhusu isainiwe search warrant inayomtafuta "Msaki and others." Msaki hakuna anae mjua hapo MwanaHALISI. Na hao "others" wanaweza kuwa wako kwenye sayari ya Zebaki (kama ambavyo Kishoka huwa anasema.)

Hizi nadhani ni faux pas zinazoweza kuboreshwa zaidi. Humo ndani pia wawe na watu wanapitia vitu wanavyoandika. Vinginevyo wanaweza kuishia kulipa mapesa kama yale ya Sumaye. Tukikosoa press ya Bongo ni katika kujaribu kuijenga vile vile.
 
Sasa kama Kubenea alikuwa na akli atakuwa anao ule mkanda ambao utaonyesha mkutano wake na Lowassa ambao alkubaliana na Lowassa apewe pesa ili a back down huku ofisi ya waziri mkuu ikiendelea kumtafutia matangazo

wasi wasi wangu ni kuwa KUBENEA isnt that sophisticated kama ilivyoelezwa miezi kadhaa iliyopita kuwa:
3. Saed Kubenea – Stan Katabalo impostor, only without the education, the sophistication, the principles and steely determination for which Katabalo is remembered for. A little Kingmaker in the making, if only he would be aware that he needs to stop being a pawn in the great political game. He gets direct congratulatory calls from Sumaye, Magufuli, Butiku, Warioba and others whenever his paper comes out. He is welcome at Salim A. Salim house. This is such an awesome achievement for a person who is half-schooled and who has never read any major literary work of non-fiction (and who might not get this joke). That our politicians would embrace Kubenea, who still milks the "acid incident", speaks of the level of their desperation to smear each other (in the name of "saving the country").
 
Hivi bado Lowasa ambaye alitakiwa kuwa jela bado ana nguvu? Mimi nilifikiria nguvu yake iko CCM hata huku nje? Lowassa asiwatishe kama ni makosa atakuwa nayo tu.
 
Wanabodi,
Kwanza kabisa nitasema hakuna sheria yoyote inayozuia vyombo vya habari kutoa Account za watu iwe amount ama namba zake dunia nzima ikiwa kuna ukweli wa kuwepo hizo account.
Kama kuna uvujaji wa habari hizi toka Benki inayohusika basi ndiko kunakotakiwa kuelekezwa mashtaka ama upelelezi..
Hadi sasa hivi nachoona ni Ubabe wa viongozi wetu lakini kisheria sioni kabisa sababu ya kulishtaki gazeti ati kwa kutoa account za watu as if hayo magazeti ndio wanaomiliki hizo account..
Mkataba wa siri za account upo kati ya mwenye account na benki, Mwanahalisi anaweza kuwa shahidi kuonyesha kwamba siri hiyo imevunjwa..
 
Sasa mahakama imewapaje search warrant ambayo ina neno "criminal" something, kama ambavyo Kubenea alitamka redioni?

Unajua katika sheria sio busara kuseme lolote kabla hujaona, sio tu shitaka, bali hata ushahidi, ambao mwenzio atakuja nao mahakamani. Huwezi kuanza kusema hakuna kesi hapa wakati hujui mwenzio analalamika nini.

Ingekuwa ni nchi yenye viable press tungekuwa tumeshafahamu yule Jaji alitoa search warrant kuhusiana na uvunjaji wa sheria gani. Bahati mbaya press yenyewe ndio hivyo tena.
 
"MASWALI MAGUMU"
Hakika, kesi hii itamdhalilisha sana Lowassa tena kwa muda mrefu usiotabirika kuanzia sasa. Ningekuwa mshauri wake ningemwambia "mzee mezea tu!" Kama ilivyokuwa kwa Richmond, katumia jazba, anakwenda mahakamani! Sasa itabidi ajibu mahakamani maswali magumu yafuatayo kwa ukamilifu:
(a) Je, kwa nini utekelezaji wa mradi wa jengo la vijana umeanza bila mkataba mahsusi kusainiwa kwanza?
(b) Je, alitumia vigezo vipi kumwingiza Bosi wa Tan Roads, Mrema, kwenye kampuni ya Vijana Development Corporation?
(c) Je, kwa nini alimtoa Mhe. Wilson Masilingi kwenye Baraza la Wadhamini la UVCCM bila sababu wala taarifa yoyote?
(d) Je, alitumia msingi upi kumteua fisadi Nazir Karamagi kuziba nafasi ya Masilingi?
(e) Je, kwa msingi upi mwekezaji amepewa asilimia 75 ya ya umiliki wa kiwanja (ardhi) bila kibali cha Kabidhi Wasii wa Serikali?
(f) Je, uhalali wa utekelezaji wa mradi huu unatoka wapi wakati wenye mali, Baraza Kuu la UVCCM, hawakuridhia?
(g) Je, kulikuwa na Mkataba wa Utekelezaji au MOU tu? Kama ni MOU tu, basi jibu katika (a) hapo juu linatosha. Ikiwa kuna Mkataba wa Utekelezaji, kama MwanaHalisi na wanasheria wake wanavyodai, kwa nini Lowasa na wenzake wasishitakiwe kwa udanganyifu?
Yapo maswali mengine mengi ambayo Lowassa atalazimika kuyajibu atakapotinga mahakamani. Nachelea kusema, Lowassa atashindwa kuyajibu kwa kinaganaga maswali yote! Lazaros
 
Moja ya kitu cha msingi MwanaHALISI wanahitaji ni uwakilishi mzuri zaidi wa kisheria. Mwanasheria wake anafanya miscues fulani ambazo zinaweza kuboreshwa zaidi.

