Safari ya Andrew Chenge kuwania Uspika wa JMT

Chenge bado hawajamfukuza bungeni kwa tuhuma za pollonium 210?
 
Sasa kwa nini wanayafanya mafichoni?

kwa sababu ni wachawi... hivi unafikiri unaweza kuingia "Los Alamos" kiurahisi rahisi.. si na huko ni mafichoni vile vile.. au unataka watu wa infringe haki zao za ujuzi wa teknolojia nyeusi.? Mambo ya intellectual property rights yanawahusu wachawi pia. Ndio maana kuna wengine wamechukizwa na kitendo cha Mheshimiwa kutofa "onesho" la bure.
 
Ndugu zangu wadanganyika!...
Hivi lini mtashtukia vitu kama hivi?... yaani kila linalosemwa magazetini basi mnalichukulia kama ni habari njema maadam mhusika ni Fisadi...
jamani sio nyie mloandika mengi mabaya ya Six mwenyewe na kuwa yupo pale kwa mkono wa mafisadi?..
Siye huyu Sitta aliyesitisha vikao vya kwanza vinavyohusiana na Richmond hadi Kikwete alipoingilia na kuundwa kwa kamati maalum ya mheshimiwa Mwakyembe?. Haya toka report hiyo itoke ni lini huyu Spika kaiweka mbele zaidi ya hizi ahadi ambazo leo watuhumiwa wote bado wapo bungeni kama vile hapakutokea kitu.
Je, Mnakumbuka kuwa ni huyu spika kwa kumtetea fisadi Karamagi ndiye alipitisha kufungiwa kwa Zitto within week moja ya tukio bungeni lakini leo tunaona mangapi wabunge wakidanganya bungeni na hakuna hatua za kisheria kizichukuliwa!...
navosikia ni huyu tena Mr. Six anayesitisha hoja ya wabunge kuwaondoa wabunge wote mafisadi bungeni maadam bado wana nafasi zao ndani ya chama CCM kama wawakilishi. Kuondolewa kwa watu hawa Ubunge ina maana wilaya zao zitakuwa na mbunge wa Upinzani ama kura kurudiwa tena, CCM hawataki hilo litokee!...
Hivi kweli mnafikiria kama huyo alokutwa akiweka Ulozi sijui usiku angekuwa Mama yetu Anna, Dr.Slaa kungekuwa na mjadala zaidi!...
Jamani nyie jamani amkeni... Lowassa, Karamagi, Maghji wote hawa walipoteza nafasi zao ktk serikali kuu na hatukuwaona wakija bungeni usiku kutafuta kiti wakati viti vyote vitupu.. Sijui huyu mkuu angeweza vipi kuchagua kiti cha nyuma wakati wabunge hawapo vitini -hicho kiti vacant angekiona vipi?... Na hayo maswala ya kusema ati ingekuwa inconvinience kuchagua kiti wakati wa bunge linaanza ni uongo mtupu kwani wabunge siku zote hutoka nje kwenda chooni, wengine hawahudhulii kutokana na matatizo na hata wengine kuchelewa kidogo... Ni jambo la kawaida kabisa bungeni...Hivyo msitake kujenga hoja zaidi kumsikiliza mtu hapa..
Hizi hadithi za kushikana wao mashati haziwezi kuondoa fukuduku letu kuona hatua za kisheria zinachukuliwa haraka iwezekanavyo dhidi ya mafisadi wote!...
Na Mr. Six hadi sasa hivi hajanionyesha lolote dhidi ya Ufisadi isipokuwa kulindana...
 
Mkandara,

Hoja yako kwamba CCM wanahofia kupoteza viti vya wabunge kwa wapinzani mara baada ya kuwatosa mafisadi nadhani hiyo ndiyo inayowafanya CCM washindwe kuwachukulia hatua mafisadi. Fisadi yeyote atakayefukuzwa kwenye chama atakuwa kapoteza ubunge pia na hivyo kuitisha uchaguzi mdogo.

Hakuna fisadi ambaye atatoswa, bali watakaotoswa ni akina Mwakapugi, Mrindoko sijui na Hoseah na vidagaa wengine wadogo wadogo ambao walitumika kufanikisha dili la Richmonduli. Kutoswa kwa hao dagaa hakutakuwa na madhara kisiasa ama kupunguza wabunge wa Chama Tawala Bungeni maana kipindi hiki ni kibaya kuitisha uchaguzi mdogo huku chama kikiwa kimeelemewa na tuhuma za rushwa na ufisadi na huku serikali yake nayo ikiwa imegubikwa na wingu zito la ufisadi.

