Mke wa Pogba awajia juu wanaomkosoa mume wake

Mke wa Pogba awajia juu wanaomkosoa mume wake

Miss Halima

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
221
Reaction score
487
Mke wa nyota wa As Monaco Paul Pogba, Zulay Pogba amejitokeza hadharani kumtetea mume wake, na kukataa madai ya watu kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 anapaswa kustaafu soka na aliamua kurejea kucheza soka ili kutafuta fedha.

Kauli imekuja wakati Monaco ikiripotiwa kutaka kuvunja mkataba wa Pogba kufuatia mfululizo wa majeraha anayoyapitia tangu walipomsajili mchezaji huyo..

Paul pogba alifanikiwa kucheza mechi sita pekee msimu uliopita, huku akijaribu kuanza upya maisha yake ya soka baada ya kusimamishwa kwa muda mrefu kucheza soka kutokana na suala la matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku.

Akiwa katika maandalizi ya msimu mpya Pogba ameripotiwa kusumbuliwa na tatizo la goti, Huku mashabiki na wachambuzi wakisema kwamba mwili wake hauwezi tena kuendelea kucheza soka la kiwango cha juu, Lakini mkewe alitoka na aliwajibu moja kwa moja wakosoaji hao..

“Kwa watu wote wanaosema Paul anapaswa kustaafu au kwamba amerudi kwenye soka kwa ajili ya pesa, napenda kuweka hili wazi, anayejua ni lini pogba atastaafu ni Mungu pekee.”

Kisha akaongeza,
“Na kwa wale wanaosema amerudi kwa ajili ya pesa, niaminini sisi tuko vizuri sana kifedha, namshukuru Mungu.”

Wanandoa hao, walifunga ndoa mwaka 2019 na wana watoto wawili wa kiume, Na wamepitia miaka kadhaa yenye changamoto nyingi nje ya uwanja.

Pogba aliwahi kuelezea kujiunga kwake na Monaco ni kama mwanzo mpya baada ya kile alichokiita “kipindi cha giza”, kilichohusisha kusimamishwa kwake na baadaye kuvunjwa kwa mkataba wake na Juventus mwishoni mwa mwaka 2024.
Screenshot 2026-08-14 114951.png
 
Kwani hataki fedha ziendelee kumiminika benki?Sasa,naye Pogba asizuzuke na kumuandika umiliki wa mali na fedha zake zote halafu mwisho awe ombaomba.Huyo "Miss Blandish" ni tapeli tu.
 
Halafu huyu ndiyo chanzo kikuu cha kijana wetu kufungiwa kipindi kile baada ya kumnywesha madawa yaliyopigwa marufuku. Ona sasa kijana amebakiwa na jina pekee. Kiwango chote kimepotelea kusikojulikana.
 
Back
Top Bottom