Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Yebo Yebo.. ndio maana mimi n nilimuuliza point blank.. kwanini asiende tu kutoa rushwa na kuplay ball na wakubwa na mambo yakamnyokea? yeye hataki kuwapigia magoti na kuwashirikisha katika hii keki. Sasa wakimuambia "sawa Dr. tutaleta wagonjwa kwako lakini sisi tutapata nini" yeye awaambieje wakati kule India walipoulizwa hilo swali jibu lake linajulikana?

Dr. Masau angekaa kimya na kuzungumza nao chemba bila kusema mambo ya mikataba. Angefanya kimya kimya. Hivi unafikiri sasa miye na kamtaji kangu nikiamua kufungua radio si ndo itakuwa vurugu!?
 
Hivi kumbe Manji ndio anataka kuchukua jengo hilo. Hii sasa haivumiliki!!!!!!!!!!!!!!!!!..
 
Eee bwana, wewe unawajua hawa wazee. Sasa huyu anatakiwa asaidiwe, ikibidi hata kuanzisha kamchango kakum-boost.

Sasa kaswali kidogo, hivi Tanzania Medical Association, ambayo ni professional body, wanasemaje kuhusu huyu bwana? Wanamtambua au hawamtambui?

Kitila,Tanzania Medical Association ni kama vile imekufa,baada ya madaktari vijana kutumia wingi wao na nguvu ya kura kuwaondoa madarakani madaktari hawa 'wazee'wakiongozwa na Prof.kahamba,ambao waliongoza MAT kama kitengo cha serikali na wakala waUsalama wa Taifa,kuwabana na kuwafanyizia madaktari wote waliokuwa wakijitokeza kupigania maslahi ya madaktari nchini wazee hawa wamerudi kupitia mlango wa Nyuma na kuwashitaki baadhi ya madaktari vijana na kuwavua uongozi kisha kupandikiza vibaraka wao.MAT kwa miaka nenda rudi imekuwa hodari wa kupooza migomo kwa kujifanya kuingia majidiliano na wizara kila ukijitokeza mgomo.Huwezi kuamini MAT mpaka leo,ina kaofisi kadogo kando ya bweni la wanafunzi la RUVU pale MUHI2,chumba ambacho hakiwezi kuketisha hata watu watano kwa wakati,chumba ambacho na hakika hakilipiwi kodi,kwani ni sehemu ya bweni la wanafunzi!hata hiyo medical council of Tanzania ina kaofisi kadogo pale wizarani na mfanyakazi mmoja msajili wa madaktari mr.Luena,kwa kifupi hakuna chombo kinachoweza kuitwa kinawakilisha wanataaluma madaktari kwa ujumla wao
 
ndio tunakubaliana sote huyu bwana ni mtaalamu mzuri sana wa moyo na tatizo lake kubwa kw sasa ni yeye na nssf ambao wanamdai kodi ya pango, hivi yeye kama mtaalamu hatakiwi kufuata taratibu ? ikiwamo kulipa kodi za pango?
 
Binafsi kutokana na madai makubwa aliyoyatoa na ya kuwahusisha mawaziri, ningependa kuona Kamati Teule ya Bunge inaundwa kuyafanyia uchunguzi na kutafuta ukweli wa jambo hili.

This is the only logical step to take. Nashangaa sana wabunge wa upinzani hili jambo hawataki kulibebea njuga!!

Lakini kadri mambo ynavyokwenda, ukweli utakuwa wazi na huyu daktari atakuwa vindicated. Rushwa na ufisadi unaitafuna ile nchi kuliko maelezo.

By the way, wale washenzi wasingekubali kuingia mktaba na wajerumani kwa sababu wanajua wajerumani wasingekubali ushenzi wa ten percent. Yaani hawana hata aibu, wanaingia mikataba haramu ya ten percent hadi kwa wagonjwa, walaaniwa tena milele!!

Namshukuru sana Dr Masau kwa kuweza kusimama vile moyo wake unavyotuma na kushinda vishawishi vya rushwa vya hawa washenzi wanaofikiri wataishi milele. Nasema tena walaaniwe sana!!
 
Dr. anakiri kuwa hilo jengo halikuwa designed kuwa hospitali siajabu hata mazingira yake hayafai kwa wangonjwa, anakiri kuwa hana uwezo wa kulipa pango baada ya business plan zake kufeli. Inaonyesha Dr. ni mbishi ndo maana mzozo wao umeishia mahakamani.

Way forward:
1. Asigangamale sana akubali kuhama na kujipanga upya, akiendelea kukomaa ataonekana mtu korofi. Ajadiliane na nssf wamsamehe deni wasijepiga mnada vifaa vyake.