Hata kama CCM wanajiamini sana kwamba wananchi wataendelea kuwapa kura lakini nguvu itakayotumika kuendelea kuyashika majimbo hayo inaweza kuwa kubwa sana na pia mafisadi wanaweza kuamua kuhujumu uchaguzi huo ili kukikomoa chama tawala kwa ule msemo maarufu wa kijiweni kwamba ukimwaga mboga, mimi nitamwaga ugali ili wote tukose! CCM iko njia panda na ndiyo maana JK hajui hata afanye nini maana yuko kwenye dilemma.

Ngoja tusubiri tuone Pinda atatoa taarifa gani kuhusu mapendekezo ya Richmonduli.
 
Mhe.Chenge amedai kwamba Spika amemchafulia jina Nationally and Internationally.
He says he is going to push for a Parliamentary Disciplinary Committee to oversee this issue.
His Lawyers are going to act promptly.
Kivumbi hichooo!

Bado sijaona, na nataka kujua, Chenge amesema Sitta kafanya nini hasa!

Chenge amesema Sitta kamwambia yeye Mchawi?

Tanzania hakuna Press. Na hakuna anaejua kinachoendelea!

Tunajadili vitu ambavyo hata hatujui kama vinatokea kwa sababu hatuna Press.
 
Keil,
Hii ndiyo ngao kubwa ya CCM nba wengi wetu hapa tunafikiria kuna vita ndani ya CCM hali hawa watu bado wanalindana kwa manufaa ya chama..kisha tunaambiwa tusikilaumu chama kwa makosa ya watu binafsi as if hawa watu sio wawakilishi wa chama. Mazuri yote waliyoyafanya hawahawa watu binafsi ktk nyadhifazao ni hongera kwa CCM na ushahidi wao ndio huo wanauwakilisha bungeni kama mafanikio ya mwaka 2007...leo mabaya sio swala la chama ambacho bado kinawalinda ama kinajilinda... kisha hawa hawa wanamlalamikia Mugabe..Kuna tofauti gani ikiwa kosa ni kung'ang'ania madaraka!... mengine yote ni matokeo tu. Process ya Udikteta ni hiyo hiyo, viongozi wachache kuunda utawala wa mabavu.

Kuhani,
Hii ni habari ambayo binafsi hainishtui mshipa hata kidogo. Maswala yamefanyika Bungeni na kama kuna mashtaka yoyote ni lazima yaende kulingana na sheria za bunge, sijasikia Mr.Six akimtaja Chenge nje ya Bunge kama mhalifu ama mchawi, leo Chenge anataka kuyatoa Bungeni na kuyaweka nje ktk korti zetu ambazo sina uhakika wataanzia wapi!..Huyo wakili wake anafahamu sheria za bunge letu na yeye nani hata kuingia ktk kiti cha Spika kumwambia nini aseme na nini hana ruhusa ya kusema...
kwanza huyui Chenge alikuwa akitafuta kiti safu ya nyuma ilikuwaje akaenda hadi kiti cha Spika?... sasa kama wewe sii mchawi (mkemia mkuu) sijui atajieleza vipi ama kuna kiti kimoja karibu ubavuni mwa Spika nacho kilikuwa wazi!
 
Change+3.JPG


CHENGE AKIAPA, MKONO WA KULIA AMESHIKA BIBLIA TAKATIFU.

Fisadi Chenge akiapa Mungu amuepusha na hukumu ya mahakama pindi atakapolazimika kujiuzulu uwaziri.
 
Chenge bado hawajamfukuza bungeni kwa tuhuma za pollonium 210?

Toka lini watu huhukumiwa kwa tuhuma?
Ungesema wamsimamishe kuhudhuria vikao wakati uchunguzi ukiendelea, ingeleta mantiki kidogo...
 
kwanza huyui Chenge alikuwa akitafuta kiti safu ya nyuma ilikuwaje akaenda hadi kiti cha Spika?... sasa kama wewe sii mchawi (mkemia mkuu) sijui atajieleza vipi ama kuna kiti kimoja karibu ubavuni mwa Spika nacho kilikuwa wazi!

Speculations, Mkuu! Kama Mkuu mmoja alivyohoji, kwa nini asiende kwenye kiti cha Spika? Je kama alikuwa anataka kuona ni viti gani Spika anaviona kwa urahisi? Aliongozana na afisa wa bunge ili amwelekeze wapi anapostahili na wapi panamfaa! Je akisema kuwa afisa alimwambia waende akamwonyesha physically wapi anastahili kukaa?

Yote haya ni plausible. Kwa nini tumeshikilia ulozi?
 
Speculations, Mkuu! Kama Mkuu mmoja alivyohoji, kwa nini asiende kwenye kiti cha Spika? Je kama alikuwa anataka kuona ni viti gani Spika anaviona kwa urahisi? Aliongozana na afisa wa bunge ili amwelekeze wapi anapostahili na wapi panamfaa! Je akisema kuwa afisa alimwambia waende akamwonyesha physically wapi anastahili kukaa?

