Safari yangu ya dhahabu Botswana - Sehemu ya pili

Hii kweli ni safari, maana likuwa April na imekua November, tutegemee utarudi June.
 
Tumeweka kambi..ila uisahau kutupa stori ya mizigo ya huko na sikia ina chura balaa..

#MaendeleoHayanaChama
 
"MALAIKA AMEGEUKA SHETANI"

Naendelea nilipoishia. Tabia ya kupenda kunywa pombe Sana niliipata huko huko nilikotoka, na ubaya zaidi nilikuwa nikidhani inanisaidia kumbe najiangamiza zaidi.na nikirejea comment ya ndugu mmoja hapa akisema kule Botswana wanawake wanapenda kuvaa vinguo vifupi kweli kweli ni kweli kabisa, maana hata nguo zao za kitamaduni ni kama wanavaa nusu utupu.

Baada ya kuachana na Boss Malopelope, niliamua kujishikiza kidogo kwa jamaa furani hivi waliokuwa wanafanya kazi ile ile sawa na sisi. Sasa hapo ndipo nilipokiona kile wanachosemaga wahenga cha "mtema kuni utakiona" yaani yule aliyekuwa ndugu MALAIKA kwangu akageuka sheetwani kabisa, tena mwenye mapembe saba.
Niliemwona MALAIKA, wakati huu alikuwa ni ndugu ibilisi muuaji, mnyonya damu na asiye na huruma kabisa.

"Usije ukamwamini mtu awaye yote katika kuyatetea maisha yako, sisi ni maadui, mashetani na kila kitu kibaya kipo mioyoni mwetu. Kwa uzoefu wangu na miaka yangu hii niliyonayo nawashauri msiaminiane sana, hata mke wako kaa nae macho macho maana kuna wakati huwa tunageuka mashetani.
Basi nilianza kuandamwa na visa mbali mbali toka kwa boss wangu yule wa kwanza aliyenipa kazi na hifadhi pamoja na mambo mengine yote na kuujua mji. Mara anitangazie mimi jambazi, kibaka, mtanzania, na maugomvi kibao kila siku kisa ntampokonya wateja zake nilizokuwa na wafahamu pamoja na connection zake ninazozijua.
Nikaona isiwe taabu sana, kwanini nifanye kazi kwa mashaka mashaka na pia nisije nikawagombanisha zaidi wenyeji wangu mwisho tukaja kutekana bureee...

SAFARI MACHIMBONI

Nilikaa nyumbani kwa Boi, huyu alikuwa mjomba wa hiari, na ikumbukwe rafiki yangu yule tulietoka wote DSM alikuwa akimsaidia mjomba Boi shughuli zake ndogo ndogo binafsi alizokuwa akizifanya nje ya kazi yake ya kitalii.
Tukirudi nyuma kidogo, unamkumbuka yule jamaa wetu wa tatu tulietoka nae Dar? Yeye aliishia Tunduma baada ya kutekwa na mtoto mmoja mzuri hivi... Na kwa tabia zake kama angefika huku Francis sijui Kama angepona either ukimwi ungemwondosha Duniani au angechanganyikiwa kichwa chake kwa kukutana na madem wazuri mchanganyiko mchanganyiko.
Kule Botswana pia kuna utajiri wa madini Kama ilivyo hapa nyumbani Tanzania, pia kuna vivutio vingine vingi tu na tamaduni na lugha mbali mbali za kupendeza. Pia kuna uchimbaji madini ya Diamond, Salt, Copper, Soda Ash, Uranium, Nickel na Gold na mji wa Francis town haupo mbali kabisa na baadhi ya migodi inayopatikana madini tajwa hapo juu.
Msidanganywe na government kuwaambia nchi yetu ni tajiri, huo ni uongo kabisa, maana kama utamaanisha utajiri uliopo ardhini na misituni basi nchi zote za Afrika ni tajiri mno, sioni nchi masikini katika Afrika. Mfano Mgodi wa jwaneng diamond mine ni mgodi unaoshika nafasi ya kwanza hadi ya pili kwa migodi yenye thamani Duniani na mgodi huo upo Botswana kule inapotokea timu iliyopindua meza kibabe dhidi ya watani zetu ndugu Makolokolo Fc, pia kuna mgodi wa Orapa nao ni wa almasi pia na kwenye nafasi ya migodi kumi bora ya almasi Duniani mgodi huu upo,

