Wakuu, leo nimekumbuka tukio la miaka 20 iliyopita. 😂 Nimeona si mbaya nikawasimulia ili tucheke kidogo, tufurahie simulizi, lakini pia tukumbuke kwamba maisha yanaweza kukugeukia kwa sekunde moja tu.
Mwaka 2006 nilikuwa nasafiri kwenda mkoani Iringa, kisha niende Njombe kwa ajili ya kufuatilia uhamisho wa mdogo wangu wa shule. Kipindi hicho nilikuwa below 20.
Nilifika Stendi ya Mabasi Ubungo mida ya saa 4 asubuhi. Nikakata tiketi, lakini bahati mbaya sikupata basi la moja kwa moja kwenda Iringa. Nikapata gari lililokuwa linaenda Kilombero, hivyo nikakata tiketi mpaka Mikumi. Gari ilikuwa inaondoka saa 6 mchana.
Kwa kuwa muda ulikuwepo, nikaamua kwanza nijipe nguvu. Nikala supu ya kuku na vitumbua, nikamalizia na Pepsi baridi. 😄 Baada ya hapo nikachukua maji yangu makubwa pamoja na biscuit za Eat Sum More, kisha nikaenda kukaa kwenye siti nikisubiri safari ianze.
Nikiwa nimekaa kwenye siti, akaingia jamaa mmoja akinionyesha simu nzuri sana ya Nokia 2600.
Kumbe yule alikuwa mzee wa change quarter.
Nikaanza kubargain. Nikamwambia:
Nilikuwa tayari nimepanga biashara kichwani. Nikaamini nikifika kwa cousin wangu, mume wake atanipa hela, halafu nitamuuzia ile simu kwa faida kidogo.
Jamaa akaanza kuringa.
Anadai simu ni mpya.
Anasema kaiokota.
Na kipindi kile... ushamba nilikuwa nao. 😂
Nikamuambia:
Nikampigia mume wa cousin wangu nikamweleza kila kitu.
Akanijibu:
Basi nikarudi kwa yule jamaa.
Akakubali deal.
Simu alikuwa ameifunga ndani ya bahasha ya kaki.
Gari ikawa inawaka.
Akanambia:
Nikazima simu yangu, nikatoa line, nikampa simu pamoja na shilingi 50,000.
Moyoni nilikuwa na uhakika kabisa kwamba nikifika Iringa nitauza ile Nokia kwa faida.
Tulipofika maeneo ya Tanesco ya zamani, yule jamaa akashuka.
Kabla hajashuka akanambia:
😂😂😂
Aliposhuka...
Ndipo nikafungua bahasha.
Nikafungua kwa hamu ili niweke line yangu.
Duh.😅
Ndani hakukuwa na Nokia.
Kulikuwa na kipande cha sabuni.
Mwili wote ulinilowa jasho.
Nilitamani kulia 😭.
Nilitamani kushuka😂.
Lakini nikawaza...
"Nikirudi nyumbani, Bi Mkubwa hatanielewa."
Huenda angenipiga na kuniumiza.
Nikabaki nimekaa.
Sielewi hata kesho itakuwaje.
Hata hamu ya kula sikuwa tena nayo.
Nilikuwa natamani kulia lakini machozi yalikuwa yanakataa kutoka.
Kwenye begi langu kulikuwa na diary niliyoandika namba za simu za watu wengi, mpaka watu wa Songea.
Kumbukeni...
Kipindi kile hakukuwa na Mobile Banking.
Ukipoteza hela, umezipoteza kweli.
Safari ya kuelekea Mikumi ilikuwa ya uchungu sana.
Tulifika Mikumi karibu saa 12 jioni.
Tukiwa tunakaribia kufika nikamuomba kondakta wa lile gari simu ili niwasiliane na mwenyeji wangu wa Iringa.
Jamaa akanipa simu.
Nikampigia.
Fresh tu.
Nikashuka pale njia panda.
Nilikuwa nimeingia kwenye huzuni na simanzi kubwa sana.😢
Nikauliza:
Nikaambiwa:
Nikaanza kutembea.
Nikawa nalia. 😂
Njiani nikakuta kibanda cha polisi.
Nikaenda kuwasalimia vizuri.
Nikawaomba:
Aisee...
Wale polisi walikuwa na roho ngumu.
Wakanifukuza kama mbwa.🐕
Wakanambia:
Halafu wakaongeza:
Niliondoka.
Sina msaada.
Sina nguvu.
Sina matumaini.
Bodaboda kipindi kile hazikuwepo.
Nikakodi baiskeli.
Jamaa akanipakiza mpaka sehemu magari yanaposhusha na kupakia abiria.
Nikampa shilingi mia mbili. 😄
Nikakaa pale kama dakika 25 hadi 30.
Kulikuwa na mbu wanene.🦟
Walikuwa wanang'ata balaa.
Mara likaja basi la Scandinavia VIP.
Wanaolikumbuka basi hilo wanajua.
Hata abiria wakiwa wachache, safari ilikuwa lazima iendelee.
Nikaingia.
Ndani kulikuwa na abiria wasiozidi ishirini.
Kondakta akaniangalia.
Uso wangu ulikuwa umejaa huzuni.
Macho yamevimba kwa kilio.
Akauliza:
Nikamsimulia kila kitu.
Nikalia tena.
Kilio cha kweli.
Jamaa akanambia:
Nilikaa.
Usingizi ukachukua nafasi ya huzuni.
Nilipoamka...
Tayari tulikuwa tumeshapita Mlima Kitonga.
Kondakta alikuwa ananionea huruma sana.
Akanipa soda.
