Sababu za mke kumdharau Mume nyumbani

Wapo mamii, tena ndio wa hovyo kweli hao. Niliwahi kusoma kwenye makala moja kwenye gazeti kuhusu kuzeeka kwa akili ya mwanaume mapema kabla ya umri wake! Mojawapo ya sababu walizozitoa ni kuoa mwanamke mbishi na ambaye ni ''unresonable''.
Dah nimeipenda hii Komrade dah maisha gani ya kuzeeshana mapema wakati maisha yenyewe mafupi??
 
Hahahahaha unajua mama siku hizi sinywi nimeacha kunywa nakunywa maji tu.
Nimebadilika nimekuwa kijana mwema na mwaminifu namshukuru Charity, F1, Lily F, bht na Preta kwa maombi yao mazito mpaka wamenibadilisha kijana.
Kakangue!

Lakini hapo kwenye red, hebu tuelezane kidogo.
Hawa hawa, walimchuchumalia AK 47 mpaka akabadili tabia, na sasa amejipatia Pearl na ametulia kabisa.
Lakini unasema wao wao, wamekuombea, ina maana walikuchuchumalia ikashindikana?
Hadi maombi kaka??!!
 
kama alikuwa na wanaume wengi kipindi cha nyuma na akikulinganisha na wewe anaona hauna lolote, hovyo hapo ameolewa na wewe kwaajili ya pesa tu labda, siyo mambo mengine ya ndani. hapo ndo mtajua umuhimu wa kumwomba Mungu akupatie kifaa kipyaaaa, au walau ambacho hakijasasambuliwa mara nyingi. hata kama ukiwa unamdunda kila siku, kama anaona unamfaa ndani ya chumbani, atakuheshimu tu. sasa, akiwa hakuwa amejitunza, yaani alikubuhu kipindi cha nyuma, ukamdunda na ndani kwenyewe ndo hakueleweki, basi ndo anakudharau na kuhamia nyumba ndogo kisirisiri hasa kama hajaokoka. ila kama ameokoka, labda kidogo image ya mambo ya kale yawezabadilika kidogo kwasababu Mungu hubadilisha chochote akitakacho. ushauri, oa mwanamke aliyeokoka (ambaye hautampata kama wewe haujaokoka), au kama mambo ndani yameshaanza kuharibika, kimbilieni kanisa la walokole haraka kabla hamjamalizana ndani.

Mie mbona nimempata! Nani aliyeokoka na nani ambaye hajaokoka! Kuokoka maana yake nini?
 
hapo kwenye red- hivi kuna wanawake wanaochonga pasipo sababu?

Offcourse sababu zinakuwepo, Lakini kuna namna nzuri ya kuwasilisha ujumbe, inawezekana , makosa yasiwe ya mwanamke , yakawa ni ya mwanaume, lakini jinsi ya uwasilishaji ujumbe inakuwa tatizo. Unakuta mama jambo dogo atasema weeeeee, hamalizi. Hajali watoto wapo yeye ni kusemaa tu.
Lakini ikiwepo namna nzuri ya kuwasilisha ujumbe mbona peace tu.
Nina dada yangu, aliolewa na jamaa mpole kishenzi, yaani shemeji akifanya kitu kidogo dada alikuwa anachonga mpaka siye alikuwa anatuboa. Na yule shemeji alikuwa anajibu kitu basi? kimyaaa. Mambo gani hayo sasa? Noma.
 
wapwaaz nimerudi kiaina lakini naona hii sredi imeshanipita mbio!
HIVI SASA HIVI MNAJADILI NINI?
 
Asante kwa mada nzuri
wanawake vyanzo vizuri
Vipato vyao kero nzuri
Elimu yao sumbuko zuri
Wanawake hawana ustahimilivu
Hasa wanapokuwa wameshika makali
 
Kakangue!

Lakini hapo kwenye red, hebu tuelezane kidogo.
Hawa hawa, walimchuchumalia AK 47 mpaka akabadili tabia, na sasa amejipatia Pearl na ametulia kabisa.
Lakini unasema wao wao, wamekuombea, ina maana walikuchuchumalia ikashindikana?
Hadi maombi kaka??!!

B moja wapo ya sifa muhimu ya mtoto w akike ni ulimi mwema....hii ni silaha kubwa sana n ainaweza kukusaidia kushinda vita....thats how we fought and won the war!!

Hata Fidel is just a matter of time....we gonna be there!!

afu huo msamiati wa buluu ndo matumizi yake hapo jamani???
 
Exactly my point. Good sex inapatikana pale ambapo hakuna stress and everything is harmonised.
Ni kweli kabisa.Sex mara zote ina mahusiano sana na brain. Mtu ambaye akili yake ipo sehemu nyingine sidhani kama anaweza kuenjoy sex, kiasi cha kufika kileleni. Kama akili za wanandoa ziko tulivu na wana aminiana kufika kileleni is a matter of few minutes if not seconds.
 
B moja wapo ya sifa muhimu ya mtoto w akike ni ulimi mwema....hii ni silaha kubwa sana n ainaweza kukusaidia kushinda vita....thats how we fought and won the war!!

Hata Fidel is just a matter of time....we gonna be there!!

afu huo msamiati wa buluu ndo matumizi yake hapo jamani???
Mimi BAKITA no kuelewa, si unajua kilatini ndo maza tang yangu?
 
Nakwambia acha tu sikia kwa mwenzio maana hawa viumbe wakipata mbadala utajuta kuolewa. Ila kuna vitu vingine ambavyo vinabore na vikiwa kwa muda mrefu heshma hupungua mf.
1. Ulevi wa kupindukia
2. Kutokumheshimu au msikiliza mke anapokuasa kitu mara kwa mara
3. Kuwa na gubu na kugomba kila mara pasipo sababu
4. Kutokupenda kukosolewa -ukikosolewa wewe unakimbilia kutishia kuacha mke
5. Tabia za kususa kama mtoto mdogo yaani kitu kidogo tu (sometime cha maana) we unasusa hee!
6. Kutotoa au hudumia familia yako ipasavyo- mama ndo mtafutaji mkuu wewe hujali kazi yako ni kudai ubadilishiwe balanced diet kila siku hujui vinatoka wapi (Mpemba shop) n.k.
7. Si kwamba huna pesa basi tu hujui majukumu yako
8. Ubabe usio na maana wakati unaonekana kabisa kuwa huwezikuimudu familia- sasa mama akiamua kutake charge -mnalalamika ni dharau/ubeijing n.k.
Powerful words. Duuh, kama mmeo hakusikilizi na haya mapoint unayomwaga basi tena!
 
Powerful words. Duuh, kama mmeo hakusikilizi na haya mapoint unayomwaga basi tena!
Tangawizi ndio maana nasema si mara zote mwanamke anaamua tu kumdharau mume pasipo sababu. Lakini pia mwanamke asiyejua majukumu yake kama mke kwka wote mume na familia kwa ujumla anajichimbia kaburi la dharau.
- Mwenye tamaa kupita uwezo- we kila siku mume akirudi unadai mara chain, mara perfume na ukiona vipi basi wakopa hata bila ya idhini yake atajiju- lazima akuone uko unreasonable. Kuna kina wenzie na sisi ambao wana vijipato vyao- basi hata kama anafanya kazi na pesa ni yake basi atatumia apendavyo atanunua atakavyo - ni sawa but bado mume anayo nafasi yake kumwomba ushauri au kushauriana- huwezi tu kurupuka eti una pesa yake basi mume anarudi analikuta liji-hammer limepaki hapo eti umejinunulia (labda kama ni zawadi ya Mr!!)
 
Asilimia kubwa ya akina mama au dada huwa wana upendo na kuheshimu sana mahusiano yao. Tatizo wanaume wanalikoroga wenyewe na kuharibu misingi ile ya heshima. Mwanamke ni neno dogo tu na kulimaanisha "ninakupenda mke/mpenzi wangu" na litabadilisha kila siku yenu na ndoa/mahusiano itadumu/yatadumu milele na heshima tele. Hata kama wewe si tajiri lakini upendo wa dhati utajenga ndoa yenu. Mbona wazazi wetu mpaka mabibi na mababu tuliwakuta wanaheshimiana sana?? Tena hakuna hata kuhitilafiana mbele ya wageni au watoto?? Take it from me, sikuwahi kuwaona wazazi wangu wakitofautiana au hata kususiana chakula na kuvimbiana. Kila wakati mama alikuwa akishatupakulia chakula wote, tukimaliza kula, tena baba alikuwa wa kwanza kusema "Asante mama kwa chakula kitamu" hata kama siku hiyo mama alipika pengine chakula ambacho sisi watoto tuna-consider cha kawaida but baba kila siku chakula cha mama ni kitamu. Na sisi tulikua wakubwa na kuwa na miji yetu na maisha yale yale ya upendo, kwani pia nilikuwa makini kuhakikisha mwenza wangu ana angalao malezi yanafananafanana ya yale ya kwetu. Na mpaka leo kwa miaka mingi ya ndoa hakuna tofauti kubwa za kupoteza ile heshima yetu. I hope kwa watoto wangu na wajukuu will be the same, ila kwa wale ambao wako nje au watakuwa nje ya nchi tatizo lao kubwa kupata owanja mkubwa wa kuchagua the right couple!!! Msinipige marungu, ukweli ndiyo huo, uwanja wenue wa kuchezea ni mdogo, ni almost rezo grazing, so you end up landing to whoever ambaye pengine hakupata mtu, hanging but not nungayembe!!!
 
Back
Top Bottom