Mgomo wa Kariakoo; Serikali Iwasikilize Wafanyabiashara

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
610
1,540
Idara ya ACT Wazalendo ya Kuisimamia Serikali (Baraza Kivuli la Mawaziri) linafuatilia kwa karibu mgomo wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Kariakoo (JWK) uliotangazwa kuanza leo Mei 15, 2023 na kuendelea hadi changamoto zao zitakapotatuliwa.

Madai ya Wafanyabiashara hao ni pamoja na;

i) Kuishinikiza Serikali kutazama upya Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022 kifungu cha 45A kilichopo chini ya Sheria ya Usimamizi wa kodi kinachowataka wamiliki au watumiaji wa maeneo ya kuhifadhia bidhaa, kusajili maeneo hayo kwa Kamishna Mkuu.

ii) Vilevile, kumekuwa na malalamiko makubwa ya rushwa katika utozaji wa Kodi katika Eneo la Kariakoo ambapo maafisa wa TRA. Hali hii imefukuza wateja wengi kutumia Soko la Kariakoo katika Eneo la Maziwa Makuu
Kutokana na ukweli kuwa Eneo la Karikoo ni kitovu muhimu cha Biashara katika eneo la maziwa Makuu, ACT Wazalendo tunaitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kupata jawabu la kudumu la Eneo la Kariakoo ikiwemo kulitamka eneo hilo kisheria kama ENEO HURU LA BIASHARA.Hivyo basi, kufuatiwa na mgomo wa Wafanyabiashara unaoendelea sasa tunapendekeza zichukuliwe hatua zifuatazo;

i. Tunaitaka Serikali kupitia Waziri wa Viwanda na Biashara pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango kukutana na Wafanyabiashara wa Kariakoo haraka ili kuwasikiliza kwa kina, kujadiliana na wadau wote kwenye mnyororo wa thamani na hatimaye kutatua changamoto za Wafanyabiashara hao.

ii. Tunamtaka Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kufumua Uongozi mzima wa Mkoa wa kikodi wa Kariakoo na kuhamisha Wafanyakazi wote wa TRA eneo hilo na kuleta wengine kutoka mikoani nje ya Dar es Salaam.

iii. Mamlaka ya Mapato Tanzania izuie mara moja kamata kamata ya mizigo ya wateja kwa kisingizio cha thamani ya bidhaa mpaka hapo majadiliano na Wafanyabiashara yatapokamilika.

iv. Tunatoa rai kwa Wafanyabiashara kuwa na mshikamano usioyumba ili kuhakikisha changamoto zao zinatatuliwa kikamilifu.
ACT Wazalendo tunaendelea kusisitiza kwa Serikali kuchukua njia ya majadiliano, ushirikishaji ili kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi. Tunarejea wito wetu wa kufanya Kariakoo kuwa Eneo huru la Biashara kama jawabu la kudumu la changamoto za Wafanyabiashara wa Kariakoo.

Imetolewa na;
Ndg. Halima Yusuf Nabalang’anya
Twitter: @HalimaYusuf_N
Waziri Kivuli wa Viwanda na Biashara
ACT Wazalendo.
15 Mei, 2023
 
Hamna mgomo, nimeonda kununua sabufa KKOO Leo hii trh 15/5/2023.

Wafanyabishara makini wanaendelea kusaka pesa
 
Wafanyabiashara wa kariakooo tumemuwlewa sana waziri Mkuu, kuanzia sasa Maduka yaliyo kuwa yamefungwa yanafumhuliwa.
 
Ni mpumbavu kujiita waziri kivuli wakati hauko Bungeni pia kodi ni lazima

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wafanyabiashara tumemuelewa waziri Mkuu na kuanzia sasa hivi tunafungua maduka na biashara inaendelea kama kawaida.
Kazi iendeleee
 
Kwahiyo mgomo umeisha shida zimetatuliwa
Tanzania ni nchi yetu, na tunawaamini viongozi wetu kuwa watatatua changamoto zetu.

Kitendo Cha waziri Mkuu kufika na kusikiliza shida zetu ni dalili tosha ya kuzitatua.
Hatuna budi kuendelea na biashara ili tulijenge Taifa letu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom