Safari yangu ya dhahabu Botswana - Sehemu ya pili

Midnight

JF-Expert Member
Apr 24, 2021
229
675
"Itakuwa furaha Sana kwangu Kama mods mtauacha huu uzi hapa hapa na sio kuunganisha na ule wa sehemu ya kwanza... Natanguliza shukrani kwenu na kazi iendelee kwa pamoja tukiwa Kama Wana jamuhuri wa jamuhuri tukufu ya muungano wa Tanzania,
Mungu ibariki Tanzania."

Kwanza kabisa napenda kuwaomba radhi ndugu zangu Wana JF wote kwa kuwaacha kwenye mataa. Haikuwa kusudio langu, kutomalizia jambo nililolianzisha mwenyewe bila kuombwa bali ni changamoto kidogo tu za maisha zilinisukuma kukaa kimya. Na sasa nimerudi upya tunaendelea mbele zaidi. Ahsanteni.

"Death comes to all of us"

Msemo huu una miongo kadhaa sasa kwangu, na Kama ukiangalia mambo mengi ninayozungumzia huwa sikosi kugusia gusia mambo yahusuyo vifo, kifo au kumbukumbu furani kuhusiana na issue hizo. Hii imebeba sehemu kubwa ya maisha yangu, umekuwa ugonjwa sugu wa kumbukumbu na maulizo tokea Francistown Hadi hii leo.

Katika safari yetu tulitegemea kuishia mjini Gaborone, mji mkubwa zaidi Botswana na tungeanzisha maisha yetu huko huko mjini Gabo.

Lakini kiukweli hadi hii leo ukiachana na kuuona kwenye runinga na picha mnato hatukuwahi kugusa kabisa ardhi ya mjini Gabo, yaani tulikwama Francis town jumla na reja reja. Pale Francis town kuna kila kitu ambacho mwanadamu mwenye tamaa anakiwazia kichwani mwake ni sawa na vile watu wa mikoa mingine Tanzania wanavyokwamia mjini Tanga na vitongoji vyake au tuseme ni sawa na mtu mgeni wa Tanzania apange kuja TZ kimagendo kisha mji wa kwanza kushukia ukawa Mwanza au A town pale, kiukweli nakwambia asipokuwa makini DSM ataishia kuisikia redioni.

Francis town ni mji wa pili kwa ukubwa pale Botswana, hivyo ndio maana baada ya kujishikiza pale ikawa ngumu kutoka kabisa kulingana na mishe za usaidizi katika karakana ya utengenezaji majeneza pale, ilituchukua siku chache tu kupata connection ya vibarua, kwa kuwa pale wanazungumza kiingereza kidogo na lugha zao za kikabila, hivyo sio watu wote walikuwa wanajua vyema kuongea kiingereza na hiyo ilisaidia Sana kuona ni kana kwamba wote tunabahatisha bahatisha tu... Ila usiombe ukakutana na msomi.

Pia uzuri wa mji ule ulikuwa umechanganya watu wengi toka mataifa mbali mbali hasa kutoka Zimbabwe, South Afrika, Zambia, Namibia na nchi nchi za ukanda ule na kutokea East Afrika ilikuwa ngumu sana kukutana na watu kutoka Kenya, Burundi , Uganda au hata Tanzania kidogo watu kutokea Zambia tulikuwa ndio tunawaona kama watz wenzetu sababu ya ujirani wa nchi zetu na walau kidogo tunaelewana tabia.

Na kwa wakati wote kule kuna kitu kizuri cha kujifunza toka kwao AMANI kama unataka kuweka listi ya nchi salama kwa wageni usiisahau Botswana.

Baada ya kupata kibarua kwa jamaa mmoja hivi pale Area A makabulini, mkabala kabisa na hospitali kongwe pale ya (Nyanga) nini sijui... Jina kidogo limenitoka nikiwa na mwenzangu kazi yetu ilikuwa ni kupiga msasa majeneza tu... Yaani kuanzia jua linavyoamka hadi linaporudi kulala sisi na majeneza tu majeneza na sisi.

