Sababu ya za Nissan Dualis kuwaka moto… Sio tatizo la kiwandani bali uzoefu mdogo wa mafundi wetu kwenye magari ya Nissan hata ukizingatia service

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
1,910
Reaction score
5,450
Sio kwamba Nissan Dualis zina kasoro ya kiwandani hadi zote ziungue moto. Tatizo kubwa ni service duni na mafundi wasio wataalam wa Nissan.


1. Kuna Plastiki ya kuzuia joto (heat shield/insulation) nyuma ya engine na lipo karibu sana na bomba la moshi, loki za plastiki, zikipata joto kali Zinakatika, Plastiki inagusa bomba la moshi na moto unaanzia hapo 🔥

2. Paipu za mafuta (fuel lines) ziko karibu, yakivuja mafuta kidogo tu, yakigusa sehemu yenye joto kali, Moto unaanza haraka sana.

3. Thermostat nazo zinalalamikiwa kuwahi kuharibika inaweza kusababisha moto.

3, Mafundi wasio wataalam wa magari ya Nissan, hawakagui hali ya lock za plastiki, wakiona loki imelegea wanakaza na hufanya iwe karibu zaidi na engine, wanabadili lock za plastiki na zinaweza kuwa feki za bei rahisi, Hawana ujuzi au vifaa maalum vya kufanya tests kujua kama mafuta yanavuja bila kugundulika

Jinsi ya kuepuka hatari ya moto

  • Fanya service gereji yenye mafundi wtaalam wa Nissan, hizo gerej za mtaani achia roho za paka toyota
  • Hakikisha Heat shield iko salama na imefungwa kwa vitu vinavyostahimili joto
  • Ukaguzi mkubwa kuhakikisha hakuna fuel leak hata kidogo
  • hakikisha Exhaust haigusani na plastiki yoyote
  • angali hali ya themostat kama inahitaji kubadilishwa
  • Usipuuze harufu ya mafuta au moshi wa ajabu
  • Usiwe mbahili, Nissan haitaki ubahili, nunua spea original na peleka gari kwenye gereji zenye wataalam wa Nissan.
 
1. Kuna Plastiki ya kuzuia joto (heat shield/insulation) nyuma ya engine na lipo karibu sana na bomba la moshi, loki za plastiki, zikipata joto kali Zinakatika, Plastiki inagusa bomba la moshi na moto unaanzia hapo 🔥
Bado unasema sio issue ya kiwanda
 
Bado unasema sio issue ya kiwanda
Hiyo plastiki/heat insulation si kasoro ya kiwandani, ni consumable part (sehemu inayochoka kadri muda unavyokwenda).

gari zetu wengi ni za mitumba, zimeshatumika sana huko nje, Baada ya miaka mingi ya matumizi, joto hufanya lock za plastiki kuchoka plastiki kupoteza uimara wake

Ni jukumu la fundi kujua gari imetumika sana inahitaji kubadilishwa hio lock.

Tunapotumia magari ya mitumba tuwe tunayapa matengenezo ya mtumba tusiige huko youtube wenzetu wanaonunua vitu vipya 0KM
 
The Nissan Dualis (Qashqai) (2007-2013) is primarily associated with significant technical issues regarding its Continuously Variable Transmission (CVT), which often suffers from premature failure, whirring noises, and acceleration lag. Other common problems include faulty rear suspension bushes (clunking noises), failed wheel bearings, fragile door handles, and electrical issues like shorting tail light circuits.
 
Naona Kwa Sasa Zile Picha Za Dualis kuungua Zimepungua Mtandaoni.... Ina Maana uwenda Mafundi washagundua Tatizo lipo wapi
 
Sasa kwanini tatizo liwe zaidi kwenye mtumba Nissan na sio mtumba Toyota and the likes?kubali tu mjomba tatizo ni la tokea kiwandani...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…