Sababu ya Siasa: Biashara Kariakoo zinakufa kisa kuwapenda na kuwakumbatia machinga

We jamaa ,hili nilitaka kuliandika mapema .kimsingi pale kaliakoo mapato ya serikali yanapotea sana. Yaani ni hivi. wenye maduka wanawapa wale wauzaji wa nje kwa mkopo halafu wanarejesha jion.kumbuka hayo mauzo hayana reciept wala nini.

Cha pili.Pale kariakoo pamekuwa sio rafiki tena yaani hakuna stendi hakuna njia za waenda kwa miguu.yaani ni vurugu tupu kwa kwa kweli.hakuna utaratibu yaani ni hovyo.angalia ukitoka Ilala sokoni mpaka Stesheni pembeni barabara imeshakuwa finyu,ile njia ya waenda kwa miguu toka karume sokoni mpaka mataa yale ya mnazi mmoja kote zimekuwa biashara.si dahani kama hawa wote wana vile vitambulisho vya mmchinga.

Haya angalia pia ile barabara ya msimbazi,toka makutano ya uhuru na msimbazi mpaka fire ile barabara kila upande imeshajazwa biashara.mji una fujo nyingi zaidi,yaani hakuna utaratibu.
 
Wakifukuzwa, zitapanda nyuzi hapa kama mvua.." Machinga wanyanyaswa kama mbwa kariakoo"
Yani hamueleweki nini shida yenu.
Any way
Na wewe kuwa na uzalendp. nchi ni yetu sote kila mmoja ana haki sio upendeleo wa kijinga kama huo kwa Machinga
 
kama upi? usiishie kusema hivyo tu. wewe unaweza ukabuni utaratibu ukaona ni mzuri lakini wamachinga na wengine wasione kama ni mzuri
Ndiyo maana tumeweka viongozi wetu watuongoze, waumize vichwa watafute suluhisho, huo utaratibu mzuri.

Ndiyo maana tumeajiri maafisa wizara I na manispaa ya jiji na kwingineko watafute suluhisho.

Ndiyo maana mjadala umeletwa hapa ili tujadili, katika mawazo ya wachangiaji tunawaza kupata huo utaratibu mzuri.
Siyo lazima ushauri utoke kwangu.
 
aseme huo utaratibu. kila mtu anaweza sema hivyo. utaratiby kwako unaweza uona mzuri ila kwa wengine usiwe mzuri
Nimemtunuku sifa hii kutokana na kutumia kwake akili (angalau)katika kujibu hoja. Lakini kuna watu humu instead of giving out their view, wanaanza kuponda na kukashfu.

Watu hao hawawezi kutufikisha sehemu yoyote. Ni vema zaidi kama tukichangia kwa kutoa hoja zenye msingi na kujenga.
 
Back
Top Bottom