Safari ya Andrew Chenge kuwania Uspika wa JMT

chenge au lowassa au rostam au ridhiwani moja wao akichaguliwa kuwa spika ndiyo biashara itakuwa imekwisha, maana hautasikia hoja za wapinzani zikijadiliwa. Hii itakuwa kama enzi ya uspika wa pius msekwa, alikuwa anapinga hoja za wapinzani live pamoja na kujua zilikuwa zinaukweli.


sitta ni mbaya kuliko chenge,sababu wote tunajua chenge na lowassa ni mafisadi lakini sitta ni fisadi anayejifanya anapambana na ufisadi..si unakumbuka issue ya richmond alivyoiua kibabe kuwatetea mafisadi wenzake...
 
Mimi ambacho nimesikia magazetini leo ni kwa Vijicent, Anna mbunge wa Same na Getrude ndio wameshachukua form....
 
Bora kwa ccm achukue yule mbunge wa kongwa anafaa kiasi..Bwana JOB NDUGAI...ila sitta nae anauzoefu na pia anaweza kuhimili mikikimikiki ya chama twawala.
Hivi kwa upande wa wapinzani bado hawajajipanga kwa hili la uspika?
 
Nilisikia kuwa endapo JK atakuwa raisi Lowasa atateuliwa kuwa Waziri Mkuu(Mwanakijiji akija atalielezea vizuri hili)
So sidhani kama atachukuwa fomu ya uspika.
.
 
Me hata sioni shida, naona kama Slaa hatashinda basi ni wazi Mnuso atatangazwa kuwa rais wa jamuhuri ya wadanganyika, so lowasa akiwa Spika basi Chenge awe waziri wa sheria na mambo ya katiba hapo ndo patakuwa patamu kwetu. Tutaanza kampeni baada ya Mafisadi kuapishwa (Kama Slaa atakuwa hakutangazwa kuwa mshindi)
 
SOURCE TBC , TAHARIFA YA HABARI SAA 2

Andrew chenge, mzee wa vijisent naye amechukua form ya kugombania usipika
 
CCM itakuwa mzoga kabisaaaaaaa. hawa wanavyoonekana kuna kitu wamejipanga na wanataka kukifanya na 2015 utaona kabisa EL anagombea urais
 
Ivi CCM kuna maadili ya viongozi kweli of all the people huyu nae anachukua form?
 
Kuna nini hapo ,mbona wanakimbilia sana? Hawa mafisadi sijui kama wana conscience!
 
Chenge achukue fomu kwani anastahili kuwa spika. Kuna tatizo gani kama mafisadi wanamchagua fisadi mwenzao awe kiongozi wao. Hivi Watazania bado tunaendelea kuulizia maadili katika safu ya viongozi wa CCM? Huo msamiati 'maadili' mnadhani bado upo? mbona watu mnataka kuvuna karanga wakati kilichopandwa ni mbigiri?
 
sasa mpira unakua kati aya mafisadi(kina chenge) na wapinga mafisadi(hata kama wanajiita tu ) kina Kilango lakini wanakinzana.......yetu macho tutaona nani atachukua?ila mtu kama chenge akipita naweza hata nikazimia tutakuwa hata tunawatukana wale wananchi wa jimbo la Mramba
 
sita anaweza kuwa na hali ngumu sana, mwaka coz mafisadi watakuwa wamempania na wameamua kuweka m2 wao
 
huyo chenge ataweza kuuzui moto wa akina tundu lisu,zitto,mbowe hapo bungeni?ni mwendelezo wa anguko la ccm
 
Back
Top Bottom