Sababu ya Waziri Bashe kukataa msaada wa mchele wa Wamarekani: Je, ni uwepo wa virutubisho, kutokuwa na utapiamlo nchini au hatuna shida ya mchele?

Bashe pale kaleta siasa tu. Wanasiasa Tz saivi wamekua na tabia kwamba ikitokea yakifanyika maamuzi yakaleta kelele kwa raia, basi wanaibuka kujifanya wapo upande wa raia huku wakitoa kauli za vishindo. Watu wasiopenda kufikiri ndo hua wanawaelewa
 
Nimefuatilia kwa makini clip ya Mh Bashe kuhusu suala hili. Kweli speech yake imeniacha na maswali mengi. Listerning between his wording (alivyo-paraphrase) na tone ya speech yake utajiuliza je ni ubabe? je ni overconfidence? je ni kweli tunajitosheleza? ni kiburi, je ni kweli hatuna shida?, je ni kweli hatuna utapiamlo?, je ni kweli hatuhitaji huo msaada?, au ni kweli tunahitaji huo msaada ila for sustainability reasons na kwa ajili ya medical precaution tungependa tupewe kwa namna nyingine? Hakika ni maswali yasiyo na majibu.

Kuna mtaalamu mmoja wa Theologia wa Marekani( ni padre na professor) alishawahi kusema unaweza ukawa na hoja, ila lugha uliyotumia ikaondoa mantiki nzima ya hoja yako ya msingi, pia unaweza ukawa na hoja pia na ukaweza kutumia lugha nzuri ila tone ya utoaji wa hoja hiyo ikaondoa au chafua hoja yako na mantiki kabisa. Na hilo ndilo nililoliona kwa Mh Bashe, mpangilio wa sentensi (alivyo- paraphrase hoja) na tone ya speech yake vinaleta taswira tofauti na kuondoa hoja yake ya msingi.

Watu wa kanda ya ziwa (Kagera) wanamsemo wa hatari kabisa, msemo wa kiburi mbuzi eti " Kamwe siwezi kuramba Mbwa miguu" eti " Tindamba e-mbwa magulu". Maana yake nini? hata nikiwa na shida, nikiwa na njaa, siwezi kunyenyekea ili nipate msaada ili nijikwamue. kwamba ni bora nife kuliko kunyenyekea kwa binadamu mwenye damu kama mimi. Hakika nakuhakikishia, wengi walioweza kufanikiwa kwenye maisha kuna kipindi ilibidi wawe wanyenyekevu, kiburi, majivuno , majigambo havijawahi kumuacha mtu salama.

Turudi kwenye hoja ya msingi sasa, je ni kweli hatuna utapiamlo mashuleni? je ni kweli wanafunzi hawashindi njaa mashuleni na majumbani? je sisi wazazi hatushindi njaa na kuby-pass baadhi ya milo mbali ya kuwa na mchele tele, unga kibao, maharagwe ya kumwaga masokoni na kwenye masupermarket ya kisasa kabisa kama ulaya vile. Wazungu walisema "The end justify the means". lakini watu wa program management wakaongezea " Thinking from the ends-results is key for sustainable changes and reaching the intended goal" . Sasa kuwepo kwa mpunga wa kumwaga, kuwepo kwa mchele wa kutosha, maharage ya kutosha, mahindi na udaga wa kutosha, mbogamboga za kumwaga madukani, mashambani , kwenye stoo za vyakula, masokoni ,kwenye masupermarket haimaanisha wananchi, watoto wetu wa shule wanapata vitu hivyo. kupatikana ndiyo end -results yetu, tambo nyingine ni uswaahili tu na siasa

kama wewe ni Mtanzania, kama wewe unafahamu statistics za nchi hii kwa miaka zaidi ya kumi kuhusu utapiamlo hasa kwa under fives na watoto wa shule, kama unafahamu umasikini wafamilia nyingi vijijini kwetu na jinsi ambavyo familia nyingi zimebadilisha ratiba ya kula, kutoka angalau milo 2 na kubaki na mmoja tu na kipasha tumbo asubuhi utanielewa kwa nini nakataa Tambo za Mh Bashe hata kama kuna some logic behind. Narudia tena denial will never put us free, Denial is a preliguisite to failure. Sisi ni masikini, much hatuwezi kunyenyekea ukweli ni kwamba sisi ni masikini na tutaendelea kuhitaji msaada na tunahuhitaji, jana, leo na kesho.

Leo tunapokea TRILIONS of USG funding kwenye Country multisectoral Economic Development Plans za donor mbalimbali; kwenye Kilimo (mafunzo, utafiti, umwagiliaji n.k), Upande wa Afya (mafunzo, utafiti, matibabu, hata vifaa tiba na madawa, majego etc), kwenye elimu ndio husiseme ( mafunzo, mitaalam, wataalamu etc). Hizi zote ni strategic investment kama alivyopendekeza Bashe tayari watoa misaada wa mchele huo wamekwisha wekeza huko.Sasa ukishakuwa na watoto wenye utapiamlo, imediate solution ni chakula na si porojo, it is an emergence situation, ingekuwa si sheria ya Takwimu ningeweka recent national statistics za new publication upande wa National Malaria and Nutrition Status hasa kwa watoto wenye utapiamlo kwa kila mkoa na vifo vitokanavyo na utapiamlo.

kama huo mchele wetu mzuri ungekuwepo tusingekuwa na utapiamlo, tusingekuwa na vifo vya watoto vinavyosababishwa na utapiamlo. The truth is" availability of commodities or services is not necessarily equal/equivalent to accessibility of those commodities or services (Jikumbushe tofauti ya equity and equality). Huo mradi umelenga accessibility wakati misaada yao mingine ya huyo funderer tunayembeza (USG) imelenga kuboresha availability na hapo ndipo kwenye epidermiology tunasema hawa funderers wako smart na sahihi kuinvest kwenye multiple but correlated programs which brings additive effect to each other. Accessibility inahusu vitu vingi hasahasa uchumi, locality etc na uchumi wa hizi familia za watoto wa shule hautabadilika ghafla hasa kwa siasa, mipango ya uchumi wetuna ufisadi tulionao.Leo kila mtanzania is a beneficery of USG funds either directly au indirectly. We need to watch our languages and tone on very sensitive issues like this.

Ni vizuri Kiongozi kuonyesha msimamo tena kama nchi, ni vizuri kabisa kiongozi kukataa baadhi ya misaada hatarishi lakini ni vibaya kuonyesha Tambo na kujimwambafai kwamba wewe huitaji msaada wakati una shida hiyo sana tena sana, yawezekana wewe huna shida hiyo , je umati wa masikini unaowaongoza. Sio vizuri kabisa kutumia lugha ya nenda kamwambie aliyekupatia hatuhitaji sisi msaada huu" Nafikiri tusingepungukiwa kitu kama tungetumia diplomatic language na tone nzuri kuwakilisha hoja pinzani, pia angetafuta appropriate platform kupeleka ujumbe kwa watoa fedha, kwani ni haohao wametusaidia kwenye sector nyingi na kwa cheo chake ingekuwa rahisi kabisa. Rudia maeneo na kiasi cha USG funds kwa mwaka tu, ndugu msomaji leo hii USG fund zikikatika tu at least asilimia zaidi ya 20% ya quality ya health services across different disease conditions zitapungua, tena kwa naadhi ya magojwa kama HIV/AIDS asilimia zaidi ya 35% ya huduma hii (upimaji, madawa etc)itapungua. Mbona chanjo, madawa, vifaa tiba ni eneo hatarishi kudhuru maisha yetu kuliko hata mchele ulioboreshwa.

