Mungu, Nafsi, na Uumbaji Tafsiri Mpya ya "Aliyeitwa"

Mungu, Nafsi, na Uumbaji Tafsiri Mpya ya "Aliyeitwa"

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
136
Reaction score
292
Mungu, Nafsi, na Uumbaji Tafsiri Mpya ya "Aliyeitwa"

“Mungu” Ni Nani?
Neno "Mungu", kwa kiingereza "God", linatokana na chimbuko la Kijerumani la kale, likimaanisha "aliyeitwa" au "the invoked." Hili ni neno la uwakilishi, si jina takatifu kama vile "YHWH" katika Uyahudi, ambalo hutajwa kwa heshima kuu na hata matamshi yake halisi hufichwa kimakusudi. Kwa hiyo, hata kabla ya kuuliza “Mungu ni nani?”, tunapaswa kuuliza: “Tunamwelewa vipi huyo tunayemwita Mungu?”
Katika tamaduni nyingi za binadamu, kuna imani ya kuwa kuna uwepo wa juu, nguvu fulani isiyo ya kawaida, inayovukwa mipaka ya maumbile. Kwa kuwa neno "Mungu" lina maana ya "aliyeitwa", basi kilicho muhimu zaidi ni kitu au yule tunayemwita — na hapa ndipo dhana ya Mungu huanza kugeuka kuwa ya kibinafsi, ya kiutamaduni, na ya kimaisha.

SOTE TUNAMWITA MTU/FIKRA HATA WANAODAI KUWA HAWAAMINI
Atheism (kutokuamini katika Mungu) hufasiliwa kama ukosefu wa imani katika uwepo wa Mungu. Lakini, kama Mungu ni "aliyeitwa" – basi swali ni: nani au nini unamwita kwenye akili yako unapohitaji msaada, maana, au mwelekeo?
Atheist anaweza kusema haamini Mungu, lakini anaita sayansi, akili, au maumbile atakapopata changamoto.

Mtaalamu wa akili anaweza kusema haamini Mungu, lakini anaamini kwenye muundo wa akili na tabia za binadamu.

Mwanamazingira anaamini ardhi ni mama, na anajitoa kuilinda — hiyo ni "invocation" pia.


Kwa hivyo, tunaweza kusema: Sote tuna Mungu wetu — lakini hatumwiti kwa jina moja.

Mungu Wangu Ni Uhalisia Usioonekana: Chanzo cha Uhai na Maumbile

Mimi ni muumini wa uhalisia ulio juu ya kuona.
Uhalisia unaoeleza:

kwa nini ulimwengu upo,

kwa nini kuna uhai,

kwa nini mimi nipo.


Huu uhalisia ni Mungu wangu. Si lazima awe mtu. Anaweza kuwa impersonal (kama nguvu ya fizikia), lakini pia personalised (anavyojitokeza katika viumbe hai kama mimi na wewe).

Mungu huyu wangu amejificha kwenye sheria za fizikia, kemia, na baiolojia. Tunaambatanisha nguvu ya uvutano (gravity) au mwanga (light) kama vitu vya kawaida, lakini vimebeba muundo na utulivu wa ulimwengu mzima. Katika kutafuta kuelewa hizo sheria, tunamwita Mungu hata bila kulitambua.

Mungu Kama Mfumo wa Uwezekano Usio na Mwisho

String theory — nadharia ya kisayansi inayojaribu kueleza muungano wa kila kitu — inasema uhalisia wetu unaundwa na mitetemo midogo kama nyuzi za muziki. Nadharia hii husema mitetemo hiyo hufanya ulimwengu "uimbe" kwa muundo wake maalum.

Kwenye mtazamo huu:

Mungu ni seti isiyo na mwisho ya mitetemo chanya, iliyopangwa vizuri, na inayozaa uhalisia wenye uwiano.



Kila ulimwengu unaweza kuwa mafanikio ya aina yake ya “Mungu.” Ulimwengu wetu una mungu wake — mwingine unaweza kuwa na muundo tofauti, sheria tofauti, maisha tofauti. Hii inazua wazo la kwamba kuna “Miungu mingi” (Gods) — lakini kila mmoja akiwa ni mionekano ya UMOJA mmoja: uwepo usio na mipaka.

Mungu na Nafsi ya Binadamu

Ndani ya mwanadamu, kuna kitu tofauti. Tuna uwezo wa:

kutafakari uhalisia wetu,

kuumba vitu vipya,

kuamua kati ya jema na baya.


Huu ni uwezo wa kipekee.
Ni kitu kinachomfanya binadamu kuwa mpenyo wa Mungu katika jambo la kuumba.

Kama tutaamini kuwa uumbaji ni tabia ya Mungu, basi kila binadamu anayechagua kuumba — kwa wazo, kwa kitendo, au kwa maadili — anajionyesha kama sura ya Mungu.

Roho ya Mungu vs. Ufahamu wa Binadamu

Zamani waliita “Roho ya Mungu.” Leo tunaiita Consciousness — akili ya uhalisia.

Ulimwengu umejengwa na ufahamu (consciousness). Na akili ya mwanadamu inaweza kuwasiliana na hiyo consciousness ya juu – Mungu.

Hapo ndipo mtu hupata:

msukumo wa wazo jipya,

ndoto kubwa isiyoisha,

msukumo wa kimaadili unaopita tamaa ya kibinadamu.


Na katika kila hatua ya uumbaji, uhuru wa kuchagua (free will) ni silaha takatifu zaidi.
Kama Mungu ndiye chimbuko la kila chaguo la kweli — basi binadamu pekee ndiye viumbe anayeweza kuwa karibu naye.


Mungu ni Nani Basi?

Mungu ni uhalisia ulio na maelewano ya milele (infinite harmony).
Mungu ni mwalimu asiyeonekana wa sheria zote za maisha.
Mungu ni ndani ya wimbo wa maisha, ndani ya mwanga, ndani ya akili ya mwanadamu, ndani ya chaguo la kutenda jema.

Kazi ya Mungu Ni Nini?

Kazi ya Mungu ni KUUMBA na KUSTAWISHA UWIANO (balance).
Ndiyo maana kuna maisha, ndoto, na sheria zisizovunjika.



Na kazi yetu sisi binadamu ni kuiga hiyo asili ya Mungu — kwa kuumba, kwa kuunganisha, kwa kuleta uwiano. Maisha yenye uwiano ni maisha yenye utulivu, furaha, na thamani.

Mwanadamu Kama Mrithi wa Uumbaji

“Kuumba ni zawadi. Kuishi ni fursa ya kuonesha asili ya Mungu katika mwili.”



Mimi ni muumini.
Najua Mungu, na najua kuwa Mungu ananijua.
Sote ni miwani inayopenyesha nuru ya Mungu.
Na tumepewa uhuru wa kuchagua kuwa kama Yeye.

Furahia maisha. Simama. Uumbe.
Hiyo ndiyo ibada halisi.

By It's MalekoGJ

On X @GoodluckMalekoJ
 
Mungu analo jina.

Na Mungu ni mmoja tu,

Na JINA LA Mungu huyo mmoja aliyekuja Katika mwili wa Mwanadamu ni Yesu Kristo /Yeshua Hamashiach
 
Huo ni uzushi.
Hakuna Atheist wa namna hiyo.
 
Back
Top Bottom