msem
JF-Expert Member
- Nov 7, 2015
- 1,837
- 1,631
Ili mwanaume aheshimike ndani ya ndoa:Timiza majukumu yako. Majukumu nayagawanya katika sehemu mbili (a) Jukumu la msingi ;hapa namaanisha tendo la ndoa.Hapa pakilega lega uwezekano wa kushuka kwa heshima ya baba ni mkubwa. (b)majukumu ya muhimu-hapa namaanisha mambo kama chakula,mavazi na malazi( vyenye ubora) kwa familia,bila kusahau elimu kwa watoto. kipengele hiki nacho kikilega lega pia heshima ya baba itaporomoka tu.
Vipengele vyote "a" na "b" vina thamani kubwa ukikidharau kimoja na kuweka kipaumbele kwenye kingine hicho unachokidharau "utasaidiwa" na ndiyo mwanzo wa dharau.Ukitimiza vyote kwa utimilifu mama anaweza kuteleza kibinadamu tu kwa kuwa binadamu sio mtimilifu lakini akarudi kwenye mstari kwa wakati.Ingawa pia wapo kina mama ambao wanaonesha "uzalendo" hata kama vipengele hivyo vinalega lega lakini ni wachache na hii inategemea pia na malezi na hulka ya mtu.
Ili mwanamke apendwe ndani ya ndoa:Mwanaume hana mambo mengi sana ili kumpenda mke wake, mambo makubwa ni mawili tu, (a) Mwanamke asimbanie mume "ile kitu" (b) Heshima-kwenye heshima kuna vitu kama uaminifu wa ndoa na kuchunga ulimi katika mawasiliano nk. Mwanamke hata awe mzuri kuliko malaika akichemsha haya ndoa yake lazima itayumba.