Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Akihitimisha ziara yake Mkoani Mwanza, Naibu Waziri Sagini alitembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa maghorofa ya Polisi Mabatini, mradi wa ujenzi wa nyumba za Polisi pamoja na kituo cha Polisi Nyamuhongoro, kituo cha Polisi Malya Wilayani Kwimba, kituo cha Polisi Kwimba, Chuo cha Polisi wanamaji Mwanza, mradi wa ujenzi wa mfumo wa majitaka Gereza Kuu la Butimba, Kiwanda cha Ushonaji na Useketaji cha Gereza Kuu Butimba na baadaye kupokea taarifa ya hali ya usalama Mkoani humo pamoja na utendeji kazi wa Vyombo vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.