Kuna mmoja nikakuta kazalishwa ila mtoto wake yuko kwa bibi yake ambaye ni mama wa ex wake.
Nikasema hapa sawa nitaishi na huyu kwa vile haishi na mtoto maana kuitwa baba nikavimba ilihal sio damu yangu nisimgeweza kabisa, au sijui school fees 1.5m ya medium school naambiwa baby mlipie mwanetu, ilihal ndugu zangu kijijin wanatembea naashati yamechanika mgongoni nisingeweza kabisa.
Basi ikafika siku ikapigwa simu na yule mama wa x wake anaeishi na mtoto kafura kweli kweli, eti mmenikabidhi mtoto hapa na kila mmoja wenu anakula bata mm nahangaika na mwanenu, augue nimtibu, nimfulie, nihakikishe kala na kalala, nyie mpo mpo tu hata nikiwaambia kuna uhitaji wa swala fulani jibu lenu nisubiri hamna fedha sasa kwa nini mlizaa?
Jumamosi hii ufike Mkoani nilipo tujue mwafaka wa malezi ya huyu mtoto. Mdada akaniaga bwana nimeitwa kwa mwanangu ngoja niende chapu na kurudi, nikaona swala la mtoto ni sensitive na hata nikimkataza tutaishia lumbana kwamba sijali mwanae.
Huyoo akaenda zake, kumbe yule ex wake kaambiwa afike same day wapate mwafaka, [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] jioni kuna chumba pale analala mdada wa yule maza, akaambiwa fulani utoe vutu vyako hicho chumba cha nje uwaachie hawa nafasi ya kulala.
Piga simu usiku haipatikan, mpaka saa tatu asubuhi mtu katafuta upenyo sijui kajifanya anaenda dukan nunua sukari ndo kunipigia, naambiwa sorry sana mme wangu ni story ndefu kukuelezea kuwa mvumilivu nikija nitakuambia nini kilijiri hapa, ila kuaa na amani.
Alivyokuja nilivyombana kwa sura ya ukali zaidi ndo kunambia hilo jibu kwamba aliaambiwa fulani wapishe fulani na fulani chumba che nje walale je ungekuwa wewe mme wangu ungekataa wakat wenyeji ndo wanapanga namna ya kulala pale kwao.
Ila tulilala tu hatukufanya lolote maana siwez fanya na mtu sijamuona muda mrefu sijui afya yake.
Alivyobanwa vizuri akasema tulifanya kamoja tu kwa kunilazimisha [emoji3][emoji3][emoji2]
Nikaamin single Mother sio wako na huna Mamlaka nae.