Wachungaji, Mitume na Manabii wote pita Huku: Ahadi za utabiri wenu haujatimia.

WeedLiquorz

JF-Expert Member
May 30, 2022
3,291
5,466
Habarini ndugu katika jukwaa, Hongereni kwa uvumilivu kuelekea kuumaliza mwaka na tumshukuru Allah kwa kuturehem sisi.

Hawa wenzetu manabii na mitume plus wachungaji katika majukum yao hututabiria baraka kem kem ilihali wao wenyewe hawajua chochote kuhusu kesho, utasikia huu kwaka ni wako nakutabiria utanunua gari, utajenga nyumba, utapata kazi, utaoa au kuolewa, utapata na blas blaa zingine nyingi.

Sasa ahadi zenu hazijatimia kutokana na kwamba uwezo huo wa kumpangia Allah cha kututendea hamna, Watu waliuanza mwaka kwa matumaini makubwa lakini umeisha kama ulivyowakuta na pengine mmewarudisha nyuma kiuchumi, mmevunja ndoa za watu na hasara zingine.

Binafsi sikutia maanani ahadi zote za manabii huu mwaka walipokua wakijaribu kunishawish nijiunge makaisani mwao ila niliwambia nikihitaji kumtumikia bwana nitakuja bila hata ahadi kwakua ninajua lengo la kumtumikia bwana si baraka za duniani tu bali uzima wa milele.

1.Naomba kujua mwaka huu mnakuja na swagga gani ili kutulaghai na kuendelea kupiga vibunda vyetu kwa jina tukufu la "sadaka ya shukran".

2.Wale mliotabiriwa na mkatendewa kujeni hapa pia mtushawishi na sisi kama sehem ya ushuhuda wenu, karibuni.

Huu mwaka kataa uhuni wa kiroho na wa kisiasa, Kheli ya mwaka mpya 2024 ndugu zanguni.
NB: MUNGU YUPO.
 
download.jpeg.jpg
 

Attachments

  • images.jpeg-5.jpg
    images.jpeg-5.jpg
    25.2 KB · Views: 2
Utasikia... Mtu hakufanikiwa kwa vile hakulitendea neno kazi.... Oooh wengine walijichanganya wakazuia baraka zao... Oh... Ili mradi blablaaa nyingi za kitapeli !!!
Sasa hapo jiulize ambao hawakuahidiwa wanetoboa kwa nguvu za nani?
Na kwanini asitoe ahadi isiyo na shaka maana hayo masharti wanakua ka waganga tu.
 
Back
Top Bottom