Sababu za mke kumdharau Mume nyumbani

Sababu za mke kumdharau Mume nyumbani

.................................................
7. Si kwamba huna pesa basi tu hujui majukumu yako
8. Ubabe usio na maana wakati unaonekana kabisa kuwa huwezikuimudu familia- sasa mama akiamua kutake charge -mnalalamika ni dharau/ubeijing n.k.

Hilo ndio tatizo. Una-take charge kutoka na kwenda wapi? Unapindua nyumba au ni kiburi tu. Mwanamke mwenye busara ha-take charge anabadilisha weaknesses za mumewe na kuwa strenghes na sio ku-take charge.
 
Tangawizi ndio maana nasema si mara zote mwanamke anaamua tu kumdharau mume pasipo sababu. Lakini pia mwanamke asiyejua majukumu yake kama mke kwka wote mume na familia kwa ujumla anajichimbia kaburi la dharau.
- Mwenye tamaa kupita uwezo- we kila siku mume akirudi unadai mara chain, mara perfume na ukiona vipi basi wakopa hata bila ya idhini yake atajiju- lazima akuone uko unreasonable. Kuna kina wenzie na sisi ambao wana vijipato vyao- basi hata kama anafanya kazi na pesa ni yake basi atatumia apendavyo atanunua atakavyo - ni sawa but bado mume anayo nafasi yake kumwomba ushauri au kushauriana- huwezi tu kurupuka eti una pesa yake basi mume anarudi analikuta liji-hammer limepaki hapo eti umejinunulia (labda kama ni zawadi ya Mr!!)
Kosa kubwa linalofanyika kwa kizazi chetu ni kuchukua juu juu suala muhimu la mahusiano ndani ya ndoa. Kigezo kisiwe ni pesa na maisha ya kifahari na kusahau kuwa pesa ni kitu kinachoweza kutafutwa. Ila working relationship sio kitu rahisi kama tunavyoona kabla ya kuingia kwenye ndoa. Mwanaume akikutongoza kwa hela jua atakuendesha kwa hizo hizo hela maana una uhakika gani hata muona mwingine akamuhonga au kumshawishi nawe mpenzi wake/ Na sisi wanaume wengi ndo tumekuwa kina baba haambiliki. Yote tunajua sisi, uongo mwingi, nyumba ndogo zakutosha yaani hizi ndoa zimekuwa balaa.
Ila kina mama wengi nao siku hizi hawajabaki nyuma.Tunaenda nao sambamba.
 
......Ni kweli kabisa

hapo kwenye red ni mada inayojitosheleza maana ukisema uulize sababu za kina baba kuwa na nyumba ndogo utaambiwa ni mke nyumbani ila kwa kina mama itabidi uanzishe mada Tangawizi.
 
Haahaaa, naona ni kujifunza tu namna michezo ya luninga inavyotuelekeza.Sijui tumechulia rahisi sana kuanzisha mahusiano kiasi kwamba we have reached a point where we do not care anymore?
Anyway, mimi kama baba naomba amani na utulivu ili nijifunze kusikiliza mke wangu hata kama ntaona ananipigia makelele tu.
 
Ukweli uliovua nguo ni kwamba mwanamume asiyemfikisha mke wake "kileleni" atadharauliwa!

Mengine ni matokeo tu! Kitu pekee kinacho keep stong bond kwenye ndoa NI tendo la ndoa timilifu.

...aaah wapi! akiamua kukutafutia sababu hata hiyo nguvu ya utimilifu itakuwepo kaka? ...Utasimamia vidole na macho kuikodoa, mwenzio ana 'fake' tu!
 
Akina baba nao wakipata tu Nyumba ndo ni dharau tosha kwa wife ..
Ataanza mambo ya kumlinganisha mke na nyumba ndogo
tayari dharau ndani ya nyumba itaanza

...hao ni wale wachache wanaoshindwa kutofautisha baina ya "making love to a darling wife", na "having sex with 'nyumba ndogo'."
Muwasamehe tu kwani hawajui wayatendayo.
 
