Yesu Anakuja
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 9,515
- 19,341
Leo nilikuwa najadili na mke wangu, tukafikia discussion moja, wanawake wengi sana wanapenda kuita wachungaji wao "baba yangu", wanawapa heshima kubwa kuliko hata ile wangewapa waume zao au baba zao. mchungaji au nabii au padre anainuliwa sana, anaonekana yeye ni mtu special sanaaaa, treatment anayostahili ni special sanaaaa, na yeye asipokuwa treated hivyo anachukia kwasababu anajiinua na kuona sio sawa na wengine. mimi na Mke wangu huwa tunapinga sana hili jambo. Yesu alikemea sana jambo hili baada ya kuona waalimu wa sheria na viongozi wa kwenye masinagogi wanapandisha mabega, wanapenda watu wawaite "mwalimu", baba n.k na wakipita hata masokoni au popote watu wawape recognition fulani ya special. na ndivyo ilivyo na siku hizi.
MATHAYO 23:9 INASEMA; Wala msimwite mtu baba duniani; maana Baba yenu ni mmoja, aliye wa mbinguni. Wala msiitwe viongozi, maana Kiongozi wenu ni mmoja, naye ndiye Kristo. Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu. Na yeyote atakayejikweza, atadhiliwa, na yeyote atakayejidhili atakwezwa.
Wachungaji, manabii, mitume, mapadre na mafather, wengi huwa wanapenda sana recognition, wengine wamefikia hatua wanaamini wao ni baba wa kiroho wa mtu fulani as if wao wameokoa roho yake au labda walikuwa na uwezo wa option ya kuamua kumfanya aokoke au asiokoke. Enzi za Yesu alipokuwa katika mwili haya pia yalikuwepo, Mafarisayo na masadukayo na waalimu wa sheria walikuwa wanapenda sana recognition, Yesu akafuta icho cheo kwao, kilichokuwa kinawafanya wajiinue kujiona wapo bora kuliko wengine, ndio maana aliongea mstari huo hapo juu.
Wengine wanashindwa kuelewa, kwani Yesu alimaanisha tusiite biological parents baba? Au alimaanisha nini? JIBU: alimaanisha baba wa kiroho, kamwe usimfanye mchungaji wako, mwalimu, anayejiita nabii au mtume kuwa ni BABA yako, ukiangalia kwenye tv utaona watu wanampa sifa mchungaji ati “baba”, imefika mahali watu wanaita fulani ni baba yangu. Yesu alikataza hilo.
KUTOKA 20:12 anasema waheshimu baba yako na mama yako…, hapa alikuwa anaongelea baba na mama kimwili (biological), ila ukija kwenye mambo ya Mungu, acha kuita wachungaji au manabii wenu hao baba, kwasababu tunaye baba mmoja tu, aliye mbinguni, wala msiwaite waalimu kwa maana ya kuwainua wao. Hao hawana uwezo wowote kuwazaa kiroho, hata kama wamewahubiria wametumiwa kama vyombo tu ila anayewazaa kiroho ni Mungu, hao mnaowatukuza na kuwaita waalimu hawana uwezo wowote wa kufundisha na kubadilisha mioyo yenu, wajiite tu watumishi au vyombo vya Bwana, kwasababu hata wawe na uwezo mzuri namna gani kufundisha anayebadilisha roho ni Mungu wala sio uwezo wao wa kupangilia maneno. Mwenye kunielewa amenielewa, achene kutukuza watu. Na ninyi mnaotukuzwa msikubali kutukuzwa, achene anayestahili utukufu, Mungu wa mbinguni, apate utukufu wake wote, msiibe utukufu wake. Mungu awabarikini nyote muelewe hili.