Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,272
Jana nilipanda treni kwa safari ya masaa manne. Mlangoni alikuwepo mhudumu na kipima joto na kuhakikisha wote tuna barakoa kabla ya kuingia ndani pia kulikua na meza yenye sanizer pembeni.
Tuliambiwa tukae mbali na abiria wengine la kama mmetoka nyumba moja mnaweza kukaa pamoja. Sasa alikuja mwanaume mmoja aliomba ku charge simu kwani nilipokaa kulikuwa na socket ambayo sikuitumia.
Alisema ni muhimu awe na simu kwani kuna maombi anaendelea nayo kupitia You Tube. Niliposikia maombi nilimdadisi zaidi, alisema ni maombi ya Bhudaism. Nilimuuliza wewe ni Bhuddist? Alisema yeye hana dini ingawa alizaliwa Mkristu wa Anglicana na kupata sakramenti zote.
Wakati huo maongezi yetu ya yamekolea na barakoa tumeziweka videvuni, alisema baada ya kuzunguka dunia kikazi amegundua nguvu ya sala na maombi ya dini nyingine ambazo wala hazina uhusiano na Yesu. Anaamini kuwa kuna Mungu na anaamini jua lina nguvu sana. Aliniambia kuna ibada inayohusisha jua na ukimaliza hiyo ibada unaweza usilale kwa masaa 72, unakuwa na nguvu za ajabu.
Kwakweli nilimueleza kwangu mimi Ukristu nimerithi kutoka kwa wazazi. Kama walionileta duniani wameishi kwa imani hiyo na kunifundisha mema kwenye muongozo huo sioni sababu ya kuachana nao, pia mimi binafsi umenijenga kumjua Mungu na maombi.
Mwisho wa safari yetu tuliagana. Nilijifikira sana nikiwa nyumbani kuwa Yesu alisema yeye ni njia ya kweli, sasa hawa wanaoabudu kupitia jua siku ya hukumu itakuwaje kwao?