Wote hamana majibu sasa mimi nawapa Tulieni;
1. Tupate raha, raha ya maisha, yaani kila kitu kina kutii tuna miliki na kutawala, viumbe vyote havina ubishi kwa mwanadamu, ana fanya anavo taka.Mfano kuku ana uhai lkn unachinja, Gari, Train, Farasi, Mbwa, waweza kuvifanya chochote havina ubishi, sometimes hata mwanadamu mwenzio japo hapa si rahisi ni kwa ubishi sana.
2.Kuacha thamani ya kumbukumbu ya urithi, kwa unao waacha nyuma, wa vitu mbalimbali ulivofanya, ambavyo wewe hukuvikuta hapa Duniani ila umevipata baada ya kuja sasa unawaachia. mfano Majumba,Mashamaba, Uhuru nk.
3.Kupenda, hasa kupenda Mazingira yanayo kuzunguka na kuwapenda wengine na kuwafanya sehemu ya maisha yako, kama mke watoto, majirani, marafiki.itakufanya uishi zaidi Duniani, na kuepuka magonjwa yasiyo ya lazima kama BP.Sonono, IDDM. kumbuka hili neno '' itakufanya uishi/maisha marefu''
Huwezijipenda wewe tu pekee. wahangaikaji wote mjini, wavaa uzuri, gari zuri ni kwa ajili ya wengine, mke watoto, wageni ambao ni ndg na marafiki.
4.Wewe ni jibu, Maisha ni kutengeneza u maana wa nafsi yako. ni kitu tunacho kitengeneza sisi wenyewe na kukitolea matunda ajiri ya wengine, kama baadhi ya avatar humu zina maana sana ktk mantiki ya uchangiaji wao, utasikia; Mshana jr uko wapi? njoo huku.
5.Kufanya mambo chanya tofauti tofauti, na kuyaweka kwa walimwengu, Mfano wewe ukienda mwezini mwenzako anaenda tengeneza maisha Mars. kuweka mghorofa wa maana Masaki, au Njiro, amabao wameweza wachache hii yote ni sababu ya maisha/kuishi.
6. Sababu ya kuishi Duniani ni kupata utaalamu na uzoefu mbalimbali mkuu. mfano Miaka 25 nyuma hukufanya unayo yafanya leo. uongo?
kutajirika, Elimu nzuri na kundesha gari la fahari ni uzoefu na raha pia. au tuseme Rubani-mbongo umeburuza Bombardier kutoka USA mpaka Bongo ya jiwe.
vitu km Burudani, kutembelea sehemu mbalimbali ni nuzoefu tosha unapata, nk
7.Kupata suluhisho la mahangaiko yako. kam vile kupigika/ kuhangaika ni sehemu ya maisha, unapojitahidi kujiepusha na mahangaiko hayo na kupata suluhu la kudumu, unapata nafuu na raha, hapa jua ndo sababu ya wewe kuishi. mark my word;
''He has a why to live can bear almost any how!''
8.All these I just picked aside from Biblical Jargon.