muhuni mpya
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 300
- 166
- Thread starter
- #61
nmekuelewa mkuu, lakini kama lipo kusudi lakuwa hapa kwanini iwe siri
Hili swali binadamu amekuwa akijiuliza miaka na miaka hadi leo....nini kusudio la maisha?
Je tulifikaje hapa duniani? Tukitokea wapi? Na kwa kusudi gani?
Je ni ili tuishi, tufe then ndiyo iishie hapo?
Je ni kupata mali nyingi, ambazo tunapofariki hatuchukui hata moja?
Kusudio la maisha ni nini hasa?
Binafsi naona kuwa kamwe huwezi kupata majibu ya msingi kuhusu maswali ya aina hii bila kumhusisha Mungu.
Pamoja na mambo mengine, tupo hapa kwa sababu Mungu alituweka hapa ili tuwe na uhusiano naye while living.