Yote haya ni plausible. Kwa nini tumeshikilia ulozi?

Wacheni kuupaka mafuta ni ulozi period! msomi mzima unaleta usangoma?? what a shame! halafu tuwalaumu wanao ua vibibi kule shy?
 
Nadhani hao lawyers wa Chenge wangemshauri jinsi nzuri ya kusafisha jina lake kuwa siyo kuwatishia 'nyau' wanaosema ukweli bali ni kuachia ubunge na kukaa kimya usubiri uchunguzi.

Tatizo hao ma-lawyer wake wanajua mzee ana 'vijisenti' kila kona hivyo kumshauri akae kimya ni kukosa mradi wao wa kila siku.S i mmesikia siku hizi watoto wa shule wakiulizwa unataka kuwa nani ukikua hawasemi tena mwanasheria wa mwalimu, wanataka kuwa MAFISADI!.Ufisadi siyo kuchota vya umma tu hata kujina uko sawa wakati unanuka nao ni ufisadi wa aina yake.

Tumwache apambane na mzee wa spidi na standadi kama anao ubavu.Haachi kutapatapa!
 
Wacheni kuupaka mafuta ni ulozi period! msomi mzima unaleta usangoma?? what a shame! halafu tuwalaumu wanao ua vibibi kule shy?

Contradictory dont you think! Kwa hiyo unataka tuamini kuwa wale wanaoua wazee kule shinyanga wanafanya jambo la maana! How do we conclude kuwa kilichofanyika ni ulozi? Hivi pale Bungeni una uhakika gani kuwa atakayekaa kwenye kiti ulichoweka dawa ni unayemkusudia! Please think objectively before uttering such strong words. Huwa naangalia pale Bungeni jinsi ambavyo wabunge wanazunguka zunguka kuongea na wenzao na jinsi ambavyo wengi wao wanachelewa au hawafiki kabisa. So you cannot with mathematical precision say that Mwakembe au Sitta will be in that morning so I should put poison in his seat. Na hiyo dawa sijui ni kwanini iwe that selective. Akikaa huyu, atoke aje akae mwingine haitamdhuru wa pili.

Ndugu zangu katika dunia hii ya kisayansi tujaribu kureason kisayansi, lest our young ones will not see a difference between ourselves na wale wanaoua vizee kule Shinyanga.
 
Nadhani hao lawyers wa Chenge wangemshauri jinsi nzuri ya kusafisha jina lake kuwa siyo kuwatishia 'nyau' wanaosema ukweli bali ni kuachia ubunge na kukaa kimya usubiri uchunguzi.

Tatizo hao ma-lawyer wake wanajua mzee ana 'vijisenti' kila kona hivyo kumshauri akae kimya ni kukosa mradi wao wa kila siku.S i mmesikia siku hizi watoto wa shule wakiulizwa unataka kuwa nani ukikua hawasemi tena mwanasheria wa mwalimu, wanataka kuwa MAFISADI!.Ufisadi siyo kuchota vya umma tu hata kujina uko sawa wakati unanuka nao ni ufisadi wa aina yake.

Tumwache apambane na mzee wa spidi na standadi kama anao ubavu.Haachi kutapatapa!

Yetu macho! Mnyantuzu na Mnyamwezi! Hawa ni visa tu, hakuna urozi hapo.
 
Nimesikia habari kupitia magazeti ya leo kwamba Chenge naye amechukua fomu ya kuwania uspika. Kulikuwa na tetesi kuwa ile kambi ya mafisadi wameamua kuongoza bunge katika nafasi ya uspika, chenge kuchukua fomu inamaanisha ni kweli kwamba jamaa wamepania ili wajisafishe (mafisadi) kwa kutumia uspika.

Hizi ni habari mbaya kwangu kwani hawa jamaa wana nguvu ya kifisadi wanaweza kuwashawishi wabunge uchwara (wa CCM) ili wawapigie kura na hivyo kuutwaa uspika.

Hivi kutakuwa na mijadala ya kifisadi tena, Bunge litakuwaje. Napata wasiwasi.

Wengine waliochukua fomu ni Anna Makinda na Samwel Sitta.
 
Mh. Tundu Lisu, Mh. JJ Myika, Mh. Freeman Mbowe, Mh. Halima Mdee, Mh. SUGU:
Ogopa sana hizo mashine hata kama spika na Lt. Gen Shimbo.
 
Well:Well:Well

Bunge lijalo halitazungmzia tena:-

- Meremeta/DEEP Green
- RichMond
- EPA/Kagoda
- E.T.C

Regardless nani ni SPIKA! Binafsi pia nisingependa kumsikia Mbunge akiongelea hayo masuala - Yabaki kama historia BASI!
 
Back
Top Bottom