Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) yakagua ujenzi wa Makazi ya Askari Zimamoto - Dodoma

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Kamati ya Kudumu ya Bunge Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vincent Mbogo (Mb) imefanya ziara na kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji unaoendelea katika eneo la Kikombo Jijini Dodoma Novemba 04, 2023.

Kamati hiyo ilipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb) na kupitishwa kwenye maeneo mbalimbali kisha kufanya majadiliano mafupi juu ya umaliziaji wa ujenzi wa nyumba hizo.
3568ff1b-9481-4b9d-9d3e-194fbcd8d96f.jpeg

6c2df606-74d8-4ba4-8210-b799f90a1188.jpeg

Ikumbukwe kuwa Kamati za Bunge hufanya ziara mbalimbali za ukaguzi wa miradi kwa lengo la kupata taarifa, kujielimisha, kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na hatimaye kutoa taarifa Bungeni.

Aidha, wakati wa ziara, Kamati hukutana na wadau kwa lengo la kupata ufafanuzi, maoni na michango yao kuhusiana na madhumuni ya ziara husika.
d4d5cd91-9b41-41e9-a984-546b6317f17b.jpeg
 
Duuuu wizara mbovu kuliko zoote......maslahi adkari wake hasa magereza zimamoto hovyo kabisaaa....hakuna anaejali wala kuwafikiriaaa
 
Back
Top Bottom