Kwa mfano, Kubenea alipohojiwa kuhusu uhalali wa utoaji taarifa za akaunti za watu, aliiambia KLH News kwamba wao hawatoi akaunti za "walima Kahawa wa vijijini," na wa wananchi wa "huko Buhemba" na kwingineko. Ila ni viongozi fulani fulani wa nchi. Sasa, huhitaji kuwa mwanasheria kujua kwamba, kama ni makosa kuvujisha akaunti za benki - assuming ndilo kosa - basi ni wazi kwamba kila mteja mwenye hizi akaunti analindwa na sheria ya nchi, na sio mlima Kahawa tu. Wakili wake hatakiwi kumruhusu atoe justification kama hivi za kujifunga kitanzi.

Mfano mwingine, wakili aliyeitwa kuja eneo la tukio, hakutakiwa kuruhusu isainiwe search warrant inayomtafuta "Msaki and others." Msaki hakuna anae mjua hapo MwanaHALISI. Na hao "others" wanaweza kuwa wako kwenye sayari ya Zebaki (kama ambavyo Kishoka huwa anasema.)

Hizi nadhani ni faux pas zinazoweza kuboreshwa zaidi. Humo ndani pia wawe na watu wanapitia vitu wanavyoandika. Vinginevyo wanaweza kuishia kulipa mapesa kama yale ya Sumaye. Tukikosoa press ya Bongo ni katika kujaribu kuijenga vile vile.
Umeshauri vyema na nimekupata safi mkuu, nadhani kwa akili zangu uko sawa kabisa. Majibu kama yalikuwa hayo inatakiwa marekebisho ya haraka maana hao mafisadi wako macho sana upande huo. Hata hivyo yawezekana Kubenea alikuwa akiendeshwa na hasira za nchi kuliwa na yeye kuulizwa kwanini atoe taarifa kwamba nchi inaliwa. Alikuwa anataka kuwalenga wahusika "on the spot", lakini kisheria pale aliteleza kidogo. Nadhani anahitaji kupunguza munkari ili apate stamina ya kuongea maana nadhani haya hata yeye akitafakari anaweza kuwajibu vyema zaidi. Kuhusu search warranty yaonekana ni mtego na wao kwa vile walivamiwa wakashikwa na hasira wakashindwa kutulia na kufikiria, hutokea hivyo. NADHANI KUBENEA ANAHITAJI KUPUNGUZA KASI YA KU-REACT ANAPOPATA JAMBO KAMA HILI maana wanamtafuta akosee ili wampate...!
 
Moja ya kitu cha msingi MwanaHALISI wanahitaji ni uwakilishi mzuri zaidi wa kisheria. Mwanasheria wake anafanya miscues fulani ambazo zinaweza kuboreshwa zaidi.

Kwa mfano, Kubenea alipohojiwa kuhusu uhalali wa utoaji taarifa za akaunti za watu, aliiambia KLH News kwamba wao hawatoi akaunti za "walima Kahawa wa vijijini," na wa wananchi wa "huko Buhemba" na kwingineko. Ila ni viongozi fulani fulani wa nchi. Sasa, huhitaji kuwa mwanasheria kujua kwamba, kama ni makosa kuvujisha akaunti za benki - assuming ndilo kosa - basi ni wazi kwamba kila mteja mwenye hizi akaunti analindwa na sheria ya nchi, na sio mlima Kahawa tu. Wakili wake hatakiwi kumruhusu atoe justification kama hivi za kujifunga kitanzi.

Mfano mwingine, wakili aliyeitwa kuja eneo la tukio, hakutakiwa kuruhusu isainiwe search warrant inayomtafuta "Msaki and others." Msaki hakuna anae mjua hapo MwanaHALISI. Na hao "others" wanaweza kuwa wako kwenye sayari ya Zebaki (kama ambavyo Kishoka huwa anasema.)

Hizi nadhani ni faux pas zinazoweza kuboreshwa zaidi. Humo ndani pia wawe na watu wanapitia vitu wanavyoandika. Vinginevyo wanaweza kuishia kulipa mapesa kama yale ya Sumaye. Tukikosoa press ya Bongo ni katika kujaribu kuijenga vile vile.

Nakubaliana na wewe hapo kwenye haki za wateja.
Lakini sparks za REVOLUTION HUANZA kama hivyo...Inanikumbushia ile commercial ya zamani ya maumivu ya kichwa huanza pole pole.
Ukweli hapa ni kwamba wakijaribu kumnyanyasa Kubenea zaidi ya madhara ambayo wameshampatia..Basi ndugu yangu wanaweza kuamsha hisia na nguvu ya umma.
Na hapo the spark will lead to FIRE...TRUST ME.
 