Hilo ndio tatizo. Una-take charge kutoka na kwenda wapi? Unapindua nyumba au ni kiburi tu. Mwanamke mwenye busara ha-take charge anabadilisha weaknesses za mumewe na kuwa strenghes na sio ku-take charge.
NAdhani hujanielewa hapa nina maanisha kutake charge ya kuhudumia familia yaani kama kila ukimwomba huduma za nyumbani mfano nyumba inahitaji kukarabatiwa au watoto wanatakiwa kulipiwa ada na kila siku unamwambia mumeo juu ya hili lakini hakuna linalofanyika nikiamua kutake charge yaani nihangaike nitafute resources nitoe hizo missing huduma mnalalamika

Umenena vema tunatakiwa kuchange weakness za waume zetu na kuzifanya strength- how about you guys accepting our weakness before running to the hands of nyumba ndogos?
 
Wote tuna weakness, ila nyumba ndogo ni tabia zetu tu za kutaka kula kila kinachoonekana mbele yetu. Hata hivyo wanawake nao wana contribution kubwa katika kuendeleza nyumba ndogo maana mtu anajua umeoa, ila yumo tu, tena mara nyingine kwa kutumia all power in her hands. Unategemea itakuwaje sasa?
Si tabia nzuri, tuombe Mungu tuache na kujirekebisha.
 
kama alikuwa na wanaume wengi kipindi cha nyuma na akikulinganisha na wewe anaona hauna lolote, hovyo hapo ameolewa na wewe kwaajili ya pesa tu labda, siyo mambo mengine ya ndani. hapo ndo mtajua umuhimu wa kumwomba Mungu akupatie kifaa kipyaaaa, au walau ambacho hakijasasambuliwa mara nyingi. hata kama ukiwa unamdunda kila siku, kama anaona unamfaa ndani ya chumbani, atakuheshimu tu. sasa, akiwa hakuwa amejitunza, yaani alikubuhu kipindi cha nyuma, ukamdunda na ndani kwenyewe ndo hakueleweki, basi ndo anakudharau na kuhamia nyumba ndogo kisirisiri hasa kama hajaokoka. ila kama ameokoka, labda kidogo image ya mambo ya kale yawezabadilika kidogo kwasababu Mungu hubadilisha chochote akitakacho. ushauri, oa mwanamke aliyeokoka (ambaye hautampata kama wewe haujaokoka), au kama mambo ndani yameshaanza kuharibika, kimbilieni kanisa la walokole haraka kabla hamjamalizana ndani.
Mwanamke kumdharau mme inaweza kuepukika iwapo SISI WANAUME TUTA;
1.Wajibika,timiza wajibu wako.
2.Kuwapenda kwa moyo wote.
3.Tutapambana na changamoto mbalimbali za kimaisha
Ukiyatekeleza hayo na mengine,utaheshimika milele
 
Kuokoka sikuhizi kunatumiwa kama kilemba tu cha kuficha mambo yao. Na wao wanaibana kama kawaida tu sema wanaona dhambi kutembea na asiyeokoka. Kwani hujasikia mtumishi wa bwana aliyempa mimba mke wa mtu hukohuko kwenye ulokole?
 
