Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini ametembelea Gereza Mkoani Geita

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini (Mb), ametembelea Gereza Geita lililopo Mkoani Geita na kuzungumza na Wafungwa pamoja na Mahabusu wakati alipofanya ziara yake ya Kikazi Mkoani humo Novemba 25, 2023.

Mhe. Sagini amefika Mkoani Geita ikiwa ni ziara yake ya kawaida kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazojitokeza lengo likiwa ni kuboresha utendaji kazi.

Waziri moja.JPG

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akipokea salamu ya heshima kutoka Gwaride Maalam lililoandaliwa na Askari Polisi mara baada ya kuwasili Mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na kusikiliza na kutatua kero zinazojitokeza Novemba 25, 2023.
Waziri moja 1.JPG

Gere.JPG

Gere1.JPG

Geree.JPG
 
Back
Top Bottom