Mushi njoo kule kwa Mziray.

Hayo mambo ya chadema mimi simo tena.
Nimeshatowa ushauri wangu kama vile nilivyofanya kabla hawajakupa umakamu wenyekiti.
Na hivyo basi mimi nawaambia kuwa chadema kinaelekea kusambaratika kama hatua madhubhuti hazitachukuliwa.
 
Hatua zimechukuliwa kusimamishwa makamu mwenyekiti, usijitoe Mangi atabaki nani Chadema kama na wewe utajitoa? au unataka kupunguza namba ya watu wa kilimanjaro ili chama kiwe na sura ya kitaifa kuliko ilivyo sasa kinaonekana chama cha mkoa wa kilimanjaro.

njoo bwana Mangi kule kwa Mziray na ripoti yake kamambe ambayo imejaa umahiri wa kiwango cha kimataifa.
 
kama mkataba haujasainiwa kwa nini mwekezaji kaanza kujenga kwa kweli lowasa kashikwa pabaya
 
Kuhani,

Mkuu kilichotumika ni maguvu hakuna haki wala sheria inayoweza kuruhusu chombo cha habari kivamiwe kwa sababu wana report za account za mtu fulani.. unless bank wenyewe wawe washtaka kwa kuibiwa report za account hizo. Hizi report zimevujishwa benki na zipo mikononi mwa wananchi kibao acha mbali Mwanahalisi..

Mkuu hata JF ilivamiwa na pengine search warrant ilitolewa lakini haina maana kabisa kwamba kulikuwepo na haki ama sheria kuvamia ofisi ya mtu kutokana na tetesi za mtaani ama malalamiko ya kiongozi fulani kuhusiana na maisha yake. Kama huamini ebu nambie, iweje mkuu wa Upelelezi alikubali kutoa samahani kwa vijana wetu na hata ktk vyombo vya habari kwa kitendo walichokifanya!..Na ilikuwaje Taasisi zote za haki za utoaji habari wali laani kitendo hicho cha kuvamia na kuwakamata vijana wale..! Huu Uhuru unaozungumziwa ni Uhuru gani kwa maoni yako!..

Mkuu sio mara moja wala haitakuwa mara ya mwisho kwa vyombo vya usalama ana mahakama zetu kutmiwa vibaya na viongozi hasa mafisadi..

Leo ktk kuangalia kipindi kimoja kinachohusiana na Urusi kuna msomi mmoja alisema.. haya..

Katika harakati za mageuzi ya uchumi na hasa pale demokrasia inapotakiwa.. Hatua ya kwanza ya mageuzi hutokea makundi ya MAFISADI wakaichukua nchi kiuchumi..Hofu na mashaka ktk future ya nchi hujitokeza kwa haraka sana na hivyo viongozi makini hujitokeza, viongozi ambao huchukua mkondo wa Kidikteta kwa malengo ya kupambana na adui wa ndani (Ufisadi)..

Vita hii huwa kubwa sana, viongozi wengi huondoka, watu wengi hupoteza mali zao, sheria nyingi huvunjwa, Consumption hupanda kuisukuma demand juu kiasi kwamba mabadiliko ya haraka huwa hatari ya maendeleo ya nchi hizo...blaa blaa blaa na mwisho alisema

"Ni vigumu kupata demokrasia ya kweli ktk Taifa lisilokuwa na Malengo zaidi ya Utajiri!..."
 
lowassa ananuka ufisadi ......hadi ndani ya chama!
mwache aende mahakamani ili atuwekee na mengine wazi zaidi
 
Tunamjua ni muoga sana kwenmda mahakamani....maana kulee yatasemwa yote na atashangaa na kambi yake...hakika muda wa yeye kutuachia nchi yetu safi umefika kila deal yumo tu ina maaana yeye ndio anajua sana pesa kuliko wengine?hatumtakiii.....atoke hata kwenye chama....tutakutana nae mahakamani......
 
huu ni mchezo wa kuigiaza. wakati wanasema mkataba haujasainiwa jengo limesha anza kujengwa... jamani mbona wanatuona mambumbu sana?
 
Hivi bado Lowasa ambaye alitakiwa kuwa jela bado ana nguvu? Mimi nilifikiria nguvu yake iko CCM hata huku nje? Lowassa asiwatishe kama ni makosa atakuwa nayo tu.

Naweza kusema kuwa kuna concesus among mafisadi kuwa Kubenea anatakiwa kuondolewa kwenye ulingo wa habari. Na kimsingi hilo ni kama linasubiri tu window of opportunity, kama ikitokea kweli atapelekwa mahakamni keshi yake itakuwa kama ile ya Ditopole, yaani hukumu tayari imepangwa ni kufuata formalities tu.
Hapa kwetu ni kawaida kabisa kwamba mwenye nguvu ndio mwenye haki, hakuna ile gibberish ya kusema sheria ni msumeno. Kubenea sasa hivi anatakiwa aangalie sana vidole vyake, mdomo wake na mgongo wake. Sitashangaa kusikia kuwa Lowassa anashinda na Kubenea anashindwa.
 
Back
Top Bottom