Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo aichangia CHADEMA milioni mia moja

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ngambo Ngali, Jul 12, 2010.

 1. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,161
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  SABODO AICHANGIA CHADEMA MILIONI MIA MOJA

  [​IMG]

  Juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, BW. Mustapha Jaffar Sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa leo jijini Dar. Chini Bw. Sabodo akiongea na Mh. Mbowe na Dk. Slaa

  [​IMG]

  CHANZO:
  Michuzi Blog
  CHADEMA wapokea mshiko?
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  MKuu hii ya kujitangaza hadharani ndio mara yangu ya kwanza naona.
   
 3. p

  p53 JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 613
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kama chadema kachanga m100 tena waziwazi hivi,basi ccm usikute alishapeleka billions kadhaa.Ndiyo walivyo wafanyabiashara,wanauma huku na huku,ili walindwe na yeyote ateshika dola.
   
 4. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #4
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145


  Juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, BW. Mustapha Jaffar Sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Mh.Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa leo jijini Dar. Chini Bw. Sabodo akiongea na Mh. Mbowe na Dk. Slaa

  *ASIFU UMAKINI WAKE NDANI NA NJE YA BUNGE
  *AWAPONGEZA MBOWE NA DR SLAA
  *AAHIDI KUCHANGIA ZAIDI


  Mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, Mustapha Jaffar Sabodo amekichangia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA shilingi milioni mia moja ili kuimarisha upinzani na demokrasia nchini.

  Bw. Sabodo amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha leo jijini Dar kwa Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe aliyeambatana na Katibu Mkuu wake Dr Wilibrod Slaa na Mkurugenzi wa Fedha wa chama hicho Bw. Antony Komu.


  Akikabidhi hundi hiyo Bw. Sabodo amesema pamoja na kwamba yeye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi lakini anapenda kuona upinzani na demokrasia vinaimarika nchini huku akikitaja CHADEMA kuwa ni chama makini na safi cha upinzani.


  Bw. Sabodo amekuwa mmoja wa wazee walio wazi katika kukosoa utendaji wa serikali ya chama chake CCM hasa inapokiuka misingi ya utawala bora iliyojengwa na Mwasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.


  “Mimi ni mwanachama wa CCM lakini napenda kuona demokrasia ikikua huku kambi ya upinzani ikiimarika kwa kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini……na nawachangia CHADEMA kwa kuwa natambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa Bungeni”, Alisema.


  Bw. Sabodo amesema kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo la muhimu katika kutoa upinzani kwa CCM na kusukuma maendeleo ya wananchi huku akikitaka CHADEMA kuongeza nguvu zaidi katika harakati zake za kisiasa na kumwelezea Dr Slaa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchungu wa kweli na watanzania.


  Aidha Bw. Sabodo amesema ana mpango wa kuichangia fedha zaidi CHADEMA ili kuimarisha harakati zake za kisiasa na kuahidi kufanya hivyo atakaporejea nchini akitokea India kwenye matibabu.


  Akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa Bw. Sabodo Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameshukuru na kutaja msaada huo kuwa ni wa kihistoria katika siasa za vyama vingi nchini.


  Amesema mara nyingi imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa wa kada ya Bw. Sabodo kuchangia kwa uwazi tena kiasi kikubwa cha fedha na kutaka hatua hiyo kuigwa na wafanyabiashara wengine nchini.


  “Kwa kweli tunashukuru sana hii ni historia mpya katika siasa za vyama vingi nchini, ni wajibu wa wafanyabiashara wakubwa kuona umuhimu wa kusaidia vyama vyote makini nchini bili kuwa na ubaguzi wala woga, Mzee ameonyesha njia naamini itakuwa ni mfano kwa wengine wenye uwezo, Alisema Bw. Mbowe.


  Kwa upande wake, Katibu Mkuu Dr Slaa ameshukuru kwa mchango huo na kudokeza kwamba mchango utatumika kwa kadiri ya vipaumbele vitakavyopangwa kwenye Kamati Kuu ya chama inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 Julai 2010 ikilenga zaidi katika kutekeleza mipango endelevu ya kuimarisha chama kama Operesheni Sangara na utekelezaji wa mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.


  “Nawaomba watanzania wengine wa kada na uwezo mbalimbali kuichangia CHADEMA ili kuondokana na ukiritimba wa chama kimoja kwani ni hatari kwa maendeleo na usalama wa nchi kama michango yote ikielekezwa kwa chama tawala pekee.


  "Natoa mwito kwa vyombo vya dola kuacha kuwatisha watanzania wenye mapenzi mema wanaochangia vyama mbadala kama CHADEMA kwani kufanya hivyo ni kuhujumu taifa na kukwamisha maendeleo ya nchi”, alisema  Imetolewa tarehe 12 Julai na:  Erasto Tumbo

  Mkurugenzi wa Habari na Uenezi

  CHANZO: Habari hii imesambazwa na Erasto Tumbo kwa kushirikiana na John Mnyika kwa vyombo vya habari

  Mh! Interesting tunataka watu kama hawa but why Chadema?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,305
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  :sick:
   
 6. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #6
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,161
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kufika tarehe ya uchaguzi tutaona mengi
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,919
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Duuh hii safi sana na mfano wa kuigwa kutoka kwa Bw.sabodo.kweli watu sasa wanaanza kuonesha uwazi wa kuchukizwa na jinsi ccm wanaendesha mambo bila hata kuogopa huko mbeleni kitachotokea.


  Najua hapa kinachofuata ni Bw.Sabodo kuzushiwa kesi ya ajabu ajabu hili kummaliza,yetu macho na tutaona.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jul 12, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,161
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hapo sasa ndo patamu!!!!!!!
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Yes, this make a lot of sense!!!
   
 10. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #10
  Jul 12, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,623
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kuna wenzetu wako mbele kimawazo... huyo ni mmoja wao....
   
 11. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #11
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,352
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Hongera Bw. Sabodo, huu ni mfano mzuri tena tumefurahi kwa kuwa muwazi.

  Shida ipo kwa wazee wa kijani na njano; subirini watatuma watu kumtafuta katika shughuli zake, tena wakianzia TRA.

  Hata kama ni mlipaji mzuri, wata-frustrate tu hii.............
   
 12. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #12
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mkuu usemayo ni kweli kabisa, usishangae lile wimbi la kurudisha kadi za vyama kuelekea CCM likajirudia.
   
 13. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #13
  Jul 12, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,534
  Likes Received: 21,013
  Trophy Points: 280
  safi sana
   
 14. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #14
  Jul 12, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,586
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Yaani CHADEMA wameingia kwenye nyavu za CCM hivihivi. Hivi kuna muhindi gani mwenye jeuri ya kuchangia upinzani na kujitangaza hadharani?. Huyu jamaa katumwa afanye hivi makusudi, na lengo kuu ni kuiondoa hoja ya ufisadi katika uchaguzi huu. Yaani kwa kukubali hili chadema wamejitia kitanzi, upinzani kwisha kazi. Sasa chadema watapigia wapi kelele zao kuwa CCM inafadhiliwa na mafisadi wafanya biashara na wengi wao wenye asili ya asia?.

  Haya shuguli imeisha sasa kwa mwenye akili timamu ni kwamba vita ya ufisadi leo ndiyo mwisho na kwa hili ninawaambieni hawawezi tena kuwashinda CCM kwa hoja hii. Shs Mil 100 ni hela ndogo sana kwa mafisadi na CCM kwa ujumla ila kwa wananchi wa kawaida hiyo ni big deal, na vyombo vya habari vimesetiwa kuionesha hii kwa walalahoi ili kuonesha kuwa anayechukua hela za wahindi ni CHADEMA si CCM. Underground CCM wamezikusanya zisizo na hesabu kama hivi ila kuwatega CHADEMA wawe publicized ni bao la kisigino kwa CCM.
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Jul 12, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Angekichangia chama tawala angeitwa fisadi... siasa bana... nachoka kabisa!
   
 16. minda

  minda JF-Expert Member

  #16
  Jul 12, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,069
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tunataka watu wenye uweledi kama sabodo. Katika siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu.
   
 17. MwanaHaki

  MwanaHaki JF-Expert Member

  #17
  Jul 12, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,348
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Huyu CCM hawamwezi. Ndio maana ana ubavu! Wenzake hawajitangazi hadharani, wanatoa kimya kimya!
   
 18. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #18
  Jul 12, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,474
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  X-P
  Chama cha kudumu kimeshakuwa kifisadi. That is why.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Jul 12, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,069
  Likes Received: 5,194
  Trophy Points: 280
  Hili ni zuri na bora liwe hivyo tu mchango without any preconditions.. usije kugeuka kuwa mkopo. Wakajikuta anayechangia zaidi ndiye mwenye sauti zaidi kama "fulani"... good job!

  [​IMG]
  [​IMG]
   
 20. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #20
  Jul 12, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,919
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  nime kusoma hapa mkuu.
   
Loading...