...Mkuu hawa sisiem huwa hawaeleweki kabisa siku zote wanapenda mambo mazuri yaende kwao tu. Hapo nina uhakika wale akina Chili..., Ma-rope na wengine utasikia tu siku si nyingi wanaanza kashfa!!....Tunataka watu wenye uweledi kama sabodo. Katika siasa hakuna rafiki au adui wa kudumu.
juu mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, bw. Mustapha jaffar sabodo akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 100 mwenyekiti wa taifa wa chadema mh.freeman mbowe aliyeambatana na katibu mkuu wake dr wilibrod slaa leo jijini dar. Chini bw. Sabodo akiongea na mh. Mbowe na dk. Slaa
*asifu umakini wake ndani na nje ya bunge
*awapongeza mbowe na dr slaa
*aahidi kuchangia zaidi
mfanyabiashara maarufu na muumini wa maendeleo ya kijamii nchini, mustapha jaffar sabodo amekichangia chama cha demokrasia na maendeleo-chadema shilingi milioni mia moja ili kuimarisha upinzani na demokrasia nchini.
Bw. Sabodo amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha leo jijini dar kwa mwenyekiti wa taifa wa chadema bw. Freeman mbowe aliyeambatana na katibu mkuu wake dr wilibrod slaa na mkurugenzi wa fedha wa chama hicho bw. Antony komu.
akikabidhi hundi hiyo bw. Sabodo amesema pamoja na kwamba yeye ni mwanachama wa chama cha mapinduzi lakini anapenda kuona upinzani na demokrasia vinaimarika nchini huku akikitaja chadema kuwa ni chama makini na safi cha upinzani.
bw. Sabodo amekuwa mmoja wa wazee walio wazi katika kukosoa utendaji wa serikali ya chama chake ccm hasa inapokiuka misingi ya utawala bora iliyojengwa na mwasisi wa tanzania mwalimu julius nyerere.
mimi ni mwanachama wa ccm lakini napenda kuona demokrasia ikikua huku kambi ya upinzani ikiimarika kwa kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini na nawachangia chadema kwa kuwa natambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa bungeni, alisema.
bw. Sabodo amesema kuongezeka kwa wabunge wa upinzani bungeni ni jambo la muhimu katika kutoa upinzani kwa ccm na kusukuma maendeleo ya wananchi huku akikitaka chadema kuongeza nguvu zaidi katika harakati zake za kisiasa na kumwelezea dr slaa kuwa ni mwanasiasa mwenye uchungu wa kweli na watanzania.
aidha bw. Sabodo amesema ana mpango wa kuichangia fedha zaidi chadema ili kuimarisha harakati zake za kisiasa na kuahidi kufanya hivyo atakaporejea nchini akitokea india kwenye matibabu.
akizungumza katika makabidhiano hayo yaliyofanyika nyumbani kwa bw. Sabodo mtaa wa upanga jijini dar es salaam mwenyekiti wa chadema freeman mbowe ameshukuru na kutaja msaada huo kuwa ni wa kihistoria katika siasa za vyama vingi nchini.
amesema mara nyingi imekuwa ni vigumu kwa wafanyabiashara wakubwa wa kada ya bw. Sabodo kuchangia kwa uwazi tena kiasi kikubwa cha fedha na kutaka hatua hiyo kuigwa na wafanyabiashara wengine nchini.
kwa kweli tunashukuru sana hii ni historia mpya katika siasa za vyama vingi nchini, ni wajibu wa wafanyabiashara wakubwa kuona umuhimu wa kusaidia vyama vyote makini nchini bili kuwa na ubaguzi wala woga, mzee ameonyesha njia naamini itakuwa ni mfano kwa wengine wenye uwezo, alisema bw. Mbowe.
kwa upande wake, katibu mkuu dr slaa ameshukuru kwa mchango huo na kudokeza kwamba mchango utatumika kwa kadiri ya vipaumbele vitakavyopangwa kwenye kamati kuu ya chama inayotarajiwa kufanyika tarehe 20 julai 2010 ikilenga zaidi katika kutekeleza mipango endelevu ya kuimarisha chama kama operesheni sangara na utekelezaji wa mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
nawaomba watanzania wengine wa kada na uwezo mbalimbali kuichangia chadema ili kuondokana na ukiritimba wa chama kimoja kwani ni hatari kwa maendeleo na usalama wa nchi kama michango yote ikielekezwa kwa chama tawala pekee.
"natoa mwito kwa vyombo vya dola kuacha kuwatisha watanzania wenye mapenzi mema wanaochangia vyama mbadala kama chadema kwani kufanya hivyo ni kuhujumu taifa na kukwamisha maendeleo ya nchi, alisema
imetolewa tarehe 12 julai na:
erasto tumbo
mkurugenzi wa habari na uenezi
chanzo: habari hii imesambazwa na erasto tumbo kwa kushirikiana na john mnyika kwa vyombo vya habari
mh! Interesting tunataka watu kama hawa but why chadema?
kwenye hizi picha huyu mzee anaonekana kama kapalalaizi au ni macho yangu tu?
wewe unalako jambo! wewe unafikiria bila michango na mali upinzani utasimama hiyo 100 million na mabilioni ya fedha zinazoibiwa tena za misaada (Sitta gave figures some times ago) kipi bora? sometimes it takes to befriend ur enemy to win! haswa ukizingatia jinsi system ilivyo repressive namna hii!This requires more than just transparency, we surely need transparency, but we also need caps on these amounts.
The best thieves steal in broad daylight, usidanganyike na show za photo ops.
Tujue kitu kimoja, kwamba bila sheria watu hawalazimiki ku act in the best interest of all, wata act in their own best interest. Bila strict campaign finance laws hawa matajiri pamoja na viongozi wa vyama vya kisiasa hawalazimiki ku act in the best interest of the people, and can easily cut deal consciously or even get into temptations and be trapped unconsciously.
Hata baada ya strict campaign finance laws, inabidi tuwe macho sana tu, sembuse sasa hivi ambako hatuna hata hizo sheria ?
Mimi hii supposed transparency hainipi any level of comfort at all, kwa sababu ukweli unabaki kibopa akichangia shilingi milioni 100 anapata power sana chamani na anaweza kutaka kulipwa fadhila kwa namna yoyote, na CHADEMA wakishaonja utamu wa mamilioni ya michango who is to say how will they react ?
T.H White katika "The Once and Future King" aliandika "What is not forbidden is compulsory" . Tusipokataza huu mwanya wa rushwa katika michango ya kampeni, tutawalazimisha wafanyabiashara wote watumie mbinu za michango ya kampeni kwa njia za kutoa rushwa.
wewe unalako jambo! wewe unafikiria bila michango na mali upinzani utasimama hiyo 100 million na mabilioni ya fedha zinazoibiwa tena za misaada (Sitta gave figures some times ago) kipi bora? sometimes it takes to befriend ur enemy to win! haswa ukizingatia jinsi system ilivyo repressive namna hii!
Sijakataa michango, nimeeleza umuhimu wa wanachama kuchangia vyama vyao, nimeeleza umuhimu wa wanachama ku own vyama vyao, nimeeleza hatari ya matajiri wachache kununua influence katika vyama vyetu visivyo na resources.
Mabilioni ya fedha za misaada kuibiwa ni vibaya, lakini kuibiwa huku kwa mabilioni ya fedha hakuhalalishi mianya ya rushwa mingine iachwe. Two wrongs do not make a right, wrong is wrong and will still be wrong.
Not having a tough campaign finance law is wrong. Chama kukubali michango mikubwa kutoka kwa matajiri wachache si sawa, unwaweka matajiri hawa na viongozi wa vyama katika temptation ya rushwa hata kama hawana nia hiyo.
I am not talking about winning or losing, I am talking principle. I bet you can't understand that. We are a nation without principles.
Hata hao wanaopigana against ufisadi hawaoni ubaya kupigwa picha wanapokea mihela kibao kutoka kwa matajiri. Hata hao wanaopinga ufisadi hapa JF wanaupinga ukiwa CCM tu, ukiwa CHADEMA mswano.
CHADEMA inanunuliwa na matajiri polepole, mwisho wake itakuwa haina tofauti na CCM.
Kwa kweli huyu mzee amefanya jambo la busara sana, anastahili kuungwa mkono na kila mtu mpenda demokrasia kwani itasaidia sana kuondoa ukiritimba wa chama TAWALA kudhani kwamba wao tu ndio wanaostahili kuchangiwa na wafanya biashara wakubwa.
Naamini kabisa huyu mheshimiwa si miongoni mwa mafisadi kwani angekuwa mmoja wao asingefanya hivyo.
Ahsante sana Mr Sabodo kwa ujasiri uliyouonesha kwa mstakabali wa demokrasia yetu.
Mkuu wewe katika taratibu za kibank hutakuwa hujui hapo inafanyika TT Teregraphic Transfer
Wapenda demokrasia wa kweli hawapendi matajiri wachache kununua influence katika vyama kwa jinsi ambayo inaweza kuzaa rushwa.
Demokrasia maana yake ni utawala wa wengi, wapenda demokrasia wa kweli watapenda sana vyama vya upinzani vikiweza ku raise hela kama hizi kutokana na michango ya wanachama wake in general, sio kutokana na mchango wa tajiri mmoja.
Michango kama hii amabayo kwa juu juu inaonekana kama inakuza demokrasia actually inaweza kuwa inaua demokrasia, in the sense kwamba tunaanza ku create tabaka la matajiri wanaokuwa na influence kubwa sana katika vyama vya siasa, na viongozi wa vyama vya siasa wanaokosa uhuru wa maamuzi kwa sababu ya utegemezi wao mkubwa kwa tabaka fulani dogo la matajiri.
Kwa hiyo wapenda demokrasia wa kweli wangependa kuona campaign finance laws zinawekwa kuondoa mianya ya rushwa, wangependa kuona Tanzania inaongeza GDP per capita, wangependa kuona Wtanzania wanaweza kuwa na disposable income na political awareness ya kutosha kuchangia vyama vyao.
Wapenda demokrasia wa kweli hawawezi kufurahia matajiri wachache kuchangia hela nyingi.Hii ni kualika disaster.
Naona watu hatuelewi maana ya ufisadi ndiyo maana Dr Slaa aliwaambia wapiganaji wa CCM wanapinga kitu wasichokijua ni kama wamedandia train kwa mbele.
Kuwa na hela nyingi si ufisadi ila channel iliyotumika kuzipata hizo hela ndiyo inaweza ku define ufisadi, ina maana mimi leo nikijitokeza kutoa mil.100 utaniita fisadi hata kama ulikuwa hunijui?
Kitendo cha Sabodo kina faida na hasara kwa upinzani lakini faida ndizo nyingi kuliko hasara, kwanza kimeonyesha kwa wananchi siasa si uadui kimetoa uoga waliokuwa nao hasa ndugu zetu jamii ya kiasia kila wakati uchaguzi unapokaribia.
Kimekijengea chama heshima mbele ya jamii kuwa Chadema haikujengwa kwa misingi ya matabaka watu wote ni sawa hii itafanya baadhi ya jamii ya kiasia kujiunga na kuvisaidia vyama vya upinzani.
Pia chama kime demonstrate sheria mpya ya uchaguzi kwa vitendo 'transparency' endapo kama nchi yetu ingekuwa ya kidemkrasia halisi viongozi waliotia saini sheria hii mpya wangekipongeza kitendo hiki.
Last but not least Chadema kinaendelea kuonekana ni chama cha kistaarabu kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na bunge, kwa vile kilikuwa na option ya kuamua kupokea kimya kimya na hakuna mtu yeyote angejua.
Leo watu wanakuja na maoni ya maximum limit kwa vile tu Chadema kimeamua kufuata sheria(to be transparent), unapofuata sheria vizuri ndipo utapokuwa na uwezo wa kugundua mapungufu yake otherwise sheria zisingefuatwa leo tusingekuja na wazo la maximum limit.
Naona watu hatuelewi maana ya ufisadi ndiyo maana Dr Slaa aliwaambia wapiganaji wa CCM wanapinga kitu wasichokijua ni kama wamedandia train kwa mbele.
Kuwa na hela nyingi si ufisadi ila channel uliyotumia kuzipata hizo hela ndiyo inaweza ku define ufisadi, ina maana mimi leo nikijitokeza kutoa mil.100 utaniita fisadi hata kama ulikuwa hunijui?
Kitendo cha Sabodo kina faida na hasara kwa upinzani lakini faida ndizo nyingi kuliko hasara, kwanza kimeonyesha kwa wananchi siasa si uadui kimetoa uoga waliokuwa nao hasa ndugu zetu jamii ya kiasia kila wakati uchaguzi unapokaribia.
Kimekijengea chama heshima mbele ya jamii kuwa Chadema haikujengwa kwa misingi ya matabaka watu wote ni sawa hii itafanya baadhi ya jamii ya kiasia kujiunga na kuvisaidia vyama vya upinzani.
Pia chama kime demonstrate sheria mpya ya uchaguzi kwa vitendo 'transparency' endapo kama nchi yetu ingekuwa ya kidemkrasia halisi viongozi waliotia saini sheria hii mpya wangekipongeza kitendo hiki.
Last but not least Chadema kinaendelea kuonekana ni chama cha kistaarabu kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na bunge, kwa vile kilikuwa na option ya kuamua kupokea kimya kimya na hakuna mtu yeyote angejua.
Leo watu wanakuja na maoni ya maximum limit kwa vile tu Chadema kimeamua kufuata sheria(to be transparent), unapofuata sheria vizuri ndipo utapokuwa na uwezo wa kugundua mapungufu yake otherwise sheria zisingefuatwa leo tusingekuja na wazo la maximum limit.
Asante majibu mengine huwa yanafariji. mkuu luteni nashukuru