Najua kuna watakao nibeza kwamba hatutaki ujinga sisi watanzania, huwezi ukawa ombaomba au kukubali misaada ya masharti, nikweli kabisa lakini big brain zinakuambia siku zote angalia sana EGO zetu na epuka gradious zetu zisiaffect our responses, most importantly our decision making. Sasa kama ni virutubisho kwenye mchele, kwa taarifa tu vyakula karibu vyote kwao marekani ni inorganic tokana na genetic technologies ilivyopamba moto na vimekuwa enhanced kuongeza nutrition components, it is not a big issues kwao, purely-organic food ni chache sana na aghali kwelikweli. Mbona leo angalia vyakula vyetu hasa hasa mahindi yetu, angalia mananasi yetu, angalia maembe yetu, sio yale ya zamani, inamaana Mh Bashe hajui yameisha fanyiwa genetic engeering huko SUA, je anajua mbegu za mazao yetu zinatoka wapi? na je process hiyo hajui inaongeza au kupunguza virutubisho pia.

Ifike mahali tuache sizitaki mbivu hizi, tuwe wapole tukishajikwamua ndipo tusimame na kusema hatutaki. Please I should declare mimi sina interest yeyote na donor huyu, ila sijapenda hizi Tambo wakati nafahamu njaa na umasikini wetu, wewe unaweza kuwa uko fresh ila ukweli uko palepale. Nafahamu misaada mingi ya huyu donor na manufaa kwa wanyonge. Hujawahi kujiuliza kwa nini funds hizi zinaelekezwa kwa walengwa wenyewe; hii ni mada nyingine.
bashe amefanya la maana sana kukataa mchele, kama kweli amekataa. Tanzania hatuna njaa ya kuhitaji mchele toka marekani, labda ungekuwa umenunuliwa hapahapa ukasambazwa kwasababu upo. wameweka nini huko marekani, nani kasema Tanzania tunakufa na njaa hadi watuletee mchele? watu wenyewe siku hizi wanapaka homoni hadi kwenye nguo ili watu wawe na hormonal imbalance dunia iongezeke mashoga wawe wengi ili wapiganie haki dunia yote iweke sheria za mshoga. sisi sio manguruwe au mifugo ya kufanyiwa experiment kwenye vyakula. kuweni makini sana na hao wazungu. walitukosa kwenye corona, watatutafuta tu kwa kingine.
 
bashe amefanya la maana sana kukataa mchele, kama kweli amekataa. Tanzania hatuna njaa ya kuhitaji mchele toka marekani, labda ungekuwa umenunuliwa hapahapa ukasambazwa kwasababu upo. wameweka nini huko marekani, nani kasema Tanzania tunakufa na njaa hadi watuletee mchele? watu wenyewe siku hizi wanapaka homoni hadi kwenye nguo ili watu wawe na hormonal imbalance dunia iongezeke mashoga wawe wengi ili wapiganie haki dunia yote iweke sheria za mshoga. sisi sio manguruwe au mifugo ya kufanyiwa experiment kwenye vyakula. kuweni makini sana na hao wazungu. walitukosa kwenye corona, watatutafuta tu kwa kingine.
Walikukosaje kwenye corona? 'Nchi hii ina wajinga wengi sana' alipata kusema NW wa Afya. Mimi ni nani nipingane na mtu mwenye data za afya zetu
 
Walikukosaje kwenye corona? 'Nchi hii ina wajinga wengi sana' alipata kusema NW wa Afya. Mimi ni nani nipingane na mtu mwenye data za afya zetu
mkuu, najua wewe mchele ule watoto wako hawatakula, wala wewe hautakula. kama basi nchi imejaa wajinga na unatuita wajinga, basi nenda kapike huo ubwabwa ule wewe na watoto wako.
 
mkuu, najua wewe mchele ule watoto wako hawatakula, wala wewe hautakula. kama basi nchi imejaa wajinga na unatuita wajinga, basi nenda kapike huo ubwabwa ule wewe na watoto wako.
Wewe ambaye watoto wako hutaki wale umejaribu kuwapelekea huo mchele wa ndani wenye uhitaji ili wasile huo wa nje? Wewe ni mtu wa hovyo kwa sababu unajaribu kuzuia jirani yako aliyelala njaa asipewe chakula na msamalia mwema ilhali wewe huwezi msaidia na hutaki kumsaidia?! Je, lengo lako ni ili afe njaa?
 
Kupokea msaada wa Chakula wakati hatuna janga lolote ni Kuivua ngoa Serkali na Nchi nzima kiujumla, wacha tukaze ila Beshe aje na solution.
 
Elimu ya Tanzania imezalisha watu wajinga sijawahi kuona. Hivi wewe bila hao wazungu ungekuwa hai sasa hivi? Hivi wakisema kuanzia leo kila mtu ajifungie kwake, hakuna kuuziana, hujui hata hiyo simu unayoandikia ujinga kama huu hutakuwa nayo?
kwani wao bila waafrika wangekua hapo walipo?
kama maandishi yalitoka Misri nafikiri hii nchi ipo kwa wazungu!
Nafikiri pamoja na nia nzuri kwao lakini ni vyema Mahindi na mpunga vitoke kwetu na hayo madawa yakachanganyiwa hapa shida iko wapi?
 
Elimu ya Tanzania imezalisha watu wajinga sijawahi kuona. Hivi wewe bila hao wazungu ungekuwa hai sasa hivi? Hivi wakisema kuanzia leo kila mtu ajifungie kwake, hakuna kuuziana, hujui hata hiyo simu unayoandikia ujinga kama huu hutakuwa nayo?
mwenzetu umesoma wapi? wanapotoa watu waelevu waliotayari kukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji?
 
mwenzetu umesoma wapi? wanapotoa watu waelevu waliotayari kukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji?
Sijawahi kusema tukubali kila kitu cha mzungu bila kuhoji. Siyo cha mzungu tu ila hata cha hawa hawa wakoloni weusi, kina Bashe. Tatizo lipo pale unapohoji na hoja yako ni ya kipumbavu kabisa.
 
kwani wao bila waafrika wangekua hapo walipo?
kama maandishi yalitoka Misri nafikiri hii nchi ipo kwa wazungu!
Nafikiri pamoja na nia nzuri kwao lakini ni vyema Mahindi na mpunga vitoke kwetu na hayo madawa yakachanganyiwa hapa shida iko wapi?
Tulikuwa wapi tusione hilo tatizo mpaka mgeni alione? Hivi wewe unaamini kabisa kuwa serikali hii ya CCM inajali watoto wa shule kula? Hayo mahindi au mchele kama tunayo kwa nini hatuwalishi? Au wewe mwenzangu maisha ya vijijini huyajui? Mzungu yeye anatoa surplus aliyonayo. Una njaa unapewa msosi halafu unagoma eti upewe fedha! Hii ni akili?
 
Bashe pale kaleta siasa tu. Wanasiasa Tz saivi wamekua na tabia kwamba ikitokea yakifanyika maamuzi yakaleta kelele kwa raia, basi wanaibuka kujifanya wapo upande wa raia huku wakitoa kauli za vishindo. Watu wasiopenda kufikiri ndo hua wanawaelewa
Sahihi
 
Udini naushamba kwelimukoa yadodoma nakandayakati haliya utapia mlonikubwa waacheushamba uwezikumpangia mtuakusaidienini
 
Mkuu una uhakika nchi haina tatizo lolote la chakula au ni ule msemo wa ashibae hamjui mwenye njaa? Mimi huwa natembelea sana vijijini na ukifika huko utaona watu wenye shinda ambazo wala hukudhania kama kuna binadamu wanazo. Siyo vijijini tu hata hapo Dar kuna watu wenye shinda kuu. Nakuhakikishia huo mchele ukiletwa leo, watu watagombania na hata kuuana ili tu wapte hata kilo moja. Busara ni uletwe na kama kuna watu wenye uhitaji wachukuwe.
Wewe unashindwa kutofautisha shida binafsi ya mtu na shida inayoikumba nchi. Tz haijatangaza baa la njaa. Kuwepo kwa baadhi ya watu wenye uhitaji wa chakula haihalalishi kuomba msaada wa chakula kutoka nje. Hii nchi si kame. Kusaidiwa basic need kama chakula inaleta taswira mbaya sana. Sijasikia nchini watu wanakufa kwa kukosa chakula. Tatizo ni maarifa tu.
 
Back
Top Bottom