Nikanywa.
Akanipa na cake walizokuwa wanagawiwa abiria.
Cha kushangaza...
Sikulipa nauli mpaka Iringa.
Mpaka leo simjui jina lake.
Lakini sitamsahau.
Tuliingia Iringa mjini saa 4 usiku.
Simu sikuwa nayo.
Nikaenda kwenye kibanda cha simu kumpigia mwenyeji wangu.
Hakupatikana.
Nikabaki nimekaa.
Baridi inanipiga.
Nilikuwa nimevaa sweta, lakini bado baridi ilikuwa kali.
Kama muujiza...
Akatokea jamaa mmoja.
Akaniuliza:
Nikamwambia:
Nikamtambulisha.
Ni dereva wa kampuni iliyokuwa inafanya safari za Iringa–Njombe.
Kumbe...
Walikuwa marafiki.
Jamaa akasema:
Nikamuambia aliyemuoa ni binamu yangu.
Jamaa akasema:
Sikuwa na namna.
Nilikuwa nimebaki na shilingi 24,350 tu.
Tukafika kwao.
Alikuwa anakaa na mama yake pamoja na wadogo zake wawili.
Yule jamaa alikuwa mkarimu sana.
Tulikuwa tunapiga stori nyingi za Songea.
Nikawa namtajia baadhi ya matajiri wa Songea waliokuwa marafiki wa karibu wa Mshua.
Jamaa alikuwa anafurahi sana. 😄
Mimi niliondoka Songea mwaka 2003.
Lakini nilikulia kule.
Mitaa.
Watu.
Majina.
Nilikuwa nawajua vizuri.
Hapo moyo ukaanza kutulia kidogo.
Tulipofika nyumbani kwa yule jamaa...
Akamwamsha mama yake usiku.
Akanitambulisha.
Nikamsalimia vizuri.
Tukaletewa chakula.
Maziwa ya moto.
Maandazi makubwa kama ngumi. ✊
Nikala andazi moja na kikombe cha maziwa na nikashiba.
Yeye akala kama manne. 😆
Kweli watu wanaokaa sehemu xa baridi wanakula sana.
Yule jamaa alikuwa na chumba na sebule.
Akatoa godoro sebuleni.
Yeye akalala sebuleni.
Mimi akanipisha chumbani.
Huo ulikuwa upendo wa hali ya juu.
Kuoga nikasema:
Nikapumzika vizuri.
Asubuhi saa mbili akaniamsha.
Nikaoga maji ya moto.
Tukanywa chai.
Na chapati za maji.
Nikashukuru sana.
Baada ya hapo tukaondoka.
Nikamuomba simu yake.
Nikampigia mwenyeji wangu.
Akapatikana.
Akaniambia:
Nikamsimulia mkasa wote.
Akamwelekeza yule jamaa nyumba kwake Kihesa.
Akanipeleka mpaka kwa cousin wangu tulipofika Cousin akatoka nje.
Nikamsimulia kila kitu.
Yule dereva akaulizwa:
Akasema:
Cousin akaingia ndani.
Akamlipa.
Cha kushangaza...
Jamaa alipopewa ile hela akanipa shilingi elfu moja.😄
Nikawa nimefika salama.
Baadaye nikaonyeshwa chumba cha kupumzika.
Mchana tukala.
Nikapumzika.
Usiku saa tatu yule shemeji akarudi.
Tukasalimiana.
Nikamwambia kesho naenda Njombe kufuatilia uhamisho wa dogo.
Kumbukeni...
Simu tayari nimeshatapeliwa.
Shilingi 50,000 zimekwenda.
Nilikuwa nimebaki na shilingi 25,350 tu baada ya kuongezewa ile elfu moja.
Kulipopambazuka...
Yule shemeji alikuwa tofauti kabisa.
Hakukuwa tena na ukarimu wa jana.
Hakukuwa na stori.
Nilianza tena kujiona mnyonge.😔
Akatoka haraka.
Nikamkimbilia.
Tukapanda daladala moja.
Cha kushangaza...
Hata nauli yangu hakunilipia.
Mimi nilikuwa bado natarajia tutapanda gari yake kwenda Njombe.
Lakini hali ilikuwa imebadilika.
Tulipofika alipokuwa anapaki gari...
Baada ya muda tukaondoka.
Alikuwa anaendesha Coaster Hiace.
Abiria walikuwa wengi.
Baadaye gari ikajaa.
Mimi nilikuwa nimekaa siti ya mbele.
Ghafla akanifokea.
Hapo nikaanza kuona vitimbi na manyanyaso.
Tulipofika Makambako njia panda ya Mbeya na Makete, tukasimama kwenye mgahawa.
Akaniambia:
Madereva walikuwa wanakula bure pale.
Tukala.
Safari ikaendelea.
Mwishowe tukaingia Njombe saa 9 alasiri.😂😂😂
Lakini kulikuwa na jambo ambalo sikulijua.
Yule dereva alikuwa na uhusiano wa kifamilia na Shangazi niliyokuwa naenda kwake.
Na baya zaidi...
Mimi zamani nilishawahi kumuandikia mume wa Shangazi barua za kumtukana na kumsema vibaya.
Yaani alikuwa Ba Mkwe wa huyo dereva.
Tulipofika stendi...
Mjomba akatokea.
Yule dereva akamshitakia kila kitu.
Halafu akanigeukia.
Halafu akaongeza.
😔😔😔
Nikabaki nimesimama Njombe Stand.
Kama kifaranga.
Sina mbele.
Sina nyuma.
Simu sina.
Na sielewi nifanye nini.
Itaendelea.........