Inahitajika Sheria ya Maadili kwa Viongozi wa Imani Tanzania

RWEZAURAJOHN

Member
Jul 5, 2011
24
26
UHURU wa kujieleza na uhuru wa imani ni mema. Lakini mapungufu yake yanaporuhusu maadili kukiukwa, hiyo sheria inatakiwa kurekebishwa.

Maadili yana aina nyingi.
_Maadili katika kusema,
_Maadili katika matendo,
_Maadili katika kuwaelekeza waumini cha kufanya.
_Maadili katika mwonekano wa nje.
_Na mambo mengine mengi yanayokwaza jamii.

Taasisi za umma/serikali zinazosimamia sheria mbalimbali, zimelemewa na migogoro kutoka taasisi za dini. Zinashindwa kuwalinda wanaoonewa. Zinashindwa wakati mwingine kutoa maamuzi kwa kuwa hakuna sheria ya maadili kwa viongozi wa dini.

Sheria ya jinai inashindwa kufika mahali pa kufanya maamuzi sahihi. Mabaraza yaliyosajiliwa hayana uwezo wa kuthibiti migogoro. Vyombo vya mamlaka havina mahali pa kwenda ili kupata mwongozo wa kisheria. Mamlaka hizi zimeshindwa kuwasaidia viongozi wanaoonewa, kama zinavyoshindwa kuwaadibisha viongozi wanaoonea.

Ukiukwaji wa maadili umeifanya Tanzania kupokea viongozi wa imani wenye mafundisho hatari. Kuna watumishi wa uongo wanazalishwa hapa Tanzania, Nchi jirani nazo inamwaga hadi waganga kwa jina la watumishi wa Mungu, na nyingine zinaleta humu humu wapiga dili! Ni kwa sababu hapana sheria ya maadili kwa viongozi wa imani.

Watu wametapeliwa kwa kigezo cha sadaka, kwa kuwa hakuna sheria inayoongoza maadili ya viongozi wa dini.

Nimeshuhudia katiba zikirekebishwa mara nyingi kabla ya kusajiri chama cha dini. Mtu anapeleka katika, anaambiwa rekebisha baadhi ya vipengele ili iweze kupita. Kinachorekebishwa ni maandishi tu. Nia ya mwanzo inayohusika na maadili iko palepale na ataitekeleza mbele ya safari.

Masuala ya dini yanasimamiwa na Katiba ikisaidiana na Katiba za madhehebu husika. Mfano: Sidhani kama wanaouza udongo, maji, mafuta, mbegu, na bidhaa mbalimbali, sajili zao zina vipengere hivyo kama mojawapo ya MALENGO (objective) yao. Kwa kuwa haipo katika katiba zao, wanapoikiuka katiba, ni kwa nini sheria inakaa kimya na kusema hayo ni mambo ya imani? Kama ni hivyo, hakuna sababu ya kusajili katiba zao.

Sote tunajua kuwa Waganga wa jadi wana sheria inayowatambua kuagua. Watumishi wa umma wana sheria zinazowaongoza. Lakini hawa wanaoagua kwenye dini ni sheria ipi inawalinda kati ya Katiba ya nchi na katiba zao? Ni sheria ipi inawapa ruhusa kufanya biashara kwa jina la imani?

Kama mtu anaamini kuua, kuzini, kuiba siyo dhambi, basi na katiba yake ieleze hivyo. Ili watu wake wakiiba, ijulikane ndiyo imani yao. Kama mchungaji kwake Biblia si kitabu cha imani yake, katiba yake iseme hivyo. Kama anakusudia kuuza nguvu ya mungu wake, iwemo katika katiba yake. Siyo katika katiba iliyosajliwa anasema Biblia ndio msingi wa imani yake, halafu asikike anasema Hategemei Biblia kwa kuwa kimebadilishwa mara 1000. Huyo amekiuka maadili aliyoyasajili.

Sisi Viongozi wa imani (waadilifu) tuna wajibu wa kuisaidia serikali kutengeneza sheria ya maadili itakayotumika kusajili, kufuatilia nyendo za maswala ya imani, mafundisho yao, matendo yao, na kuisaidia serikali kufanya maamuzi sahihi yasiyomwonea mtu wala kuingilia uhuru mzuri wa kuamini na kuabudu.

"NAWASILISHA"
 
Back
Top Bottom