2. Atafute business administrators wazuri, yeye ni daktari lakini biashara inawataalamu wake. Atafule eneo lenye pango la bei nafuu hata kama ni nje ya mji.

3. Sio lazima awe dar anaweza kutafuta pango bugando hospital au peramiho tena anaweza pewa bure. Wagonjwa wa moyo hawaji wakiwa cashuality kama wamepata ajari barabarani! wengi wao huja kwa appointment.

Watu waenda piga ramli bariadi, watakupata tu hata ukiwa wapi.
 
Hawa ndio Board of Directors wa THI, hivi wameshinwaje kumshauri Dr?

Board of Directors
Chairman: Dr. Ferdinand B. Masau, MD, Founder and President of the Tanzania Heart Institute
Secretary: Mr. Deo Lyato ,MBA, Tanzania
Dr. Edwin Mung'ong'o Representative from Ministry of Health, Tanzania
Dr. Ramadhani Dau CEO – National Social Security Fund, Tanzania
Dr. Adelhelm Meru Engineer and Training Specialist, Tanzania
Mr. Alfred Philip Representative from CRDB Bank LTD, Tanzania
Mrs. S.M.J. Mwambenja CEO – Exim Bank, Tanzania
Hon. Getrude Mongella MP and President of the African Unity Parliament, Tanzania
Dr. Doreen Rosenstrauch Assistant Professor, Texas Heart Institute and University of Texas Health Science Center at Houston, USA
Mr. Lee Evey Ass. Director, Respiratory Therapy, Texas Children's Hospital, USA
Ms. Rita Lenz CEO – Project Open Hearts, USA
Dr. Thomas Pezzella, President and CEO-World Heart Foundation and ICHF, USA
Dr. Guenter Hennersdorf Consultant Cardiologist, SES-Germany
Representative from Heart Centre Verde – Denmark
 
ndio tunakubaliana sote huyu bwana ni mtaalamu mzuri sana wa moyo na tatizo lake kubwa kw sasa ni yeye na nssf ambao wanamdai kodi ya pango, hivi yeye kama mtaalamu hatakiwi kufuata taratibu ? ikiwamo kulipa kodi za pango?

Hilo wote tumeshalinote na tunakubaliana nalo,akini mkuu hapo juu inakuwaje mtu aliyekwama kama huyu serikali ishindwe kumpiga jeki?mbona TRL ambao sio hata wazalendo serikali mara moja ikaahidi kuwapiga jeki na ikawapa kweli hizo pesa mgomo ule ukaisha?tena kwa mkopo zilikuwa zaidi ya hizo bilioni 1 anazodaiwa Dr.Masau,sasa wawekezaji wa nje ni bora kuliko wa Tanzania?Unajua wakuu sote tukubali hii ni institute kazi zake mbali na utabibu ni kufanya utafiti kuhusiana na mambo ya moyo,iwapo serikali ingewaboost au hata kuaqcuie share ikiwezekana basi taasisi hii ingeweza kusonga mbele sana na kucreate ajira nyingi hata kwa wenzetu pale Muhas,gharama za kubeba watu hadi India zingepungua sana kama sio kuondoka kabisa.Lions badala ya kusponsor India trips wangesponsor THI.Sasa opportunities zote hizi tunazikosa,wakati huo huo bado serikali yetu inalalama wasomi kukimbia nchi kweli kuna nia ya dhati ya kuwasaidia wazalendo?hawa wanapokwama kama hivi?
 
Yebo Yebo.. ndio maana mimi n nilimuuliza point blank.. kwanini asiende tu kutoa rushwa na kuplay ball na wakubwa na mambo yakamnyokea? yeye hataki kuwapigia magoti na kuwashirikisha katika hii keki. Sasa wakimuambia "sawa Dr. tutaleta wagonjwa kwako lakini sisi tutapata nini" yeye awaambieje wakati kule India walipoulizwa hilo swali jibu lake linajulikana?

Dr. Masau angekaa kimya na kuzungumza nao chemba bila kusema mambo ya mikataba. Angefanya kimya kimya. Hivi unafikiri sasa miye na kamtaji kangu nikiamua kufungua radio si ndo itakuwa vurugu!?

Nchi hii inayoitwa Tanzania hata uwe msomi vipi, bado ukitaka mambo yako yaende vizuri katika hatua za awali lazima ukubali kutoa rushwa hata kama hupendi ukijifanya kichwa ngumu tu ndio haswa haya ya Dr.Masau.Kwa kuwa nchi yetu sasa ufisadi umegeuka kuwa mfumo,yaani kila utakakogeukia utakutana nao tu,sekretari ili afikishe barua yako kwa bosi lazima umtip,mhasibu ili akulipe malipo yako halali kabisa lazima umwachie ten percent la sivyo watalipwa wengine wee utasubiri miezi 8.Ili ufike home mapema lazima ukubali kumlipa konda nauli ya shilingi 600 badala ya 300 halali nk.Haya na mengine mengi yanaanzia juu yanashuka chini huku kwa akina yakhe.
 
