Peter Gasaya, Boss wa JATU apandishwa Mahakamani. Wale mliotapeliwa na JATU poleni

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
18,200
27,255
Jatu ni wale jamaa wa kipindi waliokuna na ule mchezo wa unatoa pesa alafu unalimiwa unauziwa. Mwisho wa siku watu wakatapeliwa.

Hatimaye kaingia kwenye 18, serikali imemkamata na kumshtaki kwa kujipatia bil 5 kwa njia za udanganyifu wa kutapeli watu.

Naipongeza serikali, Ila pia na nyie wabongo wenzangu tumieni akili. Nani akulimie akuuzie, wewe kazi yako kusubiri pesa tu.

Mtatapeliwa hadi lini? Mr.Kuku aliwachapa, Ila hamkusikia, Kuna vanilla aliwachaapa pia, namaingo , akaja Jatu, na Sasa Kuna wale soila.

Mbaya zaidi hawa watu hupata vibaraka na watetezi wengi sana pale wanapoanza huu utapeli, wenye akili wakionya tu basi hushambuliwa.

Naiomba serikali hii iwe mara ya mwisho, wakitapeliwa tena achaneni na hizi kesi. Acheni watu watapeliwe mpaka akili ziwakae sawa

Screenshot_20221229-171452_1.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (katikati) akiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisitu, baada ya kusomewa kesi ya kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.​

  • Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.
Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya (32) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.
Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Alhamisi Desemba 29, 2022 na kusomewa shtaka lake na wakili wa Serikali Tumaini Mafuru, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mary Mrio.
Akisomewa shtaka hilo, wakili Mafuru amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa na kesi ya jinai namba 207/2022 yenye shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Wakili Mafuru amedai mshtakiwa andaiwa kutenda kosa hilo, katika ya Januari Mosi, 2020 na Desemba 31, 2021 katika Jiji la Dar es Salaam, akiwa kama Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, kwa njia ya udanganyifu alijipatia Sh 5,139,865,733 kutoka Saccos ya JATU.

"Mshtakiwa wanadaiwa kujipatia fedha hizo kwa njia ya udanganyifu kutoka Saccos ya JATU kwa kujipambanua kwamba fedha hiyo ataipanda kwenye kilimo na kuzalisha faida zaidi jambo ambalo alijua kuwa sio kweli" amedai wakili Mafuru.
Mshtakiwa baada ya kusomewa shtaka lake, alikana kutenda kosa hilo na upande wa mashtaka umedai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Hakimu Mrio baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote, amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana kwa kesi yenye mashtaka au shtaka linalozidi kiwango cha Sh300 milioni.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Mrio ameahirisha kesi hiyo hadi Januari 11, 2023 itakapotajwa na mshtakiwa amerudishwa rumande.

Chanzo: Mwananchi
 
29/12/2022 Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya( 32) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kujibu shtaka moja la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kiasi cha Sh 5.1bilioni. Gasaya anadaiwa kujipatia fedha hizo kutoka katika Saccos ya JATU kwa madai kuwa fedha hizo atazipanda kwenye kilimo ili kuzalisha faida zaidi, wakati akijua kuwa ni uongo.

Public Limited Company registered with DSE (Dar es Salaam Stock Exchange)
The company was founded by Peter Isare Gasaya, Mohamed Issa Simbano, Mary Richard Chulle and Moses Lukoo William on October 20, 2016 and is headquartered in Dar es Salaam, Tanzania.

JATU PLC​

Dar es Salaam Stock Exchange
Watchlist

Market Closed
Sh 290.00
JATU
0.00
0.00%
Dec 8, 2022 12:00 a.m. EAT
Real Time Quote

www.dse.co.tz
jatu's audited financial statements 2019


19 May 2020 — JATU PUBLIC LIMITED COMPANY. P.O.BOX 42155. DAR ES SALAAM

PSSSF House 11th & 06th Floor
Samora Avenue
Morogoro Road, Ilala CBD
Dar es Salaam DS
Tanzania, United Republic Of

Board of Directors​

Name/TitleCurrent Board Membership
Zaipuna Obedi Yonah PhD ChairmanJATU Plc
Abdallah Khalfan GonziNon-Executive DirectorJATU Plc
Emmanuela Mtatifikolo KagandaNon-Executive DirectorJATU Plc, SEWOTA GmbH
Mwajuma Hassan HamzaVice ChairmanJATU Plc, Tanzania Women Chamber of Commerce
Phinias Samweli OpangaNon-Executive DirectorJATU Plc
Ian SamakandeNon-Executive DirectorJATU Plc

All Executives​

Source : WSJ Wall Street Journal


AfricanFinancials
https://africanfinancials.com › jatu-...
JATU PLC ( Tanzania) revenue surges by
304%in HY2021

29 Nov 2021 — However, the final ordinary dividends decisions are subject to adoption by shareholders at the Annual General Meeting
 
Jatu ni wale jamaa wa kipindi waliokuna na ule mchezo wa unatoa pesa alafu unalimiwa unauziwa. Mwisho wa siku watu wakatapeliwa.

Hatimaye kaingia kwenye 18, serikali imemkamata na kumshtaki kwa kujipatia bil 5 kwa njia za udanganyifu wa kutapeli watu.

Naipongeza serikali, Ila pia na nyie wabongo wenzangu tumieni akili. Nani akulimie akuuzie, wewe kazi yako kusubiri pesa tu.

Mtatapeliwa hadi lini? Mr.Kuku aliwachapa, Ila hamkusikia, Kuna vanilla aliwachaapa pia, namaingo , akaja Jatu, na Sasa Kuna wale soila.

Mbaya zaidi hawa watu hupata vibaraka na watetezi wengi sana pale wanapoanza huu utapeli, wenye akili wakionya tu basi hushambuliwa.

Naiomba serikali hii iwe mara ya mwisho, wakitapeliwa tena achaneni na hizi kesi. Acheni watu watapeliwe mpaka akili ziwakae sawa

View attachment 2462342
Hapa serikali inatelekeza wajibu wake, japo sitashangaa kama msukumo umetokea kwa kuwa kuna aliye ndani ya serikali naye ameathirika, serikali yetu ni vitu butu sana.
 
Back
Top Bottom