Mchele wa msaada ugawiwe mashuleni kama ilivyodhamiriwa!

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,660
20,991
Tuache kuonyesha ujinga wetu katika ngazi ya kimataifa juu ya uwezo wa akili zetu kufikiri, tumepewa msaada na marafiki zetu wa muda mrefu, waliwahi kutupatia, mafuta, mahindi, samaki na vingi tu ndani ya nchi yetu,

Pia izingatiwe wangelikuwa na uovu, basi kwa kuwa chanjo, dawa na vingi tu hupata kutoka western countries, wasingeweza kutukosa katika kufanya ubaya wa aina yoyote waupendao, sisi wa enzi hizo tulikula ugali wa njano ukiwa ni msaada toka kwa marafiki zetu hawa wa damu na hakuna baya lolote lilitupata.

Tupuuze akili zisizo na msingi wowote na ukweli halisi, tunaishi kwa hisia hasi na mawazo hasi,Akili zetu negativity tumeweka kwa 85%.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~

#HABARI Shirika la Viwango nchini Tanzania (TBS) limesema kwamba chakula cha msaada kilichoongezwa virutubishi kilichotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani, kwa ajili ya baadhi ya shule za mkoa wa Dodoma kilifuata taratibu za uingizwaji wa chakula nchini na kilipofika kilifanyiwa ukaguzi na uchunguzi wa kimaabara na kuthibitishwa kuwa ni salama kwa matumizi.

Taarifa ya TBS imekuja saa chache tu mara baada ya Waziri wa Kilimo @bashehussein kuitaka taasisi inayofanya mradi wa kutoa misaada ya chakula ikiwemo mchele ulioongezewa virutubisho katika shule mbalimbali mkoani Dodoma, waiambie Marekani kwamba Tanzania kuna mchele na maharage kwahiyo zile fedha wanazowapa wakulima wa Marekani wawape wakulima wa Tanzania na virutubisho viongezwe hapa nchini wakati Watanzania wakiwa wanaona.

Aidha TBS wameongeza kuwa, utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.

"TBS itaendelea kusimamia kikamilifu jukumu la kuhakikisha kuwa chakula kinachoingia nchini kinakidhi vigezo vya usalama na ubora kwa mujibu wa matakwa ya viwango ili kuendelea kulinda afya za walaji," imeeleza taarifa ya TBS

#EastAfricaRadio

IMG_20240317_135208_022.jpg
 
Hauna uthibitisho huo,
Huko wanapokula GMO lifespan yao ni miaka 80 wakati huku mnapodengua lifespan yenu ni miaka 60.

Life span ina factors nyingi sana na siyo chakula tu.

Sasa huko factors nyingi zinawabeba kwahiyo GMO ni minor tu ila huku kwetu mtu anafariki kwa kukosa elfu mbili ya matibabu au mateja wanauana kwa kudaina Tsh 50 , mtu analala na jiko la mkaa ndani(elimu elimu elimu) ,wao huko wana gesi ,umeme ndani wa kutosha na haukatiki ,hawapikii kuni wala mkaa.
 
Ujawahi kula parachichi kuubwa?, ujawahi kula tikiti kuubwa?, ujawahi kula tango kuubwa?, matango yetu ya asili ni madogo kweli na hayanenepe kamwe!

Yametoka marekani hayo maparachichi au matango? Bashe amesema hivyo virutibsho waviweke kwenye michele au mahindi yalivyozaliwa humu humu nchini.

Matango na maparachichi tunayokula yanatoka mkoani au burundi.....Matango tunakula yaliyoliwa na waha.
 
Hauna uthibitisho huo,
Huko wanapokula GMO lifespan yao ni miaka 80 wakati huku mnapodengua lifespan yenu ni miaka 60.
Hawa jamaa wagehitaji kutupata waafrika tungekamatika kirahisi mno hata tu kwenye nguo za mitumba! /
Hofu kuwa ya wazungu kwa sasa ni jinsi waafrika tunavyozaliana kwa kasi, ikipigwa hesabu inaonekana by future robo tatu ya wana dunia itakuwa ni waafrika!
 
Tuache kuonyesha ujinga wetu katika ngazi ya kimataifa juu ya uwezo wa akili zetu kufikiri, tumepewa msaada na marafiki zetu wa muda mrefu, waliwahi kutupatia, mafuta, mahindi, samaki na vingi tu ndani ya nchi yetu,
Pia izingatiwe wangelikuwa na uovu, basi kwa kuwa chanjo, dawa na vingi tu hupata kutoka western countries, wasingeweza kutukosa katika kufanya ubaya wa aina yoyote waupendao, sisi wa enzi hizo tulikula ugali wa njano ukiwa ni msaada toka kwa marafiki zetu hawa wa damu na hakuna baya lolote lilitupata.
Tupuuze akili zisizo na msingi wowote na ukweli halisi, tunaishi kwa hisia hasi na mawazo hasi,tulio wengi wetu.View attachment 2937128
Nchi inadanganywa na lisomali limoja lijinga na watu mnasema Yes you are right.

Was the consignment not inspected by TBS? Why is it there?
Kwa akili za kitaahira za viongozi wenu hawa. Marekani akimuamua kutufanyia lolote anaweza bila hayo maatahira kujua.
Uwezo wetu umeishia kwenye kuzurura
 
Ukikataa GMO za mchele na mahindi utazikuta GMO za dawa, zipo dawa nyingi zimetokana na GMO

GMOs have also been developed in other fields, such as medicine and industry. In medicine, GMOs are used to produce pharmaceuticals, vaccines, and other medical products. In industry, GMOs can be engineered to produce enzymes, biofuels, or other industrial chemicals.
 
Nchi inadanganywa na lisomali limoja lijinga na watu mnasema Yes you are right.

Was the consignment not inspected by TBS? Why is it there?
Kwa akili za kitaahira za viongozi wenu hawa. Marekani akimuamua kutufanyia lolote anaweza bila hayo maatahira kujua.
Uwezo wetu umeishia kwenye kuzurura
Wewe ndo msenge huna akili, hapo Kwenye port yetu vinapita vitu feki kibao na visivyo na ubora unaotakiwa kwa wingi mno, hao TBS kwani hakuna hapo hadi vinapita..?
Nyie wafuasi wa chadema kachukueni huo mchele mle na familia zenu
 
Tuache kuonyesha ujinga wetu katika ngazi ya kimataifa juu ya uwezo wa akili zetu kufikiri, tumepewa msaada na marafiki zetu wa muda mrefu, waliwahi kutupatia, mafuta, mahindi, samaki na vingi tu ndani ya nchi yetu,

Pia izingatiwe wangelikuwa na uovu, basi kwa kuwa chanjo, dawa na vingi tu hupata kutoka western countries, wasingeweza kutukosa katika kufanya ubaya wa aina yoyote waupendao, sisi wa enzi hizo tulikula ugali wa njano ukiwa ni msaada toka kwa marafiki zetu hawa wa damu na hakuna baya lolote lilitupata.

Tupuuze akili zisizo na msingi wowote na ukweli halisi, tunaishi kwa hisia hasi na mawazo hasi,tulio wengi wetu.

View attachment 2937128
Zamani tukiwa wadogo tulikuwa tunauita ugali wa Yanga😀😀
 
Acha kukariri kama ulikuwa unafanyiwa ubaya nyuma ndoa usifanyiwe sasa wazungu sio watu wa kuamini ata kidogo hao wanaenda na mabadiliko ya kisayansi na technologia mfano huu wanataka kupunguza population duniani kutokana na madai ya rasilimali ni chache kuliko population zidi siku zinavyokwenda hvo wanataka kuzingatia speed ya watu duniani inapungua ndoa unaona wanaanzisha ndoa za jinsia moja
 
Nchi inadanganywa na lisomali limoja lijinga na watu mnasema Yes you are right.

Was the consignment not inspected by TBS? Why is it there?
Kwa akili za kitaahira za viongozi wenu hawa. Marekani akimuamua kutufanyia lolote anaweza bila hayo maatahira kujua.
Uwezo wetu umeishia kwenye kuzurura
Tik tok wameizuia kwa khofu ya jamii zao kuharibikiwa.na cc tunazuia kwasababu zetu.walete pesa mchele upo hapa na maharage wakutosha.

Sent from my SM-G985F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom