Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Sababu zinazonifanya nisimpende Mungu

Kila siku tunasema humu, kwamba HAKUNA mungu.Kama kuna mtu anaushahidi wa uwepo wa mwenyez mungu aweke ushahidi hapa ili ikiwezekana na mm nianze kuabudu.
 
Mwanaume mbishi hushikiki,nahis kama muumba aliekuumba unambishia ivo si ajabu viumbe vilivokuzunguka unaishi nao kwa tabu
Viumbe vilivyonizunguka vyote nimevikatia credit card za angalau USD $ 10,000 halafu haina bajeti.

Nalipa mimi.

Halafu navipet balaa.

Hujajibu swali.

Kwa nini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana kutokea, wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?
 
Swala la kuamini uwepo wa mungu ni swala la kuamua tu kwa maana hakuna ushahidi wa uwepo wake?
 
Swala la kuamini uwepo wa mungu ni swala la kuamua tu kwa maana hakuna ushahidi wa uwepo wake?
Kama vile unavyoweza kuamua kuamini Santa Claus yupo na anaishi North Pole.

Hakuna tofauti ya msingi kati yaimani hizi mbili.

800px-SantaWithKids2014.jpg
 
Kuna maswali mengi kuhusu Mungu huwa najiuliza, mpaka SAA nyingine huwa namkasirikia Mungu (maybe nakufuru lakini acha iwe hivyo).Bcoz kwa ninavomuwazia Mungu ingekuwa ni heri nisingezaliwa.

1) Kama kweli Mungu ni upendo, kwanini aumbe Jehanamu ya kutuchoma milele sisi tulio waovu (lyk for billions and trillions of years). Si heri angetumaliza tu kuliko kututesa milele? Kwenye shuhuda nyingine wakristo huenda motoni kwa dhambi moja tu ambayo hawakutubu. (I know hell was originally intended for the devil and his demons & not 4 humans)

2) Kwanini alimruhusu shetani kumjaribu Adam ikiwa alijua kuwa wanadamu wengi tutateseka duniani, tutaanguka maovuni, na atatutupa Jehanamu?

3) Kama Mungu anatuambia tukitenda dhambi na tusipomtii tutachomwa motoni, Je wakristo na waislamu (baadhi yetu) tutakuwa tunamtumikia Mungu kwasababu tunampenda na tunataka kumjua zaidi? Au tutakuwa tunamtumikia kwasababu tunaogopa kwenda Jehanamu?

4) Mungu husema mawazo yake si kama ya kwetu, na njia zake zipo juu zaidi, nakubaliana na hilo. Maybe kutuchoma motoni it's in his nature, that's the way he is and we have to live with it.

5)All in all Mungu ana hekima kuliko mimi, coz ni muumba wa kila kitu. Maybe katika hekima yake yote, hii ndo decision bora aliokuja nayo. Labda ana reason nzuri behind all this ambayo mm siijui. Maybe Mungu mwenyewe akinijibu face 2 face, nitabadili mtazamo wangu kuhusu yeye.

6) Kingine kinachonikasirisha pia ni yeye kuruhusu mimi kuja hapa duniani, naona ni heri nguvu aliotumia kuniumba mimi angetumia kufanya kitu kingine, nachukia + najuta kuwa hapa duniani to see all this, dunia imejaa waovu (mimi nikiwa mmoja wapo) pamoja na mateso ya kila namna.

Haya ndo mawazo yangu nimeamua ku-share nanyi, najua hata povu linitoke vipi it won't change the facts. Samahani kwa nitakaekuwa nimewakwaza humu jukwaani, naamini Mungu alishayajua mawazo yangu kuhusu yeye toka kitambo.

So im just keeping it real.
Mungu alikuumba na alikutuma! uwaokoe wengine walio danganywa na shetani! either katika familia yako au ukoo wako! ok, vyovyote vile!! Mungu alijua akikuleta, utamsaidia kufanya 1.2.3 katika kazi yake!! lakini pia alikupa na akiri, ya kutambua! pia alikupa na ulinzi! la sivyo ungepotea kitambo! leo unajeuri hata ya kuinua hicho kinywa still bado yuko nawe!, ilikuwa lazima uwepo, na katika uwepo wako, kunawatu watapatikana kupitia wewe! tatizo linalo kuja, pamoja na hivyo vitu vyoote,, wewe bado unaendelea kupiga dili na shetani! bado unaurafiki na yeye! bado unaendelea kumpinga Mungu! ndio maana, unaongea hayo, kwakuwa! roho ya kipingamizi yaani roho ya shetani ipo ndani yako! ndio maana poit ya kwanza kwako, umeiona ni kukosoa Mungu!! kwanini sio shetani! shetani ni mjomba wako? shetani ni nani kwako! think again and again! utagundua kusudi la Mungu kwako ni Neema,upendo amani na furaha!
 
Yote hayathibitishi kwamba Mungu yupo.

Na zaidi, yanaonyesha Mungu hayupo.

Chukulia kifo. Kinaonyesha Mungu hayupo.

Haiyumkiniki Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote aruhusu kifo kitenganishe viumbe wake wanaopendana na anaowapenda.

Kuwepo kwa kifo kunaonyesha Mungu huyo hayupo.

Habari nyingine ni hadithi tu.
Kwa hyo binadamu akifa,huishia hapo?
 
Kama unamchukia Mungu sababu ya jehanum take from me jehanum hakuna iliingizwa kimakosa kwenye biblia kwa rengo LA kuonya watu sasa hawa evangelist wamechukulia kama kitu halisi. So love your God he is there might and good.
Duh! Interesting ........., Kwa hiyo mkuu hakuna cha moto wala nini ni kula bata tu bila kujali umetenda mambo gani hapa duniani?
 
Pole sana Mkuu, lakini bahati mbaya ni kwamba unamchukia Mungu bila sababu kwa sababu zifuatato.
1. Kwanza unaweza thibisha kwamba Mungu anampango wa kumchoma mtu yeyote yule for billions & trillions of years kama ulivyosema, na pia ukathibisha juu ya hell kuandiliwa kwa ajiri ya Devil & Demons na sio Binaadamu kama ulivyosema.

2. Kuhusu Adamu, ule ni ujinga wake mwenyewe sababu kila kitu alichoelezwa na Shetani alikuwa ameisha elezwa na Mungu lakini akaamua kumsikiliza shetani, na alielezwa madhara ya maamuzi ya kwenda kinyume na maelekezo ya Mungu lakini akafanya, hapo unamulaumu Mungu kivipi?

3. Swala la kuchomana moto, kama nilivyokuomba kwenye no.1 hapo juu, thibitisha kwamba Mungu anampango huo.
4. Naona unaogopa sana Moto, thibisha kama amesema anampango kwa kukuchoma.
5. Thibitisha hayo mambo ya moto wako.
6. Swala la kujutia kuja duniani ntalichangia ukielezea mambo ya moto kwanza.

Wasalaam.
 
Mtoa mada ndani ya siku chache utakufa. Tafuta mtu wako karibu aje atupe TANZIA yako. Usimjaribu Bwana Mungu na Muumba wako. Naona unachokitafuta utakipata tu.
Ungekaa kimya ungeficha upumbavu wako,ona sasa umeongea wote tunajua.Vitu vingine msikurupuke kujibu, mambo ya Mungu hayahitaji mihemuko.
 
Yohana 3:16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
 
Ungekaa kimya ungeficha upumbavu wako,ona sasa umeongea wote tunajua.Vitu vingine msikurupuke kujibu, mambo ya Mungu hayahitaji mihemuko.
Nadhani we ndo mpumbavu mkuu. Tena mshenzi mkubwa. Ungekaa kimya maana sikumquote mtu.
 
Duh! Interesting ........., Kwa hiyo mkuu hakuna cha moto wala nini ni kula bata tu bila kujali umetenda mambo gani hapa duniani?
Kamahakuna moto wala mbingu,hiyo ni sababu kubwa sana ya kufanya mema hapa duniani na kuifanya hii dunia kuwa kama mbingu. Heaven on earth.
 
Huu uzi utafika mahal watu watatoleana matusi,jaman mnaoamin mungu yupo msibishane na hawa wasiaf wanaomfuata lucifer,jibu kubwa na lamaana ni kukaa kimya kutokujib kitu
 
1.kukujib swal la kwanza,..ndio ana councious kamil kabsa ila ni wel developed,imagine the councious iliyopo everywea.councios iliyo vunja laws of matter.(hop unazijua laws of matter)..kwasabab huwez tengneza kitu usichokijua maana yake,iwapo bnadam ana councious je ambae created him itakuaje.2.chanzo chake ni swali gum ambalo halina jibu,..na ndomana hata maandiko meng ya wanadam yameshindwa,kwa akili yangu ndogo hili jib limeshindikana,nikiweza jib hil bas namim ntakua Mungu.3.lengo la uumbaji ni lengo binafsi la any councious,hata wew kuna vitu unaweza amka tuu asubuh ukaanza vifanya,ni moja ya projects zake mwenyew binafsi na uwezo wake,kama wew unaeza amka asubuh ukasema,wel kwa nafas yangu ya kiuchumi n elim yangu let me make labda viatu vya ngoz or chuma,wateva,u do wat u like..so its a project.4.ushahid,ni kwamba,kuna pande mbili za mifumo ulimwenguni,mfumo hai na mfumo usio hai.jinsi mifumo ambayo sio hai creation zake mara nying hua random,yan mfumo unaojitengeneza ambao hau involve any councios ya being mingi hua inakua random,ila,mifumo ambayo hua inakua created na councious hua ina create vitu vyenye mifumo systematic,sasa ukiangalia,mifumo ya ulimwengu yote ni systematic,kuanzia sayar kuzunguka nyota,au mwili wa binadam ni ushahid tosha ,kwa madaktar watathibitisha haya,na kwa wanasayans ya atomic watathibitisha haya,so hili linatupa mwangaza kua kuna a councious ambayo ina lead haya yote.jinsi viumbe hai vnavyotegemeana ,etc ni vtu complex kwakwel.5.wanasayansi hufanya mambo kwa ku reason na pia,hutumia laws of nature kutafsiri maswala mbalimbali,kutokana na the great creator kuumba ulimwengu kwa kutumia sayansi basi kuna baadhi ya mantiki hua wanazi discuss,halaf wanasayans weng sio kwamba hukataa kua creator or the initiator of all hayuko,hukubali hili,ndomana hata einstein mwanasayans namba moja alikubali,..wasichokubal ni stori hizi zilizopo ambazo znalengo la kushape watu kwenye mlengo fulani,na reasoning ya watu wa religion hua very cheap yan mtu mwenye akili zake akiskia hua anaona ni kama hamna kitu or ni pumba ndomana hua hawatak kujishugulisha,
Kuna points za kisomi ndani ya ulichoandika.

Tatizo umeandika kama vile umemsikia msimamizi wa mtihani akisema

"three minutes left"
 
Back
Top Bottom