Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Umejuaje kuwa fenesi lina ladha? Kwa nini usiulize ladha ya tofali? Kila jambo linaweza kuwa ndani ya uwezo wako mkuu, ikiwamo uwezo wa kuhoji kuhusu ladha ya fenesi. Ni zaidi ya kuwa na sense ya ladha. Binadamu akiamua, teknolojia inaweza kukusaidia kuteste ladha ya fenesi. We dont have to limit ourselves to our veryown created idea of God.

Asante sana kwa jibu hili
 
Hakuna lolote yote haya unayoyaona huku diniani ni sababu za uasi wa binadamu toka mwanzo.
Adamu angetii masharti aliyoambiwa na Mungu leo ungekuta tunaishi paradise life.
 
Just watched "God is not Dead" the movie kulikuwa na mtu ana idea kama hii lakini haikufanikiwa labda kwasababu ile ni movie. Kwani mtoa mada unaamini uwepo wa Mungu ?
 
Kwani mungu hakujua kwamba adam ataasi?
Swali mujarabu mkuu. Yaani maelezo ya jamaa ni sawa tu na angeuliza ni kwa nini Adam hakuongeza uvumilivu kidogo. Jambo lililokuwa ndani ya uwezo wake pia.

Wazo la Mungu ni ukomo wa kufikiri. Ni namna tu ya kupata majibu rahisi kwa maswali magumu. Kila jambo lipo ndani ya uwezo wetu.

Hata kifo kimefanywa kuwa kigumu mno kueleweka. Watu wameweka dhana za roho na mwili, mambo ambayo hayapo katu.

Eti roho inaacha mwili. Hivi injini ya gari inaposhindwa kufanya kabisa na ukashindwa hata kuibadilisha na hivyo gari likashindwa kufanya kazi kabisa, tunasema nini kimeacha nini?

Kwa viumbe hai, kuna kuwepo au kutokuwepo. Hali ya mifumo ya kiumbe hai kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ndio uwepo. Hali ya mifumo kushindwa kufanya kazi milele ni kutokuwepo (kufa). Ndio maana kiumbe huozaa na kupotea kabisa.
 
Sijajua wewe ni dini gani
But Mimi ni mkristo na siamimi katika moto wa milele Mungu atawaangamiza tu waovu wala hatawachoma milele naamini hizi theory za everlasting fire zilikuwa influenced na paganic concepts kama the so called "moto wa dante"

I believe God is not cruel as some depict him to be .And if he is merciful then it is meaningless kuchoma watu milele that's my belief
 
Umejuaje kuwa fenesi lina ladha? Kwa nini usiulize ladha ya tofali? Kila jambo linaweza kuwa ndani ya uwezo wako mkuu, ikiwamo uwezo wa kuhoji kuhusu ladha ya fenesi. Ni zaidi ya kuwa na sense ya ladha. Binadamu akiamua, teknolojia inaweza kukusaidia kuteste ladha ya fenesi. We dont have to limit ourselves to our veryown created idea of God.
Nimejua kuwa linaladha kwa sababu nimeambiwa lina ladha...sali ni ladha gani au utanielewesha vip nijue ladhayake ? Tumia tech yoyote kueleza ladha yake..kama vile unavyonisimulia sifa za mtu hadi napata picha..
Hapa ndio ugumu ulipo wa kumuelezea mungu haliyakuwa yupo beyond of our sense.
 
Sijajua wewe ni dini gani
But Mimi ni mkristo na siamimi katika moto wa milele Mungu atawaangamiza tu waovu wala hatawachoma milele naamini hizi theory za everlasting fire zilikuwa influenced na paganic concepts kama the so called "moto wa dante"

I believe God is not cruel as some depict him to be .And if he is merciful then it is meaningless kuchoma watu milele that's my belief
Mungu ni ukamilifu, ni unadhifu, ni uwepo, ni hali isiyo na doa, ni utu. Kwa hiyo hakuna namna Mungu anaweza kuwa mkatili, wa kulipiza kisasi, n.k. Mungu hayupo kama kitu kinachojitegemea, Mungu ni hali ya uwepo wa kila kitu, namna kilivyo na kinavyofanya kazi.

Je, tunaweza kuuona uhai wa jiwe? Kwamba uhai wa jiwe ni hali yake ya kutokuwa hai? Tusijisahau siye wanadamu kwa kuwa tupo hai tukajiona tumekamilika kuliko viumbe visivyo hai. uhai wa visivyo hai, ni hali ya kutokuwa hai kwavyo. Jiwe likiongea, tunashikwa na butwaa, siyo?

Mungu ni dhana nyepesi sana ikiwa tutakubali kuwa huru kifikra. Ila tukikubali kupokea tu yale tunayoaminishwa, dhana hii kwa hakika ni ngumu mno na nni utumwa mtakatifu.
 
Comments ni nyingi sana nimeshindwa kupitia zote, ningependa mwenye majibu au aliyeona post yenye majibu ya maswali ya hao jamaa anielekeze. Nampenda Mwenyezi Mungu ila kuna maswali mengi humo nami nimetamani kupata majibu yake.
 
mwenyezi Mungu ni hakimu muadilifu kuliko mahakimu ote .. Mwenyezi Mungu anaupendo mkubwa kwa watu wake .. amini kila mtu atapewa haki yake hakuna atakaye dhurumiwa
 
Mpende Mungu siku zote za maisha yako, usiache kumuabudu kwa kweli na haki usimkosee kwa kufanya dhambi.
 
My friend its easy to blame God for things than for man to take responsibilty for their actions. God gave us free will, the right to chose good and bad, right and wrong. He does not force us to chose Him simply because He wants us to chose Him as a result of love. But i understand your struggle because there has been times i have wondered why God gave us free will and why theirs so much suffering in the world. In it all i have see God work and move...and no God doesnt send us to hell, its we ourselves who do. Like the kiswahili saying says mtoto akililia wembe, mpe umkate. God kinda works in a similar way, He gives us His Word but if we dont accept it we can not blame Him for that but ourselves...and i appreciate your realness, its rare
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way He is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mm nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa ntakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo. So im just keeping it real.
Pole sana. Hasira zako ni justifiable to the limit of your knowledge about God. Sasa swali kwako, kwa nini unaendelea kukaa uovuni huku ukijua waovu watachomwa na huku ameweka wokovu bure kwa wanaotaka kuokolewa bure?
Ngoja nikupe dokezo. Mungu haumbi marobot ya kuenda kwa remote control yake. Badala yake anawapa viumbe wake uchaguzi wa uzima au mauti na huwezi kuvipata vyote kwa mpigo.
 
Back
Top Bottom