Yeah, ndiyo Tanzania yetu,,, yenyekuhitaji wataalamu warudi nyumbani,,, kufanya nini? Masau na wenzako mnaonyesha ni jinsi gani mnavyojali baba zenu, mama, dada, kaka, watoto wenu,,, Maskini wee binadamu hawa walioko madarakani hawaoni,,,ingawa macho wanayo,,, hawasikii ingawa maskio wanayo. Sitakuwa mbali sana na wanaomwambia Masau aondoke,,, lakini pia najiuliza aondoke aende wapi? Wakwake wako hapahapa, aende kufanya nini huko anakoenda? Kama ni fedha aliziona sana huko Marekani. Hazikumtuma wala kumsukuma akae huko,,,, alihitaji kuwasaidia wakwake wa Uchagani, wa Upareni, wa Usukumani, Wahaya, Wanyakyusa, Wangoni, Wadengereko, Wazanaki, Wamasai, Wamanda na kila aliye na anayeitwa Mtanzania!!!! ukimuuliza ndilo jibu lake. Jemedari wa kweli hakimbii wanajeshi wake ila hukaa nao hadi mwisho! Masau ameonyesha hilo. Kuwakimbia na kuwaachia akina Mwakyusa watambe sio tiba ya tatizo hili. Masau na team yake wanatakiwa waendeleze mchakato wa THI hadi waone mwisho wake.
Kwa faida ya wengi siyo Prof. Masau peke yake anayekwamishwa katika masuala mbalimbali yanayohusu kuendeleza Taifa hili. Jaribu kufuatilia hata katika sekta binafsi ambazo zinatoa huduma,,,, Mtanzania kupata kibali ni kwa zaidi ya miezi 3,,, wakati kwa mgeni yeyote, mhindi, mzungu na hatamwafrika mwenzetu wa hapo kwa Mandela ni deal ya siku chache tu kama sio masaa.
Lakini pia tukumbuke kuwa Biblia ilitangulia kutoa angalizo kuwa Nabii hakubaliki kwao,,, Sina maana ya kumfananisha Masau na nabii! La hasha,, ila ni hayo hayo kuwa Kilicho bora ni lazima kitoke nje ya mipaka yetu!!! Sijui labda hata baadae viongozi bora nao watatoka nje ya mipaka yetu? Sina Uhakika,,,, ila kwa leo Wasalaam
 
sasa Dr MASAU amekimbilia kwa Selemani Kova RPC na hivi sasa kuna kikao ofisini kwa Kova, time nzima ipo.Na tokea day break Dr/PR officer/Media consultant/ bwana Masau amewaalika waandishi wa habari kibao na wamekuwa wakiconduct interviews na wagonjwa

(makes you wonder kama ndio procedures zenyewe hizo au vipi)

sasa sijui hiii hali itaishaje lakini nina wasi wasi kutakuwa na kusomeana Riot act!
 
GT, nadhani ulisema jana jamaa aliitwa na akakiri makosa or whatever you said.. waandishi wa habari kuwepo wana haki kwani habari muhimu, au ulitaka waandishi wasishuhudie jambo hilo?
 
Mwana kijiji

nashukuru kwa kuleta habari hii lakini nilikuwa nina maswali:

- Hebu naomba ulete walau links zenye kuripoti kuwa Prof Masau anafanyiwa Fitna

-Kama hizo ftna zipo ni zipi?

-Zimefanywa na nani?

-Je huyo profesa kalalamika? kupitia authority zipi?

-Hizo authority zimetoa tamko gani?

-Kama si prof Masau, je hiyo THI imefanyiwa fitna vipi, na nani?

ni hayo tu kwa sasa walau tupate picha kamilimheshimiwa

Huyu dr kalamika sana kupitia vyombo vya habari vya tz... lkn ndo kama hivo who cares
 
GT, nadhani ulisema jana jamaa aliitwa na akakiri makosa or whatever you said.. waandishi wa habari kuwepo wana haki kwani habari muhimu, au ulitaka waandishi wasishuhudie jambo hilo?

nimekusikia ulimuuliza hilo swali la kuitwa sema hukumbana kwani angekwambia jana saa 5 asubuhi alikuwa wapi na alikutana nani na alisema nini kama suluhu ukizingatia juzi alisema kuwa hahami ng'o!

Kuhusu waandishi wa habari kuwepo hilo si tatizo kwani ni habari muhimu lakini issue iko kwenye hii ya kuwaingiza wodini kufanya endless interviews na wagonjwa

sasa huhitaji kujua kama hapa kuna suala la ethics na maswali ya kujiuliza je je kabla ya hizi interviews kulipatikana patient's right of consent wahojiwe na media?

kwa sababu wagonjwa ni watu ambao wako vurnable je ndugu au next of kin wa wagonjwa wameombwa/waliombwa ruhusa kabla ya kuwapiga mapicha na kuwarekodi?

Je medical ethics na patient privacy zinalindwa vipi kwenye hii tug of war between THI na NSSF?

Je ni haki kwa THI kutumia wagonjwa kama human shield kwenye hili?

Je Tanzania Medical Board wanasemaje kuhusu hili...(assuming kuwa Dr Masau ana ugomvi na wizara ya Afya)

Je NO WIN NO FEE LAWYERS wakiamua kushitaki on behalf of patients ambao hawajatoa consent wahojiwe Dr Masau atasemaje?

surely kwa mtu ambaye kasoma na kufanya kazi kwenye nchi kama USA atajua mambo haya jinsi yalivyo na considering jinsi University of Dar Es salaam inavyoproduce ma law grads ambao washaapishwa na hawana kazi surely hapa kuna ulaji unaukia kwa hawa malawyers ambao si big shots kama akina Mkono advocates
 
Mkuu unajua sijakuelewa kidogo......yaani unataka Dr Masau atimuliwe mjengoni au? sisi ni watanzania je kama ungekuwa wewe lets say mama yako ni mmoja ya wagonjwa wale watano5 wanaosubiri operesheni THI sasa hivi ungetetea THI wafukuzwe mjengoni?
 
Ukisoma thread hii tangu mwanzo utaona kuwa nilikuwa namtetea sana huyu dhidi ya Serikali mpaka ikaja hii issue yake dhidi ya NSSF

Jamaa alisign contract kuwa atalipa kodi kisha baadae anagoma kulipa kodi na on top of hiyo NSSF ilikuwa inamlipia:

MAJI

UMEME

ULINZI

RENOVATION YA JENGO

sasa huyu Masau alijua wazi kuwa hizo 2.3 BILLION ni deni na kila akidaiwa alienda kushitaki kwa Lowassa naye akamwambia hilo liko nje ya uwezo wake amalizane na NSSF.

Alipodaiwa tena akaamua kumwita mke wa rais kutembelea Hospitali

Alipoambiwa alipe kwa awamu akagoma

alipoambiwa alipie Umeme akagoma

alipoambiwa alipie maji akagoma

sasa hebu tuache emotions hapa. Ni kweli nia yake huyu masau inaweza ikawa ni nzuri lakini inawezekana vipi akashindwa kuelewana na hao NSSF akakubali kulipa kwa awamu hilo deni?

Kesi ilipofika mahakamani akatoa statement kuwa hahami ng'o sasa hebu niambie ilikuwa vipi au ilishindikana hivi hiyo board of trustees ya THI(KAMA IPO ) asiongee nao na kuwaambia kuwa kuna tatizo hilo?

Surely ndio serikali yetu ina matatizo yake lakini kwa hili nadhani tuache sheria ifuate mkondo wake. Kinachoudhi ni wagonjwa kutumiwa kama HUMAN SHIELD kwenye hili na sidhani kama ni kitendo cha busara kuwatumia hawa ili aendelee kubaki pale rent and service free

Kweli serikali inaweza ikaamua kulilipa hilo deni la MASAU lakini why should it?

hizo pesa kwa nini zisipelekwe Muhimbili?

and where does it stop?

kesho Mwanakijiji akitaka naye alipiwe bill ya simu na bandwidh ya redio kwa kisingizio kuwa anatupa habari serkali itakubali?

au

Hizo 2.3 billion zinaweza kujenga dispensary ngapi kule Pemba?

and serikali ikianza kubail out hawa akina MASAU where does it stop?

Hivi mshasahu nilivyokuwa nikipinga serikali ambayo ni SECULAR kuwalipia MAHUJAJI?

in short incopetence ya MASAU isitufunike au isituzuie kuuliza basic questions kuwa ilikuwaje mpaka hali ikafikia hapa ilipofikia?
 
...........udhaifu na ufisadi wa viongozi wetu ndio unasababisha watu wafikirie ndivyo sivyo........

...GT nakubaliana sana na maelezo yako............sasa mimi na wewe na yule tujiulize...........je kweli serikali/viongozi wetu wanafikir kama ulivyoandika hapo juu??...................unakumbuka Mizengo alivyowasaidia TRL financially?..........sidhani kama alikuwa na mawazo mazuri kama yako hapo juu...............

....in short the rule of the game Tanzania ni mwiko...........your maelezo hapo juu......ndio hiyo hiyo itakayotumika kumchapa Dr Masau........

...God Bless our Nation!!
 
Back
Top Bottom