Sakata la Dr. Masau: Msimamo wa Serikali na Hatima ya Taasisi ya Moyo (THI)

Dr. Ferdinand Masau (Bingwa wa Magonjwa wa Moyo na Upasuaji) aliamua kuacha kazi nzuri ya kulipa huko Marekani na kurudi nyumbani kuleta ujuzi wake na vipaji vyake ili kusaidia Watanzania wenzake. Daktari huyo alisomea chini ya Daktari Bingwa wa Kimarekani Dr. Denton Cooley ambaye ni Mwanzilishi na Mpasuaji Mkuu katika Taasisi ya Moyo ya Texas (Texas Heart Institute). Kwa wale wasiofahamu Dr. Cooley na wenzake ndio waliofanya upandikizaji wa moyo wa kwanza Marekani na kituo chake hicho kimefanya upasuaji wazi wa moyo mara 97,000 kuliko kituo kingine chochote duniani!!

dacbnite.jpg

Jengo la Dr. Denton Cooley (THI) kwenye Hospitali ya Mt. Luka, Texas

Sasa, Mtanzania ambaye amefuzu, ana uwezo na anaweza kuishi na kuhudumia wamarekani na kulipwa "kishenzi" anapoamua kuachana na hayo yote na kuamua kurudi nyumbani kwake, ilistahili siyo tu apokelewe kwa mikono miwili bali pia kwa shukurani na kutiwa moyo. Hilo halijatokea kwa Dr. Masau na sitashangaa akiamua kufunga taasisi yake na kurudi Marekani kwani wabongo "hawana mpango wala shukurani"!
THIentry.jpg

jengo jipya la taasisi ya moyo Tanzania

Hivi karibuni kumekuwa na majaribio ya mara kadhaa ya kuikejeli na kuidhihaki taasisi hii ya moyo na kwa namna fulani kuikatisha tamaa. Juhudi hizi zimeongozwa na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Afya ambao wamedaiwa kukwamisha mipango ya maendeleo ya taasisi hiyo ikiwemo kukataa kutia sahihi mkataba ambao ungekiwezesha kituo hicho kuwa cha kisasa zaidi na kikitoa huduma bora zaidi.

Ninachosema ni kuwa, wakati wa malumbano na migongano isiyo ya lazima umepita. Serikali badala ya kumfanya Dr. Masau na timu yake wakate tamaa au kuona ya kuwa "wanawekewa magogo" waamue kwa dhati kuisaidia taasisi hiyo. Ilani ya CCM ya 2005-2010 inasema hivi kuhusu suala la utoaji wa huduma za jamii:

Kukamilisha mipango itakayowezesha huduma za upasuaji wa moyo kutolewa humu humu nchini. Ibara ya 66 (g)

Sasa nafasi ipo kwanini tusiitumie. Ni kweli kuwa mara nyingi Watanzania hatutukuzi vitu vyetu wenyewe ila vile vinavyoletwa na wageni. Tatizo jingine ni kuwa Watanzania hatupendi vitu vizuri, kwani tunaona hatuvistahili kwani ni "vya wazungu". Zinapowekwa nguzo za taa mtaani, watu wanazitungua kwa manati!, tunajenga barabara za lami tunataka kupitisha maboti kupita uzito unaoruhusiwa! Jamani tupende vitu vyote na tuhakikishe vinadumu tusiviharibu au kusubiri viharibike!!

Tunaiomba serikali imuwezeshe Dr. Masau na Taasisi yake kwani haya si mashindano! Kuendelea kuikandia taasisi hiyo na kuiacha ihangaike wakati ina mtu mwenye uwezo na ujuzi wa kuiongoza ni kujipiga ngwala wenyewe! Au hadi taasisi ya namna hiyo ianzishwe na mtu "mkubwa"?
Huyu ni yule aliyeanzisha hospitali pale klabu ya Tazara?
 
Watu wanakumbuka tuliyoyasahau..Sakata la Dr. Masau ni mojawapo ya mambo ya aibu Sana kutokea wakati was Kikwete.
 
Back
Top Bottom