Wakristo wengi kwa kukosa maarifa wanajiangamiza sana na kujikuta hawajielewi

Minjingu Jingu

Senior Member
Nov 2, 2023
116
477
Nimeamua kuandika huu uzi baada ya kusoma nyuzi kadhaa na maoni ya watu mbalimbali.

Hizi Dini kuu mbilii za Ukristo na Uislamu ni Mkusanyiko wa Tamaduni za Makabila makuu mawili.
1. Kiyahudi
2. Kiarabu.

1. Ukristo chimbuko lake ni Uyahudi ambapo Yesu Kristo pia alikuja kuregeza baadhi ya tamaduni za Kiyahudi na kutaka matumizi ya akili na tafakuri (roho mtakatifu) kuna sheria kali ambazo baadaye alikuja kuziboresha. Kama ubaguzi kwa wasio wayahudi, ulaji wa vyakula, matendo siku ya Sabato n.k.

Aligundua kulikuwa na unafiki mwingi wa hukumu kwa kuzingatia kanuni au sheria za kiyahudi. Kumbuka hadithi ya mwanamke yule aliyekuwa amezini. Kisheria alipaswa apigwe mawe. Lakini kumbuka alipelekwa peke yake. Mwenzi wake hakuwepo. Na pia wale waliompeleka je walikuwa na usafi ule wa kusema wanafaa kuhukumu mwenzao afe kikatili kwa kupigwa mawe?

Suala la Ndoa Kikristo ni jepesi sana. Makubaliano ya watu wawili. Wakashirikisha wazazi. Ikatolewa mahari. Mchungaji akawaunganisha. Harusi??? Ni uchaguzi. Si lazima. Wengine huwa wakimaliza kufungishwa ndoa wanarudi home wanaanza maisha. But utakuta mtu kwa ujinga anasema Ndoa zetu zina ugumu zinataka sana pesa. Wapi unatakiwa utoe 200,000 kufungishwa ndoo Kanisani? Ni ujinga unakufanya uamini hivyo.

Suala la mazishi. Yesu alikufa the same day akaenda zikwa. Wala hakuna kifungu kinachosema mpaka waje wajomba au mchungaji au nani kufanya maombi. Biblia inasema " kama ilivyoandikwa kufa mara moja na baada ya kifo hukumu"

Hapo mtu akifa acheni ujinga wa kutaka misa kuuubwa na mapadre, wachungaji,. Maaskofu, Makadinari n.k hawa hata wakuombee siku 365 haitabadilisha hukumu yako. Unaikumbuka hadithi ya Lazaro?

Mtu akishakufa amefunga mahesabu kuwekwa pema peponi kunategemeana na alivyoishi mpaka mauti. Na akishakufa ule mwili its nothing hata ukimzika na sanduku la dhahabu haisaidii kitu. Ukiamua kumzungushia tu kanga ukamzika kwa Mungu hana tofauti na yule aliyezikwa kaburi la marumaru.

So ujinga mwingi upo kutokana na watu kutosoma na kuielewa Biblia. Wanachukua mapokeo au mafundisho ya kidini na kusahau msingi wa Biblia.

"BIBLIA INASEMA WATU WANGU WANAANGAMIA KWA KUKOSA MAARIFA"
 
Back
Top Bottom