Sasa pale mjini Francis kama nilivyokwambia kuwa kumechangamka kweli kweli na kila kitu kinapatikana pale na kipindi hicho kulikuwa na mgodi wa dhahabu mpya uliofunguliwa karibu kabisa na mji ni Kama kilomita 25 tu hivi kutoka Francistown, mgodi huu ulikuwa ni bora zaidi kwangu kujaribu kutafuta maisha tofauti kabisa na sehemu nyingine kama kule jwaneng ambapo unakuwa unaelekea katika jangwa la Kalahari huko mwishoni mwishoni kuitafuta Namibia nchi niliyosikia uzuri wake wa sehemu moja hivi jangwa limekutana na bahari.
Wakati ule mgodi unaanza shughuli zake ulikuwa unaitwa Galan Gold mining, sijui kama bado unafanyia kazi siku hizi, na haikuwa mgodi wa changanyikeni ovyo ovyo Kama baadhi ya migodi mingi tunayoijua, utofauti ni kuwa wamiliki pamoja na serikali ya eneo husi walikuwa wazingativu sana kupangilia mambo, si unajua wazungu tena.
Basi nikiwa na rafiki yangu mmojo mwenyeji wa kulekule tulishauliana na kuamua kujisogeza mgodi kutafuta chochote huko, huku wakati huo yule rafiki yangu tulietoka wote DSM yeye anaendelea na kazi ndogo ndogo anazopewa na Boi kwa mapatano yao wanaojua wenyewe, na kwa bahati nzuri alitokea kukubalika sana na kuwa maarufu mno maeneo yote anayokaa.
Lakini kabla hatujawasili sehemu tuliyokusudia ndio tulipopata fursa nzuri ya kazi rasmi kabisa katika mgodi wa kuchimba Nickel ambapo kutokana na ukongwe na kazi yake ya udereva mjomba Boi aliambiwa kunahitajika madereva wa mitambo na maroli pale mgodini na safari hii hawaitaji watu kutokea Zimbabwe sababu ya kutokuwa watendaji wazuri wa kazi na kutaka maslahi makubwa.
Shida ikawa kwetu sasa, yaani hatujui hata kuwasha gari wakati huo, na magari yenyewe sasa mamitambo tu.
Basi ikawa Kama upepo tu tukaambiwa kama tupo tayari kila kitu tutajifunza huko huko kazini na sharti likiwa tutaanzia kuwa tunafanya kazi zozote tutakazo pangiwa hapo.
Moja kwa moja tukaelekea District ya tati huko ulipo mgodi wenyewe pembezoni kabisa kilomita chache tu kuingia nchini Zimbabwe kwa hayati Mugabe.

Kambi hapa nachungulia kila baada ya lisaa kama kuna apdate yeyote

Kambi hapa nachungulia kila baada ya lisaa kama kuna apdate yeyote
 
Tayari, ijapokuwa mtaniwia radhi naandika kidogo kidogo kutokana na ukosefu wa muda, pia changamoto katika uandishi kwa kutumia simu ya mkononi, maana macho yangu kidogo yana shida.
Muendelezo mwakani tena.
 
Tayari, ijapokuwa mtaniwia radhi naandika kidogo kidogo kutokana na ukosefu wa muda, pia changamoto katika uandishi kwa kutumia simu ya mkononi, maana macho yangu kidogo yana shida.
Sawasawa mtafutaji tuna subiria
 
Tayari, ijapokuwa mtaniwia radhi naandika kidogo kidogo kutokana na ukosefu wa muda, pia changamoto katika uandishi kwa kutumia simu ya mkononi, maana macho yangu kidogo yana shida.
Wala usijali mkuu mambo mazuri hayahitaji haraka. Story ya kuanzia wknd hii
 
We nae stori yako unaitoa vipande viwili alaf muendelezo n baada ya miez 8 Bora ukaushe tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom