Sababu tatu kwanini Wachungaji wengi wanasumbuliwa na Zinaa

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,602
15,400
Utangulizi

Kaka watatu huko kusini mwa afrika wameapa kumpiga Mchungaji kila jumapili hadi atakapokubali Mimba aliyoikana ya Dada yao.https://www.faceofmalawi.com/2022/04/07/3-men-beat-pastor-for-impregnating-their-sister-and-denying-the-pregnancy-vows-to-continue-beating-him-every-sunday-until-he-accepts-the-pregnancy/

Hii imekuwa shida kubwa ya makasisi na viongozi wa kiroho.

Nimetafiti nimegundua hizi ndio sababu kuu.

1: Wanakuwa wamezungukwa Muda mwingi na wanawake

Wateja wakuu wa mambo ya Mungu huwa ni wakina mama. Hata Yesu walimzunguka lakini alikuwa na mipaka. Akiachana nao anaenda kukesha ila wengi wanalala na kuomba kidogo. Hapo Mtumishi utaangushwa.

2: Wana migogoro kwenye Ndoa zao
Hekima ya kushindwa kubalance ndoa na utume wanajikuta familia au Mke katelekezwa. Wafariji wakuu wanakuwa wana wa kike makanisani. Rahisi kuporwa hisia na kuzichepusha kwa wamama au wadada wanaomzunguka.

3: Ushauri nasaha
Katika maandiko hakuna Mtumishi eti amekaa chobisi/faragha anamshauri mwanamke kuhusu Ndoa na mapenzi. Hii hufanywa na wanasaikolojia wa duniani. Utafiti katika kitabu (Stop biblical counciling start Biblical ministering) anasema Asilimia 35 ya makansela wachungaji au wadunia huzini na hao wanaowakanseli. Unatakiwa kuomba, Na kufanya awe wa kiroho ili atatue matatizo yake na Yesu wake, sio wewe uanze kumchimba. Pia Ni dhambi kumshauri MTU mmoja faragha kwa jambo linalohusu watu wawili bila upande mwingine kuwepo. Utafanya maamuzi kwa taarifa za nusu uongo.

4: Shambulizi la Ngono
Wako watu wanatumwa kuwaangusha watumishi makusudi. Ni mkakati wa makusudi kuwablackmail au kuwapoza wale watumishi wa kweli. Hii hufanywa na majasusi wa kubwa kuwafunga viongozi wa kisiasa kwa kuwatengenezea skendo duniani. IInaitwa HONEY TRAP. Sio kila Mchungaji anazini kwa kupenda wengine wameangushwa.

5: KAFARA YA NGONO
Wale wachungaji feki ngono ni ibada. Ni sujudu kwa ibirisi ili kuongeza upako wa kuzimu. Huyu atazini na wajane, vibinti, wakongwe, wake za watu bila kukoma.

Mwisho
Ukisikia MTU anakuwa Mchungaji au Mtumishi wa Mungu Muombee sana. Angusho la kingono linanzunguka 24hrs7Days.

Ni hayo tu

Karibu kwa maoni zaidi na maswali.
 
Hao wa chungaji sio kua wana udhaifu wa ngono tu, wana madhaifu mengi jaribu kumkopesha pesa, ndo utawajua vzri....
Hii nilikuwa sijui.
Ethics za watumishi wa Mungu hairuhusiwi kumkopa muumini, au kufanya kuwa full sponsor wa shughuli zako. Hii itapunguza authority yako.
 
Hapa umetengeneza www4 hii ni vita uliotengeza mkuu tena zaidi ya russia vs ukrane...ngoja waje wafia dini zao
Waje tu hahahaha
Hii itakuwa vita ya maarifa. Na ukweli kwa asili huwa unashinda hata ukifukiwa unafufuka kama Bwana Yesu.
 
Ila wamama wanashida sana, hata kwa waganga wa kienyeji wao ndo wateja wao wakubwa.

Wale waliosema ukimwelimisha mwanamke umeikomboa dunia hawajakosea.
Awapendi kutafuta maarifa wakiwa na maarifa waganga watakosa pesa
 
Shetani ana vita kubwa sana na watumishi wa Mungu wanawake utumika kama agent kuwaangusha wachungaji.
Ushauri mchungaji akianguka msitenge mmuombee lile ni shambulio la kiroho.
 
Kwenye huduma za kiroho yafaa kuwepo na kuwepo na kikundi maalumu cha kumuombea mtumishi na KILA muumini awe anamuombea mtumishi KILA siku afanyapo maombi, nazungumza haya kwa ushahidi wa waliokuwa maajent wa kuzimu kitengo cha kuwaangusha wachungaji walikuwa wakiwatumia wanawake warembo na tamaa ya pesa hivi vitu viwili kwa mwanadamu huwezi vishinda kama huna Mungu.
 
Shetani utumia wanawake warembo na tamaa ya pesa kuwaangusha wachungaji. Mtu akiwa mchungaji muombee sana
 
Awapendi kutafuta maarifa wakiwa na maarifa waganga watakosa pesa
Awapendi kutafuta maarifa wakiwa na maarifa waganga watakosa pesa
Kuna vitu vinafanyika ambavyo MTU yoyote asiyependa kusoma kureason na kuhoji hata kama ni mwanaume unaweza kujikuta mtegoni.

Mfano ukiona mfumo hauna uwazi, watu hawaruhusiwi kuuliza maswali au kufafanuliwa hata vitu vidogo rahisi kunaswa.


Elimu elimu elimu
" Funguo za maarifa " ni muhimu ili kuwa muumini unayejitambua
 
Shetani utumia wanawake warembo na tamaa ya pesa kuwaangusha wachungaji. Mtu akiwa mchungaji muombee sana
Ni kweli
Cha ajabu unakuta Mchungaji anajiweka kama Yesu hana mapungufu waumini wanadhani haitaji kuombewa.

Kumbe hata Paulo alikuwa anaandika barua aombewe.
 
Kwenye huduma za kiroho yafaa kuwepo na kuwepo na kikundi maalumu cha kumuombea mtumishi na KILA muumini awe anamuombea mtumishi KILA siku afanyapo maombi, nazungumza haya kwa ushahidi wa waliokuwa maajent wa kuzimu kitengo cha kuwaangusha wachungaji walikuwa wakiwatumia wanawake warembo na tamaa ya pesa hivi vitu viwili kwa mwanadamu huwezi vishinda kama huna Mungu.
Hii ni muhimu sana.
Mchungaji anayeombewa hudumu.
 
Ndio maana wamama wachungaji wengi rahisi kuangushwa maana huwa wametelekezwa kwa kisingizio cha huduma.

Mchungaji ambaye habalansi maisha ya Ndoa na utume ni kumuombea maana utumishi utageuka kuwa tiketi ya anguko lake.
 
Back
Top Bottom