hatuongelei watu wanaookoka ili kuficha maovu, hao wapo, tena wengi tu. tunaongelea watu wanaookoka wakijua ya kwamba Yesu anawataka waokoke, wasipofanya hivyo hukumu iko juu yao, kwasababu hukumu ya kwaza kabisa juu ya mwanadamu siku ya mwisho ni hukumu ya kumkataa Yesu Kristo mwana wa Mungu aliye hai. kama wewe ukiokoka kwa kuficha maovu, hauko serious, utaaibika, na utapigwa tu na Mungu. juu ya huyo mchungaji unayemsema, ni mtu mmoja tu, ambaye kwanza si malaika hivyo uwe wa kwanza kurusha jiwe kama wewe pia haufanyi hivyo. simtetei, namaanisha kuwa mnaweza kuwa mko daraja moja tu na wewe unayemhukumu, wote towards jehanam. kuna walokole wengi wanaoona matunda ya kuwa na Mungu, na tunayafurahia. Mungu ni mwema siku zote. wachache ambao shetani anawaangusha, tunawaombea Mungu awasimamishe na tuendelee kumwabudu yeye katika roho na kweli. hatuwachukii na kuwaombea mabaya, kwasababu kama kufanya mambo mabaya ya aibu, hawatuaibishi sisi walokole wengine, wanamwaibisha Mungu na kulitukana Jina lake takatifu. hivyo ni Mungu mwenyewe atadili nao, sisi walokole wengine ambao tuko serious hiyo haituhusu, zaidi ya kuwaombea Mungu awakomboe na kuwasimamisha. na kwenu nyinyi ambao hamjaookoka, hukumu i karibu mlangoni, Bwana Yesu anakuja kulichukua kanisa lake pamoja na kuihukumu dunia hii iliyojaa uovu. dalili zinaonyesha yu malangoni, heri yeye yule anaezingatia kuyafua mavazi yake katika damu ya mwana kondoo, ili asipate aibu siku ile ambayo watu watalia na kusaga meno. hakuna faida yoyote mtu akiupata ulimwengu wote, utajiri wote, kila kitu unachofikiria kukifanya, halafu roho yako ikaishia jehanum milele, siku hiyo inakuja na i karibu mno. siku ambayo dunia ambayo ni tegemeo na kiburi cha wengi, itakunjwa kama karatasi, wenye hekima na wanajimu watalia na kusaga meno kwasababu aibu i mbele yao, na wale wenye kuongoza wengi kutenda mema, na wale waliomkiri na kumfuata Bwana Yesu, WATARUKARUKA KAMA NDAMA, kwasababu yule waliyemsubiri amekuja. HALELUYA to the lamb of God. Mungu na atusaidie.
 
Haleluya! Amina na uje Bwana Yesu. Heri azifuaye nguo zake katika Damu ya mwana kondoo uchiwake usijeonekana siku hiyo. kwakweli Mungu atusaidie. asante kwa msg hii mwana wa mungu. asante. Mungu akubariki.
 
Fidel umesema kweli, asomaye na afahamu. lakini pia na mengine yanahitajika has kumjali mwanamke-little care, vitu vidogovidogo ndo wwanawake huwa wanamind i.e mapenzi ya huba..
 
...jamani eeeh,...kila siku mnazungumzia haya haya ya kuwazidishia vitu vidogo vidogo hawa wake zetu, Wanaume je?

Kwenye ndoa kila mmoja anapaswa kumjali mwenzake kwa hayo madogo madogo, ambayo kwa mchango wake yanajitosheleza kuwa makubwa.

Hizi tafsiri potofu ndoa zinapoanza kuyumba, eti husababishwa na wanaume kuacha majukumu yao si kweli hata kidogo.
"It takes two...!", unless mwenzenu sijaelewa maana ya hii thread.
 
- Mwenye tamaa kupita uwezo- we kila siku mume akirudi unadai mara chain, mara perfume na ukiona vipi basi wakopa hata bila ya idhini yake atajiju- lazima akuone uko unreasonable. Kuna kina wenzie na sisi ambao wana vijipato vyao- basi hata kama anafanya kazi na pesa ni yake basi atatumia apendavyo atanunua atakavyo - ni sawa but bado mume anayo nafasi yake kumwomba ushauri au kushauriana- huwezi tu kurupuka eti una pesa yake basi mume anarudi analikuta liji-hammer limepaki hapo eti umejinunulia (labda kama ni zawadi ya Mr!!)

MJ1 nakubaliana na wewe; na penda niseme huu upande wa matumizi regardless nani anayafince limekuwa ni tatizo kubwa sana inafikia mahala rafiki yangu mmoja ananiambia kuwa katu hawezi kumwachia mkewe atm card yake hata kama yuko mahututi kwa kuwa mkewe hana adbau ya matumizi; pesa ikiwapo itanunua kila nachojisikia hata hamna ualzima navyo sasa mambo kama haya yakiendlea lazima yataleta mtafaruku kwa wanandoa
 
mwanajamii nadhani unafanya utafitil, na haya yote nadhani yatakusaidia
 
Kingi acha tu yaani hadi nashawishika kutengeneza kastudy hapa halafu si unajua Tanzania study za social ni chache especially zihusuzo mahusiano ya wanandoa?
 
Back
Top Bottom