Bibi Ntilie
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 245
- 8
Hivi sasa nchi imefika pabaya, Chama Tawala nacho kimefika pabaya kiasi kwamba kinaonyesha wazi-wazi kukumbatia maovu! Wanatakiwa watu jasiri kuweza kuonyesha kidole bila woga. Wazee wa CCM wamekaa kimya labda nguvu za ujasiri zimewaishia. Vijana wa CCM ambao wana uchungu wa dhati na wanalitakia mema taifa lao na Chama chao wanapaswa kusimama imara na kuunga mkono mwenzao anayeonyesha ujasiri wa kupambana na uovu uliopo. Hata kama Nape anafanya kampeni za kuutaka uenyekiti wa UVCCM, ameonyesha ujasiri mkubwa. Nape ni jasiri. Anastahili pongezi maana ni wachache wanaoweza kujitokeza na kuwanyooshea vidole watu 'wanaoogopwa' kwa mengi!