Hali ile mwanzoni kabisa ilituwia vigumu kufanya lakini kutokana na kwamba yule Boss wetu alitupa na hifadhi na ya mahali pa kulala na kutusaidia kupata utambulisho wa makazi na vibali vya kuishi kule ilitupasa tuvumilie.

Nakumbuka nilikuwa nikiweweseka mara nyingi zaidi ya mwenzangu kutokana na jinsi kazi yetu ilivyokuwa ikitoka vizuri na haraka zaidi na kushuhudia makumi ya watu kila siku katika kutoa order au kuja kuchukua jeneza kwaajiri ya maziko.

Pia mahali tulipokuwa tukifanyia uinjinia wetu hapakuwa mbali sana na makabuli, kulala pia haikuwa mbali na makabuli, sehemu yetu pendwa wenyeji wetu wanapopumzika baada ya kazi haikuwa mbali na makabuli, hivyo nilijituta na kuwa jirani mkubwa na makabuli kwa kila kitu.

Nikawa nakumbuka makabuli ya kwa Bongololo kurasini shimo la udongo kule beach kimba kitambo Sana aisee eti nilikuwa naogopa kukatiza makabulini na Leo hii mimi naishi kwa kutegemea watu wafe!!? Maisha yaajabu sana haya. Na hapo ndipo nilipoupata ule msemo wangu bora wa kujitia moyo wa "DEATH COMES TO ALL OF US" usije ukanipingia pesa zako ukaniambia Midnight kuna kiasi kadhaa hapa kalale makabulini, utaliwa pesa zako brother na utaniita mchawi buree kumbe nina uzoefu wa kutosha Sana kwenye sector hiyo.

Kutokana na uvivu na labda kutoipenda sana kazi ile yule mwenzangu aliachana kuwepo pale na kuamua kujichanganya katika maswala ya utalii baada ya kukutana tena na brother Boipelo, Boi ni moja wapo ya watu wachache sana Duniani wenye mioyo ya dhahabu, yaani hapa Duniani kuna watu wanaupendo na huruma huwezi amini kwa kuskia kwa macho Wala kuona kwa maskio, nimesema kinyumenyume nikimaanisha ningumu sana kuamini matendo yanayofanywa na baadhi ya watu hapa Duniani hasa katika kuwasaidia wengine. Nilibaki pekee pale bila uwepo wa mwenzangu na kwa kuwa tulikuwa tukitembeleana na nilikuwa na nafasi ya kuweza kuungana nae pamoja na Boi Kama na mimi ile kazi ingenishinda. Lakini sikuona umuhimu wa kumwongezea mzigo mwenyeji wetu.

Niliizoea kazi yangu na kuipenda sana na baada ya muda kidogo nikawa nafahamu mambo mengi kwenye fani ya uselemala tukianzia vipimo, jinsi ya kukata mbao, kuunganisha na gundi, vipimo vya watu kwa urefu na upana, kujua soka na wakati sahihi wa biashara kupanda na kushuka, Ila kwenye mambo ya mauzo na mapatano ya bei sikuhusika kabisa, hivyo nilitoka kuwa mpiga msasa hadi kuwa fundi wa kati na muda mwingine kusaidia wateja zetu kwenda hospitali kuchukua miili Kama wangeitaji msaada wetu kwa njia ya malipo kidogo. Kiukweli kazi niliifurahia kwanza kabisa kwa kuwa nilikuwa huru, chakula kizuri napata, makazi napata, na sibaguliwi kabisa.

Bila kusahau watoto wa zuri kwa mbaaali, maana tajiri wetu alikuwa mtu wa mvinyo na totoz na ukitaka uende sawa na nyoka na wewe tambaa basi ilikuwa weka tuweke na vile mijeneza inaharibu akili kuiona kila siku ilibidi tuwe tunajitandika kweli kweli mapombe Kama tu wafanyakazi wa vyumba vya maiti.

Kwa kweli wakati ule sikuona ubaya kabisa watu kufa, maana sisi tusingepata kula yetu bila wao kutangulia mbele za haki. Na hali hii ndio inanisumbua sasa, inanifanya nakosa usingizi nakuwa na mawenge na hasa wakati huu nikiwa mbali na kazi zile nilizokuwa nazo ujanani.

