Sakata la JATU PLC lazidi kupamba moto, Serikali yaingilia kati mgogoro wake na wanachama

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,943
25,284
jatu_logo - Copy.png


Serikali imesema inaifuatilia Kampuni ya Jenga Afya Tokomeza Umasikini (Jatu PLC) baada ya baadhi ya wanachama wake kudai kutapeliwa mamilioni ya fedha waliyowekeza katika miradi ya kilimo. Kwa mujibu wa tovuti ya Jatu PLC, kampuni hiyo inayowaunganisha wakulima na kuwawezesha kulima kisasa, hununua mavuno yote na kuandaa bidhaa ambazo huuzwa kwa wanachama wake kupitia mfumo wanaouita Jatu Market.

Akizungumza na Gazeti la Mwananchi kwa simu Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde alisema "Serikali imesikia malalamiko hayo na inapanga kuwaita wanachama hao na uongozi wa Jatu. Hayo malalamiko tunayajua na tunayashughulikia. Tutatenga muda wakulima kutoa maelezo yao rasmi halafu tuwaite viongozi wa Jatu", alisema Mavunde.

Alipopigiwa simu mkurugenzi wa Jatu, Peter Isare kuzungumzia madai hayo, aliikata. Hata hivyo, mkurungenzi wa sheria wa kampuni hiyo , Mohamed Simbano alipokea simu akisema "Nafikiri kwa sasa hilo nisingependa kulizungumzia kwa sababu limeshajadiliwa kwenye kikao cha Jumamosi , Wakulima walikuwepo, upande wa Serikali ulikuwepo na tayari tulifanyia kazi ndani na wakulima wanafahamu"

Malalamiko ya wanachama

Katika kikao na mkurugenzi wa Jatu kilichofanyika mwisho wa wiki iliyopuita jijini Dar es Salaam walihoji sababu ya kucheleweshewa malipo yao na kutaka waonyeshwe mazao yanayodaiwa kuweka ghalani. "Sisi tumelima mazao wengi wetu ni eka 50, hayo mazao umeyaweka wapi ? TUngependa tupate wawakilishi wayaone hayo mazao. Maana ni eka na eka, hayo mazao unawekeza wapi?" Alihoji mwanachama wa Jatu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

"Watu wanahitaji mazao, wanahitaji mchelewe, wanahitaji, maharage, tupe tukauze wenyewe. Mimi nililima gunia 50 nipe nikauze mwenyewe". Pia alihoji sababu ya malipo kuanza kutolewa kwa wanachama waliokopa Saccos ya kampuni hiyo huku waliowekeza fedha zao wakitakiwa kusubiri. "Umesema unawapa kipaumbele watu waliowekeza kwa mara ya pili na watu wa Saccos, lakini watu wa malipo umewaweka mwhiso, hapo tunataka kujua kwa nini ? Hapo hakuna haki, kwa hiyo wewe unajilipa kwanza halafu sisi tuwe wa mwisho, siyo sawa kabisa" alisema mwanachama huyo.

Moses Lukoo amabaye ni mwajriiwa wa Jatu, alisema malalamiko hayo yalizuka baaada ya wanachama kudai kuzungushwa kwa muda mrefu. "Kimsingi viongozi walisema wanachama wamekuwa wengi kwa miaka ya hivi karibuni wakiwalipa wote kwa pamoja kampuni itakufa, itashindwa kulipa kodi, mishahara ya wanfanyakazi," alisema Moses aliyedai kuwekeza Jatu Sh14 Milioni.

Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Bhavika Mwesiga alidai kuwekeza zaidi ya Sh 103.92 Milioni kwa ajili ya kulimiwa eka 110 zilizopo wilayani Kilindi Mkoa wa Tanga/ "Mara ya kwanza niliwekeza Sh43 Milioni ilikuwa mwaka 2019 wakasema nitalipwa na faida ya miezi sita nikaambiwa fedha iliyopatikana imewekezwa tena. Mwaka 2020 niliona niwekeze fedha zaidi Sh60 milioni nikiamini kuwa daida itakuwa kubwa zaidi. Sikuwa na wasiwasi nao kwa sababu kwanza wamesajiliwa soko la hisa. Lakni tangu wakati huo, imekuwa ni kuzungushwa tu" alisema BHavika, ambaye kwa sasa anaishi Marekani.

Alisema alifuatilia malipo yake katika kampuni hiyo na kupewa invoice inayoonyesha kuwa anatakiwa kulipwa Sh 143.92 milioni ambazo ni mtaji na faida yake. "Nimekuwa nikimpigia simu mkurungenzi na kumweleza malipo yangu. Awali, alikuwa akipokea simu na kujibu meseji, lakini siku hizi hapokei wala hajibu mseseji. Mume wangu ni mgonjwa mimi ndiye ninayetunza watoto natakiwa kuwalipia ada, fedha yote ndioyo imekwama Jatu PLC." Alisema Bhavika.


Alkelaus Ishengoma anayedai kuwekeza zaidi ya Sh40 ikiwa ni mtaji na faida, alisema viongozi wa Jatu wamekuwa wakiwachanganya kwa maelezo yao, jambo alilosema linaleta hisia ya utapeli. Alitoa mfano wa mkutano wa wanachama uliofanyika Juni 1, 2021 akisema mkurugenzi wa kampuni hiyo (hakumtaja jina) alitangaza kuwepo kwa mavuno makubwa kwa mwaka huo. "Watu walitegemea mavuno mazuri kwa sababu hali ya mvua ilikuwa nzuri, lakini wakati wa kutangaza mavuno ya maharagwe, Jatu ilisema yalipatikiana magunia manane kwa kila eka. Mwaka 2020 kila eka ya maharagwe ilitoa magunia 13 tena chini ya makisio ya magunia 15 kwa eka moja"

Takukuru kuingilia kati

Akizungumza katika televisheni ya mtandao wa Youtube ya Clouds Media, Ofisa Uchunguzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) Mkoa wa Ilala, Heri Makawa alikiri kupokea malalamiko ya wanachama wa jatu na wanayashughulikia. "Tuliona hili jambo ni la kufanyia udhibiti. Kwanza tumetoa mapendekezo kwenye kampuni ni jinsi gani wanaweza kudhibiti migogoro, kwa sababu unapotoa huduma hutakiwi kuwa na migogogoro na wananchi," alisema Makawa.

Soma zaidi:
 
Kuna Uzi humu unasema jatu n Mr kuku mwingine ilikuwa suala la muda TU

Na hapo serikali imeshaona akaunt imenona watataifisha zote Kama DECI

Huwa naenda pale sabasaba kila wikend kula kitimoto choma jiran na kijiofis chao nawaona vijana wakiingia na kutoka wengi wao machoni hawana nuru wamechoka
 
Kuna mstari Sir Nature anaimba kua "...Chakalika Mwanaume unazubaa nini? Unataka kimini? Chanini? Mshikaji kua makini.
Mafanikio kwangu ni ubunifu, nimuige Fifte?___ wakati maisha yangu mwenyewe sawa na gari la City..."

Hawa wanaotapeliwa kila siku over and over hua hawajifunzi?? Hakuna Mafanikio bila ya kusumbuka mwili na akili
 
Kuna mstari Sir Nature anaimba kua "...Chakalika Mwanaume unazubaa nini? Unataka kimini? Chanini? Mshikaji kua makini.
Mafanikio kwangu ni ubunifu, nimuige Fifte?___ wakati maisha yangu mwenyewe sawa na gari la City..."

Hawa wanaotapeliwa kila siku over and over hua hawajifunzi?? Hakuna Mafanikio bila ya kusumbuka mwili na akili

wanapenda mteremko...hela za kudownload..
 
cha kushangaza Jatu imeingia mpaka kwemye soko la hisa DSE .na thamani ya vipande kupanda kufikia juu.hapa na chungulia naona bado hipo kwenye hisa.

inaonyesha target yao walitaka iingie kwenye hisa na kupata share kubwa kwa njia wanazojua wao. ila imestaki
 
cha kushangaza Jatu imeingia mpaka kwemye soko la hisa DSE .na thamani ya vipande kupanda kufikia juu.hapa na chungulia naona bado hipo kwenye hisa.

inaonyesha target yao walitaka iingie kwenye hisa na kupata shara kubwa kwa njia wanazojua wao. ila imestaki
😁
dse - Copy.png
 
Kuna mstari Sir Nature anaimba kua "...Chakalika Mwanaume unazubaa nini? Unataka kimini? Chanini? Mshikaji kua makini.
Mafanikio kwangu ni ubunifu, nimuige Fifte?___ wakati maisha yangu mwenyewe sawa na gari la City..."

Hawa wanaotapeliwa kila siku over and over hua hawajifunzi?? Hakuna Mafanikio bila ya kusumbuka mwili na akili
Mkuu karibu Kilimo cha Vanilla, ni utajiri uliojificha ambao wakulima wa Njombe hawataki wengine waujue😁
vanilla.png
 
Wastaafu ndio easy target ya matapeli.
Tunakumbushana tu, "Ukiona unaitwa kwenye fursa, jua wewe ndio fursa"
 
Back
Top Bottom