samahani wapendwa ninaomba niipost hii post kutoka kwa mdau mmoja wetu. Yeye anasema..................
Nimeona watu wame-point out kwamba good sex inaweza kumfanya mwanamke asimdharau mumewe. Wanaweza kuwa sahihi, lakini good sex alone haiwezi kusababisha mwanamke amheshimu mume wake.
Definition ya good sex inaendana heshima, upendo, kujali feelings za mwenzi, kumsikiliza mwenzako na mengineyo. Mfano, mume hawezi akawa anamnyanyasa mkewe, akawa anamtukana na kumkashifu, na akawa anam-hurt bila sababu yoyote, yet mwanamke akawa ana-enjoy sex, huyo mwanamke lazima atakuwa na matatizo kichwani. Good sex ni tendo la dakika chache, may be half an hr or at most one hr, siku ina masaa 24, masaa yanayobaki ni kero tupu, bado mtu atasema kwamba good sex inasababisha heshima?
Hivi kweli mtu anamdunda mangumi mke wake, anamtukana, anamkashifu kwamba ni mjinga ama mpumbafu, bado mkewe atakuwa na hamu ya kuifurahia hiyo good sex anayoipata kwa mumewe? Inawezekana if and only if hayo manyanyaso hayakeri kiasi cha kupekelea mwanamke kukereka. Good sex inaendana na mwanamke kuwa tayari kwa tendo, wengine akishakumbuka matusi, kashfa au manyanyaso hata bibi hawezi kulia tena wala kujisikia kutaka kukunwa.
Kuna walitaja pesa, lakini hapo kutakuwa na heshima ama nidhamu ya uoga, mwanamke hayuko huru ku-express feelings kwa mume wake ama kuonyesha kwamba nae ana mchango katika mali iliyopo. Wengi walio olewa kwa kufuata hela, ni kama vile walijiingiza jehanam ama jela, na hasa kama wanaume wenyewe ndo akina sisi ambao hatuna utu wa kutosha.
Mimi kwa maoni yangu, material things ni mambo ya kupita tu, tuna-acquire mali, magari, majumba na mengiyo lakini hayajengi heshima ya kweli. Kinacho-matter zaidi ni UPENDO tu. Kama kuna upendo wa kweli, mume hawezi kumtukana ama kumnyanyasa mkewe, hawezi kumpiga ama kumkashifu. Hivi kweli kitu unachokipenda unaweza kukikashifu? Basi labda kama hukukipenda. But the bottom line kwangu mimi ni upendo, esp, kwa upande wa wanaume. Mengineyo ni nyongeza tu.
Kwa upande wa wanawake, kama mtu kaolewa kwa kufuata material things na akaja kukuta material things zinaisha ama hazipo kama jinsi alivyokuwa anahisi, hapo ndipo dharau inapoweza kuanza, kashfa na mengineyo na ndipo mke ananza kufanya comparison kati ya mume wake na Baba Chanja wa jirani.
Upendo kati ya wahusika ni muhimu sana na huzaa hayo yote mengine, maana kama watu wanapendana kwa dhati, kweli msichana akiguswa tu tayari bibi kaitika. Mume hawezi kumuona mkewe ni mchafu ama ana shape mbaya, maana ndo alimchagua.
Tatizo la wanaume tumetaliwa na tamaa, huwa hatuna upendo wa dhati. Hapa ndipo signature ya Nyamayao inapohitajika, kwamba wanawake hupenda kabla ya kufanya ngono na wawapendao, sisi wanaume hutamani kwanza na baada ya kutamani huomba ngono na baada ya ngono ndipo tunapoweza kuanza kupenda. Tumeumbwa na mioyo ya tamaa. Hata Mungu aliagiza Biblia kwamba "Enyi waume wapendeni wake zenu". Wanawake wameagizwa kuwatii waume zao, kwa kuwa Mungu anajua wazi kwamba wanaume tumetaliwa na tamaa, badala ya kusema nimekutamani nitasema nimekupenda, maana nikisema nimekutamani tu, huwezi kunikubali. So ili nikupate nitasema nimekupenda ili uamini kwamba sikuhitaji kwa ajili ya jig jig tu, bali pia nina malengo ya muda mrefu.
Malengo ya muda mrefu ni outcome ya jig jig, baada ya hapo ndo upendo waweza kuja ama dharau zikaanza. Tatizo liko kwetu zaidi when you compare na wadada