Kuna wakati unatembelea hospitali pale na kutafuta wateja hasa vipindi vile vigumu kwabiashara unakuta mali ni nyingi soko limeingiliwa na watu wengi,wagonjwa wanapona, yaani ni shida tu hakuna kazi kazi kabisa basi inabidi mara kwa mara kuwa karibu na watoa huduma za vyumba vya maitia ili ikitokea kazi wawaunganishe faster na mteja.

Yaani bila connection mzee hutoboi popote pale hapa Afrika, na usione watu wanakutizama kwa huruma ukazani wanakuhurumia na msiba wako, aisee watu wapo kazini mkuu, wanatamani hata ufe hapo wao wapige pesa tu, (wauza majeneza tupo pamoja hapo?)

Kulitokea shida furani hivi ya madeni na ucheleweshwaji wa malipo au kutolipwa kabisa pesa baada ya mazoea makubwa na tajiri wangu kwakuwa wakati huo alianza kuniona Kama kijana wake wa nyumbani na kusahau Kama Mimi nimekuja kutafuta pesa huku na sio kutafutana na mipombe na wanawake kila siku na mbaya zaidi nimeshapata uzoefu na amani ya kuishi kule bila buguza yoyote sehemu yoyote ile... Nikachapa mwendo safari hii sasa ndio inabeba jina la kumbukumbu yenyewe sasa "Safari ya dhahabu Botswana"

Mwanaume nina miliki suruali za Tokyo, mji naujua, nimepata mjomba Boi wa hiari Botswana, nyota inawaka, bar nakopeshwa utaniambia nini mimi nikuelewe wakati ule.

Kabla sijajichanganya kwenye michakato mipya niliyoazimia kwanza kabisa nilitafuta day worker kwa maselemala wengine nikajishikiza huku naangalia timing nzuri ya kujilipua migodini huko, maana licha ya uzoefu wangu mkubwa kwenye sector ya kutoogopa kufa au kuogopa wafu na mambo yako bado sikuwa na roho ngumu ya kuishi migodini huko na miamba kutoka sehemu mbali mbali na waliovurugwa haswaa..

NAVUTA PUMZI KWANZA, ACHA TUANGALIE UPEPO.

Kusoma sehemu ya kwanza - Safari yangu ya dhahabu Botswana
 
Imetulia sana....napenda sana kusikia mikasa ya kimaisha sababu mi pia nimepitia mengi. Mkuu ukipumzika urudi tafadhali tunakusubiri
 
Safari hii unataka utuache miez mingap tena

NOTE: Sijasoma kabisa, nimeshuka mpaka chini nlivyoona hujaandika mwisho nkaacha kabisa kusoma
Vitu vizuri havihitaji haraka...acha tupate na muda kutafakari wakati anavuta pumzi
 
Usiofu mkuu, wakati huu tupo pamoja.
Botswana wanawake wana matako eeeehh uwii nitarudi tena na tena huko, tako, wanaruka ukuta kwao sunna tu, alafu kwao ndio ufahari, yaani wanavaa vibukta vifupii na tight fupii na ndio mavazi yao, yaani Gaborone, nitarudi kutembea tena na tena, Mungu kawaumba aisee.
 
Mkuu midnight napenda sana Mikasa ya watu juu ya maisha na vyote walivyopitia najifunza mengi zaidi na kuamini maisha ni safari ndefu
 
Mkuu umenikumbusha jambo aisee
Botswana wanawake wana matako eeeehh uwii nitarudi tena na tena huko, tako, wanaruka ukuta kwao sunna tu, alafu kwao ndio ufahari, yaani wanavaa vibukta vifupii na tight fupii na ndio mavazi yao, yaani Gaborone, nitarudi kutembea tena na tena, Mungu kawaumba aisee.
 
Mkuu umenikumbusha jambo aisee
Haaa ila Botswana kuzuri kwa kutalii, watu hawajui tu, alafu peace sana huko.
IMG_20211104_170309.jpg
 
Kambi hapa nachungulia kila baada ya lisaa kama kuna apdate yeyote
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom