Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Amesema pia kuwa yeye ni mwanasisiem. hapo hamna shida. Sasa alizopeleka kwa chadema ni hizo, kwa nini sio kafu? Za jembe na nyundo ni trilion na hapa ndipo panategemewa zaidi.
Samahani kwa kurudia swali lilikwishajibiwa (sikuelewa jibu) Nini maana ya FISADI? na ina uhusano na ngazi/ madaraka/ kiwango cha pesa alichonacho mtu? Sie hatujawahi kuwa mafisadi au wahujumu uchumi na maendeleo ya nji yetu?
 
..Ni kweli kwamba huyu Mzee Sabodo ameanzia mbali kusema kile anachoamini hata kama ni against na mtazamo wa serikali na CCM ambayo yeye ni mwanachama wake. Amekuwa pia mstari wa mbele kutoa misaada mbali mbali ya kijamii. lakini kuna swali ambalo halipati majibu. Anafanya biashara gani kupitia makampuni yake yepi? Historia yake nini? tukiishajua haya, ndio angalau tunaweza kwenda mbele zaidi kupata picha halisi ya msaada wake kwa chadema. my two cent...
 
SABODO AICHANGIA CHADEMA MILIONI MIA MOJA

DSC09396.JPG


Juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, BW. Mustapha Jaffar Sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa leo jijini Dar. Chini Bw. Sabodo akiongea na Mh. Mbowe na Dk. Slaa

DSC09389.JPG


CHANZO:
Michuzi Blog
CHADEMA wapokea mshiko?

Kiwango cha juu kinachoweza kulipwa kwa hundi ni TShs 10 million, sasa kama hundi ni 100 million hiyo benki haipiti. Let us hope he meant to contribute otherwise it may be just a media show
 
SABODO AICHANGIA CHADEMA MILIONI MIA MOJA

DSC09396.JPG


Juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, BW. Mustapha Jaffar Sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa leo jijini Dar. Chini Bw. Sabodo akiongea na Mh. Mbowe na Dk. Slaa

DSC09389.JPG


CHANZO:
Michuzi Blog
CHADEMA wapokea mshiko?

ngoja usikie baada ya miezi kuwa anashitakiwa kwa kukwepa kodi... kwa kipindi cha miaka 10 iliyopita.... eheheee utadhani walikuwa hawajui... maanaake ndio ccm walivyo mfanyabiashara akiwachangia wanampa favour kibao akiwageuka wanafufua zile favour na kuziita makosa wanambandika... kama walivyomfanya mengi
 
Nna swali kwa wanaforum ni fisadi gani tena wa kidosi amewahi kununua ukurasa mzima wa magazeti Guardian, Daily news, Nipashe, Mwananchi na si mara moja kuikandia serikali pia CCM na sera zake??????????


Wakuu sijajibiwa swali langu!!!!!!!
 
Mustafa Jaffer Sabodo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Jump to: navigation, search
Mustafa Jaffer Sabodo was born in Lindi, Tanzania to Muslim Gujarati Indian immigrants of the Khoja sect. He is an economist, consultant in international debt-finance, philanthropist and a businessman. He has business interests in India, France, Kenya, Sudan and Zimbabwe.
In 2003, he offered to finance the growing of pulse for export to the tune of TZS 100 million.[1]
The Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery was the brainchild of Sabodo, who donated TZS 800 million towards a project that established the lottery.[2][3]
 
HabariLeo 23 April, 2009

Mfanyabiashara maarufu wa Dar es Salaam, Mustafa Sabodo ameahidi kumpatia Mbunge wa Mtwara Vijijini, Hawa Ghasia, Sh milioni 100 kwa ajili ya kununulia samani za Shule ya Sekondari ya Mustafa Sabodo iliyopo mkoani Mtwara. Sabodo alitoa ahadi hiyo mwanzoni mwa wiki hii mjini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliohudhuriwa na Ghasia ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma).

"Nafahamu kuwa ujenzi unakwenda vizuri na vijana wameanza masomo yao. Lakini nimepewa taarifa kuwa kuna matatizo ya samani. Naahidi kutoa shilingi milioni mia moja kumpa mama Ghasia ili zinunulie samani," alisema Sabodo na kuahidi kutoa fedha hizo baada ya kurejea kutoka Sudan atakakokwenda kwa shughuli zake.

Alisema mbali ya ujenzi unaoendelea wa sekondari hiyo ambayo mfanyabiashara huyo alitoa Sh bilioni moja kufadhili ujenzi wake, atahakikisha eneo la shule hiyo kunakuwapo na chuo cha ualimu na ufundi ili kuwawezesha wananchi wa Mtwara kufaidika zaidi kielimu. "Lengo langu la kuwa na chuo cha ualimu na ufundi, nitahakikisha linafikiwa. Nimepanga kutumia shilingi bilioni moja na laki mbili kufanikisha ujenzi huo pale (Mtwara)," alisema Sabodo na kutoa mwito kwa watu wenye uwezo kusaidia jamii katika maeneo tofauti.

Shule ya Sekondari ya Mustafa Sabodo iko eneo la Msijute katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara, na inajengwa kwa ufadhili wa mfanyabiashara huyo baada ya kutoa Sh bilioni moja katika harambee iliyoandaliwa na Ghasia mwaka 2007 jijini Dar es Salaam. Shule hiyo iliyo ndani ya ‘Mustafa Sabodo Education Centre' patakapojengwa chuo cha ualimu na ufundi, imeanza kidato cha kwanza chenye wanafunzi 95, na imekamilisha madarasa 14.
 
Kiranga,
Unachosema ni kweli kabisa. Na kwa hili tupo ukurasa mmoja. At least CHADEMA wamekuwa wawazi kuhusu wachangiaji wao tangu uchaguzi wa 2005. CCM hawajataja hata siku moj fedha zao zinatoka wapi. Kwa hili tuwapongeze. Sasa kwa next step ni kuchukua hatua kama walivyofanya hapa Marekani, kuweka limit ya michango ya matajiri, au ya kampuni, na michango hii ijulikane wazi, si kwa upinzani tu bali hata kwa chama tawala ambacho mpaka sasa kimekataa kutaja wachangiaji wake na kiasi kilichotolewa.

CCM asilani hawawezi tangaza kiasi walichopata na source yake labda mzee Makamba awe "RIP"...hivi mnataka yeye na wazee wenzake akina kingunge wakale wapi? Manji akitoa eti itangazwe, Jeetu naye atangazwe, hii italeta mtafaruku mkubwa ndani ya chama kwani kila mmoja atakuwa anajua ulaji ulioingia, Naungana na Makamba Noooooooooo kutangaza na hawakufanyi chochote kwani wewe umejiweka na kujijenga karibu na Mkulu wa kaya wao walie tu kwani hawajui Tz ya leo kila mtu na kamhogo kake? wasikuingilie kwenye anga zako hawa watoto wa juzijuzi wanaokuja na fikra mamboleo wakati macho wanayo lakini hawaoni uhalisia wa mambo, halafu lakini Mzee Makamba mambo yako nayazimiaga sana, juzi nimekuona kwenye kikao cha Dodoma mwanangu huchezi mbali na Mkulu wa nchi, mara umenong'ona hiki mara upindue karatasi, mara ukae vizuri kama vile unamuogopa mkulu halafu uko siriasi kama vile si wewe Makamba ama kweli unajua kula na vipofu na endelea hivyo hivyo kwani li nchi lenyewe ndivyo lilivyo, Halafu nisalimie Bumbuli kwa Mbunge mtarajiwa January mwambie mgosi.... "Onga Mahundo" na amudondoshe mzee Shellukindo taratibu asije akamvunja bure kwa mihela ya akina RA
 
SABODO AICHANGIA CHADEMA MILIONI MIA MOJA


DSC09396.JPG


Juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, BW. Mustapha Jaffar Sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa leo jijini Dar. Chini Bw. Sabodo akiongea na Mh. Mbowe na Dk. Slaa​

DSC09389.JPG

CHANZO: Michuzi Blog​

CHADEMA wapokea mshiko?​
Mzee wa watu atapona na biashara zake?
 
Yaani CHADEMA wameingia kwenye nyavu za CCM hivihivi. Hivi kuna muhindi gani mwenye jeuri ya kuchangia upinzani na kujitangaza hadharani?. Huyu jamaa katumwa afanye hivi makusudi, na lengo kuu ni kuiondoa hoja ya ufisadi katika uchaguzi huu. Yaani kwa kukubali hili chadema wamejitia kitanzi, upinzani kwisha kazi. Sasa chadema watapigia wapi kelele zao kuwa CCM inafadhiliwa na mafisadi wafanya biashara na wengi wao wenye asili ya asia?.

Haya shuguli imeisha sasa kwa mwenye akili timamu ni kwamba vita ya ufisadi leo ndiyo mwisho na kwa hili ninawaambieni hawawezi tena kuwashinda CCM kwa hoja hii. Shs Mil 100 ni hela ndogo sana kwa mafisadi na CCM kwa ujumla ila kwa wananchi wa kawaida hiyo ni big deal, na vyombo vya habari vimesetiwa kuionesha hii kwa walalahoi ili kuonesha kuwa anayechukua hela za wahindi ni CHADEMA si CCM. Underground CCM wamezikusanya zisizo na hesabu kama hivi ila kuwatega CHADEMA wawe publicized ni bao la kisigino kwa CCM.

Ukishakubali kuchangiwa na wafanyabiashara kiasi kikubwa cha fedha hivi, maana yake uwe tayari kuwalinda utakapochukua madaraka. Kwa hapa CCM= CHADEMA= CUF = Infinity!
 
...Eh? Please, elaborate!


Kwa mujibu wa mwongozo wa benki kuu, malipo yanayozidi 10 million yanatakuwa yalipwe kwa direct bank transfer i.e. mfumo wa TISS. Hiyo hundi ya 100 million haiwezi kupita benki, labda ni media show tuu baadaye akafanye direct transfer
 
Kiwango cha juu kinachoweza kulipwa kwa hundi ni TShs 10 million, sasa kama hundi ni 100 million hiyo benki haipiti. Let us hope he meant to contribute otherwise it may be just a media show

Mkuu wewe katika taratibu za kibank hutakuwa hujui hapo inafanyika TT Teregraphic Transfer
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom