Inaonekana wewe mgumu wa kuelewa sana.
Malalamiko yangu yote hapa yanazunguka the fact kwamba nchi yetu haina sheria za campaign finance, na kwamba mtu yeyote mwenye hela anaweza kuja kununua influence katika chama chochote na kupiga picha na mwenyekiti wa chama chochote cha siasa au hata rais ambaye naye ni mwenyekiti wa CCM, na kuanika picha hizi kwenye front pages za magazeti na hata mtandaoni, kuzidisha influence hiyo.
Si kila kitu kinachopigiwa kelele ni lazima kiwe uvunjaji wa sheria, ndiyo maana tuna bunge ili vinavyohitaji kutungiwa sheria vitungiwe. Ukiweka standards zako katika sheria utakuwa na standards zilizo chini sana, kwa sababu vipi kesho bunge likisema "rushwa" yote inahalalishwa kama "takrima" na isijali ukweli kwamba matajiri watakuwa na access kubwa zaidi kwaa vitu na huduma ?
Kitu kutokuwa na sheria ya kukikataza hakuna maana kwamba ni sawa kufanyika (sheria zina loopholes kibao za vitu ambavyo hatujavifikiria bado) na kitu kuwa sheria kukikataza hakuna maana kwamba ni kitu kizuri (kina Martin Luther King Jr. waliandamana kupingana na sheria dhalili zilizokataza watu weusi kukaa viti vya mbele kwenye mabasi.
Kwa hiyo kuuliza "kuna sheria gani imevunjwa" quite apart from being an absolving statement on the part of CHADEMA na huyu Sabodo, actually inaweza kuwa ndiyo outrage yenyewe kama nilivyo irepresent issue hapo juu.
Quite apart from absolving the parties kwa sababu hamna sheria iliyovunjwa, the fact kwamba hamna sheria iliyovunjwa ndiyo outrage yenyewe.
Ni kama vile unaenda sehemu nyumba ya mtu ambayo inatakiwa kuwa na usalama wa kutosha, halafu unakuta wamelala mlango wazi (mlango wazi hapo ni kwamba kuna uwazi wa rushwa) halafu unapouliza "nyie mbona mnalala mlango wazi, hamuogopi kuibiwa?"
Jibu unalopewa ni "Kwani tumevunja sheria gani kulala mlango wazi? Katika vitabu vyetu vya usalama hatukatazi kulala mlango wazi"
Ukisikia nyumba iko hivi ujue hawana security policy.
Nchi ambayo haina campaign finance laws za kukataza uncapped contributions au inayoruhusu outrageous contributions haiwezi kusema kwamba iko serious katika vita dhidi ya rushwa.
Chama kinachokibali mihela yote hii kutoka kwa mfanyabiashara mmoja, kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu kabla yangu, kinapoteza moral authority yote ya kusema ufisadi na rushwa katika uchaguzi.
Worse still, mfanyabiashara mwenyewe hata si mwanachama wao. Wengine tunaweza hata kusema officially CHADEMA imehongwa na CCM mchana kweupeeeee.