Mahakama yagoma kubadili masharti ya Dhamana ya Mkurugenzi wa JATU

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali maombi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya aliyotaka apunguziwe masharti ya dhamana ili aweze kudhaminiwa.

Gusaya anakabiliwa na shtaka moja la kujipatia Sh 5.1bilioni kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo anazipanda ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Mahakama hiyo imesema haiwezi kubadilisha masharti ya dhamana ambayo iliyatoa dhidi ya mshtakiwa huyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 28, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo mahakama hiyo inampunguzia masharti ya dhamana mshtakiwa huyo ili aweze kupata dhamana au inayatupilia mbali maombi yake.

"Mahakama hii imefungwa mkono na haiwezi kubadilisha maamuzi ya masharti ya dhamana iliyoyatoa, kama mnahoja upande wa utetezi mziwasilishe Mahakama Kuu," amesema Hakimu Mrio.

Hakimu Ngimilanga baada ya kutoa uamuzi huo, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo leo aliletwa mahakamani hapo kuja kusikiliza kesi yao.

Itakumbukwa kuwa Januari 2, 2023 mahakama hiyo ilitoa masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo kwa kumtaka kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslimu Sh2.6 bilioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia ilimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha fedha taslimu Sh2.6 bilioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana siku hiyo na badala yake aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba impunguzie masharti ya dhamana ili ajidhamini.

Kupitia mawakili wake wawili, Kung'e Wabeya na Nafikire Mwamboma, mshtakiwa huyo waliomba mahakama hiyo impunguzie masharti ya dhamana kutoka Sh2.6 bilioni alizotakiwa kuwasilisha mahakamani hapo hadi Sh200 milioni au Sh150milioni.

Pia waliomba mahakama hiyo kupitia upya masharti ya dhamana dhidi yake, kwa sababu masharti aliyopewa ni magumu na ndio maana ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Serikali ilijibu hoja zake kwa kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya mshtakiwa kwa maelezo kuwa masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo ni ya haki kulingana na sheria iliyopo.

MWANANCHI
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imetupilia mbali maombi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya aliyotaka apunguziwe masharti ya dhamana ili aweze kudhaminiwa.

Gusaya anakabiliwa na shtaka moja la kujipatia Sh5.1bilioni kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo anazipanda ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Mahakama hiyo imesema haiwezi kubadilisha masharti ya dhamana ambayo iliyatoa dhidi ya mshtakiwa huyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Februari 28, 2023 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Mary Mrio wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya kutolewa uamuzi iwapo mahakama hiyo inampunguzia masharti ya dhamana mshtakiwa huyo ili aweze kupata dhamana au inayatupilia mbali maombi yake.

"Mahakama hii imefungwa mkono na haiwezi kubadilisha maamuzi ya masharti ya dhamana iliyoyatoa, kama mnahoja upande wa utetezi mziwasilishe Mahakama Kuu," amesema Hakimu Mrio.

Hakimu Ngimilanga baada ya kutoa uamuzi huo, ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 13, 2023 itakapoitwa kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo leo aliletwa mahakamani hapo kuja kusikiliza kesi yao.

Itakumbukwa kuwa Januari 2, 2023 mahakama hiyo ilitoa masharti ya dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo kwa kumtaka kuwasilisha mahakamani hapo fedha taslimu Sh2.6 bilioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Pia ilimtaka mshtakiwa huyo kuwa na wadhamini wawili watakao wasilisha fedha taslimu Sh2.6 bilioni au mali isiyohamishika yenye thamani hiyo.

Hata hivyo mshtakiwa huyo alishindwa kutimiza masharti ya dhamana siku hiyo na badala yake aliwasilisha maombi mahakamani hapo akiomba impunguzie masharti ya dhamana ili ajidhamini.

Kupitia mawakili wake wawili, Kung'e Wabeya na Nafikire Mwamboma, mshtakiwa huyo waliomba mahakama hiyo impunguzie masharti ya dhamana kutoka Sh2.6 bilioni alizotakiwa kuwasilisha mahakamani hapo hadi Sh200 milioni au Sh150milioni.

Pia waliomba mahakama hiyo kupitia upya masharti ya dhamana dhidi yake, kwa sababu masharti aliyopewa ni magumu na ndio maana ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Serikali ilijibu hoja zake kwa kuiomba mahakama hiyo kutupilia mbali maombi ya mshtakiwa kwa maelezo kuwa masharti yaliyotolewa na mahakama hiyo ni ya haki kulingana na sheria iliyopo.

MWANANCHI
Hawa wajela jela wa Magufuli wanasumbua sasa wameshapata rais wa kizanzibari

USSR
 
Acha aumie ameumiza wengi, auze lile shangingi la milioni 400 ajidhamini tatizo kajamaa ni kabahili sana
Kabahili kivipi ndugu yetu. Ebu nijuze nijue.

Je unafikiri hizo pesa kakwapua au ni vile alipata hasara kwenye uwekezaji?
 
Acha aumie ameumiza wengi, auze lile shangingi la milioni 400 ajidhamini tatizo kajamaa ni kabahili sana
Kumbe pesa anayo kama inavosemwa, ila ni mjinga angekimbilia Congo huko hakuna mtu angempata
 
Back
Top Bottom